Maisha halisi nchini Marekani

Hivi miji gani hasa ni mizuri kwa mtu anayekuja US kuanza maisha?

Mizuri namaanisha quality of life, better services, security, quality neighbourhood, n.k.

Unaweza nitajia majimbo na neighbourhood zake.
 
Watanzania wengi wetu tunaogopa risk na kufurahia comfort zone.
chief, watu wanavyoiongelea bongo utadhani kila raia anakula raha na asali. Uzuri bongo ni kwetu tunajuana hakuna haja ya kuongea mengi. tuendelee kujadili bei ya Mafuta kwanza na safari ya mama huko Yuesei kwenye royo tua.
 
Hivi miji gani hasa ni mizuri kwa mtu anayekuja US kuanza maisha?

Mizuri namaanisha quality of life, better services, security, quality neighbourhood, n.k.

Unaweza nitajia majimbo na neighbourhood zake.
Mkuu kwangu itakuwa vigumu, kwanza sijatembea States nyingi, na nimeishi State moja tu, Texas. Kwa data za sasa hivi uchumi wa Texas ni mzuri, mashirika na Makampuni mengi Yana hamia hapa, hivyo ajira za kila aina zipo, kuna baadhi ya kodi Texas hazitozwi, hivyo ni raisi kununua nyumba. Katika States nilizotembea,nimeipenda Florida,hasa mji Jacksonville, lakini pia Atlanta Georgia, na Portland Oregon. Lakini Mkuu Marekani ni nchi kubwa mno na diversity pia kubwa mno,unatoka State moja kwenda nyingine unaona vitu tofauti na ulikotoka.Hivyo mwisho wa siku inabaki wapi panakupa Maisha.Na pia hali ya hewa ni tofauti tofauti kila States, naipenda Texas weather ni kama Tanzania,ingawa joto sana summer, na mara chache kuanguka barafu. Hivyo kila anayeishi US atakupa experience tofauti tofauti, lakini kila navyoishi Marekani napenda mno kuishi miji midogo au vijijini tabu yake hakuna kazi, na diversity ya watu ni ndogo,hasa wazungu ambao hawajawahi kuishi na Waafrika,inaweza kukusumbua kidogo.
 
Shukrani sana.
 
Shukrani sana.
Kuhusu security, kila States Ina bad and good neighborhoods. Na ndugu yangu sehemu yenye watu wa masikini Hali ya usalama huwa si nzuri popote pale ulimwenguni. Kila miji mikubwa Zina sehemu hizo,ambazo unatakiwa kuziepuka kuishi.Kwa Dallas ni maeneo ya South Dallas. Uwezo wako wa kifedha mara nyingi unakupeleka kwenye maeneo mazuri yenye usalama.
 

SOUTH DALLAS​

South Dallas features major attractions like Fair Park, the Cotton Bowl Stadium, the African American Museum, and the Children’s Aquarium. Unfortunately, South Dallas has violent crime and property crime rates of 363% above and 125% above the national average, contributing to the total crime rate of 161% above the national average.
 

Mwana nafkiri tunafanana mawazo mimi nipo serikalini na nina baadhi ya vitu ulivonavyo na watu wanaona nimetoboa ila nafsini mwangu naona bado kabisaa sijafanikiwa.naplan kuacha kazi kwenda nje ya afrika kutafuta fursa na kupata exposure zaidi. shida ni the right connection
 
Doyi, safari yangu ilianzia Kufanya kazi West Africa, na nilikutana na Watanzania kutoka nchi ambazo sikutegemea, jamaa mmoja Kazi zake alikua anafanyia Chad na Mali! Niliwahi kukutana na jamaa yuko Mahakama ya UN Freetown Sierra Leone, na kwenye Miradi ya International NGO Liberia na Guinea.
Kwa wengine kutoboa ni zaidi ya simple material things !
Kazi hizi licha ya kukupa pesa but also exposure.Unaanza kujichanganya na watu wa aina na mataifa mbalimbali na kujua hulka zao na kukujengea confidence ya kuishi popote pale ulimwenguni.
 
Anazungumzia Marekani hiyohiyo, mfafanulie inakuwaje mtu akifa kusafirisha inakuwa issue?

