Maisha bila Mungu yamekuwa ya amani na furaha

Maisha bila Mungu yamekuwa ya amani na furaha

Habari wana-JF!

Najua huu uzi wafia dini watausoma kwa kusonya ila ndiyo hivyo inabidi tuvumiliane tu.

Mimi nimekulia katika Ukristo, sijaukana ila nimeliacha kanisa kimyakimya. Baada ya kuanza kukua na kujitambua nilikuwa na maswali mengi sana juu ya nadharia zote kumuhusu Mungu na maswali yangu yote yalikuwa hayana majibu yaliyonyooka.

Baada ya udadisi wa muda mrefu nikafikia hitimisho kuwa "hakuna Mungu" kwasababu angekuwepo na majibu ya maswali yangu yangekuwepo.

Uwanda wa imani ni mpana ila ukiwa ndani ya imani chini ya tawi la dini ni mwiko kudadisi uwepo wa Mungu, huko ni "ndiyo" tu hakuna kuhoji.

Maisha baada ya kulikimbia kanisa yamekuwa na amani kwasababu:

1. Maisha yangu yapo mikononi mwangu.

2. Sina hofu juu ya kifo wala kuzimu kwasababu siamini hadithi za maisha baada ya kifo.

3. Naishi kwa kufuata katiba na sheria za nchi na si vinginevyo.

4. Siishi maisha kwaajili ya kumpendeza yoyote au kitu chochote.

5. Napata muda mwingi wa kufanya mambo ya msingi, siku ya Jumapili kwangu ni kama siku nyingine ya wiki.

6. Badala ya kuhangaika kutafuta maarifa ya maisha ya mbinguni (kusoma biblia), natafuta zaidi maarifa yatakonisaidia kwenye maisha ya hapa duniani maana ndiyo sehemu pekee ninayothibitisha ni ya kweli.

7. Najiheshimu. Kwangu kulia na kuomba msaada kwa M(i)ungu ni kutojiheshimu kama binadamu.

8. Nikipata matatizo sikai chini kuomba na kusubiri miujiza badala yake natumia maarifa niliyonayo kutafuta ufumbuzi.

9. Siishi kwa matumaini ya kuzawadiwa uzima wa milele.

10. Nimepishana na utapeli. Kama wanavyosema "wajinga ndiyo waliwao".

Siamini kama kweli Mungu yupo, lakini kama yupo hawezi kuwa mjinga kama anavyoelezewa kwenye vitabu vya dini.

Mungu hayupo, lakini kama angekuwepo hastahili utukufu wala unyenyekevu kutoka kwangu.

The sweet, sweet relief of knowing I'm going to hell no matter what I do! 🙃
Endelea kukaza fuvu
 
(
Mithali 26:4 )
Usimjibu mpumbavu sawasawa na upumbavu wake;
Usije ukafanana naye.
Ambaye unasema kitu kipo halafu hapohapo huna uthibitisho wala ushahidi wa hicho kitu unachodai kipo wewe ndio mpumbavu.

Unafosi mawazo yako uchwara yasiyo na uthibitisho wowote ule yawe ukweli bila evidence yeyote.
 
View attachment 3062467
Tafuta hilo Group ujumuike mkuu.
The “Blood of Jesus” is so precious and many have received salvation of their souls through Jesus Christ. We know devil is a liar and is busy deceiving people but it is very unfortunately. The devil is the father of lies anyway. He will continue lies to people about Jesus but the truth will remain that Jesus is the son of God and through Him we have redemptions of our sins and finally we shall enter into heaven.
 
Wewe ndo Mungu anakupenda zaidi na kukuruzuku mema mengi zaidi ndo maana unaona kila kitu kimenyooka, lengo lake uguswe na wema wake, umgeukie, umwamini, akuokoe milele. Hakika siku hiyo inasubiriwa kwa shauku kubwa na kutakua na furaha kuu mbinguni siku ukitubu na kurejea kundini, zaidi ya furaha ya mwanampotevu aliporejea nyumban kwa baba yake.
 
Ambaye unasema kitu kipo halafu hapohapo huna uthibitisho wala ushahidi wa hicho kitu unachodai kipo wewe ndio mpumbavu.

Unafosi mawazo yako uchwara yasiyo na uthibitisho wowote ule yawe ukweli bila evidence yeyote.
What evidence you are looking for. Creation is more than evidence. God is there and He will be there. No body can change Him. We are nothing before Him.
 
Back
Top Bottom