Maisha ni fomula ya ulimwengu ikiwemo kupata au kukosa

Maisha ni fomula ya ulimwengu ikiwemo kupata au kukosa

dmkali

JF-Expert Member
Joined
Nov 17, 2014
Posts
11,793
Reaction score
22,552
Habari za asubuhi ndugu na marafiki!

Kupevuka kiakili ni kuyajua ya Ulimwengu!

Dini karibu zote pia zinatumia sehemu ya formula. hii ya Ulimwengu ambayo kuijua siyo lazima usali dini zilizokuja afrika kwa majahazi na meli!

Nitaufupisha Uzi huu kwa maelezo machache kwani somo hili ni pana sana kulielezea kwenye Uzi mmoja!

Ninaposema maisha ni formula maana yake kuzaliwa ni formula, kukua ni formula, kupata ni formula, kukosa ni formula, kuoa/kutoolewa ni formula, kufa ni formula n.k
Kuna watu ukiwaambia mambo haya hukejeli nakusema ni uwongo, huwa sibishani nao kwasababu wanakuwa hawajapevuka kiakili bado!

Mfano! Kila mtu anapozaliwa hutakiwa kuishi msingi maalum wa fomula ambao ni msingi wa mafanikio yake, mathalani Mtu anazaliwa akiwaamepangiwa fomula kwamba hatakiwi avuke daraja fulani la elimu ili afanikiwe lakini yeye kwa kutokujua anafeli mara ya kwanza lakini anarudia tena na tena!

Lakini kwakuwa formula ya ushindi ina siku na saa maalum kwa ajili yake inapotokea anashinda ili kupanda daraja la juu lazima huko mbeleni hafanikiwi kwa daraja la juu bali linalompa ushindi na kula yake ni lile la chini kabisa!
Mfano msanii flani wa tandale angekomaa na shule asingetoka!

Formula ya Ulimwengu ilikuwepo tangu Ulimwengu! Hii formula ndiyo ilitumiwa na watu wa kale kuishi, wajanja wakaigeuza na kujimilikisha kama sehemu ya dini na ibada! Lakini hata hivyo hawaitimizi kama inavyopaswa kuwa!

Formula ya Ulimwengu ni ngumu na inahitaji moyo mgumu sana kuifuata na machoni inaweza kuonekana kuwa na matokeo ya kikatili sana!
Mfano! Muda wako kupokea hela unaweza ukawa umepangwa kwamba siku na saa! Lakini hutakiwi kujamiiana saa kadhaa kabla, unalala vizuri na mkeo ukimgusa mapema anasogea ukutani, ajabu saa kumi na mbili asubuhi muda wa kuwahi dili lako ghafla anaanza kukutega na kutaka mfanye! Ukiingia mkenge ukafanya unakuwa umekiuka fomula ukienda kwenye dili lako unakuta aliyetakiwa kukupa pesa anakwambia kapata dharula kubwa ghafla (kumbe ni fomula umekosea)

Nitawapa mfano. Mwingine wa kijinga!
Kuna baadhi ya wanaume wanaweza kushuhudia kuwa anapotoka kufanya ngono na mwanamke mmoja ni rahisi sana kukubaliwa na mwingine endapo atatongoza ndani ya lisaa lile lile hahah hapo nimetania wanaume msilibebe!

Ukiona familia zinasherekea harusi nyingi Mara kwa mara formula inasema familia hiyo wako mbioni kukusanyika kwa msiba siku si nyingi (ni formula)

Ukiona ndoa imesambaratika vipande hiyo siyo wao bali ni formula inakuwa imewatawanya kwa maslahi yao kwa amani la sivyo wakikomaa hakuna kitachofanyika na zaidi inaweza kuwa lango la kuzimu (hii ni formula)

Ndiyo maana huwa nawaambia watu jitahidi sana kuijua siri ya formula iliyowasambaratisha kabla ya kumfanya huyo aliyekuwa kwenye ndoa kuwa wako! Ijue kwanza ndo usonge!

Naposema ndoa simaanishi lazima iwe hii ya makanisani, jiulize kwani kabla ya kuja dini huko zamani watu hawakuoana?

Haya mambo ya makanisani na msikitini ni fasheni tu ya siku hizi lakini ndoa ni kile kibari cha wazazi kwamba watoto wao wameridhiana kwenda kuishi maisha yao!