Tupe uzoefu tatizo huwa linakuwa nini?
Hivi kuna mtu anajua Idadi halisi ya Watanzania wanaofariki, kurudishwa nyumbani kwa kuchangiwa au kwa gharama zao?
Kwanza kabisa kuchangia misiba ni jadi yetu Watanzania,hivyo hilo halishangazi, kwani hata sisi huku tunachangia misiba Tanzania kwenye koo na Familia zetu.Huku Marekani ni mipangilio ya mtu na maisha yake, Watanzania baadhi walioko huku wameshindwa kujifunza nini cha kufanya mwisho wa maisha Yao! Wazungu wamenifundisha mengi! You have to take for your life to the last minute, hapo ndio inaingia Insurance, nilijiuliza kwani Wamarekani Hawafi? Mbona sijaona michango ya rambirambi, msibani tunapeleka sana sana card na maua! Hivyo nilifanya maamuzi ambayo Watanzani wengi nadhani hawafanyi,Niki huku Insurance ya ku cover funeral expenses, na niliamua nikifa nizikwe America, kwani ndio watoto wangu wapo, na wajukuu zangu watakapokuwepo.Watanzania kama mimi hutasikia tunapitisha bakuli la rambirambi.Kuna Insurance hata za kurudisha mwili nyumbani Tanzania, ni uzembe na kutojua na pia kuwabebesha mzigo wengine.Kama tunavyo plan vitu vingine katika maisha, plan pia ukifa unataka uwe disposed namna gani.Tuko nchi ya ugeni lazima tubadilike.
 

 
Ujinga wa Canada ubalozi wao wa Dar hautowi viza, Viza zitolewa Nairobi.

Kuna ofisi yao ipo kinondoni ndio wanapokea viza application na juzituma docs Nairobi then passport ikirudi ndio unapigiwa simu ukachukuwe passport yako na hapo ndio unajuwa kama wamekupa au umenyolewa, kuna advantage yake lakini kwa utaratibu huu kwa watu ambao wapo genuine. Kwahiyo minimum Canadian viza unatakiwa kuapply miezi mitatu kabla ya safari yako.

Tatizo la US Embassy wanatowa viza same day lakini consular akiamka vibaya unanyolewa, hapo ndio utaona tofauti ya viza ya Canada haitolewi kwa mihemko maombi yako yanapitiwa vizuri kwa umakini na wanatenda haki, ukiona mtu ananyolewa viza ya Canada ni ukweli documentation alikuwa na magumashi mengi.
 
Hii ni misiba hata wana Diaspora tunombwa tuchangie nyumbani.
Au ndugu zangu mlitaka sisi tuchangie na mnaona jambo gumu na ninyi mnaopombwa mchangie? Najua gharama za kurudisha maiti nyumbani ni kubwa, hivyo kama jamaa yenu kaamua kuzikwa nyumbani na hakujiandaa mtabeba jukumu, hata Tanzania tunafanya hivyo.Lakini ukjipanga na kuamua kama mwana Diaspora unaweza kabisa ku cover your own funeral expenses,na baadhi tumefanya hivyo.
 
Ni kweli kabisa,nasikia visa ya Canada wakikupa ni ten years multiple entry, sijui kama ni kweli. Na US kama uliwahi kuja na kurudi kwa wakati, visa process imekua ni rahisi,hupitii tena interview
 
Utu ni kuishi tanzania na Degree yako pamoja na Elimu uliyosoma nusu ya Maisha yako kwa mshahara wa laki 5? Au kuishi US kubeba Box na kulipwa Dola 20 kwa saaa na kuishi kwenye nyumba mzuri ambayo Bongo unazikuta Masaki na Oysterbay? Which is which? Wabongo mnapenda sana kujifariji
 
Ni kweli kabisa,nasikia visa ya Canada wakikupa ni ten years multiple entry, sijui kama ni kweli. Na US kama uliwahi kuja na kurudi kwa wakati, visa process imekua ni rahisi,hupitii tena interview
Canadian viza zipo wanazotowa mpaka miaka 10 lakini siyo zote na umri pia wanaconsider.

Ukiwa na US viza kupata viza ya Canada ni gurentee.

Kinachochelewesha wao hawawafinyii interview applicants ndio maana inachukuwa muda wanafanya screening wenyewe wakimaliza unapigiwa simu tu ukachukuwe passport, ukishachukuwa passport ndio unajuwa wamekupa au umenyolewa na barua wanakupa ni kwa nini wamekunyowa, lakini pia appeal inaruhusiwa kama timming ya muda inaruhusu kwa viza fee nyingine.

Kwa kifupi kwa watu genuine Canadian viza ni rahisi sana kama zilivyo sheghen viza.

Hizi ni viza zinazohitaji makaratasi tu yaliyosimama tofauti na Marekani kuna watu wamenyimwa viza kwa kutojuwa tu kingereza vizuri na kushindwa kumsikiliza Mmarekani na kumuelewa wakati anatema yai lakini safari zao zilikuwa genuine.
 
Kwa hapo texas, maeneo gani ya matajiri ambapo naweza nunua nyumba?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…