Mahusiano ya ndugu yanaharibika wakiingia katika ndoa

Mahusiano ya ndugu yanaharibika wakiingia katika ndoa

Moto wa volcano

JF-Expert Member
Joined
Jun 3, 2018
Posts
1,148
Reaction score
2,815
Mara nyingi mahusiano ya wanandugu huwa yanaharibika / kupungua pale wanapo oa au kuolewa , kuna wengine akili zinabadilika anaanza kutumia akili ya mke au mume zaidi na kudharau mambo ya familia aliyotoka.

Wanaume wengine wanaendleshwa na wake zao anafarakanishwa na ndugu zake
 
Mara nyingi mahusiano ya wanandugu huwa yanaharibika / kupungua pale wanapo oa au kuolewa , kuna wengine akili zinabadilika anaanza kutumia akili ya mke au mume zaidi na kudharau mambo ya familia aliyotoka . Wanaume wengine wanaendeshwa na wake zao anafarakanishwa na ndugu zake
Mimi ninachoona zaidi ni kutoka familia tegemezi unakuta mtu akioa yale matumizi yanapungua maana anaanza kujenga familia yake na unakuta pesa wanaipangia mipango na mwenzake. sasa hapo ndipo kasheshe linapoanza.
 
Sababu ni nyingi sana mleta mada sio kwamba watu wanapenda kukata mahusiano na ndugu zao la hasha kuna mambo kedekede sababishi ya kukata mahusiano ila hapa duniani kuna watu wanapitia changamoto sana acha tu mkuu, natamani siku moja nilete stori yangu jukwaani hapa ya mapito niliyopitia tuombe uzima.
 
Lazima tujue Kwanza maana ya ndoa kabla hatujaanza kulaumu watu.

Hii tabia ya kuendekeza binadamu imetufalakanisha na kutupulua sana sisi waafrika. Ndoa ni taasisi yenye mamlaka kamili,na ili taasisi yeyote iwe na ufanisi lazima kuwe na taratibu na sheria ambazo ndio zitaipambanua hiyo taasisi.

Tunapenda maisha tegemezi ndio maana lawama kwa wanandoa zinakua nyingi,maisha ya miaka 1960 na maisha ya miaka ya 2000 hayafanani,muhimu tusisahauliane ila mengine tuvumiliane.
 
Mimi ninachoona zaidi ni kutoka familia tegemezi unakuta mtu akioa yale matumizi yanapungua maana anaanza kujenga familia yake na unakuta pesa wanaipangia mipango na mwenzake. sasa hapo ndipo kasheshe linapoanza.
Hiko pia kinachangia pale inapotokea mtu waliyekuwa wanamtegemea kiuchumi ameoa/ kuolewa vita itaanza ndg wataanza kumsakama aliyeoa au kuolewa wakiona ndio anafelisha mipangoyao
 
Lazima tujue Kwanza maana ya ndoa kabla hatujaanza kulaumu watu.

Hii tabia ya kuendekeza binadamu imetufalakanisha na kutupulua sana sisi waafrika. Ndoa ni taasisi yenye mamlaka kamili,na ili taasisi yeyote iwe na ufanisi lazima kuwe na taratibu na sheria ambazo ndio zitaipambanua hiyo taasisi.

Tunapenda maisha tegemezi ndio maana lawama kwa wanandoa zinakua nyingi,maisha ya miaka 1960 na maisha ya miaka ya 2000 hayafanani,muhimu tusisahauliane ila mengine tuvumiliane.
Hahaha nimekuelewa lakini sio matatizo yote yanatokana na uchumi
 
Mara nyingi mahusiano ya wanandugu huwa yanaharibika / kupungua pale wanapo oa au kuolewa , kuna wengine akili zinabadilika anaanza kutumia akili ya mke au mume zaidi na kudharau mambo ya familia aliyotoka.

Wanaume wengine wanaendleshwa na wake zao anafarakanishwa na ndugu zake
Bora iwe hivyo Mimi nitaendelea kuishi single mpaka lini
 
Sababu ni nyingi sana mleta mada sio kwamba watu wanapenda kukata mahusiano na ndugu zake la hasha kuna mambo kedekede sababishi ya kukata mahusiano ila hapa duniani kuna watu wanapitia changamoto sana acha tu mkuu, natamani siku moja nilete stori yangu jukwaani hapa ya mapito niliyopitia tuombe uzima.
Pole sana ndg kwa maswahibu zote hizo ni changamoto za kidunia alizokuwanazo Asha sio Alizokuwanazo Anna, matatizo yanatofautiana kila mtu na simulizi yake
 
Anakuja jamaa mmoja anakuomba ushauri;

Brother, yule binti ninampenda nadhamiria kumuoa naomba ushauri wako.

