Maisha ya Dar vs Maisha ya mikoani

Maisha ya Dar vs Maisha ya mikoani

Naunga mkono hoja kwa kwa asilimia 1000000000000000ⁿ. Yaan mikoani kuna mambo ya kiwaki kinomaaaa. nshawahi kwenda mwanza misungwi huko eneo linaitwa nsumbugu, nlienda kununua mchele yaan walivojua tu kwamba mm sio msukuma basi wakanpandishia bei. Asee nlikaa week mbili nkaamua kuondoka zangu
Hata Dar wakijua wa kuja lazima utapeliwe
 
Mkuu..NAKATAA

1. sio rahisi mtu wa 220000 kukaa room ya 70k kwa mwezi..Asilimia kubwa wanakaa vya 30, 40 au 50
2. Umeme 20k Dar na 5k mwanza sijajua kama ni uhalisia...Kwani price/unit kwa dar na mza inatofautiana?...Kuna watu wanalipa 5k au 10 umeme kwa mwezi.
3. Maji...10k ni ndefu sana..
Price/unit inawezekana ikawa sawa ila matumizi tofauti

Nyanda za juu kusini hatulali na feni wala hatuwashi mafriji sana
 
Dar movement nyingi zinahitaji usafiri/nauli ukitembea kidogo tu jasho, Mikoani watu movement kwakiasi kikubwa zinategemea mguu, Ukiwa mtu wamishemishe Dar utakunywa maji sio chini ya buku kwa siku ambapo mkoani hicho kiasi cha elfu thelathini kwa mwezi utafanyia mambo mengine, huo mchele wa 1200 ni ukiwa huku mikoani huwezi kuula kwani ni kwaajili ya kupikia vitumbua
 
Tatizo unadhani asset ni nyumba, kiwanja au shamba pekee.

Hata majiji makubwa duniani watu hawanunui majumba au viwanja.

Wao wanaweka assets zao kwenye pesa, hisa, bonds n.k. hata hawa wahindi wanaoishi kwenye maghorofa kisutu, unahela kuwashinda wao? Ila ukiona bank acoount yake utashika kichwa. Wewe unabaki na kiwanja chako Illeje huko unaona umetusua maisha.

Unakuta mtu amefanya mishe miaka 20 aka-save hata $5M.

Ndo anaenda nje ya mji, ananunua nyumba anastaafia huko.
Hizi ni biashara zinazofahamika na wachache, wapambanaji wengi wa Dar hawajui kwahiyo hauwezi kuwa utetezi.

Haya ni maandishi ya keyboard tu, lakini physically nina wanangu walifeli kabisa Dar
Wapo wanaotafuta fursa warudi mikoani
 
Huwa napitia comments zao afu nakaa kmya. Mkoan mtu kupata kibarua cha kulipwa 10k ni vigumu. Afu unategemea mtu huyo huyo awe na purchasing power kubwa kweli?

Akat dar, mtu kupata kibarua cha 20k ni dakika 0 tu
Unapata 20k inaisha hapo hapo

Miaka 10 mtu anamiliki geto tu uswahilini
 
Dar movement nyingi zinahitaji usafiri/nauli ukitembea kidogo tu jasho, Mikoani watu movement kwakiasi kikubwa zinategemea mguu, Ukiwa mtu wamishemishe Dar utakunywa maji sio chini ya buku kwa siku ambapo mkoani hicho kiasi cha elfu thelathini kwa mwezi utafanyia mambo mengine, huo mchele wa 1200 ni ukiwa huku mikoani huwezi kuula kwani ni kwaajili ya kupikia vitumbua
dah ha ha ha
 
