Mahusiano ya kimapenzi bila pesa hayawezekani?

Mahusiano ya kimapenzi bila pesa hayawezekani?

Mahusiano ya kimapenzi kwa sasa kama huna pesa mwanamke atakutesa Sana Atakudharau nainawezekana akakuacha kabisa au kukawa na migogoro isiyo isha.(wanaume tutafuteni pesa)
Kama kuna mtu anabisha aje na hoja au kama una chakuongezea unaweza ongezea.
Wwe kaa ukijua kua Mapenzi hayana formula, ukiwa na pesa unaweza ukaachwa au ukagongewa,na ukiwa huna pesa vilevile unaweza kugongewa au ukaachwa! Just go with the flow!!
 
Mahusiano ya kimapenzi kwa sasa kama huna pesa mwanamke atakutesa Sana
Mj
Ni Lini mahusiano ya kimapenzi hayakuhusisha pesa? Embu taja kizazi ambacho unafikiri mwanamke hakuwahi kuhitaji pesa?
Kama kuna mtu anabisha aje na hoja au kama una chakuongezea unaweza ongezea.
Ni kiasi gani cha pesa mwanaume akiwa nacho inampa uhakika wa mapenzi yake kwa mwanamke? Ni ndoa ngapi za watu matajiri ulishawahi kusikia zimevunjika?
 
Hivi huwa na nyie mnapenda kweli,
Yani mtu unakuta yuko moyoni mwako kabisa awe na pesa asiwe nazo we sawa tu!

Amehlo nidadavulie hapa
eeh tunapenda kweli ndio sana tu alafu ujue mtu kuwa na pesa ni swala moja na kukupa ni swala lingine

anaweza asiwe nazo na akipata kidogo anakupa kutokea hapohapo kwenye kidogo😊😊
 
Mapenzi sio pesa, ila ikikosekana yanapungua😂😂
Exactly, mapenzi sio pesa lakini ni pride ya mwanaume kumsaidia na kumspoil mwenza wake hasa nyakati za uhitaji, shida inakuja hata pale unapohitajika kutoa kidogo na ukashindwa, kuna kaunyonge huwa kanakuingia as a man.

Umasikini mbaya wee Amehlo usikie kwa watu tu.
 
Kuhusu PESA

Usitafute PESA ukiwa umeweka nia kuwa hiyo PESA ni kwa ajili ya kuhudumia mahusiano.

Tafuta PESA ukiwa unajua kuwa hii PESA ni kwa ajili ya kuyaboresha MAISHA yangu na kuwa na kesho bora pamoja na kuwaninua waliopo chini.

Mwanamke anamtesa MTU aliyeamua kuteseka na sio vinginevyo.

PESA inachukua nafasi kubwa katika MAISHA ikiwemo kuhudumia mahitaji yako ya muhimu Kama AFYA ,ELIMU , n.k.

So tafuta PESA ikusaidie kukutoa katika dhiki na sio ili uwavutie wanawake.

Then kosa kubwa wanalolifanya vijana ni katika kutafuta Heshima kutoka kwa wanawake.

Kabla ya kutaka MTU akupe heshima au akukubali kupitia PESA yako unbidi kuangalia ni aina gani ya watu unataka wakuheshimu kwanza.

Ili MTU akupe heshima inabidi yeye awe anajiheshimu kwanza.

Ili MTU akupe adhi ya juu na yeye lazima awe na hiyo adhi ya juu

So usitegemee mwanamke ambaye anataka hela yako ili akuheshimu akawa na hizo sifa za kujiheshimu na kuwa na high status.

Make money
Love money
Spend it wisely

Don't go broke to impress women or people.
 
eeh tunapenda kweli ndio sana tu alafu ujue mtu kuwa na pesa ni swala moja na kukupa ni swala lingine

anaweza asiwe nazo na akipata kidogo anakupa kutokea hapohapo kwenye kidogo😊😊
Mi nasema kila siku humu, hamna mwanamke asiependa matunzo/kutunzwa....as a man jitahidi kutafuta wa level yako, wa kuendana nae, kama huna uwezo wa kuhonga "macho matatu" mbona wapo mabinti warembo tu mtaani ukimnunulia chipsi zege, ukampa hela ya vocha na kijora anaridhika tu, shida ni pale unapotaka makuu kujitutumua kwa vitu usivyoviweza, utaumia tu. Stay on your Lane.
 
Mahusiano ya kimapenzi kwa sasa kama huna pesa mwanamke atakutesa Sana Atakudharau nainawezekana akakuacha kabisa au kukawa na migogoro isiyo isha.(wanaume tutafuteni pesa)
Kama kuna mtu anabisha aje na hoja au kama una chakuongezea unaweza ongezea.
Mpende mke wako asikutawale!
 
Mi nasema kila siku humu, hamna mwanamke asiependa matunzo/kutunzwa....as a man jitahidi kutafuta wa level yako, wa kuendana nae, kama huna uwezo wa kuhonga "macho matatu" mbona wapo mabinti warembo tu mtaani ukimnunulia chipsi zege, ukampa hela ya vocha na kijora anaridhika tu, shida ni pale unapotaka makuu kujitutumua kwa vitu usivyoviweza, utaumia tu. Stay on your Lane.
kabisa yaani, tafuta mmoja wa level yako mtunze vizuri maisha yaendelee
 
kabisa yaani, tafuta mmoja wa level yako mtunze vizuri maisha yaendelee
Na shetani alivyokua na makusudi,kila ukimpata wa level yako,Shetani nae anamletea demu wako kidume kingine kinachokupita level yako na Mwanamke anakuacha! hapo ndiyo utajua kua hujui!!
 
Na shetani alivyokua na makusudi,kila ukimpata wa level yako,Shetani nae anamletea demu wako kidume kingine kinachokupita level yako na Mwanamke anakuacha! hapo ndiyo utajua kua hujui!!
Unatafuta tena wa levo yako huku ukideal na maisha yako, mwanamke akikuacha muache aende kamwe usimlilie wala akirudi usimpokee....
 
Back
Top Bottom