Mimi mpaka leo naamini kabisa, kijana mwenye nguvu uliyechomoka kijijini ukaja mjini ukapata hii elimu yetu ambayo naweza sema ni half baked education (ambayo haikupi skills za aina yoyote-by the way siikandii hii elimu maana na mimi ni product ya mfumo huo huo...;-), kwa nini ushindwe kujiongeza kutafuta fursa nje ya mipaka ya Tz?. DAIMA TAMBUA, maendeleo ni juhudi binafsi. Ukiona akina
Bavaria wanaongelea magari ya BMW au AUDI ya 100k USD wengine wanaona kama jamaa anajidai au ni utani! Lakini hivi ni vitu vya kawaida kwa wenzetu. Hivi kweli mshahara wa laki tano hardly dola mia mbili unategemea uendeshe BMW bila kuiba hela ya umma?
My point, is hakuna maisha marahisi popote pale. tunachokiongelea kuhusu US, Canada na kwingineko ni mifumo rafiki ambayo unaweza kuitumia ukapambana ukafanikiwa. Imagine bongo unafungua business. Ole wako DC au OCD waje kuomba/kuchukua hela ya mwenge au hela ya mafuta kufanya doria ukatae! utaundiwa figisu mapaka biashara zako zitakufa. Haya yote wote tunayajua na tumewaona victims wengi tuu. lazima ule na TRA! Kufungua kampuni tuu kuna utitiri wa regulators zaidi ya 30!
Kingine; watanzania tunachagua sana kazi. Nawajua watu wameenda nje kusoma..wamesafisha vyoo sana, wameendesha mabasi, wamedeki barabara sana, wamesafisha wazee sana (kazi zote ambazo wabongo wanaona ni za aibu watu wamezipiga na wanazifanya), but guess what? majority ya hao watu sasa hivi wanaishi maisha mazuri na ndo nguzo ya familia zao bongo! Hata humu wamo wengi tuu.
Hivi mnaposikia jamaa wamezamia mnaelewa nini? Kuna kazi nyingi sana za upishi na uyaya huko Middle East. Kuna kazi kibao za ulinzi huko kwenye mainchi yenye vita.....bongo ukiongelea kazi Saudi Arabia ya Uyaya watu wanakimbilia stories za kunyanyaswa nk. which I agree. Lakini pia, kuna success stories! kuna watu wameenda huko kutafuta maisha na wamefanikiwa vizuri tuu. Same na South Africa. Kuna ubaguzi na crime rate kubwa. Bongo watu wana-focus kwenye hizi changamoto. Lakini pia kuna success stories huko South haziongelewi! US watu wana focus kwa Trump na BLM wanachokiona CNN! Lakini mzee US ni nchi ya fursa dunia nzima! Ni ngumu kulielewa hili bila kuingia ukaona.
Kikubwa serikali iache umangi meza kutoa passports it should encourage its citizens waende nje wapate uraia na permanent residences! Hawa kesho na keshokutwa watoto wao utawakuta kwenye system na nafasi nyeti kwenye hizo nchi. Angalieni wahindi wanavyochomoza US...ukiangalia nafasi nyeti hata kwenye cabinet ya Biden kuna wahindi wengi tuu! its not by accident! angalia makampuni makubwa ya google nk...wahindi wamejaa! angalieni wanigeria. Angalieni wakenya. Usije ukashangaa mtoto wa mpiga box alikimbia bongo anateuliwa kuja kuwa balozi wa US Tanzania! Kwa wenzetu yote yanawezekana. Hawa ndo wanakuja kuwa mabalozi na kuzipigania nchi za wazazi wao.
waTanzania popote tulipo. Tubadilike na tubadilishe mindset!