Nimeishi mikoani pia nimeishia Dar,kwa kazi ile ile mshahara ule ile nitatoa uzoefu wangu kwenye aspect zifuatazo.
1.Social
A.Ukabila,udini
Dar ni sehemu ambayo haina ubaguzi,ni sehemu unayoweza pata rafiki mpenzi wa kabila,dini,rika na kazi yeyote ile mwenye tabia na shepu unayoitaka.
mikoani unaweza kosa mtu unayemuhitaji,kuna sehemu ukienda hakuna waislamu,zingine hakuna wakristo,zingine hakuna Madaktari,Mainginia wala wanasheria,........yaani unaweza ishi sehemu 80 % ni watu wa kabila moja tu,wanaongea kilugha chao ....Dar huu upuuzi hamna
2.Kibiashara.
Dar kila biashara inafanyika usiku na mchana hakuna kukesha,wateja wakija hawana muda wa kuulizia dini kabila wala umetoka wapi,wanahitaji bidhaa.
Mikoani ni vituko kuna sehemu ukienda kama wewe sio wa kabila lao,hupati wateja hata kama unauza bidhaa bei chini na bora sawa na wao,halafu biashara hazifanyiki muda wote .....hapa kuna sehemu nimefika mjini kabisa eti nimekosa nyama mabucha yamefungwa[emoji1][emoji1787],sasa si uhanithi huu.
Hizi biashara za kudeal na watu mikoani ndio kabisa,yaani daktari uende mkoa flani hujui kilugha chao,wakati kuna kijana kutoka kwao,watu wapo tayari wafe lakini huwagusi.
Tatizo jingine mikoani hamna kila kitu,mfano kanda ya ziwa ni ngumu sana kupata pweza,ngisi na products za baharini wakati Dar kila kitu cha mkoani utakipa kwa bei yeyote ile unayoitaka ......yaani hata sato fresh Dar
watu wanakula tu hawana habari.
3.Usafiri.
Hii sehemu nilipo boda boda ikinyesha mvua hawaendi hata iweje[emoji1787][emoji1787][emoji1][emoji1],wakati Dar hata maradi yapige usiku kucha watu hawana noma kiongozi....halafu mikoani gharama za usafiri ni ghali sana ukilinganisha na Pwani au Dar.....mfano kutoka Dar hadi Kibiti nauli elfu 5,mkoa mwengine kabisa ........kwa umbali huo huo mkoani nauli inaweza fika elfu 15 na usafiri ni wa ovyo mno
Mkoani wafanyakazi wa kawaida wanatumia hadi elfu 5 boda boda,Dar hio ni nauli wa wiki kwa wajanja wengi wanaojulia mji
4.Afya
Dar hospitali ni nyingi sana na maduka ya dawa yanakesha......mkoani kama una emeregency usiku kazi unayo aisee
Hata madaktari ni wachache pia.....yaani hata wazawa wasomi wa mikoani hua hawataki kuishi[emoji1787][emoji16][emoji119]
5.Mzunguko wa pesa
Dar ni mkubwa,viwanda,ofisi etc zipo za kutosha,mkoani ni vya kuhesabu.......kuna mikoa viwanda vya kuajili watu 100,kwa pamoja havifiki hata viwili,yaani kama hujasoma,wewe sio boda boda ulime tu kiongozi[emoji1][emoji1787][emoji1787][emoji119]
6.Giografia.
Mkoani sehemu inayofanana na Dar ni pale makao makuu tu ya mkoa tena kwa asilimia 10% tu..........ambapo utakuta labda baadhi ya watu wa makabila mengine wapo,ukienda wilayani ni vituko vitupu,huko hamna wahindi wala,wachaga,matajiri wao kwa wao tu wanaongea viligha vyao.......[emoji1787][emoji1787][emoji16],ukienda mgeni unaonekana mchawi,makazini/shuleni ndio usiseme watu wanaongea kilugha kazini kawaida tu kumkuta mwalimu anawaelekeza wanafunzi wa lugha za asili[emoji16][emoji16][emoji119]
7.Upatikanaji wa vitu/vyakula.
Mkoani vyakula ni bei rahisi vya kununua ambavyo havijaandaliwa(Raw foods),unaweza pata mkungu hata elfu 3,kuku elfu 5,mayai mia 2........ila changamoto hakuna vyakula vya aina yote.....unajua Dar kila vyakula vipo kutoka mkoa wowote ule Tz.....mikoani vilivyo cheap ni vile tu vinavozalishwa eneo husika.
General Dar ndio penyewe maana utapata unachotaka kutoka mkoa wowote ule.........ukienda mgahawani mikoani ukitaka wali maharage ni kawaida tu kuletewa wali na maharage yaliyochemshwa tu[emoji16][emoji1787][emoji1] ,hamna hata kitunguu, wakati unakuta huo mkoa unaongoza kulima vitunguu,labda na nafaka zinatoa mafuta.....

8.Psychological
Dar huwezi kua mpweke unaweza lazimisha weekend uende beach kula bata,halafu watu wapo social tu mjini mtu hata humjui munapiga tu stori kijiweni fresh tu....unaondoa stress kiaina.
Mkoani kijiweni wanaongea kilugha[emoji1787][emoji16],ukienda mgeni wanamute wanaogopa sana polisi au wanaamini unawachunguza.
9.Ustaarabu
Dar/Pwani ,watu ni wastaarabu tu,....ukienda hospitali watu wanajielewa fresh,mtu kama anajua kitu cha pesa anafight,shuleni walimu wakiagiza wanafunzi mchango wazazi wanatoa fresh tu......mkoani na hivi marehemu shujaaa waliwajaza ujinga,watu wanaweza mpiga hata mwalimu kwa kuchangisha hela ya tuition tu shillingi mia mbili apate chochote[emoji1787][emoji1][emoji1],hospitali Doctor akisema hii dawa haipatikani kanunue,tayari simu kwa DC,.....wakati mtu mtoto wake mwenyewe[emoji1787][emoji1787][emoji16].......yaani watu ni wagumu sana kujiongeza mkoani mtu yupo tayari age aisee........halafu mkoani watu wanapenda
Kuchongeana sana,mwalimu ukiwa u akula wanafunzi msala......ushawahi sikia mwalimu wa Dar kakamatwa na mwanafinzi wa sekondari .......Dar hata mazazi akijua hana noma,anajua huyo mwanafunzi wa kike,dudu kaitaka mwenyewe hajalazimishwa[emoji16].
Kwa Kifupi mkoani sio sehemu ya kuishi kwa mtu anayependa maisha social ya kawaida tu ya kibongo ya kujichanganya popote.......sio sehemu nzuri ya kutafuta maisha na ndio maana vijana wengi wa mkoa wanakuja Dar/Pwani kutafuta maisha.......ushawahi ona kijana wa kizaramo,kindengereko eti ameenda mkoani kutafuta maisha?[emoji1787][emoji1][emoji1]
Fact
 
Hivi Mkoani ni Watu, Mi nikiwa Natoka Arusha kwenda Dar huwa nasema naenda Mkoani, nikiwa natokea Mwanza kwenda Kigoma nasema naenda Mkoani, hivi kumbe Mkoani ni wapi ?
 
