Mahusiano ya kimapenzi bila pesa hayawezekani?

Mahusiano ya kimapenzi bila pesa hayawezekani?

Naweza kupenda mwanaume asie na pesa..lakini awe na uwezo wa kujikimu na kujiingizia japo kidogo.yani awe anasimama kama mwanaume.anapambana kama mwanaume..sio wale kitu kidogo ngoja nkamwombe mama au bro!
Lakini awe na upendo wa kweli.
Sasa unamvumilia mtu Maisha mnayoishi shida.bado umalaya,akipata 5000 ishahongwa Kwa akina halima na kidawa.nivumilie Nini sasa hapo?
 
Mapenzi bwana wenye hela wanalalamika tunapendwa kwa ajiri ya pesa zetu.Maskini nae anasema tafuta pesa upendwe hii ni pasua kichwa.
Mapenzi haya fomula kuna watu hapa town na huko vijijini wanapendana na hawana mbele wala nyuma na wanahaso daily lakini wanapebdana hasa.Kina bill gate nilisikia mkewe anaomba talaka sasa kma pesa zingekua zinasaidia si zingemsave abaki na mkewe.
Bora ukawa na hela ya kuweza kumudu maisha yako kuliko kua na pesa mingi maana masnich wengi hutaka kupora mali zako ww angalia swala la Marehem Mengi.
 
Mj
Ni Lini mahusiano ya kimapenzi hayakuhusisha pesa? Embu taja kizazi ambacho unafikiri mwanamke hakuwahi kuhitaji pesa?

Ni kiasi gani cha pesa mwanaume akiwa nacho inampa uhakika wa mapenzi yake kwa mwanamke? Ni ndoa ngapi za watu matajiri ulishawahi kusikia zimevunjika?
Kwa maana hiyo mapenzi hayana kanuni , ila pesa nayo nimuhimu maana kiukweli hakuna mapenzi ambayo hayajawahi kuhusishwa bila pesa
 
Exactly, mapenzi sio pesa lakini ni pride ya mwanaume kumsaidia na kumspoil mwenza wake hasa nyakati za uhitaji, shida inakuja hata pale unapohitajika kutoa kidogo na ukashindwa, kuna kaunyonge huwa kanakuingia as a man.

Umasikini mbaya wee Amehlo usikie kwa watu tu.
Kabisa😂
 
Kuhusu PESA

Usitafute PESA ukiwa umeweka nia kuwa hiyo PESA ni kwa ajili ya kuhudumia mahusiano.

Tafuta PESA ukiwa unajua kuwa hii PESA ni kwa ajili ya kuyaboresha MAISHA yangu na kuwa na kesho bora pamoja na kuwaninua waliopo chini.

Mwanamke anamtesa MTU aliyeamua kuteseka na sio vinginevyo.

PESA inachukua nafasi kubwa katika MAISHA ikiwemo kuhudumia mahitaji yako ya muhimu Kama AFYA ,ELIMU , n.k.


So tafuta PESA ikusaidie kukutoa katika dhiki na sio ili uwavutie wanawake.


Then kosa kubwa wanalolifanya vijana ni katika kutafuta Heshima kutoka kwa wanawake.

Kabla ya kutaka MTU akupe heshima au akukubali kupitia PESA yako unbidi kuangalia ni aina gani ya watu unataka wakuheshimu kwanza.

Ili MTU akupe heshima inabidi yeye awe anajiheshimu kwanza.

Ili MTU akupe adhi ya juu na yeye lazima awe na hiyo adhi ya juu

So usitegemee mwanamke ambaye anataka hela yako ili akuheshimu akawa na hizo sifa za kujiheshimu na kuwa na high status.

Make money
Love money
Spend it wisely

Don't go broke to impress women or people.
Ushauri mzuri kabisa 🙏
 
Mi nasema kila siku humu, hamna mwanamke asiependa matunzo/kutunzwa....as a man jitahidi kutafuta wa level yako, wa kuendana nae, kama huna uwezo wa kuhonga "macho matatu" mbona wapo mabinti warembo tu mtaani ukimnunulia chipsi zege, ukampa hela ya vocha na kijora anaridhika tu, shida ni pale unapotaka makuu kujitutumua kwa vitu usivyoviweza, utaumia tu. Stay on your Lane.
Kabisa
 
Unatafuta tena wa levo yako huku ukideal na maisha yako, mwanamke akikuacha muache aende kamwe usimlilie wala akirudi usimpokee....
Mkuu una misimamo mikali sana 😂
 
Na shetani alivyokua na makusudi,kila ukimpata wa level yako,Shetani nae anamletea demu wako kidume kingine kinachokupita level yako na Mwanamke anakuacha! hapo ndiyo utajua kua hujui!!
😂😂😂😂 na nyie si mkipata hela mnawaacha wa level yenu mnaenda kwa wale mliokua hamuwezi kuwapata
 
eeh tunapenda kweli ndio sana tu alafu ujue mtu kuwa na pesa ni swala moja na kukupa ni swala lingine

anaweza asiwe nazo na akipata kidogo anakupa kutokea hapohapo kwenye kidogo😊😊
Mkipewa pesa mnazidisha upendo au ndo una muona bwege mtozeni??
 
Back
Top Bottom