Maisha ya Afrika Kusini siyo poa

Maisha ya Afrika Kusini siyo poa

Nishazika washkaji wawili na mmoja alikuwa kama uncle wangu walikuwa huko south ila madogo hawa wengi mtaani hamna mtu wako uko yaani wako zaidi ya miaka 4 ila hWana kitu zaidi ya kushare nguo na kupost Instagram na fb.

Kuna wachache wakubwa walirudi miaka ya 2005 mpaka 2010 walikuwa na mitaji sasa wanaishi bongo na biashara zao..

Uchungu mmoja alirudi kawa teja kabisa sema kitaa walimlea sana mwaka 2017 katikati alichomwa moto mtaa wa jirani aliiba.

Wapo mabrodas wako huko wananiambia dogo usije ukaja huko sisi kwenye game tuko zaidi ya miaka 20 ila ngoma bado bila bila wanaona hata aibu kurudi bongo kuanza upya ila kimtindo wanasaidia wazazi wao maana washashusha hiace kadhaa zinakula vichwa town ,na Yale maboma ya wazazi wao washayakarabati ni nyumba safi ila bado Maisha ya kusave wnaaona ni Soo zaidi familia hawana wamezaa na madanga kila kona.
Hii ni true stori [emoji2] ina chekesha na ina sikitisha sana. [emoji24] ila ni life tu
 
Wakati nnaishi Sauz! Ata Police walio Off wanatembea wawiliwawili- Kuna siku tulimwalika mmoja kwenye part akaja na mwenzake ambae nae yupo off! Nilipokuwa naongea nao waliniambia kuwa wahalifu wanaowakamata mara nyingi ata kama bado awajafungwa kesi zao zinaendelea mahakamani huwavizia na kuwaua. Pale kila mmoja wao alikuwa na Bastola full loaded . Hospital za South zina askari geting pamoja na Detekta za silaha, Wakikukosa kukuhuwa Kitaa, wanakuja hospital kukumaliza[emoji24]. Kuna mitaa kutolewa Bunduki ni kawaida, Malaya kukuuza kwa Majita kama umejionyesha wewe unazo ni kitu cha kawaida.Siku moja Dogo alikuwa anatoka Super market ambayo ni kama Nusu KM. Mpaka anafika tunapokaa amekabwa mara sita na makundi tofauti tofauti ya vibaka[emoji1787] Kundi la sita walimkuta amebakiwa na pipi kifua tu.
Hivi hayo makundi yanayo kaba ni ya wazawa wa Sauzi au ni wageni wanao jitafuta ku make money nahitaji kujulidhwa hilo maana wanasemaga wenyeji wanachukazi kazi zao
 
Usijidanganye kwenda bondeni kutafuta maisha kama huna msingi, wala kibali. Kama unaweza kulipa nyumba Milioni kwa mwezi hapa Tanzania basi unaweza kuishi huko.

Kama unaweza kuishi Masaki na Mbezi beach basi unaweza kuishi huko sababu tabia za huko mazoea ya uswahilini hakuna, ukiweza kuishi South Africa na ndio umeweza kuishi nchi yoyote iliyopo Ulaya na pengine.

South Africa gredi ya uhalifu ni kubwa sana, kesi za kufa watu zipo nyingi kuliko kesi nyengine, ingekuwa tz kila siku kamanda wa polisi anatangaza mwisho hata choka.

Ngono kule ni kitu cha kawaida yani unatongoza mchana usiku unapewa, sio huku kwetu mpaka uchunwe kwanza.

Ukiwa na misosi ya kutosha na nyumba utachagua wanawake mpaka UKIMWI ukufikie, wanathamini kula sana maana maisha magumu kwao. Wezi, wauza madawa, wakwepa kodi na n.k wanaogopa kuweka pesa zao benki sababu benki za huku ni kama TRA kukuchunguza, Rais Ramaphosa ni mfano tosha.

Wizi wa magari ni kama wizi wa simu, gari nyingi zinazoingia hapa kwetu nyingi za wizi zinatoka huko. Vigogo wakubwa na wauza ngada hapa Tz wanaishi huko au kuwa na makazi ni wengi tu.

Msidanganye na wasanii wanasema wamenunua nyumba bali kule nyumba unaweza kununu tena nzuri ila ni kama umekodi, tofauti ya tanzania ardhi ina bei utadhani unanunua madini.

Kuvamiwa ni jambo la kawaida, wezi wakule usumbufu hawataki unaenda kwa order ukileta ubishi ni kugusa kaburini.

Huwezi kuchezea simu ovyo maana mitaa yote kuna wahalifu usipo kuwa makini unaweza kuona benzi kali inapita kumbe wapo wezi, ukifika nyumbani kama kuna geti lazima uchunguze mbele na nyuma nani anakufata ijalishi gari au mtembea miguu na hatua kidogo kabla ujafika getini, unaingia nao.

Vijana wetu waliozamia ukiona kaenda karudi katoboa maisha, mawili ni mchomoko au madawa.

