Maisha ya depo

Maisha ya depo

MAISHA YA DEPO

SEASON-1

EPISODE 05

Binafsi haikuwa taarifa nzuri kwangu, sikuipokea siyo tu kwa mikono miwili bali hata kwa kidole kimoja sikuweza kuipokea taarifa ile hata kwa moyo mmoja.

Mpaka muda huo sikuwa nalipenda jeshi kwa ujumla, nilizisikia taarifa nyingi ambazo zilinifanya nilichukie jeshi.

Ugumu wa kazi na mazoezi yaliyopelekea ulemavu na vifo ni miongoni mwa mambo yaliyonifanya nikalichukia jeshi hilo.Kwangu sikuhitaji kuwa maiti ndiyo nizijue mbivu na mbichi za kaburi, wala sikuhitaji niingie kati nicheze ndiyo niweze kuzijua raha za ngoma, fununu nilizozisikia mtaani zilinitosha kuhitimisha kuwa mafunzo ya jeshi ni njia ya kwenda kuzimu.

Kwakuwa Ambrose yeye alikuwa na simu ya kisasa alipata orodha ya baadhi ya wanadarasa waliochaguliwa kwenda mafunzoni.

Alinijuza miongoni mwao na kunifahamisha kuwa mimi, yeye na Linda ni miongoni mwa tuliopangiwa kushiriki mafunzo hayo kwenye kambi moja.

Nilijaribu kumuuliza kuhusu Zai naye kama kapangwa kambi sawa nasi ila aliniambia hakumuona kwenye orodha na nilipomuuliza kama anawasiliana naye majibu alinipa yaleyale ya kila siku kuwa namba aliyonayo haipatikani.

Basi bwana mrembo Zai aliendelea kuwa bidhaa adimu kwangu, hali iliyonizidishia hamu ya kutolipenda jeshi mana mbali ya kuwa nafsi iliamua kuwa sitohudhuria mafunzo ila ikitokea Zai akapangiwa kambi moja na mimi nisingesita kwenda hata kama ningekutana na kifo changu huko basi ningekuwa radhi kufa ili mradi nipate ukaribu naye mana niliamini kuwa bado ninahitaji muda wa kuwa karibu naye.

Taarifa zile ziliwafikia nyumbani ambako licha ya kujifanya sijui kinachoendelea huku nikisingizia uwezo wa simu niliyo nayo wao walitumia simu zao kufuatilia kwa undani kama nimepangiwa ama vinginevyo.

Walifanya hivyo mpaka pale walipofanikiwa kuliona jina langu na kunijuza nami sikusita kuwaambia msimamo wangu kuwa sipo tayari kwenda.

Msimamo huo ulizua mtafaruku nyumbani ingawaje wapo baadhi walitaka nisikilizwe ila shida ilikuwa kwa mkuu wa kaya ambaye yeye alitaka niende huko.

Baba mjengo huyo aliyekuwa akifahamika kwa jina la Mzee Mjuzi yeye aliamini kuwa mafunzo ya kijeshi yangenifanya niwe mkakamavu na mzalendo kwa taifa hivyo kuwa tayari wakati wowote kulitumikia taifa.

Alikuwa akiniambia kuwa serikali ina maana yake kufanya hivyo na siwezi jua mana huenda siku za mbele wale waliohudhuria mafunzo hayo wakawa ni kipaumbele kwa upande wa ajira.

Alinithibitishia hilo kwa kunipa mifano ya viongozi mbalimbali wa juu nchini wamehudhuria mafunzo ya kijeshi hivyo huenda ikawa kuna ngazi ya utawala ama uongozi wa nchi nisingeweza kuzihudumu pasi na kuwa na cheti ama historia ya kupitia mafunzo hayo kwasababu wanaamini hao watakuwa na uzalendo kwa taifa.

Mzee alinisisitiza kuwa siwezi jua mana wakati mwingine taasisi mbalimbali za kijeshi na usalama wa taifa hutumia Jeshi la kujenga taifa kupata watumishi wapya pengine ingeniangukia bahati na ikawa njia fupi kwangu ya kupata ajira ya kudumu.

Baada ya kikao hicho kikuu viliendelea vikao vidogodogo lengo likiwa ni kunisisitiza kufanya maandalizi mana siku za kuripoti zilikuwa zikikaribia.

Hakuna kauli ambazo ziliniumiza kutoka kwa mzee huyo pale aliponiambia nikienda jeshini nitakuwa mkakamavu na mzalendo.

Nafsini nilijiambia huenda nikawa siyo mzalendo kweli lakini je ameniona mimi ni legelege kiasi hicho kiasi cha kwenda kufanywa kuwa mkakamavu.

Nilichukia sana ila nilihitimisha kwa kujisemea moyoni kuwa mshua jau kauli ambayo ilinipunguza hasira juu ya kauli zake.

Wakati yote hayo yakiendelea nilikuwa nikiwasiliana na Linda ambaye yeye alifurahi mno kupangwa kambi moja na mimi na aliniambia kuwa hapo awali hakuwa tayari kwenda jeshini na wazazi wake waliriridhia.

Linda aliniambia kuwa kama itatokea niko tayari kwenda basi na yeye angekuwa tayari kuwaambia wazazi wake kuwa amebadili msimamo wake na hatimaye angekwenda.

Ama kweli penye miti hapana wajenzi yaani utayari wangu wa kwenda mafunzoni kwa ajili ya Zainabu hautofatiani na wa Linda kwangu ila ugumu uko hapo tu Linda yupo tayari kwenda kwa ajili yangu ila mimi sipo tayari kwenda kwaajili yake na kinyume chake niko tayari kwenda kwaajili ya Zainabu ingawaje sikufahamu utayari wa Zainabu kwangu.

Kifupi nilitamani sana Linda awe Zainabu ili jambo liwe jepesi.

Kadri siku zilivyokuwa zikiongeza namba ndivyo maudhi yalikuwa yakizidi maana kikubwa ilikuwa ni ukakamavu, nidhamu na uzalendo kana kwamba ni vitu ambavyo sina.

Niliamua kukaa chini na kufanya tafakuri ya kina nikaona nikiendelea kukaa humo nitakuwa nikigombana na watu wasiostahili kila siku mana hata wale waliokuwa wakiniunga mkono walinisihi sana kumsikiliza mshua kwa maana kuwa kumpinga yeye ni sawa na kumdharau.,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,

Itaendelea....................................
Samahanini sana wanajukwaa kwa kuwaweka kinyonge mambo yamekuwa mengi kwakweli ila leo tupo live msicheze mbali maana itakuwa ni kipande baada ya kipande.

Baada ya hayo naomba kufungua kikao.

MAISHA YA DEPO

SEASON-1

EPISODE 04

Nilijitetea kwa kumwambia kuwa “Namba siioni na hata leo hii mchana nimejitahidi kufukunyua kwenye begi lakini wapi, hata hivyo ile siku natoka pale bweni la Mikumi mpaka napanda basi la kuja nyumbani ilikuwa ni shughuli Mamdogo.

Nilipofika nyumbani begi lenyewe nilipokelewa nimekuja kulishika siku ya pili yaani kurupushani zilikuwa ni zaidi ya nyingi wala sijafanya kusudi kutokukutafuta”.

Baada ya maneno hayo nilisikia sauti ya Kichaga ikisema “Ewe Mungu wa majeshi embu shuka duniani uje umnusuru mtu wako huyu aliyejawa na damu ya uwongo kwenye mishipa yake, yaani anavyoongea ni kana kwamba ile namba nilimuandikia kwenye kikaratasi”
kwakweli nilijichanganya hali iliyonifanya nibaki kimya na kumuacha aongee yeye tu.

Linda aliendelea kuongea na kuniuliza “umeshindwaje kuomba kwa mtu jamani, mbona wana wengi tu wanayo”.

Nikapata nguvu za kumjibu ila kwa sauti ya upole sana nikamwambia “Samahani sikuwa na wazo hilo ila nilikuwa naamini ninayo hivyo ipo siku ningeiona tu”.

Basi mazungumzo yalikuwa ni mengi ila kikubwa ilikuwa ni kwanini sikumtafuta siku zote hizo, kwakua nilikuwa nikimfahamu vizuri sikuhitajika kutumia nguvu nyingi kujitetea nilichofanya nilimtuliza nikampooza na hatimaye jazba likamshuka.

Nilijaribu kumdodosa Linda kama kuna watu bado hawajamaliza mitihani, aliniambia kuwa wamewaacha PCB na CBG wanasubiri practical ya Biology ila kesho yake ndiyo wanamalizia.

Maneno hayo yalinipa matumaini ya kwamba huenda Zai hakunipa namba ya uongo ila bado yuko shule na ndiyo maana hapatikani kwenye simu.

Nilitamani kumuuliza Linda kama kweli Zai naye ni miongoni mwa wale aliowaacha ila nikaona ni bora niache maana ataniona kama namjali Zai kuliko yeye kitu ambacho hakipendi na zaidi ya hapo ni kuwa tumetoka kumaliza swala kama hilo la kutomjali yeye.

Niliendelea kufanya juhudi za kumtafuta Zai pasi na mafanikio kwani hata pale nilipoulizia kama wamekwisharudi nyumbani wanafunzi wote waliomaliza kidato cha sita niliambiwa wamerudi ila kila nilipompigia msichana yule majibu yalikuwa ni yale yale “hapatikani”.

Siku moja nilipokuwa naongea na Shebi nilijaribu kumdodosa kuhusu Zainabu “oya hivi Zainabu unaongea naye kweli”“Zainabu yupi?”“Zainabu Khamisi yule dada wa CBG tumemaliza naye pale kiskuli”“Anhaah yule hapana nasikia kwenye simu hapatikani hata mimi kuna siku nilimpigia ila sikumpata, vipi kwani shemeji yetu nini”.

“Hapana ni mwana tu nimempigia sana ila naona kila nikipiga hapatikani nikaona nikuulize afisa habari huenda labda una namba nyingine au mnakutana kwenye group la class whatsapp siunajua sisi wengine tunamiliki viswaswadu”.

“Akipatikana au akijoin kwa group ntakustua ila kwa sasa sina mawasiliano naye, ila mbona kama unamsaka kwa udi na uvumba hivyo kwema kweli”.

“Duuh mwanangu Shebi mbona umenishikia shilingi hivyo wala hakuna shida yoyote ile nimekwambia ni mwana tu au kwa sababu ni wa kike ndo mana unanikabia kwa juu hivyo”.

“Basi usiwaze tukimpata tutakwambia sema ungetuweka wazi tujue kama amemaliza na kichanga chetu tumboni tuongeze juhudi maradufu ya kumtafuta”.

“Hamna mwanangu amini kwamba, ni mwana tu”

“Sawa nimekuelewa mwanangu nilikuwa nakuzingua tu kwani unafikiri hatujui kuwa umekufa kwa Linda”

“Linda tena?”

“Acha uhuni baba Linda kwahiyo unataka umkane Linda mbele yangu kuwa siyo demu wako?”

