Maisha halisi nchini Marekani

Maisha halisi nchini Marekani

Kwahiyo unaenda kufanya nini kama hakuna mafanikio?.........unapoteza 20yrs ughaibuni, unarudi kuanza maisha upya hapa bongo that's life failure, na wengi wamefeli maisha kwa kufuata mawazo ya motivational speaker kama mtoa uzi,

anapotosha vijana kwa kuweka mindset yao kuwaza Marikani, US isn't as simple kama alivo andika, hayo yote kasimliwa na watu walio feli maisha ya ughaibuni, maratino wengi kutoka Mexico na latini America ni machokora hawana chochote na hawana nyuma au mbele wanaanza kua drug addicts tena ni majirani na Us ndo uanze kudaganya Msabaa wa bongo aende kupoteza mda na pesa zake, after 20yrs arudi vile vile,na kuonyesha picha za barafu tu.

Kwa wanao ende ughaibuni ni 10% ndo wanafanikisha tena their cases are special 90% wanabakiza stori na picha za barafu huo ndo ukweli, naongea hili out of experience en peacticle examples kwa ndg jamaa marafiki na mimi mwenyewe.
So mkuu ma lationa na wa mexico ni ma drug addict???

Me ninachojuwa jamaa wanapambana sana na maisha japo kuwa wanazamia nje kimagumashi na kuishia kuwa cheap labour lakini ni wachapa kqzi sana.. mtu yyte anaweza kuwa drug addict hata mzawa wa nchi husika
 
Duuuh umetaja kwetu kabisa, alafu ifakara kilimo cha kubahatisha nililima nusu nife kuulizia km mvua inenyesha au laah sintasahau
Wewe ifakara huku fursa zipo, usiilinganishe ifakara na Kentucky City iakara pesa ipo sana mzunguko wa pesa huko vijijini ni mkubwa sana me na shangaa wanaotaka kwenda State ...

Endelea kulima Mkuu, Dollar zinakuja
 
Anazungumzia Marekani hiyohiyo, mfafanulie inakuwaje mtu akifa kusafirisha inakuwa issue?

Tupe uzoefu tatizo huwa linakuwa nini?
Kaka yangu yuko mitaa ya Leicester UK, anadai kashuhudia wabongo kuzikwa huko huko wakiwa majivu! Kisa ndugu zao bongo kushindwa kuchanga mwili uletwe na hata michango ya wabongo wenzao kuwa kiduchu! Huwezi laumu aisee yawezekana life ni tough hasa kama una familia. Haya maisha ni shughuli aisee….
 
Kapige Kazi ya ulinzi South,Dubai au USA utatoboa,uza kiwanja cha familia,miezi mitatu hela imerudi.
Aiseee! Duh hii hapana! Atafute kingine cha kumpa hela hiyo. Hujuwi atakuta nini kule. Asifanye bahati nasibu
 
Kujiunga hizo platforms kunafungulia watu wengi sana fursa za kuzidi kupiga hatua.

Marekani ni marekani bhana.
Kabisa mkuu hawa wana diaspora wanajua njia ya kuingia huko mamtoni ila issue ni kwamba wana roho flan ambayo sio nyepesi ku share imfo na wenzao

Na hii roho inakwenda mbali zaidi nasikia hata wenyewe kwa wenyewe hawapendai huko ughaibuni kuna siku nilikuwa online ktk socio network moja ivi sasa wakawa wenyewe wana diaspora wana discuss changamoto za maisha ya ughaibuni na mahusiano yao ..aisee binafsi nili gaini sana nikajua kweli hatupendai as wa Tanganyikan
 
Nilishaandika kwenye Mada ya ukitaka kwenda Marekani lazima ujipange, labda niseme Marekani ni kubwa sana, hivyo experience ya huyu inaweza kuwa tofauti na Mwingine, ni vigumu sana ku generalize. Nimeingia Marekani roughly miaka 10, Nina nyumba, na karibu 90% ya Watanzania naofahamiana nao mimi walioingia kabla yangu wana nyumba. Nachoweza kusema kujua una fanyokitafuta nini Marekani, nini unachokitafuta ni muhimu sana.Kwanza kuwa na Makaratasi, pili kui study how American system work.Wengi hawafanyi hayo! Ukiwa na steady income, credit yako ikiwa nzuri utapata nyumba ya level yako. Niko Texas miaka miwili iliyopita nimeona Watanzania wakihamia Texas from other States na kununua nyumba Frisco na Celina maeneo ambayo ni ya just, hivyo inawezekana, lakini vile vile ni mipango ya mtu na priorities zake za Maisha, na mfahamu Mtanzania mwenye nyumba zaidi ya tatu.Hata Tanzania tu si wote wanajenga.Ni mipangilio ya mtu.