Mchomoko ni kuvizia nyumba wenyewe hawapo tena nyumba hizi kama nilivosema wanaoweka pesa za kutakatisha.

South sio poa.

Dah eti wez hawatak usumbufu.. yaan univamie kwangu mali/pesa zangu alafu useme hutak usumbufu nisibishane nitii Amri

Dah sio poa
 
Dah eti wez hawatak usumbufu.. yaan univamie kwangu mali/pesa zangu alafu useme hutak usumbufu nisibishane nitii Amri

Dah sio poa
Wana bunduki na ni full zimejaa risasi uta miminiwa za kitosha na hela mali zako zitaenda sasa hapo utachagua mwenyewe upotezwe na mali zako zipotee au mali ziende wewe ubaki kazi kwako [emoji3064] kule hawatanii kama huku kwetu
 
Nafikilia kuanzisha Uzi hapa kuzungumzia nguvu ya hizi numbers kwenye Maisha ya kila siku ya SA, Mitaani na Gerezani...!

26 ni Gang crew, kama ilivyo 27 na 28, hizo numbers zina nguvu sana Gerezani, Maisha yako yatakua ya dhiki kubwa kama ukienda Jela hafu ukawa sio member wa hizo numbers, japo huku Mtaani number zinageuka na kuwa na Majina ya Crew, miongoni mwa kundi Hatari na kubwa hapa Cape town, ni Americano, Mongolos, Yankees, School Boy etc.

Hawa wanauana dairy kwa kutafuta himaya ya kuuza Madawa, Wanaiba, wanakaba mtaani na kila aina ya Ufedhuri, Mf. Ndani ya Americano kuna 26, 27 na 28 wanapambana na Mongolos yenye 26, 27 na 28 pia, ila wakienda Jela, hakuna Americano, hakuna Mongolos wala majina mengine, ila wanaishi pamoja kwa numbers zao!
Japo kwenye Jela moja kubwa inaitwa Possmall, kuna mtu hatari sana, anamiliki Number 28 anaitwa John Mongol, ambaye ndo mwanzirishi wa kundi la Mongolos ambalo linasebenza Mtaani, huyu Mtu ni mtu ambaye sio mtu mzuri hata ukimtizama.

Wana salamu zao za ishara, means mtaani mtu akikusalimia unajua huyu ni 26, 27 au 28, wanaenda mbali wana Lugha yao wanaelewana wenyewe, inaitwa Sabela, hakuna mtu anaelewa hiyo Lugha zaidi yao wenyewe.

Member wa kundi lolote hajakukaba au kukuibia mpaka ajitamburishe kuwa yeye anamiliki number ipi, atapiga mguu chini, salamu ikiambatana na Kujitamburisha kwake kwako na Lugha yao ya Sabela, kama wewe unamiliki namba pia means utajibu na yeye atajua huyu ni mwenzagu, kama katika kusalimiana anatambua wewe ni mkubwa kuliko wewe, atapiga Saluti, otherwise, utaenda kuhadithia Nyumbani.
(Wako vyeo vyao ambavyo wanajichora kama Tatoo)

26- Ni Watu watafutaji pesa, Brothermen wanapenda kupendeza na wanajua kutafuta pesa.

27. Ni Wauaji straight, akipewa Amri akuue, harudi nyuma, mpaka akuue, na ni mbaya kama amri ikitoka Jela, coz asipokuua atauwawa yeye, na yeye hawezi kukubari kufa kwa ajiri yako. Kuua kunampa Cheo zaidi kwenye Crew aliyopo.

28. Wanajihusisha na Mapenzi hata ya jinsia Moja, lakini pia anaweza kuua....

Hawa ndo wanaifanya SA iwe na Ushenzi tunaousikia, Hawa wanauza Madawa straigjt kwa watu wao, lipo kundi moja lipo Cape town, town kabisa, linaitwa UnderWorld Cape gang, hili kundi lina Connection mpaka na makundi Makubwa ya kuuza Unga toka Latin America, linaingiza madawa Cape town tokea Brazil....!

Sawa Wabongo wanauza madawa, na Wanigeria pia, ila Wabongo wengi na Wanigeria wengi ni kama Machinga wa madawa mbele ya hawa Raia wa Kirangirangi.

Wageni wanaofanya kazi halali ni wengi kuliko wanaofanya Mazabe.
Daaah mzee una nondo nzito sana [emoji23] uliwahi kuishi bondeni nini.. story yako ina vutia sana msomaji na shangaa ghafla tu imekata.
 
Nimesoma uzi wote,aisee..... nimejifunza kutokana na komenti kuwa sehemu za blacks,kuna rate kubwa ya uhalifu,ngono ni rahisi na ukimwi upo wa kutosha na mengineyo.
 