“Asa mi sindo nakupangilia yule mi mshikaji wangu tu tulikua tunapeana sapoti kwenye kusoma na vitu vidogovidogo ila swala la mahusiano na yeye kwakweli halipo”

“Aah we jamaa kwakukana umenishinda tabia wakati kila mtu pale class anajua juu ya uhusiano wenu Linda mwenyewe hata ukimpigia sasa hivi ukamuita mama K anafurahi kweli na anapenda kinoma ila wewe mwanangu sababu hayupo karibu na hawezi kutusikia ndo unajifanya kumkana siyo fair hivyo”.

“Siyo kwamba anafurahi ila anakucheka kwa maana hujui juu ya unachokisema ila ni mshikaji, ni mwana ni kampani ndo ilikuwa inatufanya tuwe karibu vile wala hakuna cha ziada”

“Sawa ngoja nimuunganishe kwenye simu afu umkane akisikia wewe siunajikuta Petro unaweza kukana watu kweupe”

“Oya Shebi kwani leo umekula nini mbona umeniamulia hivyo tatizo ni nini kwani"

“Tatizo ni kwamba unawakana wadada za watu kwasababu tu hawapo subiri nifanye mpango nimuunge akusikie”

“Kausha Shebi usimuunganishe bana usije kuniletea msala nishaichoka mimi”

“Umeona eeh hutaki kumbe kweli ni demu wako”.

Siku ziliendelea kusonga mithili ya maji yaliyopita kwenye mkondo wake, siku moja jamaa yangu mmoja aitwaye Ambrose alinitafuta kwenye simu na kunipa taarifa ya kuwa nimekuwa miongoni mwa wanafunzi waliochaguliwa na Jeshi la kujenga taifa kuhudhuria mafunzo ya kijeshi kama ilivyo sera ya elimu kwa wanafunzi wanaohitimu kidato cha sita nchini Tanzania. ,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,

Itaendelea……………………………………………
 
MAISHA YA DEPO

SEASON-1

EPISODE 05

Binafsi haikuwa taarifa nzuri kwangu, sikuipokea siyo tu kwa mikono miwili bali hata kwa kidole kimoja sikuweza kuipokea taarifa ile hata kwa moyo mmoja.

Mpaka muda huo sikuwa nalipenda jeshi kwa ujumla, nilizisikia taarifa nyingi ambazo zilinifanya nilichukie jeshi.

Ugumu wa kazi na mazoezi yaliyopelekea ulemavu na vifo ni miongoni mwa mambo yaliyonifanya nikalichukia jeshi hilo.Kwangu sikuhitaji kuwa maiti ndiyo nizijue mbivu na mbichi za kaburi, wala sikuhitaji niingie kati nicheze ndiyo niweze kuzijua raha za ngoma, fununu nilizozisikia mtaani zilinitosha kuhitimisha kuwa mafunzo ya jeshi ni njia ya kwenda kuzimu.

Kwakuwa Ambrose yeye alikuwa na simu ya kisasa alipata orodha ya baadhi ya wanadarasa waliochaguliwa kwenda mafunzoni.

Alinijuza miongoni mwao na kunifahamisha kuwa mimi, yeye na Linda ni miongoni mwa tuliopangiwa kushiriki mafunzo hayo kwenye kambi moja.

Nilijaribu kumuuliza kuhusu Zai naye kama kapangwa kambi sawa nasi ila aliniambia hakumuona kwenye orodha na nilipomuuliza kama anawasiliana naye majibu alinipa yaleyale ya kila siku kuwa namba aliyonayo haipatikani.

Basi bwana mrembo Zai aliendelea kuwa bidhaa adimu kwangu, hali iliyonizidishia hamu ya kutolipenda jeshi mana mbali ya kuwa nafsi iliamua kuwa sitohudhuria mafunzo ila ikitokea Zai akapangiwa kambi moja na mimi nisingesita kwenda hata kama ningekutana na kifo changu huko basi ningekuwa radhi kufa ili mradi nipate ukaribu naye mana niliamini kuwa bado ninahitaji muda wa kuwa karibu naye.

Taarifa zile ziliwafikia nyumbani ambako licha ya kujifanya sijui kinachoendelea huku nikisingizia uwezo wa simu niliyo nayo wao walitumia simu zao kufuatilia kwa undani kama nimepangiwa ama vinginevyo.

Walifanya hivyo mpaka pale walipofanikiwa kuliona jina langu na kunijuza nami sikusita kuwaambia msimamo wangu kuwa sipo tayari kwenda.

Msimamo huo ulizua mtafaruku nyumbani ingawaje wapo baadhi walitaka nisikilizwe ila shida ilikuwa kwa mkuu wa kaya ambaye yeye alitaka niende huko.

Baba mjengo huyo aliyekuwa akifahamika kwa jina la Mzee Mjuzi yeye aliamini kuwa mafunzo ya kijeshi yangenifanya niwe mkakamavu na mzalendo kwa taifa hivyo kuwa tayari wakati wowote kulitumikia taifa.

Alikuwa akiniambia kuwa serikali ina maana yake kufanya hivyo na siwezi jua mana huenda siku za mbele wale waliohudhuria mafunzo hayo wakawa ni kipaumbele kwa upande wa ajira.

Alinithibitishia hilo kwa kunipa mifano ya viongozi mbalimbali wa juu nchini wamehudhuria mafunzo ya kijeshi hivyo huenda ikawa kuna ngazi ya utawala ama uongozi wa nchi nisingeweza kuzihudumu pasi na kuwa na cheti ama historia ya kupitia mafunzo hayo kwasababu wanaamini hao watakuwa na uzalendo kwa taifa.

Mzee alinisisitiza kuwa siwezi jua mana wakati mwingine taasisi mbalimbali za kijeshi na usalama wa taifa hutumia Jeshi la kujenga taifa kupata watumishi wapya pengine ingeniangukia bahati na ikawa njia fupi kwangu ya kupata ajira ya kudumu.

Baada ya kikao hicho kikuu viliendelea vikao vidogodogo lengo likiwa ni kunisisitiza kufanya maandalizi mana siku za kuripoti zilikuwa zikikaribia.

Hakuna kauli ambazo ziliniumiza kutoka kwa mzee huyo pale aliponiambia nikienda jeshini nitakuwa mkakamavu na mzalendo.

Nafsini nilijiambia huenda nikawa siyo mzalendo kweli lakini je ameniona mimi ni legelege kiasi hicho kiasi cha kwenda kufanywa kuwa mkakamavu.

Nilichukia sana ila nilihitimisha kwa kujisemea moyoni kuwa mshua jau kauli ambayo ilinipunguza hasira juu ya kauli zake.

Wakati yote hayo yakiendelea nilikuwa nikiwasiliana na Linda ambaye yeye alifurahi mno kupangwa kambi moja na mimi na aliniambia kuwa hapo awali hakuwa tayari kwenda jeshini na wazazi wake waliriridhia.

Linda aliniambia kuwa kama itatokea niko tayari kwenda basi na yeye angekuwa tayari kuwaambia wazazi wake kuwa amebadili msimamo wake na hatimaye angekwenda.

Ama kweli penye miti hapana wajenzi yaani utayari wangu wa kwenda mafunzoni kwa ajili ya Zainabu hautofatiani na wa Linda kwangu ila ugumu uko hapo tu Linda yupo tayari kwenda kwa ajili yangu ila mimi sipo tayari kwenda kwaajili yake na kinyume chake niko tayari kwenda kwaajili ya Zainabu ingawaje sikufahamu utayari wa Zainabu kwangu.

Kifupi nilitamani sana Linda awe Zainabu ili jambo liwe jepesi.

Kadri siku zilivyokuwa zikiongeza namba ndivyo maudhi yalikuwa yakizidi maana kikubwa ilikuwa ni ukakamavu, nidhamu na uzalendo kana kwamba ni vitu ambavyo sina.

Niliamua kukaa chini na kufanya tafakuri ya kina nikaona nikiendelea kukaa humo nitakuwa nikigombana na watu wasiostahili kila siku mana hata wale waliokuwa wakiniunga mkono walinisihi sana kumsikiliza mshua kwa maana kuwa kumpinga yeye ni sawa na kumdharau.,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,

Itaendelea....................................
MAISHA YA DEPO

SEASON-1

EPISODE 06

Nikiwa natafuta suluhisho juu ya hilo niliwaza baadhi ya vitu haswa juu ya nadharia inayodai kuwa kuhudhuria mafunzo ya jeshi ni njia ya kwenda kuzimu.

Nilijiambia kama kweli ni njia ya kuzimu je, wanajeshi walioajiriwa wametokea wapi? kuzimu au makaburini? nikaona hakuna ukweli katika hilo.

Lakini pia nikaona namba kubwa ya wanadarasa tuliochaguliwa kambi moja walikuwa na utayari wa kuhudhuria mafunzo hivyo suluhisho la zile dhihaka, dharau na maugomvi ya kila siku ni kwenda jeshini.

Mtu wa kwanza kumjuza hili alikuwa ni swahiba wangu Linda ambaye alionekana kufurahi zaidi.

Aliniambia alikwisha wabadili mawazo wazazi wake mara baada ya kujua kuwa tumepangwa kambi moja akijua ya kwamba nami nisingekataa hivyo alisubiri muda tu ufike.

Sikumwambia juu ya kilichokuwa kinaendelea nyumbani ila niliamua kumpongeza kwa ushawishi wake ili aone kama niko pamoja naye na mwenye thamani kwangu.

Kazi kubwa ilikuwa ni namna ya kuwaambia nyumbani kuwa nimebadili msimamo na niko tayari kwenda jeshini.

Basi nikawa natafuta namna ambayo nitawaambia, ilifika ile siku ya wanafunzi kuripoti kwenye kambi walizopangiwa.

Siku hiyo asubuhi yake nilijichelewesha kuamka makusudi nikijua kwamba kwa namna yoyote ile Mzee Mjuzi lazima angenigombeza huku akilitilia mkazo swala la kwenda jeshini.

Mzee Mjuzi ana kawaida ya kuja mpaka vyumbani kutuamsha pale anapoamka kabla yetu hivyo nilijua kuwa angekuja tu.

Kwakuwa kilikuwa ni kipindi cha likizo nyumba ilikuwa na utajiri wa watoto ambao walikuwa wanasaidia kazi ndogondogo za nyumbani kama vile kufagia, kudeki kuosha vyombo n.k.

Kwa mbali nilisikia sauti ya mshua ikinena “embu niamshieni huyo mtoto wa mfalme anayelala kama yupo kwenye kasri la Malikia Elizabeth”.

Niliposikia nikajisemea moyoni “Kumekucha kumekucha” mshua alikuwa haishiwi na maneno ya kejeli na maudhi nilijitahidi kumzoea ila ilikua ni vigumu kumzoea ilinibidi kuzivumilia tabu zake.

Alikuja kuniamsha mdogo wangu aitwaye Amiri aliyenijuza kuwa baba mwenye nyumba kasema niamke, nilimtingishia kichwa kuashiria kuwa nimeelewa.

Zilinichukua dakika kama kumi kutoka mule ndani nikiwa na mswaki mkononi kufuata dawa ya meno na maji yaliyokuwa jikoni.

Nilimuona mshua akiangalia uchambuzi wa habari kwenye televisheni iliyopo sebuleni ambako ndiko iliko dawa ya meno.

Nilipiga hesabu nianzie sebuleni ili nikifuata maji jikoni nitoke nje kupitia mlango wa jikoni au nianze kuchukua maji alafu nikaweke dawa na kutokea mlango wa mbele.

