Maisha haya bila kuwa na mahusiano, utaona dunia ni chungu

Maisha haya bila kuwa na mahusiano, utaona dunia ni chungu

Kila utakayekutana naye, utakuwa unamkasirikia; atakaye kusemesha neno dogo tu, unamjibu kwa ukali; ukiona uzi wa masham sham unakasirika: hii ni ishara ya kukosa mahusiano sahihi.

Ndio, ni kweli hapa duniani kuna changamoto nyingi, hasa za kiutafutaji ili kuweza kupata mkate wa kila siku; zipo changamoto za kutengwa, changamoto za kuugua, changamoto za maeneo ya kazi n.k Lakini kitu kinachokuja kumpa faraja mwanadamu, ni mahusiano tu.

Ukiwa na mahusiano na mtu sahihi, muda wote utakuwa unafuraha ata kama unapitia changamoto mbalimbali za kidunia.

Kwa nyakati hizi, wanaume halisi wamekuwa ni wachache sana, na hii inathibitishwa kwa idadi kubwa ya wanawake kutokuolewa, wengine wamezaa na hawajaolewa, wengine wameolewa lakini hawaridhishwi n.k

Lakini mwisho wa siku, wote wanahitaji mahusiano.

Kwa kifupi naweza kusema; pigania mahusiano yako, huwezi kupingana na asili ya uumbaji.​

Joannah anasemaje ?
 
Kama unamaanisha mahusiano ya kwenye ndoa rasmi nitakubaliana na wewe. Lakini kama ni mahusiano nje ya ndoa huo ni uzinzi na uasherati!! Biblia inasema hakuna amani kwa wabaya!!
Sasa hawa ambao hawajaolewa unataka nani wawafariji? Iwapo wanaume rijali wako wachache, na hawa ke wanaitaji kuwa kwenye mahusiano? Kwa uwiano tu tunaweza kukadiria 1:6 na bado hesabu inaweza isibalansi.
 
Kuna wengine wapo kwenye ndoa ila wenza wao wanawaigizia kama wanawapenda,kumbe wanadanga mpaka kwenye ndoa.

Sometimes zile style za wazee wetu wa zamani zakutafutiana wachumba,mafunzo ya jando na unyago naona walikuwa sahihi sana,ila siku hizi ni hovyo hovyo.
 
Kwa zamani ilikuwa inawezekana ila kwa mazingira ya sasa ni vigumu
 
Back
Top Bottom