Mahusiano ya hivi kitaalamu yanaitwaje?

Mahusiano ya hivi kitaalamu yanaitwaje?

Iko hivi,

Huu mkoa niliopo kuna dogo mmoja wa bodaboda huwa namuagiza vitu nikipata dharura, tumezoeana sana. Hata akipata shida ndogondogo sitosita kumsaidia.

Sasa siku moja nilimualika kwangu aje tupate chakula cha mchana. Kwenye maongezi akaniuliza, "Bro hivi huna mtoto?". Nikamjibu sina. Akauliza tena, "Mke je?". Nikamwambia sijao. Akaniuliza, "kwanini?". Na mimi nikamuuliza, "Sasa nitamuoa nani?". Akasema bro hukosi wa kuoa labda kama hujaamua tu. Akaniambia kuna dada anamfahamu anafaa kuwa mke. Kweli akanilengesha kwake.

Siku moja nikaenda kwa huyo dada. She is 28 years, ana mini-supermarket kubwa tu, lakini pia ni wakala wa M-Pesa, TigoPesa, Airtel Money, HaloPesa na CRDB. Nikashtuka kidogo kwa namna alivyo stable kiuchumi katika umri wake. Mwanzoni nikajua ni mwajiriwa, baadaye ndio nikagundua vyote ni mali yake.

Basi tukazoeana. Nikawa mteja wake mzuri tu. After a while tukawa wapenzi. Nikaanza kumdadisi, ndio nikajua umri wake. Pia akanieleza kwamba alishafunga ndoa, akazaa na mumewe wakaachana, so ana mtoto mmoja wa form one. Hakutaka tena kumzungumzia huyo mtalaka wake.

Kinachonishangaza ni hiki. Nisipomtafuta halalamiki wala hanitafuti. Nikizidiwa nikamcheki anakuja kwangu nalala nae. Akizidiwa ananicheki, naenda kwake kumuhudumia. Hajawahi kuniomba hela hata siku moja! Nikiwa na shida na hela ndogondogo kwa dharura ananitumia kwenye simu na hanidai, unakuta najishtukia mwenyewe ndio namlipa.

Kuna siku lock ya lango kuu la chuma la kuingia dukani kwake lilikataa kufunguka akaniomba nimtafutie fundi welding, nikamtuma fundi aende ila asichukue hela nitamlipa mimi. Nikaenda dukani wakati fundi anaendelea na kazi. Alipomaliza ile jioni nampigia fundi aniambie gharama, fundi ananiambia dada kashamlipa, nikamwambia kamrudishie pesa yake, dada kagoma kuipokea!

Juzi Ijumaa akaniomba nikae dukani kwake aende msikitini, nikakubali ila nikamwambia sitauza kitu, so wateja wakawa wakija nawaambia ametoka. Pembeni ya kiti chake akaacha 'safe' wazi, nikaifungua nikakuta miburungutu ya hela, nikaifunga nikanyamaza.

Leo ni siku ya 4 tangu niuze gari yangu ndogo, lengo ni kuongeza hela ninunue ingine, asubuhi kanipigia anasema kwasababu yeye anashinda dukani basi naweza kutumia gari yake kwa muda ili nisipate shida, nimeogopa nikaona huu ni mtego, nikamwambia asante nikamchomolea.

Sasa wakuu nashindwa kabisa kumuelewa huyu mwanamke! Ni kwamba ameyachoka mapenzi au nini nini hiki! Amejenga nyumba yake ya vyumba 2 na sebule, majuzi kanunua kiwanja kingine kikubwa mji mpya na ameshapeleka mchanga, kokoto, mawe na kapiga uzio.

Hebu tusaidiane wajameni, usije ukawa ni mtego huu, pengine ana sponsor naweza kujikuta naishia pabaya. Kiukweli sijawahi kuwa suspicious hata siku moja kwamba ana mahusiano mengine. Simu yake yuko free nayo sana, ndio anazidi kunichanganya!

