Nna rafiki yangu yeye ana kisa kinachofanana na chako. Akajiroga akajitosa mzima mzima. Aise mpaka nilimuhurumia.
Alikutana na huyu single maza, kwa kweli alikuwa na bonge shepu matata ile nane iliyojichora na kakiuno kaduchu na mzigo kama wote.
Shemeji mimi nilivyoombwa ushauri nikatoa go ahead, "Kama hujaona kasoro zake na unampenda, tengenezeni maisha pamoja."
Daa...! Kilichokuja kutokea sasa. Yule manzi alitulia tuli karibu mwaka baada ya wao kuwa pamoja (walimove-in pamoja bila ndoa lakini) na walifanikiwa kupata na mtoto.
Baada ya hapo sasa, sijui ndio kuchokana, manzi akaanza kushea tunda na Ex-baba mtoto wake. Mshikaji alipogundua alipiga sana kelele manzi ajirekebishe lakini ndio kwanza kama alimuongezea petroli. Dharau zikazidi mpka mshikaji anapiga simu mbele yangu manzi aje tuyasuluishe anajibiwa mbovu (loudspeaker) hadi huruma.
Fast things forward, walikuja kuachana kila mmoja anaendelea na maisha yake kwa sasa. Manzi alikimbia na mtoto akaenda kukaa kusikojulikana akawapiga biti ndugu zake wasimwambie mshikaji anapoishi ila jamaa hana hiyana anaendelea kutoa matunzo ya mtoto wake.
Hapo nikapata funzo kwa jinsi jamaa alivyopitia hilo life, siwezi mshauri mtu ajiingize huko labda ujiweke sawa kisaikojojia au baba mtoto awe hayupo hai.
NB: Si single maza wote wabaya, unaweza ukabahatika ukapata kinachofaa pia.