Maisha halisi nchini Marekani

maisha yapo africa na kama tanzania achana na dar es salaam jikiteni mikoani kama una mtaji ambao uwezi kushindana na mji wa dar.
Je maisha ni nini? Kwenda hospitali isiyo na uwezo wa kujua tatizo lako, kwenda shule au chuo usiwe na uhakika wa kuelimika, kulima kwa njia ngumu bila vifaa, na kukosa soko au kupigwa marufuku na serikali ya kuuza unapotaka, achilia mbali, kodi, tozo zisizoeleweka, polisi kukubambikia watakalo, rushwa, wizi kila sekta?
Maisha ni zaidi ya kipato.
 
Tunashukuru kwa ushuhuda mkuu. Japo mimi katika kusafir kwangu japo cjakaa kwenye hizo nchi niliona Canada inafursa zaid ya marekan. Kuanzia elimu na kazi kama hiz unazosema. Nimefika hizo nchi mbili ila marekan nilifika hiyo miji mikubwa. Na life lake ni kama Hongkong .singapore nk. Kwa mtu aliyetoka nchi masikin kama zetu ni kweli ni vizur kuish miji midogo.
 
Singapore ni balaaa marekaani ikasome ..Kule maisha ni ghali mnoo
 
Nina uhakika kwa zaidi ya 90% mleta mada hauishi marekani, ni hadithi zako za kutunga tunga. Nikikusoma between the lines naona wazi kabisa huijui Marekani. Kwa mfano:
1. Unazungumzia suala la Credit card kama kitu cha ajabu wakati ni jambo ambalo karibu kila mtu aliyepo Marekani anamiliki.

2. Unazungumzia issue za kusomea fani kama Udaktari kuwa ni issue rahisi na kawaida kwa mbongo kuweza kusomea akitaka akiwa Marekani wakati sio jambo rahisi kabisa ukiwa marekani.

3. Unasema umeshafanya kazi kwenye zaidi ya makampuni 7 ili kupata exposure tu wakati kiuhalisia huna kazi rasmi na unaishi kama kibarua tu, huku suala la ajira kwa US nalo limekuwa changamoto, na watu wanazisaka na hufanya kazi ili kuweza kuishi tu na sio their choice job.


4. Unasema mtu unatengeneza zaidi ya dola 5000 kwa mwezi lakini unaishi kwa dola 600 tu halafu hizo zote zinazobakia unazileta kuwekeza nyumbani Tz! Hizo ni hadithi za Abunawasi. Wakati kuna utitiri wa Diaspora hawana chochote Tz na hawana chochote US, wapo wapo tu, na siku wakifa huishia kuchomwa moto huko huko marekani.

5. Unazungumzia issue ya Green card kuwa unaimiliki as if ulikwenda marekani na kupewa au kuipata kama njugu, haki yako au uamuzi wako tu kuipata. Wakati kiuhalisia Green card ni mchakato mrefu, na karibu kila mtu anausaka huko Marekani na wachache hubahatika.

6. Unasema ukiwa US ni rahisi kumiliki nyumba! Huu ni uongo wa 100%. Hivi Diaspora wangapi wanamiliki nyumba marekani?
 
Jaribu kutofautisha kati ya wazamiaji haramu na waishio huku kihalali.
 
Jaribu kutofautisha kati ya wazamiaji haramu na waishio huku kihalali.
Sasa Wewe Ambaye Upo huko Kihalali Huwataki Diaspora Wenzio Waliofika huko Kwa Kuzamia.?
Sisi huku tunawatambua wote mpo Majuu,Kwaiyo ndo Kusema Mkikutana huko wala hamsalimiani na Kupeana Michongo.!
Ndo maana Wengine ni Choka mbaya ..!
 
Kwani wewe unaishi US pia?
 
Wewe ni mvivu na hauna uwezo mkubwa wa kushindana na kupambana kiakili.
 
Kwani mtu akienda kuishi Marekani lazima atoboe? Change your Stupid and Idiotic Mindset.
Kwahiyo unaenda kufanya nini kama hakuna mafanikio?.........unapoteza 20yrs ughaibuni, unarudi kuanza maisha upya hapa bongo that's life failure, na wengi wamefeli maisha kwa kufuata mawazo ya motivational speaker kama mtoa uzi,

anapotosha vijana kwa kuweka mindset yao kuwaza Marikani, US isn't as simple kama alivo andika, hayo yote kasimliwa na watu walio feli maisha ya ughaibuni, maratino wengi kutoka Mexico na latini America ni machokora hawana chochote na hawana nyuma au mbele wanaanza kua drug addicts tena ni majirani na Us ndo uanze kudaganya Msabaa wa bongo aende kupoteza mda na pesa zake, after 20yrs arudi vile vile,na kuonyesha picha za barafu tu.

Kwa wanao ende ughaibuni ni 10% ndo wanafanikisha tena their cases are special 90% wanabakiza stori na picha za barafu huo ndo ukweli, naongea hili out of experience en peacticle examples kwa ndg jamaa marafiki na mimi mwenyewe.
 
Wabongo tunapaswa kufahamu kuwa, tupate exposure yakuja kuwekeza bongo ila tusijidanganye kuwa mifumo ya nchi za magharibi zinaweza kusaidia kuvimba ugenini.
Ukiamua kupata na kutoboa kwanini usivimbe?

Raia wa nchi nyingine wanatoboa?

Angalia wachezaji wa africa kwenye ligi za ulaya. Hawavimbi?

Huu ushamba wa lazima kurudi home mnautoa wapi?
 
Ukiamua kupata na kutoboa kwanini usivimbe?

Raia wa nchi nyingine wanatoboa?

Angalia wachezaji wa africa kwenye ligi za ulaya. Hawavimbi?

Huu ushamba wa lazima kurudi home mnautoa wapi?
Kutoboa kupo popote ila nu asilimia ngapi wanao fanikisha kwa huyo njia
 
Duuuh umetaja kwetu kabisa, alafu ifakara kilimo cha kubahatisha nililima nusu nife kuulizia km mvua inenyesha au laah sintasahau
 
Shida ni kuwa hata Lemutuz mwenye konekshen amekaa marekani miaka 30 lakin leo hii karudi anaishi kwa baba na anamiaka 60+
Kama marekan panalipa endelea kuish mkuu ila ukiona hali ni mbaya usione aibu kurud maana usije ukarud mzee na huna hata familia na wenzako uliowaacha wamepiga hatua zaid
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…