Maisha ya Afrika Kusini siyo poa

Maisha ya Afrika Kusini siyo poa

Wengi ni wageni... especially dirty and armed robbery.

Kwani Kuna nchi isiyo na wahalifu? Jibu ni hakuna. Hivyo hata Wasouth wahalifu wapo.

Sasa tunajadili kwanini imekuwa kwa kiasi hicho hapo SA...

Mitanzania inatoka Kariakoo haijui inaenda kufanya nini SA! Kwasababu ya soko la ajira kubana ... for the survival wanaengage kwenye uhalifu.... Hao ni wabongo tu Kuna Mikenya, Nigerians, Zimbabweans... kila nchi ipo SA.
Nakubaliana na ww, wahuni wengi wilaya ya temeke wamekimbilia south. ..ninao wajua ni zaidi ya kumi.
Mbagala ndio usiseme wanaanza na kazi ya bodaboda then wanauza pikipiki za maboss na kukimbilia south.
Wakifika huko wanapokelewa na wahuni wenzao walioko huko muda mrefu
 
Shida ni income disparity-Nelson Mandela watu wanamuona shujaa kutokana na kuwakumbatua makaburu lakini kwa sisi wabobezi wa mambo hapo ndio tunaona alichemka.

S.A means of production zote zina milikiwa na makaburu na mbaya zaidi wameenda mpaka level ya chini-unategemea watu wako wataishi vipi?

Hata hapa Tanzania ni bahati tu kuwa ardhi getu ni mkubwa kuliko population tuliyonayo-subiri baada ya miaka 30-50 ijayo hiyo crime rate ya South itakuwa cha mtoto.
Mkuu tukiiongelea Tanzania ni hivi
Madini yanamilikiwa na nani,mbuga, gas
Hizo resources za Tanzania ni mali ya wazungu na zinawafaidisha wao na nchi zao na yote ni kwaakili mbovu ya ngozi nyeusi tu
South Afrika wana bahati kwa kuwa wazungu wanachangia pato la palepale na hela wanairudisha kwenye mzunguka wa palepale
Kuna huduma zote muhimu za kijamii kwa uhakika kabisa ni kazi ya wazungu hiyo

Wangekuwa Tanzania tungefaidika pakubwa sana na resources zetu na hata tusikuwa na njaa badala yake tungekuwa tunauza chakula nje kwa uhakika kabisa

South Afrika baadhi ya wazungu wanaofanya kazi sehemu za weusi huomba kuacha kazi au kubadilishwa vituo kutokana na urasimu wa ngozi nyeusi wanashindwa kufanya nao kazi
Kwa sasa kwenye serikali mambo ni hivyo sana
Kwa sababu wenye maamuzi zaidi ni weusi
Mfano makampuni ya kulisha wafungwa watu wanakula percent
huko majela kwa sasa hali ni mbaya tofauti na zamani
wafungwa hawapati huduma nzuri kama zamani, mtaani ni kawaida kukuta taka zinakaa hata wiki tofauti na zamani
Zikitokea ajali ilikuwa dakika tano hazifiki bila huduma kuja (kwenye majiji) kwa sasa mambo ni hovyo sana
Sababu madaraka ngozi nyeusi
BIG UP MADIBA angalau kwa kuwakumbatia hao jamaa na kujua umuhimu wao
 
South Africa idadi ya security guards (walinzi) ni over 2.4 million. Imagine. Walinzi wamewazidi polisi kwa namba ya mbali mno na bado wanakuambia kuna uhitaji sana.

Hili tu linatosha kukuonyesha kuna hali gani.
Alafu bora ukamatwe na polisi kuliko hao jamaa
 
Nimekaa 4 yrs. Nilifikia Hillbrow then Sunyside Pretoria kisha Sandton. So napajua South Kuliko Maelezo. Hillbrow nilikuwa nakaa Flamingo Hotel Jengo la Tatu toka Mnara unaoitambulisha Johanesburg. Kanisa nililokuwa Nasali hizi ndo picha za baba Askofu wetu

[emoji102][emoji30]
 
Nafikilia kuanzisha Uzi hapa kuzungumzia nguvu ya hizi numbers kwenye Maisha ya kila siku ya SA, Mitaani na Gerezani...!

26 ni Gang crew, kama ilivyo 27 na 28, hizo numbers zina nguvu sana Gerezani, Maisha yako yatakua ya dhiki kubwa kama ukienda Jela hafu ukawa sio member wa hizo numbers, japo huku Mtaani number zinageuka na kuwa na Majina ya Crew, miongoni mwa kundi Hatari na kubwa hapa Cape town, ni Americano, Mongolos, Yankees, School Boy etc.