Kwa kuwa lengo lilikuwa ni kumchangamsha mzee baba nikaamua nitokee mlango wa mbele.

Nilipofika sebuleni nilimsalimia baba aliyeitika na kunitaka nisogee kule aliko niliweka dawa na kumfuata nilipofika tu nilianza kusomewa mashitaka.

“Naona siku hizi umeshaota mapembe unaamka muda unaotaka husaidii kazi unachoweza wewe kula, kulala na kuzurura tu.

“Namtuma mdogo wako akuite bado unakuja kwa kujisikia umekua siku hizi siyo? au unaona hatuna cha kukufanya, humuogopi yeyote? Sawa Sasa nataka uniambie vyenye kueleweka utaenda jeshini au unataka kubaki hapa na kuishi kifalme kama utakavyo”.

“Na kwa mfumo huo uutakao kwangu hapana labda uende kwa bibi yako nasikia ameanza kuvuna nafikiri huko ndiko kunako kufaa”.

Naam kifupi mshua alitema nyongo na povu lilimtoka haswa, tulikaa kikao kwa muda na nilimweleza kwamba niko tayari kwenda ingawaje sijapenda ila nitaenda kwasababu ametaka.

Alionekana kufurahi na akaniambia nijiandae mchana niende mjini nikanunue vifaa vinavyohitajika jeshini likiwemo shuka za rangi ya samawati, pea ya viatu na tisheti ya rangi ya kijani sambamba na kaptula ya rangi ya buluu ya kuiva, sanduku la chuma (tranker), truck suit n.k.

Mzee Mjuzi aliniachia kiasi cha pesa ambapo mchana wake nilikwenda mjini kutafuta vitu hivyo.

Vitu vilionekana kuwa adimu sokoni na hata vilipopatikana vilikuwa bei juu yaani wafanyabiashara hawajawahi kuiacha fursa yeyote ile iwapite.

Nilirudi nyumbani nikiwa nimefanikiwa kupata shuka na viatu vya kijani ya mchongo yaani nilijitwalia zangu viatu vyenye doa la kijani maana nilizurura vya kutosha mpaka jua likaanza kuzama.

Asubuhi yake ilikuwa ni siku ya mnada kwenye moja ya gulio karibu na nyumbani.

Niliongozana na mzee aliyekuwa anahisi nimekosa vitu hivyo kwa makusudi kwakuwa sikuwa na nia ya kwenda sikutaka kujibizana naye kwasababu hakuwepo hivyo nilimuacha akajionee.

Tulifika gulioni na kilichotokea ilikuwa ni kivumbi na jasho yaani vitu vilikuwa adimu na vilivyopatikana vilipatikana kwa bei iliyochangamka. ,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,

Itaendelea………………………………………………….
 
Bad news 😂
 
MAISHA YA DEPO

SEASON-1

EPISODE 07

Tulirudi nyumbani mchana tukiwa tumechoka sana, nilitakiwa kuondoka siku hiyo mchana lakini ilibidi tughairishe.

Tulipata baadhi ya vitu na vingine tuliambiwa kuwa tunaweza vipata kulekule jeshini.

Basi siku ya pili ilikatika na angalau ilimalizika vizuri ukilinganisha na siku za nyuma tangu itoke orodha ya majina kujiunga JKT.

Usiku nilifanya maandalizi ya mwisho na kiliandaliwa chakula maalum kwa ajili ya kuagwa kifupi ulikuwa ni usiku mzuri ukiachilia mbali na mapochopocho yaliyokuwa mezani bali ni furaha ya kila mmoja wetu japo furaha yangu ilikuwa ni ya kuigiza.

Safari ilianza mapema tu kulipokucha niliwaaga nyumbani na kuongozana na mshua mpaka kilipo kituao cha mabasi ya mkoa.

Alinikatia tiketi na kunichia pesa ya kujikimu na safari ilianza mnamo saa 1:30 asubuhi yaani mzee ilibidi ahakikishe basi linaondoka maana nafikiri alihisi ningeweza kubadili ruti na kwenda sehemu nyingine.

Safari ilikuwa ni ndefu kwa upande wangu kwani ukiachilia mbali na kuchukua muda mrefu njiani lakini pia nilikuwa na mawazo mengi juu ya dhana zilizojengeka mtaani kuhusiana na mafunzo ya kijeshi.

Safari ilifika ukomo mnamo saa tisa ya alasiri ambapo tuliwasili kituo cha mabasi, tuliteremka kutoka kwenye basi na kila mmoja kuendelea na ustaarabu wake.

Kwakuwa nilikuwa na ugeni mwingi eneo hilo ilinibidi niulizie kwa wapiga debe unakopatikana usafiri wa kuelekea iliko kambi.

Nilijuzwa kuwa ni mwendo wa saa moja mpaka kufika eneo husika na usafiri upo mpaka mishale ya saa mbili za usiku.

Kwa maelezo hayo tayari nilikuwa na uhakika wa kuendelea kubaki mtaani kwa muda na kufanya niliyobakiza kabla sijaenda kujitupa kwa makamanda hata hivyo sikupenda kufika mapema niliona ni vyema nikajichelewesha kidogo.

Niliacha sanduku langu kwa moja ya ofisi ya ajenti wa kampuni ya mabasi na kutoka nje ambako nilipata wasaa wa kwenda nyumba ya ibada kumuomba Mwenyezi Mungu anijalie safari njema katika maisha ambayo sikuwahi kufikiria kuja kuyapitia na hakika nilipofika huko nilikaa kitako haswa.

Nilipomaliza nilipita saluni ambako nilikwenda kutoa nywele kichwani kuendana na mazingira ya kule niendako yaani nilienda kuangusha dongo kichwani.

Kinyozi hakuwa akiniamini nilipomwambia kuwa aninyoe para ila baadaye alinielewa alipogundua kuwa naelekea jeshini.

Nilipomaliza nilitoka na kuelekea sehemu moja ambayo watu walikuwa wakipooza nafsi zao na kumwagilia mioyo.

Niliagiza kinywaji kimoja laini ambacho hakikuwa na shida kushuka kwenye kolomeo langu yaani soda.

Niliinywa soda hiyo kwa mafungu huku nikijiuliza hivi ni kweli naenda jeshini? Ni kwa matakwa yangu mwenyewe au kuna mtu kanishikia akili? Je, itakuwaje mwisho wa siku nitarudi nikiwa hai kweli au ndo naenda kukabidhisha roho kwa malaika wavaa kombati? Maswali yalikuwa ni mengi kiasi kwamba nilikosa majibu sahihi ila lilikuja hitimisho kuwa liwalo na liwe acha niende nikirudi salama Alhamdulillah na ikitokea tofauti Familillah.

Basi nilipomaliza hapo nikaongoza kituo cha mabasi ambako yule ajenti alimuita bodaboda aliyenipeleka moja kwa moja kilipo kituo kidogo cha magari yanayoelekea kambini.

Safari iliwadia na mnamo majira ya saa kumi na moja tulifika na kushuka watu kadhaa pale kituoni.

Nilijikokota na kukaa kwenye banda la chipsi lililokuwepo eneo hilo, nilikaa kwa muda nikitafakari juu ya safari niliyokuwa nikiiendea mana ilionekana kama bado akili haijakubaliana na ninachokifanya.

Halmashauri ya kichwa ilifika hatua ikaniambia “mpaka hapa ulipofika ni hatua nyingi umeziendea huwezi kurudi nyuma malizia hizi chache ulizobakiza”.

Nafsi nayo haikusita kunena na moyo ukauambia “Hapa ndiyo bagamoyo rafiki yangu, sehemu ambayo watu kutoka bara walifika na kuibwaga mioyo yao pindi ambapo walipokutana na ngalawa zilizokuwa zikiwasubiri pwani ya Afrika mashariki zama za utumwa”.

Naam huo ndiyo ukweli niliotakiwa kuupokea kwa wakati huo ilibidi nami niubwage moyo wangu pale stendi ambapo mbele yangu niliona watu waliovaa sare wakielekea njia moja ambapo niliamini wanakwenda kambini.

Nikiwa najishauri kuondoka alitokea jamaa mmoja na kuniambia.
“Oya niaje”
“Fresh, nambie” nikamjibu
“Kama kawa si unaelekea JKT”
“Ndio vipi ”
“Hamna nakustua tu twende wote mi mwenyewe naelekea hukohuko”
“Basi poa twenzao”. ,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,

Mwisho wa Msimu wa kwaza wa simulizi ya MAISHA YA DEPO, tukutane msimu wa pili**
 
Hatujamalidhaaaaaaaa.......................

Maandalizi ya Muendelezo wa simulizi ya MAISHA YA DEPO Msimu wa pili hatimaye umejamilika.

Kwanini hutakiwi kukosa, kwasababu msimu wa kabla yake umetuacha na maswali yafuatayo :

1) Ni kweli mchizi atafika kikosini hachelewi kuchepuka akaenda kujifanyia zake kozi mtaani maana yule naye hazieleweki ni kama ubongo umechanganyika na makamasi vile. 💩

2) Hivi mna uhakika Linda (mtoto wa kishua) wazazi wake walimruhusu kweli au kamchezea akili mwana.

3) Na vipi wote Linda na mwana wakienda kambini itakuwaje maana mdada ni kama ana tuhisia fulani hivi twachinichini sijui atafunguka ama mwana ataendelea kukaza. 👹

4) Vipi Zai atapatikana kweli, je akipatikana itakuwaje🤷‍♂️

Majibu ya haya yote yanapatikana kwenye msimu wa pili (Season-2) wenye vipande (Episode) zaidi ya 30 jitahidi usikose hata kimoja.

Yaani ni mpaka kielewekeeeeee...............

LogoMakerCa-1736878269969_1.jpg
 
View attachment 3207581
Kwa nijuavyo mimi

4) Zai atapatikana

3) Watakutana halafu watakazana kwenye mashamba ya jeshi

2) Watamkubalia tu ili akakazwe hawana namna si mtoto kautaka

1) Kwa jamaa yetu apo mi naomba tumuachie Mungu

Na ukidevela naisimulia mwenyewe
 
MAISHA YA DEPO

SEASON-2

EPISODE 01

Tulipiga hatua mojamoja mpaka lilipo geti lililofahamika kama geti namba 1, moja ya maafande alitusimamisha na kutuambia.

“Nyie kule bwana harusi na mpambe wake simama apoapo” tulitii na kusimama akaendelea kutuambia.

“Chuchumaeni na mniambie ni nani nyie”
“Sisi ni wanafunzi wa form six” mwenzangu alijibu.

“Anhaah kwahiyo mmeambiwa huku kuna shule”
“Hapana tumehitimu mwaka huu braza” mwenzangu aliendelea kujibu huku mimi nikiwa kimya nikihesabu na kugundua kuwa mapigo ya moyo wangu kwa dakika yameongezeka na yapo kasi mno.

