Maisha halisi nchini Marekani

Nilishaandika kwenye Mada ya ukitaka kwenda Marekani lazima ujipange, labda niseme Marekani ni kubwa sana, hivyo experience ya huyu inaweza kuwa tofauti na Mwingine, ni vigumu sana ku generalize. Nimeingia Marekani roughly miaka 10, Nina nyumba, na karibu 90% ya Watanzania naofahamiana nao mimi walioingia kabla yangu wana nyumba. Nachoweza kusema kujua una fanyokitafuta nini Marekani, nini unachokitafuta ni muhimu sana.Kwanza kuwa na Makaratasi, pili kui study how American system work.Wengi hawafanyi hayo! Ukiwa na steady income, credit yako ikiwa nzuri utapata nyumba ya level yako. Niko Texas miaka miwili iliyopita nimeona Watanzania wakihamia Texas from other States na kununua nyumba Frisco na Celina maeneo ambayo ni ya just, hivyo inawezekana, lakini vile vile ni mipango ya mtu na priorities zake za Maisha, na mfahamu Mtanzania mwenye nyumba zaidi ya tatu.Hata Tanzania tu si wote wanajenga.Ni mipangilio ya mtu.
 
Mkuu wzungu gani hao wanoomba urai wa Tz , kumbuka kuwa Tz hawana uraia pacha, mbona ni jambo gumu kidogo????

And by the way ni rahisi kwa mtanzania kuwa mcanada au mmarekani kuliko mmarekani kupata uraia wa Tz... taratibu kwa raia wa nje kuwa mTz ni ngumu sana
 
Naona si vyema kusema kumiliki nyumba ni mambo magumu sana! Mimi ni mbeba maboksi...maana yake halisi nafanya kazi kiwandani, nilikuwa na Credit na savings zangu, nilipata options za nyumba nyingi! Siishi kwenye Slums..
wala low income apartment..
 
Tatizo ukiugua, halafu siamini kuwa katika miaka sita uliyokaa Marekani umeweza kuwekeza huku nyumbani,basi ulikuwa muuza sembe bila shaka,kwa kazi ipi hadi miaka 6 uwekeza home,umesoma muda gani hadi kuwa professional mwenye wage ya uhakika
Duuh, aisee...!
 
Najua vizuri na hata hizo credit points zinavyopatikana
Sasa kama unajuwa vizuti habari za credit score mbona uliandika kama unamshutumu lmleta mada kanakwamba kuna sehemu alizungumza anatumia vibaya credit card yake Mkuu??
 
 
Acheni kuwadanganya wana mazee.
True mbona wengi wapo nje wameanzia na ulinzi kabla awajapata ramani.
Mimi miaka 17 iliyopita wakati sina ramani baada ya chuo nilipiga ulinzi KK security one year,nikaomba night shift mchana naniga tai nafanya market promotion nguo nimeacha lindo home ni nikiwa off ndo nalala,hadi nilipopata ramani.
Maisha ni mapito na mapito ni shule
 
Ahsante kwa majibu Mkuu, natamani sana kuishi huko ama nchi yoyote Duniani nje na hapa kwetu
Embu tembelea indeed.com (browse nchi unazozi target) anagalia kazi hata za entry level kwa field yako , tafuta hata za online/remotely

Jambo lingine Resume/ CV zako ziwe katika format za US na ncho za nje... usiwe na Resume za kibongo bongo unaweka mpaka primary schoool wakati una masters,

Edit Cv yako iendane, au ihakisi na kila position unayoomba, sio Cv moja kila kazi unaombea hio hyo...!

Inabidi pia uapply atlist nafsi 20 kila siku 😂😂
 
Hapo umesema ukweli Mkuu, nimeona sana haya ma NGO makubwa wanasema wanataka mtu mwenye experience ya NGO hivo basi kuzipata hizo kazi mpaka kuwa na msingi mzuri
Yes , fanya internship na kujivolunteer ndio njia nzuri kutoboa
 
Mkuu kama mtu ni hotelier maisha ya kazi Kwa Marekani yapoje?
 
Huwa inahuzunisha zaidi pale mtu anapoishi amerika miaka 15 hadi 20 hajatoboa, halafu ikatokea amerudi bongo kuishi. Yaani huwa wanachanganyikiwa nyie acheni
Wapo wabongo wengi hapa hapa Bongo sasa ni wazee wanashinda vijiwe vya kahawa tu , wamerdika na maisha yao ya furaha hapa bongo, tusiwashutumu wa nje
 

Sawa, ndo maana sijapinga kwa 100%
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…