Nina miaka 2 sasa nipo Moshi kwa kweli hapana nishachoka.
Huwa najiuliza hv watu wa kule wanaishije asee. Moshi&Arusha is a NO for me. Labda niwe nko kwny ajira inayonilazimu mm kuishi huko. Na ndo mana wachaga wengi wamejazana Dar na mikoa mingine wanaparangana kwny biashara afu mwisho wa mwaka ndo wanaenda kusalimia familia zao,,they know how hard is their homes,,,,,unakuta mtu anaacha mke na watoto watatu, anaenda morogoro kulima mpunga
 
Hivi Mkoani ni Watu, Mi nikiwa Natoka Arusha kwenda Dar huwa nasema naenda Mkoani, nikiwa natokea Mwanza kwenda Kigoma nasema naenda Mkoani, hivi kumbe Mkoani ni wapi ?
Mkoani ni Sehem yoyote ile tofauti na Dar.
 
Mtu wa dar maisha yakimshinda anarudi mkoani.

Mtu wa mkoani maisha yakimshinda anabaki mkoani hawezi kwenda dar.

Nadhani hadi hapo umeshaelewa wapi maisha magumu.
 
Huwa najiuliza hv watu wa kule wanaishije asee. Moshi&Arusha is a NO for me. Labda niwe nko kwny ajira inayonilazimu mm kuishi huko. Na ndo mana wachaga wengi wamejazana Dar na mikoa mingine wanaparangana kwny biashara afu mwisho wa mwaka ndo wanaenda kusalimia familia zao,,they know how hard is their homes,,,,,unakuta mtu anaacha mke na watoto watatu, anaenda morogoro kulima mpunga
Acha tu mkuu. Mwaka jana nilitembelewa na bro angu yeye mtu wa mjini. Mwanzo nilimuonya huku siyo kama Dar hakunielewa kilichompata huko alipoenda kutafuta vibarua nilibaki namcheka tu.
 
Kuna watu wana amini maisha ya Dar ni magumu (kufanikiwa ni ngumu) wengine wanasema maisha mikoani ni rahisi (kufanikiwa ni rahisi)... Je, ugumu wa Dar uko wapi na urahisi wa mikoani uko wapi? (Huu ni mtazamo wa wengi humu kwa utafiti wangu mdogo nilioufanya humu ndani kwa muda kidogo).

Ningefurahi kama hii thread ichukuliwe serious na watu waweze kuweka strong arguments ambazo zitawasaidia wengine kutoa tongotongo machoni mwao (kujifunza) na kuona opportunities za kimaisha na kuchukua hatua kabla hawajaamua sehemu ya kuishi. Tofauti ya maisha mikoani na Dar ni ipi kiasi cha kuja na hitimisho kuwa Dar kugumu kuliko mikoani..Je ni kweli Dar ni kugumu kuliko mikoani?

Ni hoja zipi zinatumia katika kutoa hiyo conclusion hapo juu?. Mitazamo na hoja zetu wote zina manufaa na zina umuhimu wake hapa kwajili ya kujifunza zaidi. Ila pia nitafurahi zaidi kusikia kutoka kwa haya makundi mawili:-
1. Watu waliofeli mikoani wakafanikiwa Dar
2. watu waliofeli Dar wakafanikiwa mikoani

Karibuni tujifunze kwa hoja.

NB: Kuna watu tuta/watajifunza mambo mengi sana kupitia hapa. Sasa wale wenye lugha za kuudhi na kukejeli kila muda, itabidi wajifikirie na kujitathimini utimamu wao wa akili kabla hawajawavunjia wengine heshima..Ni bora/ vyema kukaa kimya bila kuandika chochote ikiwa utakachoandika kitakuwa kina lengo la kutukana au kuboa au ku attack watu personally.
Nimeenda mbeya, nimeenda iringa, nimeenda mafinga, nimeenda mwanza najuta kwa nini nimekomaa kukaa dar....nimepapenda sana mwanza na iringa! Hata mafinga pako poa sana. Mbeya balaa, very simpo!
Hapa nimeongelea kimamdhali, na hali ya hewa na simplicity ya kero ambazo dar zipo.
Mwanza iko poa sana
 
Mtu wa dar maisha yakimshinda anarudi mkoani.

Mtu wa mkoani maisha yakimshinda anabaki mkoani hawezi kwenda dar.

Nadhani hadi hapo umeshaelewa wapi maisha magumu.
Nimecheka sana kiongozi...Kwamba Dar ni moto wa petrol?
 
Back
Top Bottom