mHAMAS-shaji
Member
- May 31, 2024
- 63
- 177
- Thread starter
- #21
MAISHA YA DEPO
SEASON-1
EPISODE 05
Binafsi haikuwa taarifa nzuri kwangu, sikuipokea siyo tu kwa mikono miwili bali hata kwa kidole kimoja sikuweza kuipokea taarifa ile hata kwa moyo mmoja.
Mpaka muda huo sikuwa nalipenda jeshi kwa ujumla, nilizisikia taarifa nyingi ambazo zilinifanya nilichukie jeshi.
Ugumu wa kazi na mazoezi yaliyopelekea ulemavu na vifo ni miongoni mwa mambo yaliyonifanya nikalichukia jeshi hilo.Kwangu sikuhitaji kuwa maiti ndiyo nizijue mbivu na mbichi za kaburi, wala sikuhitaji niingie kati nicheze ndiyo niweze kuzijua raha za ngoma, fununu nilizozisikia mtaani zilinitosha kuhitimisha kuwa mafunzo ya jeshi ni njia ya kwenda kuzimu.
Kwakuwa Ambrose yeye alikuwa na simu ya kisasa alipata orodha ya baadhi ya wanadarasa waliochaguliwa kwenda mafunzoni.
Alinijuza miongoni mwao na kunifahamisha kuwa mimi, yeye na Linda ni miongoni mwa tuliopangiwa kushiriki mafunzo hayo kwenye kambi moja.
Nilijaribu kumuuliza kuhusu Zai naye kama kapangwa kambi sawa nasi ila aliniambia hakumuona kwenye orodha na nilipomuuliza kama anawasiliana naye majibu alinipa yaleyale ya kila siku kuwa namba aliyonayo haipatikani.
Basi bwana mrembo Zai aliendelea kuwa bidhaa adimu kwangu, hali iliyonizidishia hamu ya kutolipenda jeshi mana mbali ya kuwa nafsi iliamua kuwa sitohudhuria mafunzo ila ikitokea Zai akapangiwa kambi moja na mimi nisingesita kwenda hata kama ningekutana na kifo changu huko basi ningekuwa radhi kufa ili mradi nipate ukaribu naye mana niliamini kuwa bado ninahitaji muda wa kuwa karibu naye.
Taarifa zile ziliwafikia nyumbani ambako licha ya kujifanya sijui kinachoendelea huku nikisingizia uwezo wa simu niliyo nayo wao walitumia simu zao kufuatilia kwa undani kama nimepangiwa ama vinginevyo.
Walifanya hivyo mpaka pale walipofanikiwa kuliona jina langu na kunijuza nami sikusita kuwaambia msimamo wangu kuwa sipo tayari kwenda.
Msimamo huo ulizua mtafaruku nyumbani ingawaje wapo baadhi walitaka nisikilizwe ila shida ilikuwa kwa mkuu wa kaya ambaye yeye alitaka niende huko.
Baba mjengo huyo aliyekuwa akifahamika kwa jina la Mzee Mjuzi yeye aliamini kuwa mafunzo ya kijeshi yangenifanya niwe mkakamavu na mzalendo kwa taifa hivyo kuwa tayari wakati wowote kulitumikia taifa.
Alikuwa akiniambia kuwa serikali ina maana yake kufanya hivyo na siwezi jua mana huenda siku za mbele wale waliohudhuria mafunzo hayo wakawa ni kipaumbele kwa upande wa ajira.
Alinithibitishia hilo kwa kunipa mifano ya viongozi mbalimbali wa juu nchini wamehudhuria mafunzo ya kijeshi hivyo huenda ikawa kuna ngazi ya utawala ama uongozi wa nchi nisingeweza kuzihudumu pasi na kuwa na cheti ama historia ya kupitia mafunzo hayo kwasababu wanaamini hao watakuwa na uzalendo kwa taifa.
Mzee alinisisitiza kuwa siwezi jua mana wakati mwingine taasisi mbalimbali za kijeshi na usalama wa taifa hutumia Jeshi la kujenga taifa kupata watumishi wapya pengine ingeniangukia bahati na ikawa njia fupi kwangu ya kupata ajira ya kudumu.
Baada ya kikao hicho kikuu viliendelea vikao vidogodogo lengo likiwa ni kunisisitiza kufanya maandalizi mana siku za kuripoti zilikuwa zikikaribia.
