Maisha ya Biashara Bongo ni magumu kumaintain, Yapo Overrated kwa kuangalia wachache waliopiga mshindo, nasisitiza ajira serikalini ndio mpango

Maisha ya Biashara Bongo ni magumu kumaintain, Yapo Overrated kwa kuangalia wachache waliopiga mshindo, nasisitiza ajira serikalini ndio mpango

wastani kwa idadi

JF-Expert Member
Joined
Jun 28, 2024
Posts
503
Reaction score
1,432
Na kama unadhani ajira zenye mishahara midogo serikalini wana maisha magumu (mfano uliozoeleka walimu), basi hujui chochote kuhusu biashara, kuna watu wiki nzima hawauzi chochote, Maduka yanafungwa kila kukicha mtu hawezi lipa hata elf 50 ya frem, kufilisiwa nyumba za urithi kwa kushindwa kulipa madeni, n.k.

mifano iliyozoeleka ya kina Mo, Bakhresa na GSM hizo ni ligi nyingine kabisa, Biashara ni za vizazi, Kwa asili hao watu ni foreigners sio wabongo, wana umoja ndugu wote wanaishi nyumba moja, connections za ndugu wa nje, n.k. kutaja hio mifano sio feasible kwa hapa bongo.

Sina maana ya kuziponda biashara ni kweli zinawatoa watu lakini uwanja wa biashara wa Bongo upo tofauti sana, Hata ukichukua ushauri wa mfanyabiashara wa Marekani au ulaya mazingira ni tofauti, huko kwao sheria zinawalinda na kuwasapoti ni tofauti na hapa kwetu sheria zinaminya na kukandamiza na siasa kibao ndani yake, mfanoa mdogo tu kodi zetu zipo juu sana itabidi uzikwepe tu, Rushwa, kwenye ukusanyaji wa kodi watu wanalalamika TRA wanachota pesa zote kwenye account za benki, Polisi wanaweza kukusumbua sana na huna cha kuwafanya, n.k.

Lakini pia ili utusue kwenye biashara on average unahitaji backup ya kutosha mfano mentors kama ndugu au wazazi wa kukufundisha biashara kwa vitendo, Umoja wa kubebana kwenye familia, Mitaji, connections, n.k. ubaya ni kwamba inakuwa ngumu sababu watanzania wengi tuna ubinafsi, umoja wa kinafki, uchoyo wa connections, mitaji midogo, uvumilivu mdogo wa kuchapwa na hasara, tamaa za mashemeji na ndugu zao zimeharibu biashara kibao, n.k. exceptions ni chache sana tena ni kwa baadhi ya mambo mfano wachaga na wengine wakinga, waha, n.k. na bado ni baadhi sio wote.

Kingine ni kwamba kwenye biashara mafanikio ni kuteka soko, kufa kufaana !! mfanyabiashara yupo radhi ateke soko muda huo wenzake mia wanalala njaa na familia zao, unapomsifia mfanyabiashara flani ni tajiri kuna uwezekano mkubwa tu kalikamata soko kuna watu kibao walishafunga biashara zao, walifirisika, n.k. na kwa hali ilivyo kwa hapa Tz mambo ya Rushwa, siasa, n.k. haya mambo si ya ajabu.

hadi sasa Tanzania ni nchi masikini yenye mamilioni ya wafanyabiashara wakiwemo wachache sana waliofanikiwa na kumaintain, Kwa upande wa waajiriwa serikalini wapo wachach zaidi lakini wao wana uwakilishi mkubwa kwa idadi kwenye kundi la watanzania wachache wanaoishi walau maisha mazuri
  • Mitaa mingi sana yenye nyumba bora mijini wanaojenga na kuishi wengi ni watumishi wa serikalini.
  • Shule za private watoto wengi wanaosoma ni watoto wa watumishi wa serikalini
  • asilimia kubwa ya wenye magari ni watumishi wa serikalini
  • Watumishi wanaongoza kwa kuwa na muda mwingi wa kufanya shughuli zao nyingine ama kupumzika na familia zao tofauti na wafanyabiashara wenaondoka makwao asubuhi mpaka usiku kila siku kasoro jumapili na Idi au krismasi
  • watumishi wanaweza kufanya biashara huku wakiendelea na ajira, pia kupata mikopo kwa wepesi, wengine waliamua kuacha ajira mfano ni kina Mengi (rip), vunja bei, n.k.

