Maisha bila Mungu yamekuwa ya amani na furaha

Maisha bila Mungu yamekuwa ya amani na furaha

Maoni yngu: Alietuumba na kutuwekea system ya DNA pamoja na Natural Intelligence yupo tena anajulikana kama MKUU wa ENZI rejea bandiko la Pro. Singano Jr la "Niliemdhania kahaba kumbe bikra" Tulicho Miss sisi wanadamu ni Njia sahihi ya kumwendea! Njia karibu zote tunadanganywa, lakn trust me Kuna watu tayar wanaijua the actual path na hawako tayari kuisema hio kweli, Ukweli tumefichwa badala yake wamebaki kutuletea hadthi tuu za watu Mambo waliofanya!! Kama Jesus alipaa na alitembea juu ya maji, akabadilisha maji kuwa Divai Aminini kuwa Kuna watu wanaweza kufanya hivyo vyote mpka Leo na wapo! Lakn wanaijua Njia sahihi ya kuwa purified mpka kufika kwenye Realm ya kufany hivyo. Lakin vingi kati ya hivyo vipo Vatican vimefichwa kweny maktaba zao
Jaman Hivyo wanavyovisema vipo! Mungu yupo na kila kitu kipo Kasoro tuu hizo njia wanazozitumia na kutuaminisha sio za kweli
 
Mimi sishawishi mtu aache kuamini Mungu yupo, ila akianza kudai kwamba imani yake ya huyo Mungu ina ukweli lazima athibitishe hilo.

Na akileta habari zake kumhusu Mungu huyo lazima tuzichambue na kuzikosoa.

Otherwise ubaki na hiyo imani yako moyoni mwako usiilete hapa kwenye open forum.
Kwa mfano wewe binafsi akili yako ina doubts 😛 😛 😛 sio rahisi kumshawishi mtu .

Ugomvi na matatizo ni pale utakapomlazimisha mwngine juu ya imani yako...Kama hayupo basi unakaa kimya unaishi hakuna mtu atakufanya chochote sheria za nchi zipo.
 
Kwa mfano wewe binafsi akili yako ina doubts 😛 😛 😛 sio rahisi kumshawishi mtu .

Ugomvi na matatizo ni pale utakapomlazimisha mwngine juu ya imani yako...Kama hayupo basi unakaa kimya unaishi hakuna mtu atakufanya chochote sheria za nchi zipo.
Kuna sehemu nimekushikia fimbo kukulazimisha au kumlazimisha mtu Mungu hayupo?

Na wewe kama unajua huyo Mungu yupo kaa kimya, umwache huyo Mungu ajiongelee mwenyewe kama yupo.

Kwa nini unahangaika kumuongelea huyo Mungu?

Kwa nini unahangaika kuelezea wengine juu ya uwepo wa huyo Mungu?

Kwa nini Hukai kimya, Huyo Mungu ajiongelee mwenyewe kama yupo?
 
Habari wana-JF!

Najua huu uzi wafia dini watausoma kwa kusonya ila ndiyo hivyo inabidi tuvumiliane tu.

Mimi nimekulia katika Ukristo, sijaukana ila nimeliacha kanisa kimyakimya. Baada ya kuanza kukua na kujitambua nilikuwa na maswali mengi sana juu ya nadharia zote kumuhusu Mungu na maswali yangu yote yalikuwa hayana majibu yaliyonyooka.

Baada ya udadisi wa muda mrefu nikafikia hitimisho kuwa "hakuna Mungu" kwasababu angekuwepo na majibu ya maswali yangu yangekuwepo.

Uwanda wa imani ni mpana ila ukiwa ndani ya imani chini ya tawi la dini ni mwiko kudadisi uwepo wa Mungu, huko ni "ndiyo" tu hakuna kuhoji.

Maisha baada ya kulikimbia kanisa yamekuwa na amani kwasababu:

1. Maisha yangu yapo mikononi mwangu.

2. Sina hofu juu ya kifo wala kuzimu kwasababu siamini hadithi za maisha baada ya kifo.

3. Naishi kwa kufuata katiba na sheria za nchi na si vinginevyo.

4. Siishi maisha kwaajili ya kumpendeza yoyote au kitu chochote.

5. Napata muda mwingi wa kufanya mambo ya msingi, siku ya Jumapili kwangu ni kama siku nyingine ya wiki.

6. Badala ya kuhangaika kutafuta maarifa ya maisha ya mbinguni (kusoma biblia), natafuta zaidi maarifa yatakonisaidia kwenye maisha ya hapa duniani maana ndiyo sehemu pekee ninayothibitisha ni ya kweli.

