Maisha ni kuchagua: Ili kuagiza BMW 3 series cheap kabisa kutoka JP unatakiwa uwe na Mil 14, ila IST lazima uwe na angalau Mil 17!

Maisha ni kuchagua: Ili kuagiza BMW 3 series cheap kabisa kutoka JP unatakiwa uwe na Mil 14, ila IST lazima uwe na angalau Mil 17!

Mad Max

JF-Expert Member
Joined
Oct 21, 2010
Posts
26,961
Reaction score
77,890
Niliona juzi kati kunaa mdau anaulizia gari ambalo akiendesha watu wajue amejipata.

Sasa leo nikawa nafanya comparison ya kutaka kuagiza magari mawili, yote ya mwaka mmoja 2006.

BMW 3 series, 2006 generation ya E90, model 320i, ikiwa mpya 2006 iliuzwa $40,000 na leo naweza ipata kwa $930 bila usafiri na $2,800 hadi inafika Dar.
Screenshot_20241225-225905.png

Ukiileta ukakutana na TRA wao watakuomba kama Mil 6.5 tu.
Screenshot_20241225-230221.png

Kwahiyo roughly jumla Mil 14 top top umemiliki Germany machine.

Screenshot_20241225-230034.png

Toyota IST, 2006 ya engine ya 1.5L ilivyokua mpya huo mwaka 2006 iliuzwa kwa $16,000 ila leo used naipata kwa $1,600 bila usafiri na $3,200 hadi inafika Dar.
Screenshot_20241225-230320.png

TRA wao watataka Mil 8 kwahiyo ukijumlisha na Mil 8 ya kununua na malipo mengine top top ni Mil 17.

Hii mifano tu, ila inatufundisha nini?Mi naona Luxury cars zina depreciate kwa kasi ya ajabu sana. Umeona BMW imetoka $40,000 hadi $900 wakati IST imetoka $20,000 hadi $1,600!

KWa wanaonunua gari uku wakiwaza kuna kuliuza mbeleni, ili nalo la kulitazama.
 
Niliona juzi kati kunaa mdau anaulizia gari ambalo akiendesha watu wajue amejipata.

Sasa leo nikawa nafanya comparison ya kutaka kuagiza magari mawili, yote ya mwaka mmoja 2006.

BMW 3 series, 2006 generation ya E90, model 320i, ikiwa mpya 2006 iliuzwa $40,000 na leo naweza ipata kwa $930 bila usafiri na $2,800 hadi inafika Dar.
View attachment 3185154
Ukiileta ukakutana na TRA wao watakuomba kama Mil 6.5 tu.
View attachment 3185155
Kwahiyo roughly jumla Mil 14 top top umemiliki Germany machine.

View attachment 3185156
Toyota IST, 2006 ya engine ya 1.5L ilivyokua mpya huo mwaka 2006 iliuzwa kwa $16,000 ila leo used naipata kwa $1,600 bila usafiri na $3,200 hadi inafika Dar.
View attachment 3185157
TRA wao watataka Mil 8 kwahiyo ukijumlisha na Mil 8 ya kununua na malipo mengine top top ni Mil 17.

Hii mifano tu, ila inatufundisha nini?Mi naona Luxury cars zina depreciate kwa kasi ya ajabu sana. Umeona BMW imetoka $40,000 hadi $900 wakati IST imetoka $20,000 hadi $1,600!

KWa wanaonunua gari uku wakiwaza kuna kuliuza mbeleni, ili nalo la kulitazama.
Tatizo sio bei ya gari, tatizo kubwa liko kwenye service and mantainance cost za BMW vs Ist
 
Ukishaendesha gari la miaka 20 iliyopita, unlesss ni classic/vintage car, ushajionesha huna status tayari.

Ila nakuelewa Tanzania watu wengi hawajui hata model hii ya mwaka gani, kwao BMW ni BMW tu.
"Status" ndo nini katika maisha ya Tanzania ya watu maasikini wakati kumiliki tu gari haijalishi ya mwaka gani unakua katika class apart.
 
"Status" ndo nini katika maisha ya Tanzania ya watu maasikini wakati kumiliki tu gari haijalishi ya mwaka gani unakua katika class apart.
Ndiyo lakini ninachoona hapa ni kwamba kwenye wamiliki magari wenyewe wana madaraja yao wa BMW na wa Corolla si sawa.

Ni Status Anxiety tu. Ulimbukeni. Tunalimbuka bado.

Leo nilikuwa namsikikiza Paul Mashauri anasema alivyoanza kushika hela alifakamia magari kama yote akanunua Range Rover, Mercedes Benz, Land Cruiser, baadaye akajiuliza haya magari yote ya nini?

Kasema akauza yote sasa hivi anatumia Bolt.

Mo Dewji anasema alijisikia kununua Ferrari sijui Bugati, hata hajaliendesha akaona halihitaji akauza.

Ni ulimbukeni tu, lakini ni haki yao.
 
Miaka kama mitatu hivi (2020-2023) zimetrend sana kuanzia 1 series, 3, 5 na X1 aisee.
BMW gari poa sana, ila zikiwa mpya. Zikianza kukongoroka shida.

Kushobokea magari mara nyingi ni saikilojia ya mkosqji.

Home kulikuwa na Pajero Intercooler Turbo moja hivi mimi nilikuwa nishalizoea. Ila siku moja nilienda kwa rafiki yangu mmoja, dada yake aliona tangazo la biashara la hili gari, alizuzuka kama akipata hili gari atakuwa kafika mbingu gani sijui.

Wakati mimi nikishalichoka.

Nikasema kweli tunapishana.
 
Back
Top Bottom