Mahusiano ya Tanzania na mahakama ya haki za binadamu Afrika yaendelea kuimarika

Hamduni

Senior Member
Joined
Apr 25, 2020
Posts
172
Reaction score
118
The Diplomat

Kwa siku kadhaa kumekua na Upotoshaji katika Mitandao ya kijamii kuhusu Tanzania kujitoa katika Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu, Suala ambalo halina ukweli wowote.

Jana Mei 27, 2021 Katika muendelezo wa kuonyesha ni kwa jinsi gani masuala ya Haki za Binadamu ni kipaumbele cha Serikali ya Awamu ya Sita, Rais Samia Suluhu Hassan alikutana na kufanya mazungumzo na Rais wa Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu (African Court on Human and Peoples’ Rights) Mhe. Jaji Sylvain Orè, Ikulu Jijini Dar es Salaam.

Huu ukiwa ni muendelezo wa kuimarisha mahusiano kati ya Taifa letu na mahakama hio.

Katika mazungumzo yao Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan amemuahidi Rais wa Mahakama hiyo kuwa Serikali ya Awamu ya Sita itaendelea kutoa ushirikiano wa kutosha kwa Mahakama hiyo kwa kutatua changamoto mbali mbali kwani inatambua umuhimu wa majukumu yake katika suala zima la Haki za Binadamu.

Pia Mhe Rais ametanabaisha kuwa kuhusu msimamo wa Tanzania kuondoa kipengele kinachoruhusu Taasisi zisizo za kiserikali na watu binafsi kupeleka mashauri yao moja kwa moja kwenye Mahakama hiyo kwa kusema Serikali yake italitazama suala hilo upya lakini kwa sasa msimamao wa Tanzania ubaki kama ulivyo.

Rais wa Mahakama hiyo Mhe. Jaji Sylvain Ore', amemshukuru Mhe Rais Samia Suluhu Hassan kwa ushirikiano ambao ameendelea kuupata katika kipindi chote cha uongozi wake na kusema Tanzania ni mahali sahihi kuwepo kwa m
Mahakama ya Afrika kwani kuna Amani ya uhakika na Utulivu.

Watanzania wameendelea kushuhudia namna wale waliozusha na kusambaza uongo kuwa Tanzania imejitoa katika Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu wasivyo na nia njema kwa Taifa letu na wanavyo haha. Rai yangu ni moja, Tuendelee kuwapuuza.

The Diplomat
 
MAHUSIANO YA TANZANIA NA MAHAKAMA YA HAKI ZA BINADAMU AFRIKA YAENDELEA KUIMARIKA

Cheki vizuri facts zako. Kuna sehemu hujafanya 'homework' yako vizuri.
 
Kwa nini usiseme ukweli tu uliougusagusa humu, nao ni kwamba, baada ya Serikali iliyopita kushindwa kesi kadhaa za kukiuka haki za binadamu, iliamua kudhoofisha nguvu za kuishitaki kwa kutoruhusu asasi za kiraia kuishitaki. Hayo ndiyo mahusiano mabaya na mahakama hiyo. Mahakama za namna hii popote ulimwenguni sasa zinaruhusu asasi za kiraia na watu binafsi kushitaki serikali zao. Kuondoa hilo ni kurudi nyuma sana kwa haki za binadamu. Wewe ungejikita kusifia utayari wa rais wa sasa wa kufikiria upya mahusiano hayo
 
Back
Top Bottom