Hakuna kauli ambazo ziliniumiza kutoka kwa mzee huyo pale aliponiambia nikienda jeshini nitakuwa mkakamavu na mzalendo.
Nafsini nilijiambia huenda nikawa siyo mzalendo kweli lakini je ameniona mimi ni legelege kiasi hicho kiasi cha kwenda kufanywa kuwa mkakamavu.
Nilichukia sana ila nilihitimisha kwa kujisemea moyoni kuwa mshua jau kauli ambayo ilinipunguza hasira juu ya kauli zake.
Wakati yote hayo yakiendelea nilikuwa nikiwasiliana na Linda ambaye yeye alifurahi mno kupangwa kambi moja na mimi na aliniambia kuwa hapo awali hakuwa tayari kwenda jeshini na wazazi wake waliriridhia.
Linda aliniambia kuwa kama itatokea niko tayari kwenda basi na yeye angekuwa tayari kuwaambia wazazi wake kuwa amebadili msimamo wake na hatimaye angekwenda.
Ama kweli penye miti hapana wajenzi yaani utayari wangu wa kwenda mafunzoni kwa ajili ya Zainabu hautofatiani na wa Linda kwangu ila ugumu uko hapo tu Linda yupo tayari kwenda kwa ajili yangu ila mimi sipo tayari kwenda kwaajili yake na kinyume chake niko tayari kwenda kwaajili ya Zainabu ingawaje sikufahamu utayari wa Zainabu kwangu.
Kifupi nilitamani sana Linda awe Zainabu ili jambo liwe jepesi.
Kadri siku zilivyokuwa zikiongeza namba ndivyo maudhi yalikuwa yakizidi maana kikubwa ilikuwa ni ukakamavu, nidhamu na uzalendo kana kwamba ni vitu ambavyo sina.
Niliamua kukaa chini na kufanya tafakuri ya kina nikaona nikiendelea kukaa humo nitakuwa nikigombana na watu wasiostahili kila siku mana hata wale waliokuwa wakiniunga mkono walinisihi sana kumsikiliza mshua kwa maana kuwa kumpinga yeye ni sawa na kumdharau.,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,
Itaendelea....................................

Samahanini sana wanajukwaa kwa kuwaweka kinyonge mambo yamekuwa mengi kwakweli ila leo tupo live msicheze mbali maana itakuwa ni kipande baada ya kipande.
Baada ya hayo naomba kufungua kikao.
MAISHA YA DEPO
SEASON-1
EPISODE 04
Nilijitetea kwa kumwambia kuwa “Namba siioni na hata leo hii mchana nimejitahidi kufukunyua kwenye begi lakini wapi, hata hivyo ile siku natoka pale bweni la Mikumi mpaka napanda basi la kuja nyumbani ilikuwa ni shughuli Mamdogo.
Nilipofika nyumbani begi lenyewe nilipokelewa nimekuja kulishika siku ya pili yaani kurupushani zilikuwa ni zaidi ya nyingi wala sijafanya kusudi kutokukutafuta”.
Baada ya maneno hayo nilisikia sauti ya Kichaga ikisema “Ewe Mungu wa majeshi embu shuka duniani uje umnusuru mtu wako huyu aliyejawa na damu ya uwongo kwenye mishipa yake, yaani anavyoongea ni kana kwamba ile namba nilimuandikia kwenye kikaratasi”
kwakweli nilijichanganya hali iliyonifanya nibaki kimya na kumuacha aongee yeye tu.
Linda aliendelea kuongea na kuniuliza “umeshindwaje kuomba kwa mtu jamani, mbona wana wengi tu wanayo”.
Nikapata nguvu za kumjibu ila kwa sauti ya upole sana nikamwambia “Samahani sikuwa na wazo hilo ila nilikuwa naamini ninayo hivyo ipo siku ningeiona tu”.
Basi mazungumzo yalikuwa ni mengi ila kikubwa ilikuwa ni kwanini sikumtafuta siku zote hizo, kwakua nilikuwa nikimfahamu vizuri sikuhitajika kutumia nguvu nyingi kujitetea nilichofanya nilimtuliza nikampooza na hatimaye jazba likamshuka.
Nilijaribu kumdodosa Linda kama kuna watu bado hawajamaliza mitihani, aliniambia kuwa wamewaacha PCB na CBG wanasubiri practical ya Biology ila kesho yake ndiyo wanamalizia.
