Maisha bila Mungu yamekuwa ya amani na furaha

Habari wana-JF!

Najua huu uzi wafia dini watausoma kwa kusonya ila ndiyo hivyo inabidi tuvumiliane tu.

Mimi nimekulia katika Ukristo, sijaukana ila nimeliacha kanisa kimyakimya. Baada ya kuanza kukua na kujitambua nilikuwa na maswali mengi sana juu ya nadharia zote kumuhusu Mungu na maswali yangu yote yalikuwa hayana majibu yaliyonyooka.

Baada ya udadisi wa muda mrefu nikafikia hitimisho kuwa "hakuna Mungu" kwasababu angekuwepo na majibu ya maswali yangu yangekuwepo.

Uwanda wa imani ni mpana ila ukiwa ndani ya imani chini ya tawi la dini ni mwiko kudadisi uwepo wa Mungu, huko ni "ndiyo" tu hakuna kuhoji.

Maisha baada ya kulikimbia kanisa yamekuwa na amani kwasababu:

1. Maisha yangu yapo mikononi mwangu.

2. Sina hofu juu ya kifo wala kuzimu kwasababu siamini hadithi za maisha baada ya kifo.

3. Naishi kwa kufuata katiba na sheria za nchi na si vinginevyo.

4. Siishi maisha kwaajili ya kumpendeza yoyote au kitu chochote.

5. Napata muda mwingi wa kufanya mambo ya msingi, siku ya Jumapili kwangu ni kama siku nyingine ya wiki.

6. Badala ya kuhangaika kutafuta maarifa ya maisha ya mbinguni (kusoma biblia), natafuta zaidi maarifa yatakonisaidia kwenye maisha ya hapa duniani maana ndiyo sehemu pekee ninayothibitisha ni ya kweli.

7. Najiheshimu. Kwangu kulia na kuomba msaada kwa M(i)ungu ni kutojiheshimu kama binadamu.

8. Nikipata matatizo sikai chini kuomba na kusubiri miujiza badala yake natumia maarifa niliyonayo kutafuta ufumbuzi.

9. Siishi kwa matumaini ya kuzawadiwa uzima wa milele.

10. Nimepishana na utapeli. Kama wanavyosema "wajinga ndiyo waliwao".

Siamini kama kweli Mungu yupo, lakini kama yupo hawezi kuwa mjinga kama anavyoelezewa kwenye vitabu vya dini.

Mungu hayupo, lakini kama angekuwepo hastahili utukufu wala unyenyekevu kutoka kwangu.

The sweet, sweet relief of knowing I'm going to hell no matter what I do! 🙃
aliekutuma uwe freemason nani? ww ni seat ya mbele kabisa kuzimu
 
Ulichotakiwa kugundua kwenye huo mfano ni kwamba, ukishindwa kujua uwepo wa kitu fulani haimaanishi hicho kitu hakipo. Ni wewe tu umeshindwa kutambua uwepo wake.
Sasa wewe unayetambua uwepo wa hicho kitu, Kithibitishe basi?

Mbona unaruka ruka tu?

Thibitisha Akili ipo.

Thibitisha Mungu yupo

Wewe si unadai vipo?

Vithibitishe basi.
 
Mungu angekuwepo kweli haya mazungumzo hapa hata yasingekuwepo hizo ni nadharia tu na kadri mda unavyokwenda itapotea.
 
Habari wana-JF!

Najua huu uzi wafia dini watausoma kwa kusonya ila ndiyo hivyo inabidi tuvumiliane tu.

Mimi nimekulia katika Ukristo, sijaukana ila nimeliacha kanisa kimyakimya. Baada ya kuanza kukua na kujitambua nilikuwa na maswali mengi sana juu ya nadharia zote kumuhusu Mungu na maswali yangu yote yalikuwa hayana majibu yaliyonyooka.

Baada ya udadisi wa muda mrefu nikafikia hitimisho kuwa "hakuna Mungu" kwasababu angekuwepo na majibu ya maswali yangu yangekuwepo.

Uwanda wa imani ni mpana ila ukiwa ndani ya imani chini ya tawi la dini ni mwiko kudadisi uwepo wa Mungu, huko ni "ndiyo" tu hakuna kuhoji.

Maisha baada ya kulikimbia kanisa yamekuwa na amani kwasababu:

1. Maisha yangu yapo mikononi mwangu.

2. Sina hofu juu ya kifo wala kuzimu kwasababu siamini hadithi za maisha baada ya kifo.

3. Naishi kwa kufuata katiba na sheria za nchi na si vinginevyo.

4. Siishi maisha kwaajili ya kumpendeza yoyote au kitu chochote.

5. Napata muda mwingi wa kufanya mambo ya msingi, siku ya Jumapili kwangu ni kama siku nyingine ya wiki.

6. Badala ya kuhangaika kutafuta maarifa ya maisha ya mbinguni (kusoma biblia), natafuta zaidi maarifa yatakonisaidia kwenye maisha ya hapa duniani maana ndiyo sehemu pekee ninayothibitisha ni ya kweli.

7. Najiheshimu. Kwangu kulia na kuomba msaada kwa M(i)ungu ni kutojiheshimu kama binadamu.

8. Nikipata matatizo sikai chini kuomba na kusubiri miujiza badala yake natumia maarifa niliyonayo kutafuta ufumbuzi.

9. Siishi kwa matumaini ya kuzawadiwa uzima wa milele.

10. Nimepishana na utapeli. Kama wanavyosema "wajinga ndiyo waliwao".

Siamini kama kweli Mungu yupo, lakini kama yupo hawezi kuwa mjinga kama anavyoelezewa kwenye vitabu vya dini.

Mungu hayupo, lakini kama angekuwepo hastahili utukufu wala unyenyekevu kutoka kwangu.

The sweet, sweet relief of knowing I'm going to hell no matter what I do! 🙃
Mungu yupo mkuu na kuna umuhimu wa kumuabudu mkuu, kuna tatizo nilikuwa naonaa ni gumu kushughulika Bali leo nikatoa sala mida ya sita ila saa kumi jion nimeona Matokeo ya ile sala mkuu ingawa sitotaja ni jambo gani lilikuwa gumu kwangu ila mungu yupo na mambo yote niliyofanya kwa kumshirikisha mungu nimeona majibu yakee mkuu ni hivo tu

Povu ruksa
 
Sasa wewe unayetambua uwepo wa hicho kitu, Kithibitishe basi?

Mbona unaruka ruka tu?

Thibitisha Akili ipo.

Thibitisha Mungu yupo

Wewe si unadai vipo?

Vithibitishe basi.
Sasa kama havipo ina maana na akili haipo, kama akili haipo unakubali kua wewe huna akili (maana umesema haipo) , je unakubali hilo kwanza kisha nikupe prof ya uwepo wa akili na Mungu?
 
Back
Top Bottom