Maisha halisi nchini Marekani

Maisha halisi nchini Marekani

Mikoani hakuna fursa zozote acheni kujazana upumbavu kichwani.

Vijana wanaona bora wawe machinga dar kuliko huko unakoona kwenye fursa.
Dar hkn biashara icyolipa bila kujali mtaji ukiwa disciplined unatoboa.
 
Net saving per Month baada ya kutoa bills zote! Mimi ni picha halisi ya mbeba maboksi, sasa acha Watanzania wenzangu ambayo wameenda shule. Marekani inataka Nidhamu ya maisha,information, na kibali halali cha kuwepo hapa. Kamwe hutaganga njaa.

20220501_225722.jpg
 
Ni uvivu tu, ndio maana utakuta mtu anapiga debe apewe mia mbili mia mbili siku nzima wakati kijijini kwao kuna mapori ambayo anaweza tumia nguvu hizohizo kufyeka na kuanzisha mashamba..
Bila mtaji,yaan alime ategemee mvua!?c Bora hizo mia mbili.
 
Habari JF

leo Katika mada yangu kichwa tajwa hapo juu, Ningependa nishare nanyi Uzoefu wangu wa maisha ya marekani, maana nimeona watu wengi sana wakijadili namna watu wanavyoishi nje, ajabu kati ya mia, tano tu ndo wanaelewa maisha halisi ya marekani.

Licha mimi huwa sipendi kuishi Marekani, lakini fursa zilizopo ndo zinatufanya tuelendelee kunganagia haya maisha, ndomana maisha yangu ya uwekezaji Yapo africa lakini utafutaji ni marekani kwa vile tu sijafikia malengo yangu ya maisha.

Miaka 6 ndani ya nchi ya marekani, ninaishi kwa Green card, nina ruhusiwa sasa kuomba uraia lakini mimi kwangu huwa si kipaumbele, maana nina uwezo wa kutoa na kuingia na kukaa nje ya marekani muda wa miezi sita.

Nimeishi majimbo na kufanya kazi kampuni tofauti tofauti, Mara nyingi nafanya hivyo tu ili kujifunza maisha halisi ya marekani. Mwaka jana nimefanya kampani saba na kuishi majimbo matatu. kufanya kazi marekani huwa nafanya tu kukaa bila kazi. nilichokifanya miaka minne ya marekani niliweka nguvu kuwekeza nyumbani jambo ambalo nilifanikiwa na kunipa huakika wa kuishi hapa bila kuwa na kazi.

Katika Harakati zangu za kucompare africa na marekani sehemu nzuri ya kuishi, niligundua africa kinachotufelisha ni uchumi ila ukiwa na pesa napendekeza kuishi afrca badala ya marekani. Marekani ni sehemu tu ya utafutaji ikiwa africa huna cha kupoteza(maono yangu)

MAZURI YA MAREKANI.
naipenda nchi ya marekani ni nchi ambayo inamuwesha kila mtu bila kujali nchi uliotokea kufanya lolote na ukafanikiwa, tofauti na nchi kama vile urusi, china. marekani ni nchi ya kila mtu kufanya anachoweza yaani nchi ya fursa. ukitaka kuwa doctoe, nurse nk.. hata kama umefeli elimu katika nchi yako marekani kuna njia nyingi za kukuwezesha ukarudi shule na ukatimiza ndoto zako.

Ikiwa ndo mara ya kwanza unaingia marekani, Kitu cha kwanza jifunze sana kingereza, kitu cha pili somea fani yeyote, cha tatu kuchuka Credit card. ukiwa na hayo matatu nchi ya marekani umemaliza mambo mengine yanakuja, na hayo yote inawezekana kufanyika kwa mtu yeyote anaishi marekani kihalali.

kazi na makazi, siwezi kushauri kuishi kwenye miji kama Chicago, New york, washington nk.. mara nyingi miji hii kazi zake ni professional. tena ina gharama kubwa ya rent. badala yake nenda kwenye majimbo kama dakota, kenctuky , mara nyingi ni kazi za viwanda au Entry job alafu rent iko chini.

Watu wengi kutoka nje ya marekani wanafanya ENRTY JOBS kutokana na lugha kuwa ngumu alafu pesa zinawachanganya hawataki kusoma.

Marekani kuna uraisi wa kumiliki nyumba gari na kufanya biashara unayotaka(biashara ya import chakula na kuuza kwenye maduka ya africa inalipa). hata kama huna huwezo huo. unaweza kutumia CREDIT yako na kupata nyumba, gari, au pesa baadae utalipa taratibu. kikubwa deal na Scores zako kuwa HIGH, na Credit ni kitu muhimu sana marekani.