Hawa wanauana dairy kwa kutafuta himaya ya kuuza Madawa, Wanaiba, wanakaba mtaani na kila aina ya Ufedhuri, Mf. Ndani ya Americano kuna 26, 27 na 28 wanapambana na Mongolos yenye 26, 27 na 28 pia, ila wakienda Jela, hakuna Americano, hakuna Mongolos wala majina mengine, ila wanaishi pamoja kwa numbers zao!

Wana salamu zao za ishara, means mtaani mtu akikusalimia unajua huyu ni 26, 27 au 28, wanaenda mbali wana Lugha yao wanaelewana wenyewe, inaitwa Sabela, hakuna mtu anaelewa hiyo Lugha zaidi yao wenyewe.

Member wa kundi lolote hajakukaba au kukuibia mpaka ajitamburishe kuwa yeye anamiliki number ipi, atapiga mguu chini, salamu ikiambatana na Kujitamburisha kwake kwako na Lugha yao ya Sabela, kama wewe unamiliki namba pia means utajibu na yeye atajua huyu ni mwenzagu, otherwise, utaenda kuhadithia Nyumbani.

26- Ni Watu watafutaji pesa, Brothermen wanapenda kupendeza na wanajua kutafuta pesa.

27. Ni Wauaji straight, akipewa Amri akuue, harudi nyuma, mpaka akuue, na ni mbaya kama amri ikitoka Jela, coz asipokuua atauwawa yeye, na yeye hawezi kukubari kufa kwa ajiri yako. Kuua kunampa Cheo zaidi kwenye Crew aliyopo.

28. Wanajihusisha na Mapenzi hata ya jinsia Moja, lakini pia anaweza kuua....

Hawa ndo wanaifanya SA iwe na Ushenzi tunaousikia, Hawa wanauza Madawa straigjt kwa watu wao, lipo kundi moja lipo Cape town, town kabisa, linaitwa UnderWorld Cape gang, hili kundi lina Connection mpaka na makundi Makubwa ya kuuza Unga toka Latin America, linaingiza madawa Cape town tokea Brazil....!

Sawa Wabongo wanauza madawa, na Wanigeria pia, ila Wabongo wengi na Wanigeria wengi ni kama Machinga wa madawa mbele ya hawa Raia wa Kirangirangi.

Wageni wanaofanya kazi halali ni wengi kuliko wanaofanya Mazabe.
Bila kuwataja Pagad bado hujui historia ya Cape town na mtandao wa madawa.
 
Bila kuwataja Pagad bado hujui historia ya Cape town na mtandao wa madawa.
Sasa Pagad sio Wauzaji wa Madawa, Pagad sio Gang Crew, Pagad ni Waislam ambao waliamua kupambana na hayo Magenge ya Kihuni, Member alikua anauliza kuhusu 26, nikaamua nipe info japo kwa uchache kuhusu hizo number, hakukuwa na sehemu ningeweza kuwazungumzia Pagad, labda siku nikizungumzia Historia ya haya Makundi, then Pagad wana nafasi ya kuzungumziwa.
 
Nipo Eastern cape kuna mdada kapata tuzo ya ubunifu device ya kukamata wabakaji....kama ushaona Watoto wa shule wa SA wanavyovaa,pia sheria inaruhusu MTU mzima Ku consent kingono na binti wa miaka 16,chini ya hapo Kosa kisheria..

Inasikitisha sana,,,ila Wanawake wasouth yale maumbo yao Mashallah na wanavyopenda kuvaa uchi sasa Yan hadi wanafunzi sijui kama ubakaji utaisha kule
 
Nimeishi Johannesburg soweto, huko wanakoishi Wazulu Og, najua Life style ya Johannesburg,, nimeishi Broemfonteen - free state, huko wanapoishi Wasuthu Og mixer na Warangirangi, na hivi naandika hii comment nipo Cape town - Mitchell plain....!

Naweza kutoa uhalisia wa Maisha ya Dzonga coz nimeishi Majimbo 3 tofauti, watu hapa mnatoa Uhalisia wa South africa kwa kile uliona tu Hillbrow.....!
Mnalaumu tu Wageni wageni, hivi mnajua namna Gangstars groups 26, 27 na 28 zilivyochangia kuvuruga Maisha ya South Africa?
Na 99.9% of Gang members ni Raia.
Nakubaliana n ww kiongozi.
Mapambano yaendelee
Tunachokijua:
 
Shida ni income disparity-Nelson Mandela watu wanamuona shujaa kutokana na kuwakumbatua makaburu lakini kwa sisi wabobezi wa mambo hapo ndio tunaona alichemka.

