Maisha sio magumu tumechezewa akili tu

Kuna kabila naskia bado linaishi porini hapa tz ..ebu kajaribu kuishi nao alaf ulete mrejes
*Huko Wana winda bila kibaeli

*Wana talii bila pesa/kulipia

*hawajui kuhusu Kodi za aridhi,pango,mazao,Wala jengo,

*Hawana hospital Ila Wake zao hujifungua watoto wenye afya

*wakiumwa Wanajitibu na hupona kwa mitishamba

huwezi kujiuliza jinsi gani inavutia na kushangaza?
 
Tengeneza maji yako,tengeneza umeme wako,hospitali yako na shule yako
1)utafungwa kwa kuihujumu mamraka ya maji tz
2)utafunfugwa kwa kuwa hujumu tanesco
3)utafungwa kwa kuamini ushirikina
4)uta fungwa kwa kuenda kinyume na mitaala ya elimu ya inchi
 
Kichwa cha uzi na maelezo haviendani

Ulichoandika ni nonsense na hakina uhalisia na dunia ya sasa.
Dunia Ni Ileile na hiyo Sasa niwewe

kumbuka dunia inaweza kuishi bila wewe Ila wewe hauwezi kuishi bila

dunia kwahiyo jaribu kunisoma kwa hakiri za kuzaliwa sio za kukalilishwa/darasanišŸ™šŸ™
 
Mkuu uko sawa lakini si sawa
Mfano hiyo pampu ya kusukuma maji ni ubunifu wa mtu haikushushwa ujue,
Uendeshaji wake ni gharama kwa hiyo kuchangia ni muhimu mkuu
 
Mkuu uko sawa lakini si sawa
Mfano hiyo pampu ya kusukuma maji ni ubunifu wa mtu haikushushwa ujue,
Uendeshaji wake ni gharama kwa hiyo kuchangia ni muhimu mkuu
Mtoa mada anamaanisha mfano sisi watu wa DSM wote Milioni 6.5 kilasiku tukisikia kiu tupige mguu mpaka mto RUVU tunywe maji na kuoga then tunarudi DSM.
 
Umaskini ni wakutengenezwa , watu wanatumia trillion of money kuchochea vita huku kuna watu wana njaa .

Sheria za dunia ili umaskini uendelee kuna sheria ya aliye nacho aongezewe .
 
Umaskini ni wakutengenezwa , watu wanatumia trillion of money kuchochea vita huku kuna watu wana njaa .

Sheria za dunia ili umaskini uendelee kuna sheria ya aliye nacho aongezewe .

Ukisoma uchumi hauna uhalisia , mambo kama riba ni njia kandamizi za kitapeli kupitia mabank.
 
Hakuna cha bure duniani. Hata porini kwenye vya bure kwamba maji utayakuta mtoni ila gharama yake ni kupigana na mamba.

Unapozaliwa na kuikuta jamii yako ipo kuna nyumba za kuishi, hukimbizani na fisi wako huko porini, kuna hospitali na mashule havijaja tu, kuna watu wamefanya kazi kubwa vikawepo hapo huwezi pewa tu bure. Wewe umeleta nini?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…