“Sawa kumbe wahitimu haya niambieni mnakwenda wapi kwenye sherehe, bodi ya mikopo au mnafuata matokeo yenu baraza la mitihani”

“Hapana tumekuja Jkt, tumepangiwa kambi hii braza”
“Weeh koma hapa ni kambi ya jeshi namba HCH na unayeongea naye ni afande miongoni mwa maafande wa kambi hii braza ako umemuacha huko kwenu na sasa hivi yupo gereji anapokea pikipiki yenye pancha nne ili apate hela ya kwenda kumhonga wifi yako mmenielewa form six”.

“Ndiyo” aliitikia mwenzangu na nikasikia sauti nyinginezo zikiitika kutoka nyuma kumbe wapo wengine watatu waliungana nasi.

“Pumbavu nyinyi, sema ndiyo afande tumeelewana form six”

“Ndiyo afande” hapa tuliitikia kwa pamoja na mimi nikiwemo kidogo mwili wangu ulipata nguvu kwa wakati huu na afande aliendelea kutuambia.

“Haya simama juu up” alituambia huku akituonesha ishara ya kuamka kwa mikono yake nasi sote tukasimama kwa pamoja akatuambia tugeuke tulikotoka nasi tukafanya hivyo.

Afande yule alitukimbiza kwa raundi mbili na kuturudisha tulipokuwa awali ambapo alituamuru kila mmoja wetu kubeba vitu vyake kichwani.

Tulifanya hivyo na afande alitutaka turuke kichurachura kuelekea pale alipo binafsi nilikuwa na tranker pekee ila wapo miongoni mwetu walikuwa na begi la mgongoni na ndoo ya plastiki hawa walipata tabu afande akawaambia.

“Kama unaona huwezi kuja navyo vyote punguza vitu vyako na utavirudia kwa kichurachura nyie si mnajifanya mnakuja Jkt kama mmealikwa kwenye sendoff mnaogopa kuziharibu make up zenu fanyeni haraka”.

Tulimtii afande huyo aliyetutia jambajamba huku akitukazia uso na tulipofika alipo alituonesha uso wa tabasamu kana kwamba kamuona my wake baada ya kupotezana naye kwa siku shazi.

“Haahaahaah nimeyaweza ma form six, haya simameni muende pale walipo wenzenu” alituamuru twende sehemu ambayo ilionekana kuna wenzetu walikuwa wamekaa chini wakiendelea na taratibu nyingine.

Tulikwenda tulipoelekezwa na tukakaa ambapo moja ya afande tuliyemkuta eneo lile alikuwa akiorodhesha majina na kukusanya taarifa zetu kwenye daftari moja.

Taarifa hizo wao waliziita PARTICULARS,

Afande yule aitwaye Anna alituambia.
“Nyie maharamia ni nani kawaambia mkae huko njooni mkae hapa mbele”
Alituelekeza kukaa mbele ya meza aliyopo yeye ambapo tuliweza kutizamana naye yaani kwa kizungu naweza kusema tulikuwa naye perpendicular ama mkabala kwa Kiswahili cha kwenye kamusi.

“Wewe unaeweka kitambaa hembu toa na ukae chini zulia letu ni safi hilo halina najisi wala janaba” Afande Anna alimwambia mmoja wetu ambaye alikuwa akiweka kitambaa ardhini ili akae.

“Na nyie mlionyoa vipara nani kawaambia jeshini tunanyoa hivyo”.

“Hapana afande tumenyoa tu hakuna aliyetuambia” kwa mara hii nilifanikiwa kujibu kwa niaba ya wenzangu wawili kati ya wale watano ambao walinyoa kama mimi.

“Acha uongo wewe form six kaka ako ndo kakwambia siuna kaka mwanajeshi wewe”
“Hakuna afande sijaambiwa na mtu nanyoaga hivi tu”.

“Anhaah basi wewe utakuwa unavuta bangi uongo?” Aliniambia afande Anna huku akinitizama usoni akiwa amenikazia macho.

“Si kweli afande sivuti chochote”
“Mnnh muone macho yake mekunduu alafu unanikatalia huvuti bangi, eti nyie form six mtaani wanaovuta bangi si ndio hawa wanaonyoa midongo”.

“Hamna afande siyo wote” mmoja wetu alijibu wakati huu
“Anhaah mnateteana eeh sawa haya na nyie msio nyoa mliambiwa kuna saluni ya kuseti huku” Aliuliza afande Anna.

“Hapana afande”
“Au mmekuja kutuonesha fashion za nywele na misuko mana hapa naona kuna huyo mwenye nywele za kipemba, mwingine ana nywele ngumu za kisukuma kuna huyo katujia na twende kilioni tafadhali si mnawaona wenzenu pale wananyoana haya jiungeni nao” afande Anna aliwaambia wenzetu ambao hawakunyoa.

Afande Mbega ndiye aliyekuwepo mahala pale ambapo watu walikuwa wakinyolewa naye akawaambia“Sifa ya hapa ni kuwa na kiwembe na kama huna omba kwa wenzako ukikosa lete kichwa chako ntakunyoa na kipande cha chupa".

“Kama kuna mtu anaweza kunyoa awatoe wenzake nywele kabla jua halijazama mana hamtaruhusiwa kulala nazo”.

Afande Mbega aliendelea kuongea nasi huku akiendelea kunyoa wengine na wengine wakiwa kwenye foleni.
Afande Mbega alipoona idadi ya wanaohitaji kunyoa inaongezeka na jua linakaribia kuzama ilibidi awaambie.

“Ina maana nyie wote hamuwezi kunyoa, ok mtaweza tu” afande yule aliwagawa wawili wawili na kuwaambia.

“Sasa nyie mtanyoana tu iwe mnajua ama hamjui na ole wenu mkitoka Jkt mkafungue saluni mtaani”.

Basi waliendelea kunyoana na upande mwingine huku afande Anna aliendelea na sisi akatuambia.

“Haya nyie viumbe kama kuna mtu kutoka katerero ataje jina lake nianze naye” aliposema hivyo afande Mbega na wengine waliopo karibu waliangua vicheko na kuropoka waliyoweza kuyaropoka.

“Ina mana kati yenu hakuna yeyote kutoka katerero, na nyie huko saluni hakuna mtu wa katerero nimalizane naye kabisa” afande Anna aliuliza.

“Huku hakuna matroni ongea nao vizuri hao wanakuficha tu” Afande Mbega naye alijibu.

Kipindi yakiendelea hayo nilivuta kumbukumbu zangu zikaniambia kuwa Katerero ni moja ya sehemu inayopatikana mkoani Kagera nikawa najiuliza sasa ni kipi kinawafanya wacheke kwa ukubwa huo.

Kwa kuwa si kuwa najua kitu na kwa ugeni nilio nao nikaona si sawa kuwauliza niliamua kukaa kimya nikiamini kwamba usilolijua ni usiku giza ila ukilipa muda kutakucha na utalijua tu.

Nilijiapiza kuwa siku za mbele nitamfuata nimuulize walikuwa na maana ipi. ,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,

******Itaendelea………………………………

MAISHA YA DEPO

SEASON-1

EPISODE 07

Tulirudi nyumbani mchana tukiwa tumechoka sana, nilitakiwa kuondoka siku hiyo mchana lakini ilibidi tughairishe.

Tulipata baadhi ya vitu na vingine tuliambiwa kuwa tunaweza vipata kulekule jeshini.

Basi siku ya pili ilikatika na angalau ilimalizika vizuri ukilinganisha na siku za nyuma tangu itoke orodha ya majina kujiunga JKT.

Usiku nilifanya maandalizi ya mwisho na kiliandaliwa chakula maalum kwa ajili ya kuagwa kifupi ulikuwa ni usiku mzuri ukiachilia mbali na mapochopocho yaliyokuwa mezani bali ni furaha ya kila mmoja wetu japo furaha yangu ilikuwa ni ya kuigiza.

Safari ilianza mapema tu kulipokucha niliwaaga nyumbani na kuongozana na mshua mpaka kilipo kituao cha mabasi ya mkoa.

Alinikatia tiketi na kunichia pesa ya kujikimu na safari ilianza mnamo saa 1:30 asubuhi yaani mzee ilibidi ahakikishe basi linaondoka maana nafikiri alihisi ningeweza kubadili ruti na kwenda sehemu nyingine.

Safari ilikuwa ni ndefu kwa upande wangu kwani ukiachilia mbali na kuchukua muda mrefu njiani lakini pia nilikuwa na mawazo mengi juu ya dhana zilizojengeka mtaani kuhusiana na mafunzo ya kijeshi.

Safari ilifika ukomo mnamo saa tisa ya alasiri ambapo tuliwasili kituo cha mabasi, tuliteremka kutoka kwenye basi na kila mmoja kuendelea na ustaarabu wake.

Kwakuwa nilikuwa na ugeni mwingi eneo hilo ilinibidi niulizie kwa wapiga debe unakopatikana usafiri wa kuelekea iliko kambi.

Nilijuzwa kuwa ni mwendo wa saa moja mpaka kufika eneo husika na usafiri upo mpaka mishale ya saa mbili za usiku.

Kwa maelezo hayo tayari nilikuwa na uhakika wa kuendelea kubaki mtaani kwa muda na kufanya niliyobakiza kabla sijaenda kujitupa kwa makamanda hata hivyo sikupenda kufika mapema niliona ni vyema nikajichelewesha kidogo.

Niliacha sanduku langu kwa moja ya ofisi ya ajenti wa kampuni ya mabasi na kutoka nje ambako nilipata wasaa wa kwenda nyumba ya ibada kumuomba Mwenyezi Mungu anijalie safari njema katika maisha ambayo sikuwahi kufikiria kuja kuyapitia na hakika nilipofika huko nilikaa kitako haswa.

Nilipomaliza nilipita saluni ambako nilikwenda kutoa nywele kichwani kuendana na mazingira ya kule niendako yaani nilienda kuangusha dongo kichwani.

Kinyozi hakuwa akiniamini nilipomwambia kuwa aninyoe para ila baadaye alinielewa alipogundua kuwa naelekea jeshini.

Nilipomaliza nilitoka na kuelekea sehemu moja ambayo watu walikuwa wakipooza nafsi zao na kumwagilia mioyo.

Niliagiza kinywaji kimoja laini ambacho hakikuwa na shida kushuka kwenye kolomeo langu yaani soda.

Niliinywa soda hiyo kwa mafungu huku nikijiuliza hivi ni kweli naenda jeshini? Ni kwa matakwa yangu mwenyewe au kuna mtu kanishikia akili? Je, itakuwaje mwisho wa siku nitarudi nikiwa hai kweli au ndo naenda kukabidhisha roho kwa malaika wavaa kombati? Maswali yalikuwa ni mengi kiasi kwamba nilikosa majibu sahihi ila lilikuja hitimisho kuwa liwalo na liwe acha niende nikirudi salama Alhamdulillah na ikitokea tofauti Familillah.

Basi nilipomaliza hapo nikaongoza kituo cha mabasi ambako yule ajenti alimuita bodaboda aliyenipeleka moja kwa moja kilipo kituo kidogo cha magari yanayoelekea kambini.

Safari iliwadia na mnamo majira ya saa kumi na moja tulifika na kushuka watu kadhaa pale kituoni.

Nilijikokota na kukaa kwenye banda la chipsi lililokuwepo eneo hilo, nilikaa kwa muda nikitafakari juu ya safari niliyokuwa nikiiendea mana ilionekana kama bado akili haijakubaliana na ninachokifanya.