Ndiyo maana kwenye maandiko hutakaa uone kwamba (walifika kanisani au msikitini kuoana) Kikubwa imeandikwa kuwa FULANI AKAMJUA FULANI WAKAMZAA FULANI (hii ni ndoa)

Kwahiyo haya mambo ya ndoa kanisani ni mambo Leo tuliyoyaiga Mimi na wewe lakini hayaongezi kitu Bali uhalibifu kwenye formula ya Ulimwengu!

Ni mbinu za yule muovu ili kuisambaratisha dunia ili watu wasijitambue na wajione wakosefu sana kumbe hawana kosa lolote!

Hivyo ukiona mdada mzuri sana umri unakwenda hajaolewa usikurupukie rudi kwenye fomula, ukiona jamaa anapesa na mali hana mke usikurupuke kuna fomula! Ukiwa mkaidi utachokutana nacho utalia na wa kwenu kwa kuikosa fumula

Formula ya Ulimwengu inataka umakini mkubwa sana hasa kwenye maamuzi makubwa!

Mfano! Taifa letu linatawaliwa kwa Awamu; Awamu ya kwanza ni nguvu ya uanzilishi, ya pili,ya tatu....lakini Awamu ya tano ni ya mwendo na mbiyo nyingi lakini siyo salama!

Magari mengi na ajali nyingi hupatikana kwenye gia namba tano! Rais wetu alikufa akiwa madarakani kwenye kasi awamu ya tano!
Utawala wa Sita ni mwanzo mwingine ni utawala wenye kasi ndogo lakini imara sana ni kama gari inapoanza mwendo!

Hivyo kwa fomula ya Ulimwengu Awamu ya sita mambo yatakwenda taratibu sana hadi kuja kuchanganya tena ni mpaka huko awamu ya nane,tisa ambapo kwasababu kutakuwa na katiba mpya! Utawala wa awamu ya kumi utakuwa na kasi kubwa sana ya maendeleo lakini nao utasambaratishwa kwa maamdamano ya wapinzani kwasababu wakati huo katiba itakuwa inaruhusu mambo hayo na majeshi yatakuwa huru!

Mfano kuna watu huwa wanasema majeshi yetu hasa vitengo vya polisi, PSU n.k kwamba vina watu wa kawaida kwasababu kwenye media wanaotokeza wanaongea kawaida!

Lakini ukweli kwa ndani kabisa tembelea hapo makao makuu ya majeshi, makao Jwtz , ngerengere, intapol n.k unakuta kuna watu ni vichwa balaa! Yaani wamebobea kiasi unajiuliza Huyu angekuwa mkuu mambo yangenyooka! Lakini tatizo fomula ya Ulimwengu haimtaki!

Jana mapema kabla ya mechi niliweka Uzi humu ukielezea vile Argentina watautwaa ubingwa kwa msaada wa nguvu ya Ulimwengu iliyokuwa imefichwa kwenye masaa,tarehe, siku na mwaka!
Masaa ya ushindi wa ARGENTINA yalikuwa ni yale tu yanayogawanyika kwa mbili, saa 12 jioni huko ulaya na amaerika nguvu ya Ulimwengu ilikuwa inatoka ulaya kwenda amerika! (Ni kama mteremko)

Ndiyo maana ilipofika saa moja upepo ulibadilika maana nguvu ya upepo iligeuka kwakuwa masaa ya nguvu kwa ufaransa ilikuwa saa moja, tatu na tano kwa tarehe ya jana ( siyo kila siku) ilipofika saa 2 kamili upepo ukarudi tena amerika kusini! Hapo wafaransa hata kama golikipa wa argentina angetoka golini wasingeshinda!

Nguvu ya Ulimwengu ndo nguvu kubwa kuliko zote!
ukiijua fomula ya Ulimwengu hutaumizwa, ni rahisi kutegua mtego, ni rahisi kufanya maamuzi kwa wakati sehemu sahihi!
Hujawahi kujiuliza kwanini kuna kipindi vichaa wanakuwa wengi na kuna wakati wanapungua?

Kuna tarehe ambazo hutakiwi kabisa kuanzisha au kwenda kwenye vita na ukitia mguu unapasuka!

Unaweza kushangaa kabisa bondia mkubwa na baunsa mkubwa akapigana na mtu mwenye mwili kama mkurugenzi wa JF #melo na akamdunda! Watu wasielewe Melo kashindaje!