Kazi ni nyingi na unaruhususiwa kufanya kazi masaa yote unayotaka hata kuwa na zaidi zaidi ya kumi, Mfano mimi nina ENTRY JOBS ndo always huwa nafanya kazi za aina hii, Kazi yangu ya Sasa Ni HMI CLASS tunatengenza class, nafanya kazi masaa 8 kila siku nalipwa $21 kwa saa na overtime $27, awali ilikuwa GE Appliance nilikuwa nalipwa $19, Before GE ilikuwa Fedex nilikuwa nalipwa $19.50, kabla ya Fedex ilikuwa Amazon $20.

Now kazi yangu ya sasa nafanya masaa ninayotaka nikisema kwamba nataka nipate $5000 mwezi huu inapatikana na gharama zangu za maisha ya marekani hazifiki hata $600(bills). So hapo nina kitu cha kufanya tayari africa. Imagine miez 12 ya kazi nikiruid africa huwez kusema tunarudi tumechoka.

Fursa nyingine ambayo kwangu huwa naona ni muhumu sana hapa marekani ni technology, Iphone ilipo marekani sio iliopo africa, chrome inavyofanya kazi marekani ni tofauti kabisa na africa, System za simu na Feature baadhi za Social Media ziko tofauti. kuna software kama vile Stripe huwezi kujiunga ikiwa unaishi africa, so mambo kama hayo ni muhimu sana na ni fursa kubwa.
Hat banl system ni tofauti kabisa zinavyotumika africa.

So kuishi marekani kuna fursa ya kuelimika pia, saivi ukimwabia banker maswala ya wallet pay, wireless pay, finger pay haya ni mambo mageni kwake au anasikiaga tu, ila wewe unaelimika kutoka na fursa ya mazingira unayoishi

ITAENDELEA.......
NO PM
Hizo rent mbona husemi ni shingapi kwa miji ya gharama na miji ya kawaida? Any way kuna drivers vacancies?
 
Haya ndio mabox....Sibebi kichwani, si sogezi hata kidole, ni fork lift tu..I can go to Disney...I bought a house...send my kids to Colleges..driving a car of my choice...na kutoa support hapa na pale ndugu zangu wanasumbulia na Ada, au kupigwa mapanga na panya Road! Part time nasoma vitabu na articles malicious mbali to keep my brain sharp! Maana kazi haina kutumia brain.
 
Halafu Wakiambiwa wanang'aka

Maisha ni hapa hapa Bongo kuna kila fursa.USA nakwenda kutembea tu si kuishi.

Halafu nina mifano mingi sijui ni bahati mbaya au ndio utaratibu wa huko.Wengi wana rejea wakiwa hawana watoto.
 
Hivi mbona mmoja wenu huko akifariki huko Kusafirisha Mwili tu huwa ni Shughuli Pevu.?
Bakuli La michango linatuhusu mpaka huku Kwa Mtogole.!
Halafu Mkifiwa na Mzazi Utasikia Mtoto Kashindwa Nauli Kuja Kumzika Mzazi Wake..! Hivi Diaspora Tuelezeni shida nini?
Mi mwenyewe nilitaka Kuja kuwa Diaspora ila ninachokishuhudia Kinachowatokea huko nimeghairi..!

Katika Diaspora 20 ni Wawili au Watatu ndo Wanatoboa.
Kinje ketile, hivi utaniweka kundi gani, wakati nakuja US, nilikuwa nimeisha nyumba ambayo kwa Watanzania wengi ni ndoto, Nilikuwa na Rav4, Mark 2 na Old Ford Ranger, Shamba Kibaha, na kiwanja Kibaha, na watoto wangu hawajawahi kusoma shule ya msingi ya serikali mpaka naondoka Tanzania.Je nilikuwa nimetoboa au sijatoboa? Kwa vipimo vya wengi nilikuwa nimetoboa, kwa upande nilikuwa sijatoboa! Nina kiu ya kuona Ulimwengu, kupata challenges mpya na kuzishinda,kuwapa wa wanangu path tofauti katika maisha..Kama kutoboa ni kuwa na gari na nyumba na kamradi ka kusukuma siku, then retirement Umekwisha! Hata wanangu nawaambia wazi, maana ni American citizens kuwa wafikiri beyond US...kuna Canada, Australia, Europe nk Marekani isiwe mwisho wa Naoto zao! Kuja Marekani kumenipatia America passport, before I die nataka niwe nimetembea mabara yote ya Dunia, Kwangu huko ndio Kutoboa.
 