S.A means of production zote zina milikiwa na makaburu na mbaya zaidi wameenda mpaka level ya chini-unategemea watu wako wataishi vipi?

Hata hapa Tanzania ni bahati tu kuwa ardhi getu ni mkubwa kuliko population tuliyonayo-subiri baada ya miaka 30-50 ijayo hiyo crime rate ya South itakuwa cha mtoto.

Sasa mkuu unasema baada ya hiyo miaka 30-50 crime rate ya Tanzania itakuwa kubwa na ya South itakuwa cha mtoto...!

maana yake crime rate ya South yenyewe itakuwa imeganda tu au ina decline? Kwamba rate yao haiongezeki ila ya Tanzania ndio inaongezeka tu hadi kupita crime rate ya South?
 
Usijidanganye kwenda bondeni kutafuta maisha kama huna msingi, wala kibali. Kama unaweza kulipa nyumba Milioni kwa mwezi hapa Tanzania basi unaweza kuishi huko.

Kama unaweza kuishi Masaki na Mbezi beach basi unaweza kuishi huko sababu tabia za huko mazoea ya uswahilini hakuna, ukiweza kuishi South Africa na ndio umeweza kuishi nchi yoyote iliyopo Ulaya na pengine.

South Africa gredi ya uhalifu ni kubwa sana, kesi za kufa watu zipo nyingi kuliko kesi nyengine, ingekuwa tz kila siku kamanda wa polisi anatangaza mwisho hata choka.

Ngono kule ni kitu cha kawaida yani unatongoza mchana usiku unapewa, sio huku kwetu mpaka uchunwe kwanza.

Ukiwa na misosi ya kutosha na nyumba utachagua wanawake mpaka UKIMWI ukufikie, wanathamini kula sana maana maisha magumu kwao. Wezi, wauza madawa, wakwepa kodi na n.k wanaogopa kuweka pesa zao benki sababu benki za huku ni kama TRA kukuchunguza, Rais Ramaphosa ni mfano tosha.

Wizi wa magari ni kama wizi wa simu, gari nyingi zinazoingia hapa kwetu nyingi za wizi zinatoka huko. Vigogo wakubwa na wauza ngada hapa Tz wanaishi huko au kuwa na makazi ni wengi tu.

Msidanganye na wasanii wanasema wamenunua nyumba bali kule nyumba unaweza kununu tena nzuri ila ni kama umekodi, tofauti ya tanzania ardhi ina bei utadhani unanunua madini.

Kuvamiwa ni jambo la kawaida, wezi wakule usumbufu hawataki unaenda kwa order ukileta ubishi ni kugusa kaburini.

Huwezi kuchezea simu ovyo maana mitaa yote kuna wahalifu usipo kuwa makini unaweza kuona benzi kali inapita kumbe wapo wezi, ukifika nyumbani kama kuna geti lazima uchunguze mbele na nyuma nani anakufata ijalishi gari au mtembea miguu na hatua kidogo kabla ujafika getini, unaingia nao.

Vijana wetu waliozamia ukiona kaenda karudi katoboa maisha, mawili ni mchomoko au madawa.

Mchomoko ni kuvizia nyumba wenyewe hawapo tena nyumba hizi kama nilivosema wanaoweka pesa za kutakatisha.

South sio poa.
South Africa inahitaji msaada Mkubwa sana wa kiroho nchi Iko kwenye vita
 
Shida ni income disparity-Nelson Mandela watu wanamuona shujaa kutokana na kuwakumbatua makaburu lakini kwa sisi wabobezi wa mambo hapo ndio tunaona alichemka.

S.A means of production zote zina milikiwa na makaburu na mbaya zaidi wameenda mpaka level ya chini-unategemea watu wako wataishi vipi?

Hata hapa Tanzania ni bahati tu kuwa ardhi getu ni mkubwa kuliko population tuliyonayo-subiri baada ya miaka 30-50 ijayo hiyo crime rate ya South itakuwa cha mtoto.
Hili la income disparity na kutopenda kufanya Kazi unaliungishaje.
Mandela alihofia kufanya mistake aliyofanya Mugabe kuwapora wenye uwezo wa kuzalisha mali na kuwapa wasio na uwezo wa kuzalisha mali then uchumi ukafa, angalau hata hio Sauzi hao wachache uwabeba wengi kupitia wao ajira,kodi,bidhaa zinapitakana. Sisi tuna ardhi kubwa lakini ni useless kwetu hatunufaiki nayo, ni bora wapewe wachache wenye kumudu wazalishe Ili walishe wengi.
 
Back
Top Bottom