Maneno hayo yalinipa matumaini ya kwamba huenda Zai hakunipa namba ya uongo ila bado yuko shule na ndiyo maana hapatikani kwenye simu.
Nilitamani kumuuliza Linda kama kweli Zai naye ni miongoni mwa wale aliowaacha ila nikaona ni bora niache maana ataniona kama namjali Zai kuliko yeye kitu ambacho hakipendi na zaidi ya hapo ni kuwa tumetoka kumaliza swala kama hilo la kutomjali yeye.
Niliendelea kufanya juhudi za kumtafuta Zai pasi na mafanikio kwani hata pale nilipoulizia kama wamekwisharudi nyumbani wanafunzi wote waliomaliza kidato cha sita niliambiwa wamerudi ila kila nilipompigia msichana yule majibu yalikuwa ni yale yale “hapatikani”.
Siku moja nilipokuwa naongea na Shebi nilijaribu kumdodosa kuhusu Zainabu “oya hivi Zainabu unaongea naye kweli”“Zainabu yupi?”“Zainabu Khamisi yule dada wa CBG tumemaliza naye pale kiskuli”“Anhaah yule hapana nasikia kwenye simu hapatikani hata mimi kuna siku nilimpigia ila sikumpata, vipi kwani shemeji yetu nini”.
“Hapana ni mwana tu nimempigia sana ila naona kila nikipiga hapatikani nikaona nikuulize afisa habari huenda labda una namba nyingine au mnakutana kwenye group la class whatsapp siunajua sisi wengine tunamiliki viswaswadu”.
“Akipatikana au akijoin kwa group ntakustua ila kwa sasa sina mawasiliano naye, ila mbona kama unamsaka kwa udi na uvumba hivyo kwema kweli”.
“Duuh mwanangu Shebi mbona umenishikia shilingi hivyo wala hakuna shida yoyote ile nimekwambia ni mwana tu au kwa sababu ni wa kike ndo mana unanikabia kwa juu hivyo”.
“Basi usiwaze tukimpata tutakwambia sema ungetuweka wazi tujue kama amemaliza na kichanga chetu tumboni tuongeze juhudi maradufu ya kumtafuta”.
“Hamna mwanangu amini kwamba, ni mwana tu”
“Sawa nimekuelewa mwanangu nilikuwa nakuzingua tu kwani unafikiri hatujui kuwa umekufa kwa Linda”
“Linda tena?”
“Acha uhuni baba Linda kwahiyo unataka umkane Linda mbele yangu kuwa siyo demu wako?”
“Asa mi sindo nakupangilia yule mi mshikaji wangu tu tulikua tunapeana sapoti kwenye kusoma na vitu vidogovidogo ila swala la mahusiano na yeye kwakweli halipo”
“Aah we jamaa kwakukana umenishinda tabia wakati kila mtu pale class anajua juu ya uhusiano wenu Linda mwenyewe hata ukimpigia sasa hivi ukamuita mama K anafurahi kweli na anapenda kinoma ila wewe mwanangu sababu hayupo karibu na hawezi kutusikia ndo unajifanya kumkana siyo fair hivyo”.
“Siyo kwamba anafurahi ila anakucheka kwa maana hujui juu ya unachokisema ila ni mshikaji, ni mwana ni kampani ndo ilikuwa inatufanya tuwe karibu vile wala hakuna cha ziada”
“Sawa ngoja nimuunganishe kwenye simu afu umkane akisikia wewe siunajikuta Petro unaweza kukana watu kweupe”
“Oya Shebi kwani leo umekula nini mbona umeniamulia hivyo tatizo ni nini kwani"
“Tatizo ni kwamba unawakana wadada za watu kwasababu tu hawapo subiri nifanye mpango nimuunge akusikie”
“Kausha Shebi usimuunganishe bana usije kuniletea msala nishaichoka mimi”
“Umeona eeh hutaki kumbe kweli ni demu wako”.
Siku ziliendelea kusonga mithili ya maji yaliyopita kwenye mkondo wake, siku moja jamaa yangu mmoja aitwaye Ambrose alinitafuta kwenye simu na kunipa taarifa ya kuwa nimekuwa miongoni mwa wanafunzi waliochaguliwa na Jeshi la kujenga taifa kuhudhuria mafunzo ya kijeshi kama ilivyo sera ya elimu kwa wanafunzi wanaohitimu kidato cha sita nchini Tanzania. ,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,
Itaendelea……………………………………………