Mada moto hii
1. Biblia imesema kwamba mwanamke na mwanaume watawaacha wazazi wao na kuambatana pamoja.
2. Iwapo Wana-ndoa walitakiwa wawe na bond na wazazi wao, basi Biblia ingesema kwamba Wana-ndoa waunganishe familia watokazo na washirikiane. Lakini imetumia neno "kuachana na wazazi".
3. Ndiyo maana hata Jamii inawaasa Wana-ndoa wasikopeshe ukweni ama kujenga huko.
4. Nimewahi kushuhudia ndugu wakianza kumchukia Binti baada ya kupata mchumba na wanaleta figisu ikiwemo kugoma kupokea mahari na ama kupiga danadana suala la posa.
5. Kuna mmoja alitoa taarifa za kupata mchumba, mchumba akaahidi kwenda kwao mwezi wa 7, ilipofika wiki ya pili ya July husika, ndugu mmoja akaanza kulazimisha na kuuliza Kwa Binti vipi, July tayari mbona hatokei? Mara huyo Hana Hela huyo! Dah!
6.Mara mwingine akianza kununiwa na dada yake. Na hili nimeliona hata kwenye familia yetu.
Itoshe kusema undugu umekuwa mgumu sana Karne hii ya 21!