MUHIMU: Ukiingia mitandaoni usijae upepo kirahisi ukimuona mfanyabiashara wa Marekani au Ulaya anatoa hamasa / motivation ya kufanya biashara, Inabidi utambue kwamba mazingira yao na yetu ni tofauti sana.
 
biashara ni kama kamari kuna kupata na kukosa ila kazi yenye mshahara ni uhakika inyeshe mvia liwake jua.
Biashara ni tamu sana ukiifanya sehemu sheria zinalinda na kuhamasisha wafanya biashara ila kwa hapa bongo hali ni tofauti.

Kufuata ushauri wa mfanyabiashara wa Marekani, Ulaya, Japan, n.k. ni lazima ujiongeze sababu mazingira ni tofauti sana, ukiingia kichwa kichwa unaangukia pua
 
Kazi pekee inayozidi biashara ni UFISADI, hapa unajipigia tu bilioni zako kadhaa, unahamishwa kitengo maisha yanaendelea.

Lakini duniani kote, hata hapa Tanzania, huwezi kukuta mfanyakazi akamtambia mfanyabiashara. Unataka ushahidi tuanzie Kariakoo, maghorofa yote unayoyaona yanamilikiwa na wafanyabiashara!

TUKIONDOA WIZI SERIKALINI! utarudi hapa kutengua kauli!
 
Watakuja hapa wakisema kuajiriwa ni kupoteza muda 😂😂

Niseme kwamba biashara ni ngumu hasa kwa hii mitaji yakwaida!!
% kubwa huenda ikawa kila mmoja humu ameshajaribu biashara hata zaidi ya 5 na zoote zikafa kifo kibaya sana 😁

Ni vile tu, tuna backup ya mishahara la si hvyo tungedhalilika vibaya sana
Biashara moyo mbio muda wote
 
Mfanyabiashara akifa familia inarithi na kuendeleza mfano boss wa Sayona kafa miaka nenda lakini biashara inaendelea UKIFA mtumishi wakikuhurumia ni mazishi ya kiserikali halafu familia yako wataambulia Kikokotoo!

Unafikiri kwa nini watu wanawaza kujiajiri??
Hahaaa hajui mfanya biashara wewe unapata muda wa kwenda mpaka Dubai. Mtumishi wa Vikindu Primary hata Kkoo ana miezi 7 hajafikapo 😂😂😂
 
Kazi permanent and pensionable Kuna jamii za watu wavivu, wazembe, walevi nieleweke wazi wao Waka ajiliwe TU hakuna namna..

Ukifanya kazi private sector kwa mzungu,mhindi,mwarabu E.t.c lazima uwe very competent japo hizo race zoteee Zina tabia tofauti..

Kwenye biashara yoyote sisi ambao tumebahatika kusoma FINANCIAL BUSINESS tuna jua BIASHARA NI KAMA KIUMBE HAI ""Hupitia stage zotee za KIUMBE HAI

Biashara Ina curve yake na usipo kua flexible with time & environment lazima biashara itakufia kweupee biashara zinalipa SANAA na Zina miiko yake

Kwenye izo Kaz za permanent and pensionable changamoto ni kulemaa watu ikitokea wamefukuzwa KAZI wakirud mtaan ku scratch from beginning utawaonea huruma maana sio mchezo...

Kama hutokani na familia tajir Basi wewe ndio utengeneze utajiri Information is power

✍️ Tatizo wengi wetu huwa tuna SKIP SKIP THEN RESTORE bila kusoma VIGEZO NA MASHARTI hapo ndipo tatizo linapo anzia..


