Maisha ya bongo!

TRABSOH

JF-Expert Member
Joined
Jun 9, 2023
Posts
351
Reaction score
559
Wazee waliposema usiku mrefu waliwaza vingi bwana, leo katika harakati nimejikuta nakosa msosi na kulala pakavu tumboni, sahizi nipo natapa tapa hapakuchi!! Nimeingia kitandani toka saa nne hadi sahizi saa tisa sipati usingizi nasinzia nikishtuka nakuta nimesinzia dakika kumi au kumi tano tu.

Umeme umekatwa na wapuuzi Tanesco joto la kuoka kuku asee plus njaa nahisi kuzimia, Mungu atusaidie Watanzania wasakatonge. Na sisi tuwe na uhakika wa kujaza matumbo na kuwasha air condition kwa kutumia standby generator umeme unapokatika #onedayyes
 
1. Pole. Huo ndo uanaume
2. Nenda kumywa maji kwanza upate hata ka reserve.
3. Kama uko mji kama Dar,, sasa hv watu walishaamka, usisubirie pakuche, sepa.sasa hv ukahangaike. Huez jua utachokutana nacho. Riziki ya mbwa iko miguuni kwake
 
Mkuu

Hali unayopitia ni fursa KWAKO ya kumuomba Mungu na kuweka misingi ya nyakati zijazo maishani mwako!!

Ikitokea tena saa tisa usiku umeshtuka,muombe Mungu wako juu ya nini unataka maishani na usiombe KUHUSU kupata vya mwilini Pekee bali na vya rohoni na familia njema yenye KULETA furaha na tija TANZANIA!!

Saa za USIKU sana ukiamshwa ni saa za kumuita MWENYEZI!coz milango ya mbinguni inakua wazi kupokea MAOMBI YOTE!!
 
Asante
 
Yani bora ulale njaa ila usikose bando?
Kwa kazi zangu bundle ni jambo ambalo siwezi kulikwepa na hapa kwasbbu ya kukosa tenda ndo nimebakiwa na bundle ila sina ela , me nafanya vibiashara mtaani na kwenye website za freelancing ,fiver na upwork nafanya part time job na ndo zinanisaidiaga always ila wakati huu mambo yameenda kombo
 
Ukipata hela usiache kwenda kwa mangi hapo jirani ukatumie tumie ujenge mazoea na wauzaji hapo mtaani kwenu hata siku ukiwa huna unakopa tu unga robo mafuta robo na bando lako unalo unalala safi kabisa.
 
Ukipata hela usiache kwenda kwa mangi hapo jirani ukatumie tumie ujenge mazoea na wauzaji hapo mtaani kwenu hata siku ukiwa huna unakopa tu unga robo mafuta robo na bando lako unalo unalala safi kabisa.
😁 baada ya miaka mitano kwenda kumi hizi financial issues zitakata nitakuwa nmesajili kampuni na itakuwa na kuenea Africa mashariki na kati na kuzalisha biashara nyingine , itaondoa umaskini na shida zangu na za uzao wangu milele na milele, nitawapa ushuhuda hapa hizi ni nyakati tu zinapita comrade instagram
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…