Halmashauri ya kichwa ilifika hatua ikaniambia “mpaka hapa ulipofika ni hatua nyingi umeziendea huwezi kurudi nyuma malizia hizi chache ulizobakiza”.

Nafsi nayo haikusita kunena na moyo ukauambia “Hapa ndiyo bagamoyo rafiki yangu, sehemu ambayo watu kutoka bara walifika na kuibwaga mioyo yao pindi ambapo walipokutana na ngalawa zilizokuwa zikiwasubiri pwani ya Afrika mashariki zama za utumwa”.

Naam huo ndiyo ukweli niliotakiwa kuupokea kwa wakati huo ilibidi nami niubwage moyo wangu pale stendi ambapo mbele yangu niliona watu waliovaa sare wakielekea njia moja ambapo niliamini wanakwenda kambini.

Nikiwa najishauri kuondoka alitokea jamaa mmoja na kuniambia.
“Oya niaje”
“Fresh, nambie” nikamjibu
“Kama kawa si unaelekea JKT”
“Ndio vipi ”
“Hamna nakustua tu twende wote mi mwenyewe naelekea hukohuko”
“Basi poa twenzao”. ,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,

Mwisho wa Msimu wa kwaza wa simulizi ya MAISHA YA DEPO, tukutane msimu wa pili**
 
MAISHA YA DEPO

SEASON-2

EPISODE 01

Tulipiga hatua mojamoja mpaka lilipo geti lililofahamika kama geti namba 1, moja ya maafande alitusimamisha na kutuambia.

“Nyie kule bwana harusi na mpambe wake simama apoapo” tulitii na kusimama akaendelea kutuambia.

“Chuchumaeni na mniambie ni nani nyie”
“Sisi ni wanafunzi wa form six” mwenzangu alijibu.

“Anhaah kwahiyo mmeambiwa huku kuna shule”
“Hapana tumehitimu mwaka huu braza” mwenzangu aliendelea kujibu huku mimi nikiwa kimya nikihesabu na kugundua kuwa mapigo ya moyo wangu kwa dakika yameongezeka na yapo kasi mno.

“Sawa kumbe wahitimu haya niambieni mnakwenda wapi kwenye sherehe, bodi ya mikopo au mnafuata matokeo yenu baraza la mitihani”

“Hapana tumekuja Jkt, tumepangiwa kambi hii braza”
“Weeh koma hapa ni kambi ya jeshi namba HCH na unayeongea naye ni afande miongoni mwa maafande wa kambi hii braza ako umemuacha huko kwenu na sasa hivi yupo gereji anapokea pikipiki yenye pancha nne ili apate hela ya kwenda kumhonga wifi yako mmenielewa form six”.

“Ndiyo” aliitikia mwenzangu na nikasikia sauti nyinginezo zikiitika kutoka nyuma kumbe wapo wengine watatu waliungana nasi.

“Pumbavu nyinyi, sema ndiyo afande tumeelewana form six”

“Ndiyo afande” hapa tuliitikia kwa pamoja na mimi nikiwemo kidogo mwili wangu ulipata nguvu kwa wakati huu na afande aliendelea kutuambia.

“Haya simama juu up” alituambia huku akituonesha ishara ya kuamka kwa mikono yake nasi sote tukasimama kwa pamoja akatuambia tugeuke tulikotoka nasi tukafanya hivyo.

Afande yule alitukimbiza kwa raundi mbili na kuturudisha tulipokuwa awali ambapo alituamuru kila mmoja wetu kubeba vitu vyake kichwani.

Tulifanya hivyo na afande alitutaka turuke kichurachura kuelekea pale alipo binafsi nilikuwa na tranker pekee ila wapo miongoni mwetu walikuwa na begi la mgongoni na ndoo ya plastiki hawa walipata tabu afande akawaambia.

“Kama unaona huwezi kuja navyo vyote punguza vitu vyako na utavirudia kwa kichurachura nyie si mnajifanya mnakuja Jkt kama mmealikwa kwenye sendoff mnaogopa kuziharibu make up zenu fanyeni haraka”.

Tulimtii afande huyo aliyetutia jambajamba huku akitukazia uso na tulipofika alipo alituonesha uso wa tabasamu kana kwamba kamuona my wake baada ya kupotezana naye kwa siku shazi.

“Haahaahaah nimeyaweza ma form six, haya simameni muende pale walipo wenzenu” alituamuru twende sehemu ambayo ilionekana kuna wenzetu walikuwa wamekaa chini wakiendelea na taratibu nyingine.

Tulikwenda tulipoelekezwa na tukakaa ambapo moja ya afande tuliyemkuta eneo lile alikuwa akiorodhesha majina na kukusanya taarifa zetu kwenye daftari moja.

Taarifa hizo wao waliziita PARTICULARS,

Afande yule aitwaye Anna alituambia.
“Nyie maharamia ni nani kawaambia mkae huko njooni mkae hapa mbele”
Alituelekeza kukaa mbele ya meza aliyopo yeye ambapo tuliweza kutizamana naye yaani kwa kizungu naweza kusema tulikuwa naye perpendicular ama mkabala kwa Kiswahili cha kwenye kamusi.

“Wewe unaeweka kitambaa hembu toa na ukae chini zulia letu ni safi hilo halina najisi wala janaba” Afande Anna alimwambia mmoja wetu ambaye alikuwa akiweka kitambaa ardhini ili akae.

“Na nyie mlionyoa vipara nani kawaambia jeshini tunanyoa hivyo”.

“Hapana afande tumenyoa tu hakuna aliyetuambia” kwa mara hii nilifanikiwa kujibu kwa niaba ya wenzangu wawili kati ya wale watano ambao walinyoa kama mimi.

“Acha uongo wewe form six kaka ako ndo kakwambia siuna kaka mwanajeshi wewe”
“Hakuna afande sijaambiwa na mtu nanyoaga hivi tu”.

“Anhaah basi wewe utakuwa unavuta bangi uongo?” Aliniambia afande Anna huku akinitizama usoni akiwa amenikazia macho.

“Si kweli afande sivuti chochote”
“Mnnh muone macho yake mekunduu alafu unanikatalia huvuti bangi, eti nyie form six mtaani wanaovuta bangi si ndio hawa wanaonyoa midongo”.

“Hamna afande siyo wote” mmoja wetu alijibu wakati huu
“Anhaah mnateteana eeh sawa haya na nyie msio nyoa mliambiwa kuna saluni ya kuseti huku” Aliuliza afande Anna.

“Hapana afande”
“Au mmekuja kutuonesha fashion za nywele na misuko mana hapa naona kuna huyo mwenye nywele za kipemba, mwingine ana nywele ngumu za kisukuma kuna huyo katujia na twende kilioni tafadhali si mnawaona wenzenu pale wananyoana haya jiungeni nao” afande Anna aliwaambia wenzetu ambao hawakunyoa.

Afande Mbega ndiye aliyekuwepo mahala pale ambapo watu walikuwa wakinyolewa naye akawaambia“Sifa ya hapa ni kuwa na kiwembe na kama huna omba kwa wenzako ukikosa lete kichwa chako ntakunyoa na kipande cha chupa".

“Kama kuna mtu anaweza kunyoa awatoe wenzake nywele kabla jua halijazama mana hamtaruhusiwa kulala nazo”.

Afande Mbega aliendelea kuongea nasi huku akiendelea kunyoa wengine na wengine wakiwa kwenye foleni.
Afande Mbega alipoona idadi ya wanaohitaji kunyoa inaongezeka na jua linakaribia kuzama ilibidi awaambie.

“Ina maana nyie wote hamuwezi kunyoa, ok mtaweza tu” afande yule aliwagawa wawili wawili na kuwaambia.

“Sasa nyie mtanyoana tu iwe mnajua ama hamjui na ole wenu mkitoka Jkt mkafungue saluni mtaani”.

Basi waliendelea kunyoana na upande mwingine huku afande Anna aliendelea na sisi akatuambia.

“Haya nyie viumbe kama kuna mtu kutoka katerero ataje jina lake nianze naye” aliposema hivyo afande Mbega na wengine waliopo karibu waliangua vicheko na kuropoka waliyoweza kuyaropoka.

“Ina mana kati yenu hakuna yeyote kutoka katerero, na nyie huko saluni hakuna mtu wa katerero nimalizane naye kabisa” afande Anna aliuliza.

“Huku hakuna matroni ongea nao vizuri hao wanakuficha tu” Afande Mbega naye alijibu.

Kipindi yakiendelea hayo nilivuta kumbukumbu zangu zikaniambia kuwa Katerero ni moja ya sehemu inayopatikana mkoani Kagera nikawa najiuliza sasa ni kipi kinawafanya wacheke kwa ukubwa huo.

Kwa kuwa si kuwa najua kitu na kwa ugeni nilio nao nikaona si sawa kuwauliza niliamua kukaa kimya nikiamini kwamba usilolijua ni usiku giza ila ukilipa muda kutakucha na utalijua tu.

Nilijiapiza kuwa siku za mbele nitamfuata nimuulize walikuwa na maana ipi. ,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,

******Itaendelea………………………………
MAISHA YA DEPO

SEASON-2

EPISODE 02

Nikiwa nawaza hayo afande Anna alinitoa kwenye mawazo akasema,
“Kama hakuna mtu wa Katerero hapa tuanze na wewe uliyenyoa kama umeambiwa huku tunalima bangi” Aliongea huku akininyooshea kidole.

Nilimjibu na kumpa taarifa kadha wa kadha zinazonihusu zikiwemo majina yangu, ya wazazi, nyumbani kwetu kwa maana mkoa, kata na hadi mtaa na taarifa nyingine nyingi.

Nilikuwa mtu wa 200 kuorodheshwa na tukiwa tunaendelea na zoezi hilo walipita wenzetu wakiwa na vindoo, majembe na makwanja wakiwa katika makundi vitatu.

Viumbe hao waliostahili kuitwa wachafu kuoga walikuwa wamejipanga kwenye mistari mitatu mitatu na walikuwa wakikimbia huku wakiimba nyimbo tofauti tofauti.Kundi la kwanza walipiga makofi huku wakiimba,

“Mwanzilishi: Namba unayopiga sasa
Waitikiaji: Haipatikani
Mwanzilishi: Namba unayopiga sasa
Waitikiaji: Haipatikani
Mwanzilishi: Mwenyewe yuko zake depo
Waitikiaji: Haipatikani
Mwanzilishi: Kriih! Kriiih!
Waitikiaji: Haipatikani”

Kundi la pili nalo lilisikika,

“Mwanzilishi: Radio call
Waitikiaji: Haina vocha
Mwanzilishi: Radio call
Waitikiaji: Haina vocha
Mwanzilishi: Taara tara
Waitikiaji: Taratibu”

Na kundi la tatu pia lilisikika likiimba

"Mwanzilishi: Canadian
Waitikiaji: Eeeh
Mwanzilishi: Canadian
Waitikiaji: Eeh
Mwanzilishi: Huu mziki mkubwa
Waitikiaji: Eeh
Mwanzilishi: Kutoka kwetu
Waitikiaji: Eeh
Mwanzilishi: Ukituona
Waitikiaji: Eeh
Mwanzilishi: Ukae mbali
Waitikiaji: Eeh
Mwanzilishi: Ukituona
Waitikiaji: Eeh
Mwanzilishi: Tupishe mbali
Waitikiaji: Eeh
Mwanzilishi: Nipe chuuma
Waitikiaji: Aah chuma hicho
Mwanzilishi: Nini kinalia
Waitikiaji: Aah chuma icho kinalia (mlio waliitikia huku wakipiga makofi mara moja kuashiria wa vyuma vilivyogongana)".

