Maisha bila Mungu yamekuwa ya amani na furaha

Maisha bila Mungu yamekuwa ya amani na furaha

(Isaya 32:6 )
Maana mpumbavu atanena yaliyo upumbavu, na moyo wake utafanya maovu, ili kutenda hila na kusema yasiyo kweli juu ya BWANA, ili kuziacha nafsi za watu wenye njaa hazina kitu, na kukikomesha kinywaji chake mwenye kiu.
Huyo Mungu Alishindwaje kuumba binadamu wasio wapumbavu?

Uwepo wa binadamu wapumbavu, wasio mtambua muumba wao kama Mungu wao,

Ni uthibitisho tosha kwamba huyo Mungu muumba, Kazi yake ya uumbaji ina dosari na kasoro kwa kuumba binadamu ambao ni wapumbavu.

Na automatically Mungu huyo ni Mpumbavu vilevile kwa kuumba binadamu wenye upumbavu uliotokana na kazi yake ya uumbaji
 
What evidence you are looking for. Creation is more than evidence. God is there and He will be there. No body can change Him. We are nothing before Him.
Unahangaika sana kumuongelea huyo Mungu kwa vile hajawahi kuwepo na hayupo kujiongelea mwenyewe.

Mnafosi imani zenu uchwara na hekaya zenu za vitabuni huko kuwa ukweli ilhali kiuhalisia ni UONGO.

Huyo Mungu hajawahi kuwepo, hayupo na hata uwezekano wa kuwepo kwake Haupo.
 
Mungu huyo mwema, Alishindwaje kuumba dunia isiyo na uovu wala mabaya?

Mungu huyo mwema, Alishindwaje kuumba binadamu wema tu, wasio na uwezo wa kutenda mabaya?
Najua akili iko na fully doubts , mimi najua saikolojia usingekuwa unapata tabu kiasi hicho 😛 😛 Kama una imani hayupo ungekuwa kimya, ukafanya yako maana una uhakika.

We jamaa hauna msimamo pia sio rahisi kusawishi watu zaidi ya hivyo ,unachofuata pia ni dini baada ya kuona maisha ya wazungu.
 
Wewe ndo Mungu anakupenda zaidi na kukuruzuku mema mengi zaidi ndo maana unaona kila kitu kimenyooka, lengo lake uguswe na wema wake, umgeukie, umwamini, akuokoe milele. Hakika siku hiyo inasubiriwa kwa shauku kubwa na kutakua na furaha kuu mbinguni siku ukitubu na kurejea kundini, zaidi ya furaha ya mwanampotevu aliporejea nyumban kwa baba yake.
Huyo Mungu anashindwa kuwaokoa maelfu ya watoto wachanga wasio na hatia yeyote ile,

Wanaokufa kwa njaa, vita, magonjwa na majanga ya asili maeneo mbalimbali duniani, Halafu ndio unasema huyo Mungu ni mwema?

Wema gani???

Huyo Mungu kama yupo ni Muovu na mkatili sana na hana hata chembe ya wema.
 
(Isaya 32:6 )
Maana mpumbavu atanena yaliyo upumbavu, na moyo wake utafanya maovu, ili kutenda hila na kusema yasiyo kweli juu ya BWANA, ili kuziacha nafsi za watu wenye njaa hazina kitu, na kukikomesha kinywaji chake mwenye kiu.
Kujibu swali umeshindwa. Unaleta nukuu za mababu wa kizungu zilizotafsiriwa kwa lugha yako mtumwa wao ili uelewe mabwana zako wanakutaka uamini nini, ufanye nini.
 
Najua akili iko na fully doubts , mimi najua saikolojia usingekuwa unapata tabu kiasi hicho 😛 😛 Kama una imani hayupo ungekuwa kimya, ukafanya yako maana una uhakika.

Na wewe kama ulikuwa unajua huyo Mungu yupo, Usingehangaika kuja hapa kumwelezea na kumuongelea.

Ungemuacha huyo Mungu aje hapa yeye mwenyewe kama yupo, ajiongelee na ajidhihirishe mwenyewe kwamba yupo l.

We jamaa hauna msimamo pia sio rahisi kusawishi watu zaidi ya hivyo ,unachofuata pia ni dini baada ya kuona maisha ya wazungu.
Mimi sishawishi mtu aache kuamini Mungu yupo, ila akianza kudai kwamba imani yake ya huyo Mungu ina ukweli lazima athibitishe hilo.

Na akileta habari zake kumhusu Mungu huyo lazima tuzichambue na kuzikosoa.

Otherwise ubaki na hiyo imani yako moyoni mwako usiilete hapa kwenye open forum.
 
Back
Top Bottom