Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Huyo Mungu Alishindwaje kuumba Dunia isiyo na shetani?Miaka inazidi songa na shetani anazidi kujitwalia wafuasi.
Kwani Mungu amesema shetani hakutakiwa kuwepo?Huyo Mungu Alishindwaje kuumba Dunia isiyo na shetani?
Mungu mnayedai kwamba ni mwenye kujua yote tangu mwanzo na hata milele, Je Hakujua kwamba shetani atakuja kuwepo amdhibiti na kumzuia mapema?
Huyo Mungu anashindwa na ameshindwa kuwapatia afya njema maelfu ya wazee, watoto, wanawake na walemavu wanaokufa kila siku kwa njaa, magonjwa, vita na majanga mbalimbali ya asili duniani.Kwa sasa hivi kinachokupa jeuri ni umri(ujana) na afya ngoja, sikuombei mabaya lakini ikifika wakati mwili na akili zimechoka lazima utarudi kwenye mstari tu.
Huyo Mungu aliyetaka shetani awepo halafu hapohapo anakulaumu wewe binadamu kwa maovu yako,Kwani Mungu amesema shetani hakutakiwa kuwepo?
You are mixing a priori logical fallacy with non sequitur logical fallacy.We can prove through existence of this cosmos , and we know through the experience of intelligence he has put on his cosmos
Mungu hajawahi kumlaumu mwanadamu kwa maovu yake.Huyo Mungu aliyetaka shetani awepo halafu hapohapo anakulaumu wewe binadamu kwa maovu yako,
Ilihali alijua na anajua ni shetani huyohuyo ndio anafanya na kusababisha watu watende maovu, Ni Mungu Mpumbavu na mjinga sana.
Na wala hajielewi.
Ukiwa Mkristo, unaitwa Kafiri na Waislam na lazima uende motoni. Wakristo nao wanaamini Mungu wao ndiyo wa kweli mpaka akamtoa mwanaye wa pekee kwa ajili yao, usipomuamini huyo ni motoni.Na wewe utakuwa kuni ya kuwashia moto.
Lamomy
Bro inauma sana kuwa kuni ya kuwashia moto😅Ukiwa Mkristo, unaitwa Kafiri na Waislam na lazima uende motoni. Wakristo nao wanaamini Mungu wao ndiyo wa kweli mpaka akamtoa mwanaye wa pekee kwa ajili yao, usipomuamini huyo ni motoni.
Sasa sisi wengine tumekataa pande zote. Shetani atungojee tu! 😁
Sio kila homa ni malaria.Habari wana-JF!
Najua huu uzi wafia dini watausoma kwa kusonya ila ndiyo hivyo inabidi tuvumiliane tu.
Mimi nimekulia katika Ukristo, sijaukana ila nimeliacha kanisa kimyakimya. Baada ya kuanza kukua na kujitambua nilikuwa na maswali mengi sana juu ya nadharia zote kumuhusu Mungu na maswali yangu yote yalikuwa hayana majibu yaliyonyooka.
Baada ya udadisi wa muda mrefu nikafikia hitimisho kuwa "hakuna Mungu" kwasababu angekuwepo na majibu ya maswali yangu yangekuwepo.
Uwanda wa imani ni mpana ila ukiwa ndani ya imani chini ya tawi la dini ni mwiko kudadisi uwepo wa Mungu, huko ni "ndiyo" tu hakuna kuhoji.
Maisha baada ya kulikimbia kanisa yamekuwa na amani kwasababu:
1. Maisha yangu yapo mikononi mwangu.
2. Sina hofu juu ya kifo wala kuzimu kwasababu siamini hadithi za maisha baada ya kifo.
3. Naishi kwa kufuata katiba na sheria za nchi na si vinginevyo.
4. Siishi maisha kwaajili ya kumpendeza yoyote au kitu chochote.
5. Napata muda mwingi wa kufanya mambo ya msingi, siku ya Jumapili kwangu ni kama siku nyingine ya wiki.
6. Badala ya kuhangaika kutafuta maarifa ya maisha ya mbinguni (kusoma biblia), natafuta zaidi maarifa yatakonisaidia kwenye maisha ya hapa duniani maana ndiyo sehemu pekee ninayothibitisha ni ya kweli.
7. Najiheshimu. Kwangu kulia na kuomba msaada kwa M(i)ungu ni kutojiheshimu kama binadamu.
8. Nikipata matatizo sikai chini kuomba na kusubiri miujiza badala yake natumia maarifa niliyonayo kutafuta ufumbuzi.
9. Siishi kwa matumaini ya kuzawadiwa uzima wa milele.
10. Nimepishana na utapeli. Kama wanavyosema "wajinga ndiyo waliwao".
Siamini kama kweli Mungu yupo, lakini kama yupo hawezi kuwa mjinga kama anavyoelezewa kwenye vitabu vya dini.
Mungu hayupo, lakini kama angekuwepo hastahili utukufu wala unyenyekevu kutoka kwangu.
The sweet, sweet relief of knowing I'm going to hell no matter what I do! 🙃
Mungu anawapenda wanadamu wote.Na kama mungu angekuwepo kwann asimuuwe shetani et amuuwe mwanae
Watu wanamfanga vibaya binti ya watu na mungu anawaangalia tuu lakkni anauwezo na anaweza kutuangalia wote kila tufanyalo kila tuwazalo, mungu anaipenda israeli tuu wengine aaaahh
Mna dawa ya kuzuia uzee😁Tutembelee Mwendapole Herbal Clinic, tupo mkoani Rukwa.
Ipo ya kuzuiwa mtu asibaki dunianiMna dawa ya kuzuia uzee😁
Mwanadamu Asiangamie na nini?Mungu hajawahi kumlaumu mwanadamu kwa maovu yake.
Ila aliamua mwenyewe kufanya upatanisho ili mwanadamu asiangamie.