Basi walitupita na kuelekea wanakokujua, binafsi nilikoshwa mno na wimbo ulioimbwa na kundi la 3 siyo tu kwa maneno ila hata vibe walilokuwa nalo wakimbiaji liliniingia kwa mbali nikaanza kujihisi niko sehemu salama.

Niliwaza ikiwa wenzangu wamechafuka vile wakitoka kufanya kazi ngumu lakini bado wanarudi na furaha ile basi nami nikiufungua moyo naweza kuwa miongoni mwa wenye furaha pia.

Tukiwa tunaendelea na hayo wale ndugu zetu waliokuwa wananyoana bwana walikuwa wananyooshana kwelikweli yaani walikuwa wanatoana damu za kutosha.

Kitu cha ajabu hakukuwa na afande yeyote aliyekuwa akiwapa pole na badala yake walikuwa wakiwacheka nikamsikia afande Anna akisema
“Kwahiyo afande na watu wako hapo ni saluni au buchani mbona mnatoana damu hivyo”.

Kwa kweli walinitia hofu sana na nilikuwa nikiwaona kama wajinga fulani hivi au watu waliohamwa na akili ilikuwa ajabu kwangu kuona mtu akifurahia kuiona damu haswa ya kichwa.

Endapo angetokea mtu wa kuniambia kuwa kwa niliyoyaona naruhusiwa kuchagua kati ya kubaki ama kuondoka basi moja kwa moja ningechagua kuondoka, nilijiambia subiri kwanza nizoee mazingira yakinizidi najitorokea zangu.

Basi tukiwa tunaendele na utaratibu huo wa PARTICULARS kuna afande alikuja kupiga stori nasisi na kuna jambo alilokuwa akituambia liliniogopesha mno.

Alikuwa ni afande Shamte aliyetuonesha migomba iliyokuwa karibu na hapo na kutuambia,
“Mnaiona ile migomba kule, wale ni watu waliokufa kwa lugha nyepesi marehemu na wengi wao walikuwa wanatoroka baada ya maisha ya humu ndani kuwashinda”.

“Kwahiyo nawaasa wadogo zangu msifikirie kutoroka maana hii ni kambi ya jeshi pori unalotorokea huwezi jua limewekwa vitu gani wapo wenzenu wamefia kwenye mitego na wapo wengine waliolipukiwa na mabomu”.

“Muwe makini sana na ndiyo mana tunasisitiza usiende sehemu bila ya kupewa ruhusa na kiongozi wako maana yeye ndiye anayeijua kambi vizuri”.

Kwakweli afande Shamte alinitisha sana kwa maneno yake hayo mazito nikabaki kuduwaa, nilijiuliza amejuaje kati yetu kuna mtu ana mpango wa kutoroka ambaye ni mimi mpaka aje pale kuzungumzia jambo kama lile.

Ingawaje migomba ilikuwa mbali kidogo ila nilihisi alikuwa anatuongopea ili kututisha kwa maana migomba iliota kwa ukaribu sana kitu ambacho hakiwiani na mpangilio wa makaburi niliyokuwa nikiyaona mtaani.

Kwa upande mwingine nilihisi huenda ikawa ni kweli ikiwa watu wale walizikwa kwenye makaburi ya pamoja ambayo hayaruhusu marehemu kuachiana nafasi kubwa kama yalivyo makaburi mengine.

Nikiwa nawaza hayo ghafla lilitokea gari moja la kifahari ambalo wote tulilitupia macho kutaka kujua kinachoendelea mana wapo waliohisi ni ugeni kutoka serikalini na wengine walidhani labda ni mtu mwenye vyeo vyake jeshini.

Baada ya muda alishuka mzee mmoja ambaye alimleta binti yake mafunzoni binti yule aliyekuja na familia yake ambayo ilimsindikiza alipokelewa vizuri bila kurupushani kama tulizokutana nazo sisi.

Afande Anna alisikika kwa sauti ya chinichini
“Mnaona mwenzenu kaletwa na gari mpaka ndani, mmeona hajasumbuliwa kama nyie wenzangu na mie, kupanga ni kuchagua wadogo zangu”

“Ila nao wamezidi yaani familia nzima ndiyo imejikusanya kumleta mtu Jkt akiolewa si watampeleka mpaka kitandani” maneno hayo yalitufanya tuangue vicheko kiasi cha ile familia kuhisi tunawacheka wao.

Afande Anna alitukazia macho na kutuambia kwa sauti ya juu ili kuepusha picha mbaya ingeweza kujitokeza kwa wageni.

“Kimya nyie mnachekeshwa na kipi au nimeshakuwa mkojani” ilitubidi tukae kimya kana kwamba hakukuwa na kilichotokea.

Baada ya kuandikisha taarifa zetu afande Anna alituambia,
“Nyie form six huku jeshini hakuna kaka, mama wala baba, dada yako umemuacha nyumbani kwenu na sasa hivi anamalizia kupika mboga ili apate muda wa kwenda geto kwa shemeji yako kabla baba yako hajarudi”.

“Nachotaka kuwaambia ni kuwa humu ndani kuna maafande na WAZALENDO na kuanzia sasa nyie mtaitwa WAZALENDO kwa yeyote yule ambaye utamuona ni mkubwa kwako analingana na babu yako ama shangazi yako huyo siyo shemeji yako huyo ni afande wako tumeelewana WAZALENDO” aliendelea kumwagika afande huyo mwenye macho ya goroli.

“Ndiyo” tulimjibu afande Anna huku tukionekana kushangazwa na maneno aliyotuambia lakini kikubwa zaidi ni mapokeo ya jina jipya alilotubatiza pasi na kutumwagia maji.

“Pumbavu ndiyo nini sasa Konda, dalali au kuli mnanifananisha na wapiga debe mliowaacha stendi” alituambia hivyo huku akiwa ametukazia uso mithili ya mbogo aliyejeruhiwa.

“Ninapouliza tumeleewana mnatakiwa kujibu ndiyo afande mnapoishia kusema ndiyo mnamaanisha nini ndiyo bata au ndiyo mbwa, Narudia tena tumeelewana WAZALENDO”.

“Ndiyo afande” tulijibu sote kwa pamoja tukionekana kuwa na uoga baada ya kukalipiwa na mwanadada huyo mwenye shingo ya upanga.

Baada ya kumalizana naye afande Anna alitukabidhisha kwa afande Shamte aliyepewa maelezo na afande Mbega na kutuamuru tuambatane naye. ,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,

******Itaendelea……………………………………………...
 
EPISODE 03

Tulikokotana na afande Shamte moja kwa moja mpaka liliko duka la jeshi ambako alitupanga foleni na kutuambia tuwasubiri tuliowakuta wahudumiwe kwanza.

Afande alituambia tuandae hela ili tununue ndoo tulipomuuliza ni bei akatuambia ni shilingi 3000 halali ya kibongo.

Moyo ulishtuka na mwili ukafa ganzi baada ya kutajiwa bei, mmoja wetu aliropoka na kusema “Aftatu! Ndoo gani hizo za aftatu afande”

“Pumbaaav nani huyo anahoji bei ya ndoo? Kama unataka ndoo ya bure siungebeba ya nyumbani kwenu, yaani maafande wa jeshi waende kuwafungashia ndoo alafu mje muuziwe kwa 500 si uhanangwa huo” alifoka afande wa dukani ambaye alimsikia mwenzetu akihoji bei ya ndoo iliyochangamka kiasi kile.

Afande huyo wa dukani ambaye niligundua kuwa alikua na cheo kikubwa kumzidi afande Shamte alitutaka tumtaje aliyetoa kauli ile lakini tulisalia kimya mithili ya kuku aliyekuwa akidondosha yai kwenye moja ya pembe ya nyumba.

“Anhaah mnajikuta mmeiva siyo? hamtaki kumtaja mwenzenu sawa! We afande hembu nisogezee hao kwenye hilo jiwe kwa MWENDO MBAYA hao” Alisema afande yule ambaye kwa muda huo aliacha kutoa huduma kwa wateja na kudili na sisi.

“Wasamehe afande ndo kwanza wageni bado hawazijui taratibu bado wananukia chipsi hawa” Afande Shamte alijaribu kututetea akimwambia afande yule wa dukani.

“Unasema ni wageni wana ugeni gani si washakuwa WAZALENDO hawa unawaona na kichwani wana vipara hadi wanagoma kutajana ina maana washaiva afu unasema wageni! hawa ndo washakuwa wenyeji hivyo”.

“Tungesubiri afande wapate angalau mlo mmoja watakua washazoea” afande Shamte aliendelea kujaribu kututetea.

“We SERVICE MAN unamfundisha afande wako taratibu tangu lini au nawewe nikuunganishe ukae nyuma yao” afande yule wa dukani wakati huu aliongea huku akionekana kuwa na jazba.

“MAREKEBISHO afande” alijibu afande Shamte.
“Ala yaani mimi nakuagiza wewe unanifundisha si MAPUUZA kabisa hayo, SERVICE MAN ni jeshi la wapi hilo unajikuta mgeni na jeshi” afande aliendelea kufoka.

“MAREKEBISHO mkuu” afande Shamte alimjibu,
“Haya niletee wageni wako kama nilivyokuagiza”.

“Sawa mkuu” afande Shamte alipokea oda hiyo na wakati huu hakuwa na wakati wa kujibizana naye ila alifuata maagizo tu.

Afande Shamte alitupeleka lilipo lile jiwe na kututaka tupunguze urefu kauli ambayo hatukuielewa kwa haraka mpaka pale alipotuambia tuchuchumae nasi tukafanya hivyo.

Afande alituambia tutembee UBATABATA tukiwa tumechuchumaa, kiukweli hatukumuelewa aligundua hilo na kutubadilishia zoezi na awamu hiyo alisema turuke kichurachura mpaka zilipo ngazi zinazoelekea lilipo dirisha la dukani.

Wakati hayo yakiendelea tulimsikia yule afande wa dukani aliyetupa adhabu akisema,“We SERVICE MAN mnashauriana kitu gani apo au mnaandaa mgomo nije”.

“Hapana afande wanakuja sasa hivi” afande Shamte alimjibu.

“Fanyeni GHAFLA nawasubiri kuna wateja wengine wanataka huduma”Basi tulifanya kama tulivyotakiwa, tulipofika kwenye ngazi tulisimama na afande yule aliyeonekana kutukamia alituambia twende mmoja mmoja tukachukue ndoo.

Afande yule wa dukani bado hakuishiwa maneno kila mmoja wetu aliyekwenda alikuwa akimwambia
“Siyo wewe kweli uliyekuwa ukitaka kuuziwa ndoo kwa 500, yaani KOPLO wa jeshi nipo dukani hushtuki au unaniona kama Zuchu nafanya tangazo la chupi kwa jero”.

