tafadhali nifafanulie khs 26 group
Nafikilia kuanzisha Uzi hapa kuzungumzia nguvu ya hizi numbers kwenye Maisha ya kila siku ya SA, Mitaani na Gerezani...!
26 ni Gang crew, kama ilivyo 27 na 28, hizo numbers zina nguvu sana Gerezani, Maisha yako yatakua ya dhiki kubwa kama ukienda Jela hafu ukawa sio member wa hizo numbers, japo huku Mtaani number zinageuka na kuwa na Majina ya Crew, miongoni mwa kundi Hatari na kubwa hapa Cape town, ni Americano, Mongolos, Yankees, School Boy etc.
Hawa wanauana dairy kwa kutafuta himaya ya kuuza Madawa, Wanaiba, wanakaba mtaani na kila aina ya Ufedhuri, Mf. Ndani ya Americano kuna 26, 27 na 28 wanapambana na Mongolos yenye 26, 27 na 28 pia, ila wakienda Jela, hakuna Americano, hakuna Mongolos wala majina mengine, ila wanaishi pamoja kwa numbers zao!
Japo kwenye Jela moja kubwa inaitwa Possmall, kuna mtu hatari sana, anamiliki Number 28 anaitwa John Mongol, ambaye ndo mwanzirishi wa kundi la Mongolos ambalo linasebenza Mtaani, huyu Mtu ni mtu ambaye sio mtu mzuri hata ukimtizama.
Wana salamu zao za ishara, means mtaani mtu akikusalimia unajua huyu ni 26, 27 au 28, wanaenda mbali wana Lugha yao wanaelewana wenyewe, inaitwa Sabela, hakuna mtu anaelewa hiyo Lugha zaidi yao wenyewe.
Member wa kundi lolote hajakukaba au kukuibia mpaka ajitamburishe kuwa yeye anamiliki number ipi, atapiga mguu chini, salamu ikiambatana na Kujitamburisha kwake kwako na Lugha yao ya Sabela, kama wewe unamiliki namba pia means utajibu na yeye atajua huyu ni mwenzagu, kama katika kusalimiana anatambua wewe ni mkubwa kuliko wewe, atapiga Saluti, otherwise, utaenda kuhadithia Nyumbani.
(Wako vyeo vyao ambavyo wanajichora kama Tatoo)
26- Ni Watu watafutaji pesa, Brothermen wanapenda kupendeza na wanajua kutafuta pesa.
27. Ni Wauaji straight, akipewa Amri akuue, harudi nyuma, mpaka akuue, na ni mbaya kama amri ikitoka Jela, coz asipokuua atauwawa yeye, na yeye hawezi kukubari kufa kwa ajiri yako. Kuua kunampa Cheo zaidi kwenye Crew aliyopo.
28. Wanajihusisha na Mapenzi hata ya jinsia Moja, lakini pia anaweza kuua....
Hawa ndo wanaifanya SA iwe na Ushenzi tunaousikia, Hawa wanauza Madawa straigjt kwa watu wao, lipo kundi moja lipo Cape town, town kabisa, linaitwa UnderWorld Cape gang, hili kundi lina Connection mpaka na makundi Makubwa ya kuuza Unga toka Latin America, linaingiza madawa Cape town tokea Brazil....!
Sawa Wabongo wanauza madawa, na Wanigeria pia, ila Wabongo wengi na Wanigeria wengi ni kama Machinga wa madawa mbele ya hawa Raia wa Kirangirangi.
Wageni wanaofanya kazi halali ni wengi kuliko wanaofanya Mazabe.