Anakuja jamaa mwingine anakuomba ushauri;

Brother, yule msichana ninampenda natamani nifanye nae mahusiano, naomba ushauri wako.

Chukulia mlengwa (msichana ) anayezungumziwa ni huyo huyo mmoja mnakaa mtaa mmoja, Hawa wanaoomba ushauri hawamjui vizuri kama unavyomjua wewe unayeombwa ushauri na unajua fika yule dada ni kicheche (hajatulia).

Utatoa ushauri gani kwa hao watu wawili?

Tafakari kisha chukua hatua
 
Mara nyingi mahusiano ya wanandugu huwa yanaharibika / kupungua pale wanapo oa au kuolewa , kuna wengine akili zinabadilika anaanza kutumia akili ya mke au mume zaidi na kudharau mambo ya familia aliyotoka.

Wanaume wengine wanaendleshwa na wake zao anafarakanishwa na ndugu zake
Waache watu na ndoa yao,waache waitunze familia,Bilbllia inasema mtu atamwacha babae na mama yake na kuungana na mke wake nao watakua mwili mmoja na si miwili tena.
Mungu alitufungulia haya mapema,ukiona hashiriki muacheee.Ukimwomba asipokupa mwachee hivyo ni vyake na watoto wakee na mkee wakeee-Usijaribu kamwe kuwaingilia usiharibu ndoa za watuuu.
Na ndo maana mwanamume anaweza toka hapa akaenda Gergia/Atlanta/Gaza/Palestina kule ataoa na atakua na familia wala hatahitaji msaada wako, na wala hutamuona-Akiamua kujifungia kwenye ukuta wake muache.
Biblia inasema mpende jirani yako kama nafsi yako- Jirani yako ni nani? ni mtu yeyote awaye pamoja na wewe ndugu-akiamua kuivunja muache.
Na pia imeandikwa Adui wa mtu ni wa nyumbani kwake-ndugu-akikuona/ukimwona ni adui kila mtu apambane.
We tunza familia yako kwa upendo na wivu mkubwa saanaaa.Kiufupi fanya majukumu yako.
Wasalaam
Laii
 
Wataacha familia baba na mama ambao nao waliziacha zao hapo awalina kwenda kutengeneza zao. Ni bibilia hiyo sio mimi
Umeongea ukweli familia nyingi zimeharibiwa with this so calling ndugu,wajane wameporwa mali,watoto wameporwa haki zao za kumiliki mali za familia with this calling bamkubwa,bamdogo na mashangazi kwa kisingizio cha ndugu,aisee mi hapana ndugu akijifanya anaijua familia yangu kuliko mimi namkimbizia mbali aiseee,sitaki mazoea hata kidogoo kaka.
Nimekua nikaona dada wa baba mmoja anakula faida ya nyumba ya ujanani ya kaka,ambayo watoto wala mke wa kaka hawajaila na ana mji wake na mume wake na wote wanavipatoo-yaani kama yazungumzwayo ni kweli namuombea laana yeye na vizazi vyake vyoteee(the world is not fair) na madogo wapowapo tuu hawajui cha kufanyaa(labda umri unachangia 1st born 16yrs)
Ushauri fanya majukumu yako mkuu
 
Mada moto hii

1. Biblia imesema kwamba mwanamke na mwanaume watawaacha wazazi wao na kuambatana pamoja.

2. Iwapo Wana-ndoa walitakiwa wawe na bond na wazazi wao, basi Biblia ingesema kwamba Wana-ndoa waunganishe familia watokazo na washirikiane. Lakini imetumia neno "kuachana na wazazi".

3. Ndiyo maana hata Jamii inawaasa Wana-ndoa wasikopeshe ukweni ama kujenga huko.

4. Nimewahi kushuhudia ndugu wakianza kumchukia Binti baada ya kupata mchumba na wanaleta figisu ikiwemo kugoma kupokea mahari na ama kupiga danadana suala la posa.

5. Kuna mmoja alitoa taarifa za kupata mchumba, mchumba akaahidi kwenda kwao mwezi wa 7, ilipofika wiki ya pili ya July husika, ndugu mmoja akaanza kulazimisha na kuuliza Kwa Binti vipi, July tayari mbona hatokei? Mara huyo Hana Hela huyo! Dah!

6.Mara mwingine akianza kununiwa na dada yake. Na hili nimeliona hata kwenye familia yetu.

Itoshe kusema undugu umekuwa mgumu sana Karne hii ya 21!
 
Back
Top Bottom