Kwa kweli ilikuwa ni kivumbi na jasho yaani mpaka inafika hatua kila mmoja wetu amepata ndoo yake tulipitia kero na gadhabu za kutosha ndani ya muda huo mfupi mno.

Ile dhana ya mteja ni mfalme haikuwa na nguvu eneo hilo hata ile ya kumkirimu mgeni kwa mapokezi mazuri haikutambulika kabisa tulionekana kama mafala vile.

Yaani kama una roho ndogo kwa yale tuliyokutana nayo kule getini na dukani unaweza kusema,
“Mimi na jeshi basi tena” hata hivyo ni kwasababu tu nimetoka kukimbia kero nyumbani vinginevyo ningeweza kuwaachia sanduku na vilivyomo ndani yake na kuondoka zangu.

Tulipomaliza kuchukua ndoo afande alituita kwa mara nyingine na kutupa pipi huku akijichekesha na kutuambia kuwa hili ndiyo jeshi hivyo tunatakiwa kuwa imara na kulizoea.

Nilitabasamu kipindi anatupa pipi kwake alidhani nimefurahi kwa alichotufanyia na kutupooza na pipi lakini haikuwa hivyo kikubwa nilivuta kumbukumbu siku ambayo tukio kama lile lilinitokea.

Nilikumbuka mara ya mwisho kufanyiwa hivyo ilikuwa ni zaidi ya miaka kumi na mitano nyuma ambapo baba alinipa aidha pipi ama biskuti ili tu ninyamaze baada ya kujiliza kwa muda.

Baada ya kuona nipo kwenye hali hiyo afande aliniuliza jina langu nikamtajia akaniuliza kama nimependa zoezi tulilofanya, nilitamani kumwambia hapana ila nikahisi naweza nikamkwaza na kumtibua madudu yake kichwani.

Nilimjibu kinafki kwa kutingisha kichwa kwamba nimeipenda akaniuliza kama tunaweza kurudia wenzangu wote waligeuza vichwa vyao kunituzama.

Nilimjibu kwa kutingisha kichwa ila awamu hii nilimkatalia na nikawaona wenzangu wakiniangalia huku wamenikazia macho nishindwe kutambua uchaguzi ni upi turudie ama tusirudie.

Afande Shamte alituonesha ishara ya kuondoka nasi tukamfuata ila bado tulimsikia yule afande muuza duka akituambia
“Njooni basi turudie kazoezi ketu niwaongeze pipi nyingine”.

Hakuna aliyemjali tena moyoni nilijisemea "umetuona watoto nini” nilijizuia kutoa maneno hayo mdomoni asiye akayasikia nikazua kizaazaa kingine tena.

Sote tulisepa zetu dukani tukiongozana na afande Shamte ambaye alituambia mambo kadhaa moja wapo alitupa pole kwa yote yaliyotokea na kutuambia maafande wengine wako hivyo huwa wanapenda jeshi lionekana kama kitu kigumu sana.

Alitutoa hofu na kutuambia jeshi siyo gumu sana ila muhimu ni kufuata maelekezo tu.

Afande Shamte alitusisitiza kuwa tusiwe waropokaji na tuwapo na maafande tuchague maneno ya kuongea nao bila kuwaudhi vinginevyo yatatukuta kama yaliyotokea dukani.

Alitupongeza pia kwa kitendo cha kutomtaja aliyetoa kauli iliyomkera afande yule wa dukani na kutuambia wakati mwingine hata tungemtaja tungepewa adhabu ya pamoja mana jeshini hakuna jema wala tuzo ya msamalia mwema.

Kifupi afande Shamte alitufungua kwa kiasi chake kuhusu jeshi na kutufanya tujione wepesi mana ni kama alizishusha hasira tulizozibeba kutoka dukani.

Pia alinipa tahadhari kuwa nitasumbuliwa sana na yule afande niliyemtajia jina langu atakuwa ananitafuta mara kwa mara hivyo basi natakiwa kujiandaa kwa kila hali.

Sikujali sana zaidi ya kujiandaa kisaikolojia na hilo mana nilishajiambia nitavumilia ila yakinizidia natoroka zangu. ,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,

Afande Shamte alitufikisha mpaka sehemu ambayo walikuwepo WAZALENDO wenzetu wakiwa kwenye foleni ya chakula, alituambia tuache vitu vyetu eneo hilo na tumfuate.

Alitupeleka mpaka ilipo stoo ya vyombo tukapatiwa vikombe na sahani za bati kila mmoja wetu na tukarudi walikokuwa wakigawa chakula ambako tulikuta foleni zote zimeisha.

Moja kwa moja afande Shamte alitupeleka kwa wale waliokuwa wanagawa msosi tukawekewa cha mtume kwa ndondo na kombe la chai ya maziwa juu tukaenda kunawa na hatimaye tukarudi kukifinya.

Chakula kilibaki kingi wagawaji walimuuliza afande Shamte kama kuna WAZALENDO wengine kwenye PARTICULARS akawajibu wapo ila wasingeweza kukimaliza kilichopo.

Wale wagawaji wakawa wanawaita watu kwaajili ya kuongeza chakula lakini walifika wachache ambao nao walikuwa wakijivuta.

Nilishangazwa mno na yaliyokuwa yakiendelea, niliona kama vitu viko tofauti yaani dukani tumetoa hela zetu na bado tulipelekeshwa lakini kwenye chakula cha bure ambacho hatujatoa senti yoyote bado watu walibembelezwa kuongeza.

Niligundua kuwa maisha ya jeshini hayafanani kabisa na yale ya uraiani huku niko sehemu ya tofauti kabisa hivyo basi natakiwa kubadilika kulingana na mazingira.Nikiwa nafikiria mengi kuhusu shule hiyo mpya niliwasikia SERVICE MEN wakisema

SM 1: “Yaani WAZALENDO mnabembelezwa kuongeza ubwabwa mnaringa shauri yenu mtaukumbuka tu kozi ikinoga wakati mnatoka zenu kwenye MAFATIKI huko mta BURST zaidi ya mara saba na bado hamtashiba”.

SM 2: “Waache bana watoto wa watu bado wakibeua wananukia chipsi subiri kwanza MZABUNI awatafunishe wadudu kwenye maharage appetite za kula zitawajia tu”.

Tulipomaliza kula tulisuuza vyombo na kwenda tulikoacha vitu vyetu tuligawanywa makundi mawili kulingana na jinsi ambapo wadada wawili tuliokuwa nao waliambatana na afande niliyesikia akiitwa matroni Amina.

Kwa upande mwingine siye vijeba wazee wa xy-direction tuliongozana na afande Shamte mpaka yaliko mabweni walikofikia WAZALENDO wenzetu.

Tulikutana na vitanda visivyokuwa na magodoro ambavyo vilionekana dhahiri kuwa vilikuwa vikitumika hapo awali kabla ya watumiaji wake hawajaondoka.

Tulikusanya vitu vyetu sehemu moja tukaongozana na Afande Shamte yanakohifadhiwa magodoro ambako hatukufanikiwa kumkuta mhusika ambaye alikwenda kupata chakula cha jioni hivyo alipafunga.

Afande Shamte alituacha mahala hapo na kumfuata afande Jala aliyekuwa anahusika na maswala ya uhifadhi wa magodoro ambapo wao walimuita KITENGO magodoro.

Kipindi tunawasubiri tulisikia filimbi zikipigwa tukabaki kushangaa ni kitu gani maana mtaani hutumika kufukuza wezi hivyo basi tukabaki kushangaa inawezekanaje anatokea mwizi jeshini.

Baadaye tulipomuuliza afande Shamte alituambia kuwa kule jeshini wanatumia filimbi kama mbadala kengere na maafande hutumia kuwaita WAZALENDO hivyo basi tuisikiapo tunatakiwa kukusanyika kwa haraka.

Afande alituambia kwa wakati ule hatukutakiwa kuwa na hofu yoyote muhimu tulikuwa naye na hatukukamilisha mahitaji ya msingi kwa upande wetu.

Baada ya afande Jala kutukabidhi magodoro afande Shamte alituambia tuyapeleke HANGANI tukayaweke vitandani tukimaliza tutamkuta hapo.

Tulishindwa kumuelewa tukabaki tumeduwaa mpaka pale aliporudia kutuambia,
“Nendeni mkaweke magodoro yenu vitandani kule mlikoacha vitu vyenu halafu mkimaliza njooni hapa mtanikuta namimi nataka nile wadogo zangu”.

Tulijaribu kumuelewa alichokimaanisha ingawaje kuna msamiati mpya aliutumia ndiyo uliotuvuruga ila yeye hakuweza kugundua hilo alihisi kama anaongea na SERVICE MAN wenzake.

Tulifanya kama alivyotuagiza na baada ya muda tulirudi na kumkuta akipiga stori na wenzie, tuliongozana naye mpaka walipokusanyika WAZALENDO wengine.

Tuliwakuta wenzetu wakiwa wamekaa chini wakipiga stori za hapa na pale, eneo lile halikuwa geni kwangu lilikuwa ni lile lililotumika kugawa chakula yaani MESI.

Afande Shamte aliongea na afande aliyemkuta sehemu hiyo,
“Afande Kapanda nimekuletea watu wako hawa”

“Sawa, yalete baba ndiyo yamefika nini?”
“Ndiyo afande”
“Kwahiyo hayajala?”
“Wamekula baba labda wawe hawajashiba, walifika muda kidogo walikuwa wanasubiri magodoro”
“Sawa eti nyie WAZALENDO mumeshiba kweli?”
“Tumeshiba afande” tulimjibu afande Kapanda

“Anhaa sasa hapa hamtakiwi kushiba inabidi mpunguze shibe kidogo simameni mstari mmoja na muachiane nafasi kidogo”.

Tulisimama kama alivyotuagiza na baada ya muda akaanza kutuambia chini, juu huku akituangalia.

Tulibaki kumkodolea macho tusijue ni kipi kinachoendelea, aligundua hilo hivyo alimuamsha mmoja wa WAZALENDO tuliowakuta eneo lile na kumwambia maneno yaleyale.

MZALENDO yule alichutama alipoambiwa “chini” na kusimama alipoambiwa “juu” afande Kapanda alitugeukia na kutuambia
“haya apo KAMA YEYE” huku akionesha ishara ya vidole kwa MZALENDO huyo.

Tulimuiga na kuendelea na zoezi hilo kwa muda na baadaye afande Kapanda akaturuhusu tuungane na wenzetu.

Kichwani ilinijia picha ya kile kibao maarufu cha kijani chenye maandishi meupe barabarani kinachotamba mtandaoni kikisema
“Sasa unaingia mkoa wa Mara” maana si kwa kilichokuwa kinaendelea tuliungana na wenzetu ambao walikuwa wamekaa chini kwenye vumbi bila ya kujali.

Hakukuwa na kitu cha maana kilichokuwa kikiendelea zaidi ya kuimba nyimbo ambazo nazo pia sikuona mantiki ya nyimbo hizo.

Afande Kapanda alikuwa yuko bize kutuimbisha nyimbo hizo kana kwamba alikuwa na watoto wa chekechea wanaosubiri muda wa kunywa uji ufike.

