SEX TALK!
Niliandika kuhusu mahusiano ya kingono miongoni mwa wanafamilia. Halafu Jana nikakutana na kisa cha mjane ambaye watoto wake wawili wamepewa mimba na kaka yao.
Wengi hawaamini wanadhani ni hadithi za kufikirika. Ukweli ni kwamba haya mambo yapo ndani ya jamii ila Mara nyingi hufanywa siri sana. Ukiacha huyu ambaye wamepata mimba kuna ambao hawapati mimba na huendelea na hiyo michezo.
Niliwahi ongea na binti ambaye hataki kuolewa sababu ana mahusiano ya kingono na kaka yake. Na alikua akibeba mimba anatoa, kaka MTU alipooa ikawa vita na WiFi mpaka ndoa ikavunjika, kaka akachukua mdogo wake kuishi naye. Wazazi hawajui kinachoendelea wanajua ni upendo wa kindugu tuu.
Nyakati hizi zimebadirika sana, unapoongea na watoto wengi wanakwambia wamefundishwa ngono na ndugu zao wa karibu.
Hata wanaojihusisha na mapenzi ya jinsia moja (usagaji na ushoga) wengi wao huanzia nyumbani. Akitoka hapo ndiyo ataenda kwa watu wengine.
Nyakati hizi kuna matumizi ya simu na kompyuta, watoto wanaangalia picha za ngono. Hawa ambao wapo kwenye umri wa balehe ni hatari zaidi, wakishaona hizi picha wanatamani kujaribu walichokiona, sasa wahanga wa karibu ni wale walio karibu naye..
Mambo yamebadirika sana, usiogope kuongea na watoto wako. Ongea nao kwa uwazi kulingana na umri wao.
Pia tupunguze uzungu, mambo ya kupakatana na kukumbatiana Dada na kaka ni hatari. Unakuta binti amevaa kikaptura, tumbo wazi, vichuchu vimechomoka anazunguka humo ndani na kuna kaka zake.. Huyu kaka ambaye anakula na kushiba, anashinda nyumbani anamtizama Dada anazunguka tuu ndani, mbaya zaidi awe ametizama hizi video za ngono unatarajia nini?
Tuwafundishe watoto wetu kuwa na adabu. Wajiheshimu na kujitunza miili yao wao wenyewe. Waambie madhara ya ngono kati ya ndugu. Wajifunze kuheshimiana waoa kwa wao .
Wakati huu wapo nyumbani wasikae tuu, watafutie shughuli za kufanya katika mazingira waliyopo. Walime bustani, Michezo mbali mbali, inayoweza kuwafanya wachoke, wapangie shughuli mbalimbali za mikono, zitakazowatoa jasho. Kuna msemo usemao "an idle mind is the workshop of the devil" . Hawa vijana waliobalehe miili yao INA nguvu na wana mihemko, ndiyo maana hata shuleni huwa wana ratiba za kufanya mambo mbalimbali nje ya masomo ili wasikae bure.
Kuna ambao wanapewa masomo kwa njia ya mtandao, ni bora ukawatolea kwenye karatasi(download) kuliko ukawapa simu maana ni wadadisi, hawataishia kusoma masomo yao tuu, watatafuta zaidi.
Watoto wa kizazi hiki wanajua mengi kuliko unavyojua we we . Unaweza fikiri hajui kutumia simu, kumbe anaijua kuliko wewe unayeimiliki.
Tenga muda wa kuongea na watoto wako, watafutie filamu,vitabu na majarida yanayofundisha kuhusu vijana na ujana,mahusiano na ngono.
Zaidi ya yote WAOMBEE SANA, shetani yupo kazini,anaandaa jeshi lake na hawa watoto ndiyo wanatakiwa sana. Kwasabau wao ni rahisi kuamini na kusambaza mambo haya. Hivyo pamoja na kuongea nao wakabidhi kwa Mungu, maana kuna mambo ambayo kwa uwezo wetu ni magumu na hatuyawezi. Kuna mambo watoto wanafanya ukisikia masikio yanawasha.
#MZAZI ONGEA NA MWANAO
Mwl. Doris Mboma