Kumbe anakuwa kapiga kwa msaada wa nguvu ya Ulimwengu

Somo hili litaendelea! Maisha ni fomula kupata au kukosa ni fomula!
 
umeandika sana.
maisha yapo hivi ! Mtaji wa maskini nguvu zake mwenyewe. kwa hiyo chagua nguvu gani itakayotumika kama ni kuzurumu,kuiba,jitihada,ubabe,utapeli na mengine
 
Tuelezee hizi namba zinafanya vipi kazi na kwanini ?
Maana uliyoyaandika inaonesha kila kitu Ni namba na maisha yetu yapo katika Mfumo huo.
 
Unayoseman kweli , mfano mtuu anakataasafr gafla au anakubali ajar inatokea
 
Chief ungerahisisha kuwa Anayejua siri za ulimwengu wa roho Anamiliki na kutawala. Mambo ya rohoni yanahitaji umakini sana kuweza kung'amua..
Eg, kuna wale watu wana vision anaweza kukwambia ndani ya siku mbili hizi naona unapata hela nyingi huku wewe hujui zitatoka wapi all over sudden ndani ya siku mbili anajitokeza mtu mnapiga dili unapata mkwanja.. hiyo ndo sir juu ya ulimwengu wa roho.

Mwingine anakwambia ndoa yenu kwenye ulimwengu wa roho haipo ogopa sana wakati ninyi mnaona mpo pamoja na maisha yanakwenda inafika huko mbeleni mambo yanakwenda mrama.

Mwingine anakwambia naona mkioana naona mafanikio makubwa mbele yenu na kweli mbele ya safari mnatoboa.

Ninakubaliana na wewe 100%
 
Wewe unaijua hiyo nguvu na formula. Eti ukiijua. Vipi baada ya kuijua imekusadia nini?
Swali lako ni kama la kawaida lakini nimependa nilijibu; ukiijua fomula ya Ulimwengu hutaumizwa, ni rahisi kutegua mtego, ni rahisi kufanya maamuzi kwa wakati na sehemu sahihi!
Hujawahi kujiuliza kwanini kuna kipindi vichaa wanakuwa wengi na wakati wanapungua?

Kuna tarehe ambazo hutakiw kwenda kwenye vita ukitia mguu unapasuka!

Unaweza kushangaa kabisa bondia mkubwa na baunsa mkubwa akapigana na mtu mwenye mwili kama mkurugenzi wa jf #melo na akamdunda! Watu wasielewe!

Kumbe anakuwa kapiga kwa msaada wa nguvu ya Ulimwengu
 
Chief ungerahisisha kuwa Anayejua siri za ulimwengu wa roho Anamiliki na kutawala. Mambo ya rohoni yanahitaji umakini sana kuweza kung'amua..
Eg, kuna wale watu wana vision anaweza kukwambia ndani ya siku mbili hizi naona unapata hela nyingi huku wewe hujui zitatoka wapi all over sudden ndani ya siku mbili anajitokeza mtu mnapiga dili unapata mkwanja.. hiyo ndo sir juu ya ulimwengu wa roho.

Mwingine anakwambia ndoa yenu kwenye ulimwengu wa roho haipo ogopa sana wakati ninyi mnaona mpo pamoja na maisha yanakwenda inafika huko mbeleni mambo yanakwenda mrama.

Mwingine anakwambia naona mkioana naona mafanikio makubwa mbele yenu na kweli mbele ya safari mnatoboa.

Ninakubaliana na wewe 100%
Umeelezea vyema sana
 
Kuna mwingine niliona wanahangaika sana hakuna fedha, ajira hakuna, uchumi mgumu mtu na mke wake. Wakaenda kwa mtu ambae aliwategulia mitego aiseeh jamaa kabla hajafika home simu za kazi zinapigwa tena anafanya aende wapi.. na yule mke wake alitamani kwenda ulaya akaambiwa na ulaya utaenda tu. Siku ya siku aunt yake yule dada akampigia simu akampa mwaliko wa ulaya. Ukiijua sir ya ulimwengu aiseeeh umetoboa.

Mwingine unaweza ona mbona sipati ajira mwaka wa 4 huu wewe unaona kawaida kumbe sio hivo kuna shida kwenye ulimwengu wa roho siku ukiteguliwa tu huo mtego zile post ulizoapply miaka miwili iliopita bahasha au Cv yako inatafutwa unapigiwa simu ya kazi..very funny lakini ndio sir za ulimwengu
 
Sawa ni eb nipe odds tatu kwanza za uhakika ili nithibitishe kama ni kweli haya usemayo
 
Back
Top Bottom