Maisha ni hapa hapa Bongo kuna kila fursa.USA nakwenda kutembea tu si kuishi.

Halafu nina mifano mingi sijui ni bahati mbaya au ndio utaratibu wa huko.Wengi wana rejea wakiwa hawana watoto.
Ni kweli hayo,naona sasa ni chuki binafsi na Diaspora! Yaani hatuzai! Kuna Mtanzania alizaa mfululizo for almost four years,Nitafanya utafiti...
 
Maisha ni hapa hapa Bongo kuna kila fursa.USA nakwenda kutembea tu si kuishi.

Halafu nina mifano mingi sijui ni bahati mbaya au ndio utaratibu wa huko.Wengi wana rejea wakiwa hawana watoto.
"Bongo kuna kila fursa"wasaidie basi wabongo wazione! Nimebakia nimetabasamu tu...Sitaki kwenda mbali kwa hili, imenikumbusha tu nikiwa mdogo kijijini kwetu nikimtembelea bibi yangu,kuna tajiri alikuwa na basi mbili na Tractor,kijiji kilikua kinampigia magoti...na kumwabudu...nilikua natabasamu tu..."bongo kuna kila fursa"
 
Mimi nina uzoefu wa marekani tu, so sijuwi unaowazungumzia wewe ni wa wapi?
Kwa nini watanzania huwa hawana ushirikiano kama mapopo? ni roho mbaya au wanafiki?
Mfano;-Yupo mtu ameleta Uzi mzuri tu lakini ameandika, #NO PM. WHY SO?
 
Mama D hapo umezungumza, kupata na kukosa ni popote ulimwenguni, yaani akili zako kichwani, mpangilio wako wa maisha unatengeneza hatima ya maisha yako.Marekani kuna opportunities, ndio,lakini wengine wanaona opportunities za Malaya, ulevi,starehe.nkWengine ni wavivu wa kuzaliwa, hata wangebaki Tanzania wangefeli kimaisha.Uzuri/ubaya wa bongo tunabebana kimaisha,wazembe, wavivu,ndugu, jamaa wana wa absorb. Marekani hakuna hiyo! Lazima ulipie uzembe wako! System imetengenezwa hivyo.

Ukweli mchungu
 
"Bongo kuna kila fursa"wasaidie basi wabongo wazione! Nimebakia nimetabasamu tu...Sitaki kwenda mbali kwa hili, imenikumbusha tu nikiwa mdogo kijijini kwetu nikimtembelea bibi yangu,kuna tajiri alikuwa na basi mbili na Tractor,kijiji kilikua kinampigia magoti...na kumwabudu...nilikua natabasamu tu..."bongo kuna kila fursa"

Hata America hakuna kila fursa
Huwaoni waamerika wanaokuja kusaka fursa bongo?
 
Maisha ni hapa hapa Bongo kuna kila fursa.USA nakwenda kutembea tu si kuishi.

Halafu nina mifano mingi sijui ni bahati mbaya au ndio utaratibu wa huko.Wengi wana rejea wakiwa hawana watoto.

Umri nao umeenda wako very frustrated. Ukisema ukae nao uwaulize wanaweza kufanya nini kujikimu ndio utawahurumia zaidi maana wanakuambia vitu visivyowezekana
 
Ukienda America fanya juu chini upate papers.
Uwe na papers , afya njema + akili timamu hapo usipotoboa utakua umelogwa na hautaweza kutoboa sehem yoyote ile

Kuna dada mmoja ana akili nzuri zaidi yeye ameamua kuzaa na wanaume4 tofauti maisha yanamuendea powaa
 
Umri nao umeenda wako very frustrated. Ukisema ukae nao uwaulize wanaweza kufanya nini kujikimu ndio utawahurumia zaidi maana wanakuambia vitu visivyowezekana
Mama D naona unakuwa Irrational, Diaspora wote wana umri mmoja! Labda wa rika lako, Marekani ni kama reli ya Kati, kila leo inaingiza watu wa kila aina, type ya first class hadi third. Sample ya Diaspora ni ile ile ya watu walioko Bongo! Nawajua watu wa age yangu hawajafanya lolote,very frustrated, je my sampling inawakilisha Watanzania wote kuwa umri umekwenda na wako frustrated Argue logically Mama.
 
Back
Top Bottom