Maisha magumu sana jamani

Maisha magumu sana jamani

Hali tight sana na kwatuliomaliza vyuo aisee cio powa.
Wewe uliomaliza Kusoma Au ushauri wangu kwa waliomaliza kusoma Jaribu kuwa creative kubuni kitu ambacho pengine kinaweza kukuongozea kipato At kidg kwa siku Usikae ndani toka zunguka maeneo yenye mchanganyiko wa watu pengine akili inaweza ikazalisha kitu kutokana na elimu uliokuwa nayo Na Allah akakusaidia kwa uwezo In shaa Allah
 
IMG_1039.jpg
 
Hela inatosha kula mmoja tu.....nyie ndio mnapanga mnakula muda Gani........

Hakuna tena furaha kwenye familia na jamii kwa ujumla............

Chakula kimekuwa anasa, ukionekana unakula watu wanakushangaa........

Ukiandaa sherehe labda ufunge milango ndio ule na wageni maana watu watajaa wengine hata uwajui......

Watu wanaenda waongea peke Yao kama vichaa barabarani.........

Watu wamejaa hasira muda wote wapo siriaz kama wapo kwenye mafunzo ya kijeshi.......

Sura za watu zimekaa kishari Shari tu.......mtu ukimtazama mara mbili anakushushia tusi mpaka unashangaa...... kwenye dala dala mtu ukimwambia sogea kidogo tukae vizuri anaanza na tusi alafu ndio anakujibu...........

Sherehe za basdei zimepungua sana kama sio kuisha kabisa.....

Baba wa familia hata shikamoooo unaipata kwa mbinde......unawakuta wamenuna mpaka unakuwa mkali wewe Juma Hebu amkia........

Kwa kweli hii hali ikiendelea hivi tutamjua mwanaume maana imefikia hatua mtu ukifanikiwa kula Milo mitatu unajipongeza.........
 
Jamani huko mliko nyie wenzangu vipi? Huku naona kama kipa katoka,ngoma ngumu sana! Ile milo mitatu kwa siku imekua kwa mbinde sana..hebu fikiria yale mahitaji muhimu ya mwanadamu bado kwetu ni tatizo..

Hatuli vizuri,hatuvai vizuri, na mbaya zaidi hatulali pazuri...kuna kundi kubwa la watu wanarudisha mpira kwa kipa(wanarudi kijijini)...mijini hakukaliki,kila siku afadhali ya jana!

Biashara haziendi ,mikopo hailipiki madeni kila kona...stress tupu...hivi kwa hali hii nguvu za kiume zinatoka wapi? Usiku usingizi hauji ni kuwaza tu..hata hamu ya kula "chakula cha usiku" utaitoa wapi? Barabarani unapishana na mtu anaongea peke yake..

Hebu tupeane mbinu wakuu,wale wanaokesha kitambaa cheupe na kule bandarini kila siku meli zinaleta magari wanafanyaje? Yaani kama adhabu kumbe ndio maisha yenyewe.
Yaendelee tu kuwa magumu ilimkome kuchagua viongozi wasiojali maslahi ya wananchi
 
Back
Top Bottom