Nje ya mada:
Pamoja na miaka yangu 11 humu JF, nashindwa kuona notifications mpya, ni wiki sasa inakatika, sijui nimebonyeza wapi, wajuvi mnisaidie.

Asanteni.

Sent using Jamii Forums mobile app
Tegemea kuwa msukule karibuni. Unaliwa timing tu.
 
Miaka 28 mt
Mmh miaka 28 ana mtoto yupo form one,.
Chazo Cha huo uchumi wake ni nin urithi au mgawo kutoka Kwa mmewake coz Kwa umri huo kuwa na gari, supermarket, office ya huduma za kifedha mmh kibongobongo kweli mPambanaji.
oto form one mhhh aya
 
Mkipata wadada mambo safi mnalalamika, mkipata akina sisi hatuna kitu bado mnalalamika [emoji124][emoji124][emoji124][emoji124]
 
Cha kujiuliza ni huo usuper woman kwanza. Hapo ndo penye majibu yote.

Ni kawaida wanawake kutokuficha simu zao kama sisi. Sisi mbinu zetu ni chakavu sana mbele yao.
Kua makini aisee, sema ukakasi mwingine ni huyo dogo wa form 1 na yeye ako na 28, means alimzaa akiwa under 18.
 
Iko hivi,

Huu mkoa niliopo kuna dogo mmoja wa bodaboda huwa namuagiza vitu nikipata dharura, tumezoeana sana. Hata akipata shida ndogondogo sitosita kumsaidia.

Sasa siku moja nilimualika kwangu aje tupate chakula cha mchana. Kwenye maongezi akaniuliza, "Bro hivi huna mtoto?". Nikamjibu sina. Akauliza tena, "Mke je?". Nikamwambia sijao. Akaniuliza, "kwanini?". Na mimi nikamuuliza, "Sasa nitamuoa nani?". Akasema bro hukosi wa kuoa labda kama hujaamua tu. Akaniambia kuna dada anamfahamu anafaa kuwa mke. Kweli akanilengesha kwake.

Siku moja nikaenda kwa huyo dada. She is 28 years, ana mini-supermarket kubwa tu, lakini pia ni wakala wa M-Pesa, TigoPesa, Airtel Money, HaloPesa na CRDB. Nikashtuka kidogo kwa namna alivyo stable kiuchumi katika umri wake. Mwanzoni nikajua ni mwajiriwa, baadaye ndio nikagundua vyote ni mali yake.

Basi tukazoeana. Nikawa mteja wake mzuri tu. After a while tukawa wapenzi. Nikaanza kumdadisi, ndio nikajua umri wake. Pia akanieleza kwamba alishafunga ndoa, akazaa na mumewe wakaachana, so ana mtoto mmoja wa form one. Hakutaka tena kumzungumzia huyo mtalaka wake.

Kinachonishangaza ni hiki. Nisipomtafuta halalamiki wala hanitafuti. Nikizidiwa nikamcheki anakuja kwangu nalala nae. Akizidiwa ananicheki, naenda kwake kumuhudumia. Hajawahi kuniomba hela hata siku moja! Nikiwa na shida na hela ndogondogo kwa dharura ananitumia kwenye simu na hanidai, unakuta najishtukia mwenyewe ndio namlipa.

Kuna siku lock ya lango kuu la chuma la kuingia dukani kwake lilikataa kufunguka akaniomba nimtafutie fundi welding, nikamtuma fundi aende ila asichukue hela nitamlipa mimi. Nikaenda dukani wakati fundi anaendelea na kazi. Alipomaliza ile jioni nampigia fundi aniambie gharama, fundi ananiambia dada kashamlipa, nikamwambia kamrudishie pesa yake, dada kagoma kuipokea!

Juzi Ijumaa akaniomba nikae dukani kwake aende msikitini, nikakubali ila nikamwambia sitauza kitu, so wateja wakawa wakija nawaambia ametoka. Pembeni ya kiti chake akaacha 'safe' wazi, nikaifungua nikakuta miburungutu ya hela, nikaifunga nikanyamaza.