20220501_083401.jpg


20220501_083325.jpg


20220501_083254.jpg
 
Sasa
Habari JF

leo Katika mada yangu kichwa tajwa hapo juu, Ningependa nishare nanyi Uzoefu wangu wa maisha ya marekani, maana nimeona watu wengi sana wakijadili namna watu wanavyoishi nje, ajabu kati ya mia, tano tu ndo wanaelewa maisha halisi ya marekani.

Licha mimi huwa sipendi kuishi Marekani, lakini fursa zilizopo ndo zinatufanya tuelendelee kunganagia haya maisha, ndomana maisha yangu ya uwekezaji Yapo africa lakini utafutaji ni marekani kwa vile tu sijafikia malengo yangu ya maisha.

Miaka 6 ndani ya nchi ya marekani, ninaishi kwa Green card, nina ruhusiwa sasa kuomba uraia lakini mimi kwangu huwa si kipaumbele, maana nina uwezo wa kutoa na kuingia na kukaa nje ya marekani muda wa miezi sita.

Nimeishi majimbo na kufanya kazi kampuni tofauti tofauti, Mara nyingi nafanya hivyo tu ili kujifunza maisha halisi ya marekani. Mwaka jana nimefanya kampani saba na kuishi majimbo matatu. kufanya kazi marekani huwa nafanya tu kukaa bila kazi. nilichokifanya miaka minne ya marekani niliweka nguvu kuwekeza nyumbani jambo ambalo nilifanikiwa na kunipa huakika wa kuishi hapa bila kuwa na kazi.

Katika Harakati zangu za kucompare africa na marekani sehemu nzuri ya kuishi, niligundua africa kinachotufelisha ni uchumi ila ukiwa na pesa napendekeza kuishi afrca badala ya marekani. Marekani ni sehemu tu ya utafutaji ikiwa africa huna cha kupoteza(maono yangu)

MAZURI YA MAREKANI.
naipenda nchi ya marekani ni nchi ambayo inamuwesha kila mtu bila kujali nchi uliotokea kufanya lolote na ukafanikiwa, tofauti na nchi kama vile urusi, china. marekani ni nchi ya kila mtu kufanya anachoweza yaani nchi ya fursa. ukitaka kuwa doctoe, nurse nk.. hata kama umefeli elimu katika nchi yako marekani kuna njia nyingi za kukuwezesha ukarudi shule na ukatimiza ndoto zako.

Ikiwa ndo mara ya kwanza unaingia marekani, Kitu cha kwanza jifunze sana kingereza, kitu cha pili somea fani yeyote, cha tatu kuchuka Credit card. ukiwa na hayo matatu nchi ya marekani umemaliza mambo mengine yanakuja, na hayo yote inawezekana kufanyika kwa mtu yeyote anaishi marekani kihalali.

kazi na makazi, siwezi kushauri kuishi kwenye miji kama Chicago, New york, washington nk.. mara nyingi miji hii kazi zake ni professional. tena ina gharama kubwa ya rent. badala yake nenda kwenye majimbo kama dakota, kenctuky , mara nyingi ni kazi za viwanda au Entry job alafu rent iko chini.

Watu wengi kutoka nje ya marekani wanafanya ENRTY JOBS kutokana na lugha kuwa ngumu alafu pesa zinawachanganya hawataki kusoma.

Marekani kuna uraisi wa kumiliki nyumba gari na kufanya biashara unayotaka(biashara ya import chakula na kuuza kwenye maduka ya africa inalipa). hata kama huna huwezo huo. unaweza kutumia CREDIT yako na kupata nyumba, gari, au pesa baadae utalipa taratibu. kikubwa deal na Scores zako kuwa HIGH, na Credit ni kitu muhimu sana marekani.