UTAJIRI UNAANZIA KICHWANI ALAFU UNAOTA MOYONI☺️😊
 
Na kama unadhani ajira zenye mishahara midogo serikalini wana maisha magumu (mfano uliozoeleka walimu), basi hujui chochote kuhusu biashara, kuna watu wiki nzima hawauzi chochote, Maduka yanafungwa kila kukicha mtu hawezi lipa hata elf 50 ya frem, kufilisiwa nyumba za urithi kwa kushindwa kulipa madeni, n.k.

mifano iliyozoeleka ya kina Mo, Bakhresa na GSM hizo ni ligi nyingine kabisa, Biashara ni za vizazi, Kwa asili hao watu ni foreigners sio wabongo, wana umoja ndugu wote wanaishi nyumba moja, connections za ndugu wa nje, n.k. kutaja hio mifano sio feasible kwa hapa bongo.

Sina maana ya kuziponda biashara ni kweli zinawatoa watu lakini uwanja wa biashara wa Bongo upo tofauti sana, Hata ukichukua ushauri wa mfanyabiashara wa Marekani au ulaya mazingira ni togauti, huko kwao sheria zinawalinda na kuwasapoti ni tofauti na hapa kwetu sheria zinaminya na kukandamiza na siasa kibao ndani yake, mfanoa mdogo tu kodi zetu zipo juu sana itabidi uzikwepe tu, Rushwa, kwenye ukusanyaji wa kodi watu wanalalamika TRA wanachomoa pesa zote kwenye account, Polisi wanaweza kukusumbua sana na huna cha kuwafanya, n.k.

Lakini pia ili utusue kwenye biashara on average unahitaji backup ya kutosha mfano mentors kama ndugu au wazazi wa kukufundisha biashara kwa vitendo, Umoja wa kubebana kwenye familia, Mitaji, connections, n.k. ubaya ni kwamba inakuwa ngumu sababu watanzania wengi tuna ubinafsi, umoja wa kinafki, uchoyo wa connections, mitaji midogo, uvumilivu mdogo wa kuchapwa na hasara, kaka akioa mke wake kuzitolea macho mali za familia, n.k. exceptions ni chache sana ni wachaga na wengine wakinga, waha, n.k. tena ni baadhi sio wote. lakini bado hata mazingira ya biashara kisiasa ni magumu sana mfano

Ndio maana hadi sasa Tanzania ni nchi masikini lakini hata hivyo wenye mafanikio wengi tunawaona ni waajiriwa serikalini.

Vipimo vinavyotumika kuona wenye ajira wana nafuu kuzidi wafanyabiashara kwa kiwango cha uwakilishi wa idadi

  • Mitaa mingi sana yenye nyumba bora mijini wanaojenga na kuishi wengi ni watumishi wa serikalini.
  • Shule za private watoto wengi wanaosoma ni watoto wa watumishi
  • asilimia kubwa ya wenye magari ni watumishi wa serikalini
  • Watumishi wanaongoza kwa kuwa na muda mwingi wa kufanya shughuli zao nyingine ama kupumzika na familia zao tofauti na wafanyabiashara wengi kazi ni asubuhi mpaka usiku kila siku kasoro jumapili na Idi au krismasi
Nasoma bandiko hili huku nikiwa kwenye pilika za biashara zangu hadi muda huu karibu saa 12 jioni bilabila...dah..nguvu zaniisha kabisaa..!

Wakati huohuo napigiwa simu na bro angu mtumishi wa umma cheo cha kawaida tu jw ananiambia anakuja kufuata gari lake amenunua lingine..
Hii ndio bongo!
 
Hii mada inawez kuwa na hoj nzuri ikibeba layers.. biashara ya mtaji na return kias gan inayozungunzwa hapa. Huwez kuzungumza biashara ya mtaji million 2 ikaleta tija dhidi ya kuajiriwa serikalin mshahara 600+ mada automatic hii biashara ikileta faida kubwa kwa mwez ni 400.

Mtoa mada unaipambanisha biashara ya mtaji kias gani dhidi ya muajiriwa levo gan serikalin
 
Back
Top Bottom