Katika siku za hivi karibuni kumekuwepo na taarifa kwenye vyombo vya habari vya Kenya na vya kimataifa hususani BBC vikielezea madai ya serikali ya Kenya kwamba serikali ya Tanzania inasaidia vyama vya upinzani nchini humo kufanya maandamano na mikutano ya kisiasa na kuvuruga amani ya nchi hiyo.Madai ya serikali ya Kenya yameenda mbali kwa kumtuhumu waziwazi Rais Magufuli kwamba wakati yeye amepiga marufuku mikutano na maandamano nchini Tanzania,anamfadhili rafiki yake Raila Odinga kuandaa maandamano haramu nchini kenya.Tunaiomba serikali yetu itoe kauli kuhusu madai haya ili kudumisha na kulinusuru shirikisho la Afrika Mashariki.