Kazi ni nyingi na unaruhususiwa kufanya kazi masaa yote unayotaka hata kuwa na zaidi zaidi ya kumi, Mfano mimi nina ENTRY JOBS ndo always huwa nafanya kazi za aina hii, Kazi yangu ya Sasa Ni HMI CLASS tunatengenza class, nafanya kazi masaa 8 kila siku nalipwa $21 kwa saa na overtime $27, awali ilikuwa GE Appliance nilikuwa nalipwa $19, Before GE ilikuwa Fedex nilikuwa nalipwa $19.50, kabla ya Fedex ilikuwa Amazon $20.

Now kazi yangu ya sasa nafanya masaa ninayotaka nikisema kwamba nataka nipate $5000 mwezi huu inapatikana na gharama zangu za maisha ya marekani hazifiki hata $600(bills). So hapo nina kitu cha kufanya tayari africa. Imagine miez 12 ya kazi nikiruid africa huwez kusema tunarudi tumechoka.

Fursa nyingine ambayo kwangu huwa naona ni muhumu sana hapa marekani ni technology, Iphone ilipo marekani sio iliopo africa, chrome inavyofanya kazi marekani ni tofauti kabisa na africa, System za simu na Feature baadhi za Social Media ziko tofauti. kuna software kama vile Stripe huwezi kujiunga ikiwa unaishi africa, so mambo kama hayo ni muhimu sana na ni fursa kubwa.
Hat banl system ni tofauti kabisa zinavyotumika africa.

So kuishi marekani kuna fursa ya kuelimika pia, saivi ukimwabia banker maswala ya wallet pay, wireless pay, finger pay haya ni mambo mageni kwake au anasikiaga tu, ila wewe unaelimika kutoka na fursa ya mazingira unayoishi

ITAENDELEA.......
NO PM
Sasa kama formular ya maisha huko ni simple kiasi hicho? wale diaspora walioonekana juzi na mabango ya katiba mpya wakiwa wamechoka namna ile ni wa wapi?
 
Kuwa na akili acha uboya kubisha bisha mambo husioyajua, unafiri marekani ndo kila mtu anayo, hujuwi kama unaweza kuomba Credit na usipewe,

Hivi unajua maana ya GED Program, tafuta maana yake alafu urudi. utajua jinsi gani huna akili unapenda kuropoka mambo husiyoyajua.

Kuna akili wakati mwingine ni sahihi, kwamba amazon, fedex na GE wanaajiri wafanyakazi wasiokuwa rasmi, Hivi mimi naweza kufanya kazi ya mkataba na Amazon, au wewe unaweza kufanya kazi ya mkataba na Amazon, ukiajiriwa ni rasmi. wewe seach kwanza kabla ya kuja hapa. na marekani haina kikoma, hata unaweza kufanya kazi 10 kwa siku moja. seach kwanza ndo uje huku.

Nimeshatoa check yangu umeona sasa tena unachobisha nini, nafanya kazi HMI class, iko louisville. kentucky, nimekuambia overtime nalipwa $27 na ni kazi ya permanet. Careers - HMI Glass Angalia website yao hii alafu angalia maswala ya ajiri. wanaajiri vipi. unaweza hata kuwasiliana nao wakakupa utaratibu wao wa kazi na sheria za kazi.

Ujuwi kuna watu wanaingia marekani tayari wana GReen card, so unajua mimi nimeingia kwa njia gani Marekani, na nimepata Green ndani ya Miaka miwili tu na hapi tena ilichelewa sana.

Unachanganya mambo Kama ulisema kuwa Credit Card zinapatikana kirahisi issue ni tena kumiliki nyumba maana Credit card ndo zinawapa watu wengi nyumba ni swala tu za kujenga scores.

Google kwanza alafu uje hapa.
Binafsi nimekuelewa vyema!

Hapo kwenye jama a anasema kuosmea udakatri ni ngumu sna amarekani! Wakati hata mtu aliyemaliza high school diploma labda akajianda nakusomea fani nyingine zisizohusu sayansi kabisa hata yeye aanweza kusomea udaktari maani zipo path zakufanikisha hilo!,

Na kwa taarifa tu immigrants wengi US
wanatoboa sana kuliko wanao feli !
 
