Maina Kamanda: Tanzania's Magufuli and South Sudan's Kiir funding Raila to distabilize Kenya

Maina Kamanda: Tanzania's Magufuli and South Sudan's Kiir funding Raila to distabilize Kenya

Taarifa ya BBC ya saa ngapi iliyosema hivyo? TV au radio?
 
Kabisa kama ni kweli hii habari yahitaji kujibiw Coz ni ya kisiasa
Actually inaweza hatarisha muungano
 
Katika siku za hivi karibuni kumekuwepo na taarifa kwenye vyombo vya habari vya Kenya na vya kimataifa hususani BBC vikielezea madai ya serikali ya Kenya kwamba serikali ya Tanzania inasaidia vyama vya upinzani nchini humo kufanya maandamano na mikutano ya kisiasa na kuvuruga amani ya nchi hiyo.Madai ya serikali ya Kenya yameenda mbali kwa kumtuhumu waziwazi Rais Magufuli kwamba wakati yeye amepiga marufuku mikutano na maandamano nchini Tanzania,anamfadhili rafiki yake Raila Odinga kuandaa maandamano haramu nchini kenya.Tunaiomba serikali yetu itoe kauli kuhusu madai haya ili kudumisha na kulinusuru shirikisho la Afrika Mashariki.
Serikali makini popote pale duniani huwa haifanyi mabishano kwa namna yoyote ile na vyombo vya habari wala kufanya maamuzi yake kwa msingi ya hisia ama kupitia mihemko ya baadhi ya watu.....!!!!!!!!
 
Hivi hizo allegations ambazo zilipita hapa,ziliitaja Tanzania kama mfadhiri wa hayo mavitu yao? Tumewaomba wenzetu hawa wamalize tofauti zao za ukabila na wala wasitafute mchawi nje yao wenyewe. Labda kama kuna tamko RASMI la serikali ya Kenya ambalo binafsi limenipita kushoto
 
Ni kweli hata mimi nilisikia kutoka bbc binafsi nilishtuka sana.
 
Hasira za kukosa dili la bomba la mafuta, hasira za kukosa reli toka Rwanda, hasira kwa kuwa Odinga alienda chato kumtembelea Magu.
 
CCM huwa hawakanushi mambo hayo yangekuwa ya wapinzani hapa kutaka mikutano ungewaona mara moja wangejitokeza,
 
Watakuwa ni wale wahuni wa wenje wameona mwanza hamna deal wamehamia huko.
 
South Sudan and Tanzania can hardly sustain their own budgets, they can hardly contain their political unrests how on earth will they fund another person to cause unrest in another nation? this is just a cry of desperacy and blame game by those responsible.
 
Tatizo la Wakenya ni Ukabila malizeni matatizo yenu kwanza ndio mtasonga mbele,hii dhambi ya ukabila itawatafuna mpaka kizazi cha tatu.
 
Habari wana jf,

Nimekuwa nikifuatilia siasa za nchi jirani ya Kenya na kuutathimini muungano wa cord unavyoichachafya serikali ya rais Jommo Kenyata na kujiuliza kama kunamaelewano ya
Dhati kati ya serikali ya Kenya na ya Tanzania.

Niukweli ulio wazi pasi na shaka ndugu Raila Odinga (mpinzani) ni swahiba kweli kweli na raisi wa Jamuhuri ya muungano wa Tanzania Mh. J.P. Magufuli.

Najiuliza rais Kenyeta analitazamaje hili? Au huenda halina shida yoyote? Lakini pia nd. Raila Odinga. Alikuja kumsalimu na kumpongeza Mh. J.P.Magufuli tena akiwa mapumziko nyumbani kwao chato.

Labda alikuja kuchukua pia mbinu za kupata ushindi?? Na sasa anawasha moto mkali wa kisiasa kiasi kwamba rais Kenyata anaomba wakae mezani wayazungumze.

Sasa kwa hali ilivyo nadhani rais Kenyata huenda hamwaangalii rais j.P.Magufuli vizuri.

Wana JF, kidiplomasia na kisiasa linajadilika hili?
 
Back
Top Bottom