Mwizi jambazi ni mtu anaeomba kuuwawa so kumuacha hai ni kumkosea MUNGU. Mwizi na mchawi hawana adhabu nyingine zaidi ya kupewa haki yao ya kifo.
Mchawi? Ndio nyinyi mnaua vikongwe kwa imani za kishirikina ,uwa mwizi ,ua jambazi achana na imani za kufikirika ambazo hazipo

Sent from my Infinix X6517 using JamiiForums mobile app
 
Usijidanganye kwenda bondeni kutafuta maisha kama huna msingi, wala kibali. Kama unaweza kulipa nyumba Milioni kwa mwezi hapa Tanzania basi unaweza kuishi huko.

Kama unaweza kuishi Masaki na Mbezi beach basi unaweza kuishi huko sababu tabia za huko mazoea ya uswahilini hakuna, ukiweza kuishi South Africa na ndio umeweza kuishi nchi yoyote iliyopo Ulaya na pengine.

South Africa gredi ya uhalifu ni kubwa sana, kesi za kufa watu zipo nyingi kuliko kesi nyengine, ingekuwa tz kila siku kamanda wa polisi anatangaza mwisho hata choka.

Ngono kule ni kitu cha kawaida yani unatongoza mchana usiku unapewa, sio huku kwetu mpaka uchunwe kwanza.

Ukiwa na misosi ya kutosha na nyumba utachagua wanawake mpaka UKIMWI ukufikie, wanathamini kula sana maana maisha magumu kwao. Wezi, wauza madawa, wakwepa kodi na n.k wanaogopa kuweka pesa zao benki sababu benki za huku ni kama TRA kukuchunguza, Rais Ramaphosa ni mfano tosha.

Wizi wa magari ni kama wizi wa simu, gari nyingi zinazoingia hapa kwetu nyingi za wizi zinatoka huko. Vigogo wakubwa na wauza ngada hapa Tz wanaishi huko au kuwa na makazi ni wengi tu.

Msidanganye na wasanii wanasema wamenunua nyumba bali kule nyumba unaweza kununu tena nzuri ila ni kama umekodi, tofauti ya tanzania ardhi ina bei utadhani unanunua madini.

Kuvamiwa ni jambo la kawaida, wezi wakule usumbufu hawataki unaenda kwa order ukileta ubishi ni kugusa kaburini.

Huwezi kuchezea simu ovyo maana mitaa yote kuna wahalifu usipo kuwa makini unaweza kuona benzi kali inapita kumbe wapo wezi, ukifika nyumbani kama kuna geti lazima uchunguze mbele na nyuma nani anakufata ijalishi gari au mtembea miguu na hatua kidogo kabla ujafika getini, unaingia nao.

Vijana wetu waliozamia ukiona kaenda karudi katoboa maisha, mawili ni mchomoko au madawa.

Mchomoko ni kuvizia nyumba wenyewe hawapo tena nyumba hizi kama nilivosema wanaoweka pesa za kutakatisha.

South sio poa.
Tuliowahi kuishi huko tunaafiki na uliyoyasema. Hilo la kuingia ndani ya nyumba ni muhimu sana. Nyumba nyingi mageti hufunguliwa na kufungwa kwa remote control kuepukana na wezi wanaoweza kukufuatilia nyuma. Adha niliyoipata kule ni kuwa jitahidi kuwa nyumbani mapema kabla ya jua kuzama. Baada ya hapo usije ukajilaumu. Hapo nazungumzia Joburg.
 
Crime rate hapo SA sio poa
Kwa jinsi Wazulu walivyo makatiri, wanakupiga kabari ya "form four" waziwazi kabisa na jua linawaka, wakati huo polisi wanatizama upande wa pili kana kwamba hawajaona kitu kabisa. Kiukweli Tshaka aliwapa ujasiri hatari sana, hakikisha unarudi na assegai yako, ukirudi mikono mitupu basi kifo ni juu yako.
 
south Africa sehemu ambayo sio salama ni kwa mablacks tu, ukienda maeneo ya wazungu kupo salama sana.
Wanaopiga mchomoko wanavizia huko nyumba za wazungu ndio kuna hela, kote hakufai south sio salama, juzi rafiki yangu polisi south anarudi home wamemkaba kaleta ubishi wakamshtua na risasi ya mkono
 
Wanaopiga mchomoko wanavizia huko nyumba za wazungu ndio kuna hela, kote hakufai south sio salama, juzi rafiki yangu polisi south anarudi home wamemkaba kaleta ubishi wakamshtua na risasi ya mkono
Acha uongo.
Mimi naishi mitaa ya wazungu hapa Cape Town, sijawahi kusikia tukio lolote la uhalifu. Usalama ni 200%.
Screenshot_20240514-000622.jpg
 
Daaah mzee una nondo nzito sana [emoji23] uliwahi kuishi bondeni nini.. story yako ina vutia sana msomaji na shangaa ghafla tu imekata.
Aisee ni kisanga mwanangu yaani kuna maujuzi tuna oewa humu ni balaaa 😂🤒
 
Back
Top Bottom