Leo ni siku ya 4 tangu niuze gari yangu ndogo, lengo ni kuongeza hela ninunue ingine, asubuhi kanipigia anasema kwasababu yeye anashinda dukani basi naweza kutumia gari yake kwa muda ili nisipate shida, nimeogopa nikaona huu ni mtego, nikamwambia asante nikamchomolea.

Sasa wakuu nashindwa kabisa kumuelewa huyu mwanamke! Ni kwamba ameyachoka mapenzi au nini nini hiki! Amejenga nyumba yake ya vyumba 2 na sebule, majuzi kanunua kiwanja kingine kikubwa mji mpya na ameshapeleka mchanga, kokoto, mawe na kapiga uzio.

Hebu tusaidiane wajameni, usije ukawa ni mtego huu, pengine ana sponsor naweza kujikuta naishia pabaya. Kiukweli sijawahi kuwa suspicious hata siku moja kwamba ana mahusiano mengine. Simu yake yuko free nayo sana, ndio anazidi kunichanganya!

Nje ya mada:
Pamoja na miaka yangu 11 humu JF, nashindwa kuona notifications mpya, ni wiki sasa inakatika, sijui nimebonyeza wapi, wajuvi mnisaidie.

Asanteni.

Sent using Jamii Forums mobile app
Huyo mwanamke mshike mkuu jisshushe sana kwake ni lulu na ni wachache kuwapata
 
Mkuu, ume-digest maelezo yako vizuri sana. Acha niyafanyie kazi lakini kwa uangalifu mkubwa.

Pengine huyu mwanamke ni mwema tu, ila mashaka yangu ndio yanaweza kufanya nimpoteze.

Asante kwa ushauri mkuu.

Sent using Jamii Forums mobile app
Uwe tu na moyo mwema kibinadamu. Sio umemkuta mtu katulia,unaingia kwenye maisha yake unamvuruga,unamvurugia then unakula kona. Kumbuka hilo.
 
Mkuu, kwa umri huo na mtoto aliyenae, ni dhahili kazaa bado mdogo sana. Iwe baba mtoto au mtu mwingine,kuachana nae ni kufikia tu.
Kwanza mnunulie supu na chapati huyo dogo wa boda boda then uje hapa.

Sasa basi, ngono za mapema huwaathiri wanawake kisaikologia. Ukute yeye kama yeye,tena si demu wa kubembelezana.
Si umesema we hupigwi mizinga!?
Haya,umelala nae umegegeda. Dogo alikwambia kuna mdada anafaa kuwa mke. Je,umeshamaliza shida ilokupeleka,au umeogopa tu kusema!?
Ndoa za siku hizi ni kujitosa tu. Huku unagonga,na yeye pengine kule anagonga.
Ila sasa:
-Ukiwa kwake, anachukuliaje(anakuheshimu kama mme,au unaenda tu unalala unadinya na kusepa)
-Maongezi yenu yanaashilia nini.
-Uliwahi mtania kuhusu kuishi nae? Alijibuje!

Si kwamba kila mwanamke mwenye uwezo ana bwana;wengine wamepambana kivyao. Either kwa kujiuza, kupiga mizinga,kutapeli,kuiba, kama ilivyo tu kwa wanaume wengine.
Haimaanishi kwamba kuwa na mtalo kule chini,hata akilini ni hivo hivo kwa wote.

Wewe tu epuke pesa za bule(ukikopa rudisha).

Jaribu kutoka nae nje ya mazingira ya kazi(pasiwe mbali),enjoy, lala huko,then geuza.
Siku ukisikia anaongelea miradi yake na anakushirikisha, na pengine angependa mkasaidizane,na wewe piga hatua moja mbele.
Kwani kuachika nini? Huko unagonga, hajui. Nae pengine anagongwa,hujui.
 
Back
Top Bottom