Sasa
Sasa kama formular ya maisha huko ni simple kiasi hicho? wale diaspora walioonekana juzi na mabango ya katiba mpya wakiwa wamechoka namna ile ni wa wapi?
Hivyo hiyo hizo clips ndio zimekupa pacha za Watanzania,please be serious! Clip moja ya picha ya slum ya Afrika au watoto wakienda shuleni bila viatu inaweza kutoa picha ya Watanzania wote? Be realistic and objective jamaa yangu.
 
Miaka 6 ndani ya nchi ya marekani, ninaishi kwa Green card, nina ruhusiwa sasa kuomba uraia lakini mimi kwangu huwa si kipaumbele, maana nina uwezo wa kutoa na kuingia na kukaa nje ya marekani muda wa miezi sita.
NANI kakwambia green card hairuhusu kukaa nje ya US zaidi ya miezi sita ?

Tatizo kubwa la diaspora wengi sijui niseme ni shule ndogo au vichwani wamevurugwa, mojawapo!

Nenda kasome barua iliyokuja na green card yako inasemaje, na kama huna nenda online!
 
Tatizo wabongo huwa wajuaji sana,hapo atakuja akwambie huyo sio wewe umeweka picha za watu wengine au umezitoa google.

Naamini katika kutoka nje ya nchi,kwa mfano ungekuwa bongo kumsomesha mwanao katika shule zenye ubora kama huo wa huko ingekuwa mtihani,lakini unaweza kukuta wewe unaishi maisha ya kawaida huko lakini kuna zile huduma bora kwa wananchi wote unazipata kwa hapa nyumbani usingefikiria kuzipata....watanzania bado tupo nyuma sana kifikra,ubishi umetutawala sana vichwani.
Kwanza napenda kutumia nafasi hii kukupa shukrani kwa uwezo wako wa kutambua hulka za ndugu zetu watz. Ki ukweli sisi tupo nyuma kwa kila kitu kwa sababu ya tabia hizi za ubishi ubishi usiokuwa na maana. Mfano unaweza kumpa mtu mchongo wa jambo fulan la pesa, utasikia mtu anakwambia "mbona ww hilo jambo au huo mchongo haujaufanya, inamaana hautaki hizo pesa? au hauna ndugu yako yoyote wa kumpa huo mchongo mpaka unipe mimi tu? Hayo ndio maswali unayoweza kuulizwa pindi unapojaribu kumpa mchongo mbongo mwenzio, kwahiyo kwa aina hii ya tabia, ndo maana wabongo wengi hatugeani michongo na matokeo yake wengi wetu tunaishi maisha ya kubabaisha ukilinganisha na wenzetu kutoka Congo, Kenya, Rwanda, Uganda nk. Kuhusu shule ya ulichosema wala haujakosea mkuu. Nashukur Mungu wanangu wanapata elimu bora kabisa, sio bora elimu.
 
Mkuu kama mtu ni hotelier maisha ya kazi Kwa Marekani yapoje?
Cheki pia na fursa za mahotel kwenye Meli kubwa za kitalii kama
Royal caribbean

Issue kubwa hapa uwe na cv/resume nzuri .na hakikisha website unazotembelea ku apply ni legit, maana hizo kazi huko kuna scammers wengi kutoka Nigeria na india
 
NANI kakwambia green card hairuhusu kukaa nje ya US zaidi ya miezi sita ?

Tatizo moja kubwa la diaspora wengi sijui niseme shule ndogo au vichwani wamevurugwa, sielewi!

Nenda kasome barua iliyokuja na green card yako inasemaje, na kama huna nenda online!
Watanzania wanapenda kuambiwa sio kufanya utafiti wenyewe...
 
NANI kakwambia green card hairuhusu kukaa nje ya US zaidi ya miezi sita ?

Tatizo moja kubwa la diaspora wengi sijui niseme shule ndogo au vichwani wamevurugwa, sielewi!

Nenda kasome barua iliyokuja na green card yako inasemaje, na kama huna nenda online!
Ukiwa out of state kwa miezi sita ni lazima ujaze form nkutuma taarifa zako, na kama itakaa njeee kwa miaka na utalazimika kufanya application na ku update status zako na masuala ya visa
 
Out of state or out of United States ?

Jieleze vizuri wewe diaspora!

Hata sentensi moja tu iliyonyooka kuandika tabu, diaspora tatizo moja kubwa ni shule!
Out of USA
 
Back
Top Bottom