Na kama unadhani ajira zenye mishahara midogo serikalini wana maisha magumu (mfano uliozoeleka walimu), basi hujui chochote kuhusu biashara, kuna watu wiki nzima hawauzi chochote, Maduka yanafungwa kila kukicha mtu hawezi lipa hata elf 50 ya frem, kufilisiwa nyumba za urithi kwa kushindwa kulipa madeni, n.k.
mifano iliyozoeleka ya kina Mo, Bakhresa na GSM hizo ni ligi nyingine kabisa, Biashara ni za vizazi, Kwa asili hao watu ni foreigners sio wabongo, wana umoja ndugu wote wanaishi nyumba moja, connections za ndugu wa nje, n.k. kutaja hio mifano sio feasible kwa hapa bongo.
Sina maana ya kuziponda biashara ni kweli zinawatoa watu lakini uwanja wa biashara wa Bongo upo tofauti sana, Hata ukichukua ushauri wa mfanyabiashara wa Marekani au ulaya mazingira ni tofauti, huko kwao sheria zinawalinda na kuwasapoti ni tofauti na hapa kwetu sheria zinaminya na kukandamiza na siasa kibao ndani yake, mfanoa mdogo tu kodi zetu zipo juu sana itabidi uzikwepe tu, Rushwa, kwenye ukusanyaji wa kodi watu wanalalamika TRA wanachota pesa zote kwenye account za benki, Polisi wanaweza kukusumbua sana na huna cha kuwafanya, n.k.
Lakini pia ili utusue kwenye biashara on average unahitaji backup ya kutosha mfano mentors kama ndugu au wazazi wa kukufundisha biashara kwa vitendo, Umoja wa kubebana kwenye familia, Mitaji, connections, n.k. ubaya ni kwamba inakuwa ngumu sababu watanzania wengi tuna ubinafsi, umoja wa kinafki, uchoyo wa connections, mitaji midogo, uvumilivu mdogo wa kuchapwa na hasara, tamaa za mashemeji na ndugu zao zimeharibu biashara kibao, n.k. exceptions ni chache sana tena ni kwa baadhi ya mambo mfano wachaga na wengine wakinga, waha, n.k. na bado ni baadhi sio wote.
Kingine ni kwamba kwenye biashara mafanikio ni kuteka soko, kufa kufaana !! mfanyabiashara yupo radhi ateke soko muda huo wenzake mia wanalala njaa na familia zao, unapomsifia mfanyabiashara flani ni tajiri kuna uwezekano mkubwa tu kalikamata soko kuna watu kibao walishafunga biashara zao, walifirisika, n.k. na kwa hali ilivyo kwa hapa Tz mambo ya Rushwa, siasa, n.k. haya mambo si ya ajabu.
hadi sasa Tanzania ni nchi masikini yenye mamilioni ya wafanyabiashara wakiwemo wachache sana waliofanikiwa na kumaintain, Kwa upande wa waajiriwa serikalini wapo wachach zaidi lakini wao wana uwakilishi mkubwa kwa idadi kwenye kundi la watanzania wachache wanaoishi walau maisha mazuri
- Mitaa mingi sana yenye nyumba bora mijini wanaojenga na kuishi wengi ni watumishi wa serikalini.
- Shule za private watoto wengi wanaosoma ni watoto wa watumishi wa serikalini
- asilimia kubwa ya wenye magari ni watumishi wa serikalini
- Watumishi wanaongoza kwa kuwa na muda mwingi wa kufanya shughuli zao nyingine ama kupumzika na familia zao tofauti na wafanyabiashara wenaondoka makwao asubuhi mpaka usiku kila siku kasoro jumapili na Idi au krismasi
- watumishi wanaweza kufanya biashara huku wakiendelea na ajira, pia kupata mikopo kwa wepesi, wengine waliamua kuacha ajira mfano ni kina Mengi (rip), vunja bei, n.k.
MUHIMU: Ukiingia mitandaoni usijae upepo kirahisi ukimuona mfanyabiashara wa Marekani au Ulaya anatoa hamasa / motivation ya kufanya biashara, Inabidi utambue kwamba mazingira yao na yetu ni tofauti sana.