7. Najiheshimu. Kwangu kulia na kuomba msaada kwa M(i)ungu ni kutojiheshimu kama binadamu.

8. Nikipata matatizo sikai chini kuomba na kusubiri miujiza badala yake natumia maarifa niliyonayo kutafuta ufumbuzi.

9. Siishi kwa matumaini ya kuzawadiwa uzima wa milele.

10. Nimepishana na utapeli. Kama wanavyosema "wajinga ndiyo waliwao".

Siamini kama kweli Mungu yupo, lakini kama yupo hawezi kuwa mjinga kama anavyoelezewa kwenye vitabu vya dini.

Mungu hayupo, lakini kama angekuwepo hastahili utukufu wala unyenyekevu kutoka kwangu.

The sweet, sweet relief of knowing I'm going to hell no matter what I do! 🙃
Binafsi fikra kuwa MUNGU yupo zinanipa amani, naaply hoja yako namba 8 na ninapofika kwenye sehemu ambayo nimefeli na sina la kufanya, fikra kuwa MUNGU yupo inanipa amani na sijui huwa kuna siri gani kati ya matumaini na uhalisia, always ninapobaki na tumaini tu baada ya kufanya waibu wangu na kila kitu kushindikana, tumaini hugeuka uhalisia kwa kuvuka linalonisibu kupitia fikra kuwa sasa namwachia MUNGU afanye sehemu yake maana nimeshafanya yangu.

Kwangu imani ya uwepo wa MUNGU ni muhimu mno mno mno na siku ikithibitika kuwa hayupo, somehow saikolojia yangu itakuwa challanged na nitahitaji akili za ziada kuikubali hiyo hali.

NB: Mimi Sio mtu mfia dini.
 
Mtu kama wewe unatakiwa upelekwe Mtwara ama Tanga ama Kigoma Sasa ukishapata KUJUA kuwa kuna ulimwengu halisi kabisakabisa wa roho, hapohapo unapata KUJUA kuwa MUNGU yupo...
Average mind ajaribu kufanya mambo makubwa bila Mungu au ndumba akitoboa aje na hizi ngonjera. Kamwe hauwezi thamini nuru kama hujawai kaa gizani
 
Mungu asipojitokeza aise naona huko mbele ni kubaya aise.
1722621780393.jpg
1722856824671.jpg
 
👇Swali langu kwako ni hilo. Usitunge maswali
Akili ni neno la kufikirika tu.

Nomino yenye kuonyesha utendaji kazi wa ubongo.

Huwezi kuthibitisha uwepo wa akili, Akili si kitu cha kuonekana, kushikika, kusikika au kuhisika.

Hata ukipasua kichwa huwezi kuthibitisha uwepo wa akili kwenye ubongo.

Hivyo akili ni neno la kufikirika tu, si kitu cha kuonekana kuthibitishika kipo.

Una elewa hilo?
 
Kuna sehemu nimekushikia fimbo kukulazimisha au kumlazimisha mtu Mungu hayupo?

Na wewe kama unajua huyo Mungu yupo kaa kimya, umwache huyo Mungu ajiongelee mwenyewe kama yupo.

Kwa nini unahangaika kumuongelea huyo Mungu?

Kwa nini unahangaika kuelezea wengine juu ya uwepo wa huyo Mungu?

Kwa nini Hukai kimya, Huyo Mungu ajiongelee mwenyewe kama yupo?
Ku'reply comments zote naona unapata tabu , moyo unaenda mbio ...kuwa na msimamo kama wenzio 😛 😛
 
Akili ni neno la kufikirika tu.

Nomino yenye kuonyesha utendaji kazi wa ubongo.

Huwezi kuthibitisha uwepo wa akili, Akili si kitu cha kuonekana, kushikika, kusikika au kuhisika.

Hata ukipasua kichwa huwezi kuthibitisha uwepo wa akili kwenye ubongo.

Hivyo akili ni neno la kufikirika tu, si kitu cha kuonekana kuthibitishika kipo.

Una elewa hilo?
Kuna tofauti kati ya akili ni nini na kuthibitisha kama una akili.
Mimi nimetaka unithibitishie kuwa una akili, sio unielezee akili ni nini.
 
Nimeielewa sana hii post yako mkuu Forgotten.

Unajisikia huru, ni kama vile umefungua pingu flani zilizokuwa zikikurudisha nyuma.

Kwangu mimi faida kubwa niliyopata kwenye kugundua ukweli huu, ni kwamba siishi kwa hofu tena, hofu ya adhabu ya milele, hofu ya laana na mikosi.
Kipindi nimejitambua kwenye hicho kifungo nilifuatwa na viongozi wa dini mno , kidogo nirushe ngumi , nilikua tayari kukichafua kuliko kurudi kwenye hilo gereza la fikra.
 
Back
Top Bottom