Equation x
JF-Expert Member
- Sep 3, 2017
- 33,679
- 49,841
Kila utakayekutana naye, utakuwa unamkasirikia; atakaye kusemesha neno dogo tu, unamjibu kwa ukali; ukiona uzi wa masham sham unakasirika: hii ni ishara ya kukosa mahusiano sahihi.
Ndio, ni kweli hapa duniani kuna changamoto nyingi, hasa za kiutafutaji ili kuweza kupata mkate wa kila siku; zipo changamoto za kutengwa, changamoto za kuugua, changamoto za maeneo ya kazi n.k Lakini kitu kinachokuja kumpa faraja mwanadamu, ni mahusiano tu.
Ukiwa na mahusiano na mtu sahihi, muda wote utakuwa unafuraha ata kama unapitia changamoto mbalimbali za kidunia.
Kwa nyakati hizi, wanaume halisi wamekuwa ni wachache sana, na hii inathibitishwa kwa idadi kubwa ya wanawake kutokuolewa, wengine wamezaa na hawajaolewa, wengine wameolewa lakini hawaridhishwi n.k
Lakini mwisho wa siku, wote wanahitaji mahusiano.
Kwa kifupi naweza kusema; pigania mahusiano yako, huwezi kupingana na asili ya uumbaji.