Mbali na kuimba nyimbo hizo afande Kapanda aliendelea kupokea wageni (yaani WAZALENDO wapya) waliokuwa wakiwasili kadri muda ulivyosonga mbele.

Tulikuwa tukibadilishana mawazo pale afande Kapanda alipokuwa akipokea na kuongea na wageni na kupitia mazungumzo hayo niliweza kung’amua ratiba ya hapo ilivyo.

Kwanza alfajiri ya saa 10 tunaamshwa na kukusanyika eneo lifahamikalo kama UWANJA WA DAMU na kukimbia mchakamchaka saa 11.

Saa 12 tunafanya usafi kambini na kukusanyika KOMBANIA saa 1 ya asubuhi baada ya hapo tunaenda kwenye FATIKI mpaka muda wa chai saa 4 asubuhi.

Tukiwa tunaendelea na hayo afande Kapanda alitukatiza na kusema,“WAZALENDO WIIII”
“WAA” akajibiwa
“Mbona mmepooza WAZALENDO ndenge nini? nini shida? haya aje mmoja mbele atuimbie” palibaki kimya na hakukuwa na aliyejitokeza.

Akasikika tena afande Kapanda “Eeh mmegoma WAZALENDO aya twende, moja, mbili, tatu” Afande Kapanda alinyoosha mikono juu na kuanza kupiga makofi nasi tukaungana naye na pakawa panasikika paah! paah! paah! ,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,

******Itaendelea……………………………………………
 
“EWIII”,
“EWAA”,
“EWIII”,
“EWAA”,
“ELEWIII”,
“ELEWAA” afande Kapanda alianza kuimba nasi tukimfuatisha.

Afande Kapanda: Honey wangu fanya ujirembe.
Sisi: Honey wangu fanya ujirembe.
Afande Kapanda: Ujirembe nataka tutoke.
Sisi: Ujirembe nataka tutoke.
Afande Kapanda: Nina mzuka na wewe.
Sisi: Nina mzuka na wewe (Afande Kapanda alimuamshaMZALENDO mmoja wa kike na kumshika mikono wakawa wanacheza huku wakitizamana)

Afande Kapanda: Nina morali na wewe.
Sisi: Nina morali na wewe.
Afande Kapanda: Haya haya kipenzi wee
Sisi: Haya haya kipenzi wee
Afande Kapanda: Haya haya laazizi wee
Sisi: Haya haya laazizi wee
Afande Kapanda: Haya haya my queen wee
Sisi: Haya haya my queen wee
Afande Kapanda: Haya haya sweetheart wee
Sisi: Haya haya sweetheart wee.

Wimbo huo ulinogeshwa kwa nakshi za miruzi na vigeregere kutoka kwetu, ilionekana kuna wenzetu walikwishaanza kuyazoea mazingira ya kambi kwani kila walichokifanya walifanya kwa morali ya hali ya juu.

Tuliendelea na ratiba hizo mpaka pale ilipofika mida ya saa 4 ambapo afande wa zamu waliyemuita afande Mvamba alifika na kuchukua idadi yetu.

Nilimsikia afande Mvamba akisema, “Haya MADAWILI wote mbele” nikawaona watu wakienda nami nikaliunga mpaka mbele japo sikuelewa maana ya neno MADAWILI.

Nilijaribu kujiongeza maana hapo awali afande Kapanda alituita wageni wote mbele na kutuhesabu nakumbuka siku hiyo tulikuwa wageni 63.

Afande Kapanda alituamuru tuhesabu namba, niliitika namba 22 nikasikia vicheko vya chinichini.

Tuliendelea kuhesabu ila ilipofika namba 28 afande Kapanda akaamuru tuache kuhesabu.

Afande aliwaambia waliokuwa wakicheka wanyamaze tuhesabu namba ili tukalale mapema.

Ukimya ukarejea tukahesabu upya na hakukuwepo tofauti na hapo mwanzo kwani pale ilipofika zamu yangu watu waliangua vicheko.

Sikugundua kuwa mimi ndiye niliyekuwa sababu ya wao kucheka ila awamu hii nilimsikia afande Kapanda akisema,

“anhaah kumbe kuna NANGA limevamia BOGI kaingia cha kike ndo mana mnacheka” vicheko vikaendelea walicheka mpaka pale afande alipowanyamazisha na tukahesabu tena.

Tulihesabu tena na alipoitika mtu wa 35 umakini ulionekana kupungua, afande Mvamba akasema,

“AZI WEA, acha acha kuhesabu acheni kucheka tuchukue lokoo haraka tukalale mapema na wewe namba 22 embu songa mbele hapa unatupotezea muda”.

Nilijitenga na wale MADAWILI na kuelekea alipo afande Mgaza nikiwa na uoga mwingi, afande Kapanda akaniongelesha

“Nawewe ni DAWILI?”
” Hapana” nikamjibu
“Sasa kimekupeleka kipi pale?” nilibaki kimya nikakosa cha kujibu akaniambia niondoke niende kwa wenzangu lakini kabla sijaanza kuondoka nikamsikia afande Mgaza akisema

“Subiri kwanza tusidanganyike na sauti afande Kapanda usikute mwenzetu DAWILI kweli ngoja tuone”

“We MZALENDO hapo ulipo umevaa singilendi au sidiria?” Afande Mvamba aliniuliza.
“Nina singilendi afande”

“Una uhakika?”
“Ndiyo afande”
“Ngoja tuone na kama unatudanganya leo hulali tutakesha wote kwenye lindo”.

Maneno ya afande Mvamba yalianza kunipa hofu na kunitia uoga ikabidi nianze kujikagua kujihakikishia kama kweli nimevaa singilendi.

“Haya vua hiyo shati tuone” nilivua na kubaki na singilendi nikaanza kusikia vicheko vya chinichini kutoka kwa WAZALENDO.

“Anhah kumbe kweli una singilendi, hivi afande Kapanda MADAWILI huwa wanavaa singilendi na sidiria wakati mmoja?”

“Nadhani iko hivyo mkuu” afande Kapanda alijibu.
“Haya vua na hiyo singilendi tuone” nilivua na kubaki kifua wazi ambapo niliruhusu sasa vicheko vya waziwazi.

Si afande Mvamba, wala Kapanda ama WAZALENDO hakuna aliyevumilia kucheka kila aliyekuwa eneo hilo hakuacha kucheka isipokuwa mimi ambaye nilibaki kimya nisijue ni kipi kinachoendelea.

Nikiwa najiuliza ni kipi kinachoendelea afande Mvamba aliwanyamazisha na kuniuliza ni lini nimeripoti kambini nikamwambia leo jioni.

Afande akasema “Kumbe ni mgeni mnacheka bure mwenzenu” aliendelea kusema,

“Kwa faida ya wengi ni kuwa DAWILI alikuwa ni mwanamke wa kwanza kujiunga na jeshi hivyo basi kwa kumpa heshima kamanda yule ilibidi maafande wote wa jinsia ya kike waitwe MADAWILI ingawaje wana majina mengine ambayo mtayasikia kadri kozi itakavyowanogea afande Kapanda hembu watajie moja wapo”.

“WACHIMBA CHINI” afande Kapanda alijibu.
“Maana yake” aliuliza afande Mvamba
“Si wakikojoa wanaacha vishimo afande”

“Mmesikia sasa sijasema mimi afande wenu ndiyo kasema kwahiyo mnatakiwa myajue vizuri msije mkavamia MABOGI kama mwenzenu tumeelewana WAZALENDO”.

Alipomaliza kusema hivyo afande Mvamba aliniruhusu nijiunge na wanaume wenzangu na ndipo MADAWILI wakahesabu namba.

Walihesabu MADAWILI 47 kisha wakaungana nasi na kuhesabu namba kwa pamoja nami nilihesabu mtu wa 60.

Tulikuwa watu 238 mahala hapo wakati hesabu aliyokuja nayo afande Mvamba kutoka geti kuu wanakoandika PARTICULARS inasema tuko 243 kwa maana ya kuwa kuna upungufu wa WAZALENDO 5 ambao hawapo eneo hilo.
libidi tuhesabu tena ili kujihakikishia usahihi wa idadi hiyo tukaanza moja, mbili, tatu na kuendelea na ilipofika zamu yangu nikajikuta naropoka “hamsina kumi” nikasikia miguno iliyofuatiwa na vicheko.

Nikamsikia afande Mvamba akisema
“aje mbele huyo” nilitaka nijikaushe ila nikaona nisije nikaponza wenzangu kama ilivyokuwa dukani lakini pia nikaona waliohesabu namba 58,59 na 61 wananitupia macho nikagundua hawana kaba la kutonitaja nikaona bora nijitokeze tu.

Ile nafika mbele tu nilimsikia afande Kapanda akisema “
Duuh! ni wewe tena”
“Huyu si yule mshikaji aliyevamia BOGI la MADAWILI” akadakia afande Mvamba
“Ndiyo mwenyewe” alijibu afande Kapanda huku akicheka.

“Dogo we NANGA kweli tena NANGA SELULE hembu rudi zako huko hamsina kumi ndo namba gani za kirumi au za kiajemi” aliniambia afande Mvamba.

“Hata jeshi la Somalia halihesabu hivyo afande” afande Kapanda alimwambia afande Mvamba.

“Hili si NANGA, hembu hesabuni upya na msikosee tunataka tukalale zetu mapema,
mtahesabu moja mpaka kumi wa kumi atasimama na hilo NANGA LA DEMO hembu liwekeni katikati lisije likatuharibia” Alituamuru afande Mvamba huku akitusisitiza umakini wakati wa kuhesabu.

Tuliendelea kuhesabu na hakuna kilichobadilika kwani tuliendelea kukosea kutokana na kutoelewa kile tulichoelekezwa.

Waliohesabu moja mpaka kumi wote walisimama tukaambiwa haitakiwi kuwa hivyo wakakaa chini na kuhesabu upya.

Wapo waliohesabu wakaendelea kukaa chini alipoitika mtu wa kumi wakaamka na kusimama, wengine waliendelea kuhesabu namba kumi na moja kumi na mbili na kuendelea.

Hapa napo mvurugano ulikuwepo haswa kwa mfano zilisikika sauti “kumi na nane” “kumi na tisa”
“kumi na kumi”
“ishina moja”. ,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,

Afande Kapanda alibaki kucheka kutokana na jinsi namba zilivyokuwa zikihesabiwa huku afande Mvamba yeye akionekana kukasirishwa na mwenendo ule wa uhesabu.

Alisikika akisema“Acha! acha! acheni usenge nyie ndiyo namba gani hizo mnazohesabu? inamana hamuwezi kuhesabu nyie? kwani si tumeambiwa nyie ni form six!”

“Si mmetoka shule juzi nyie na isitoshe mlifanya na mitihani sasa madudu gani haya mnatufanyia?”

Aliendelea kuwaka kwa kusema,
“Yaani kuhesabu namba tu hamuwezi! naapa kwa Mungu baba aliye mbinguni hata mtoto wa darasa la kwanza hahesabu hivyo tena siku hizi wanafunzi wa kindergaten wanajua kuhesabu vizuri tu kushinda hata hiki mnachokifanya tena kwa kizungu kabisa na ushahidi ninao nitakuja na mwanangu kesho awahesabu nyie si hamuwezi”.

“Alafu afande usikute PCM ndiyo wanaoongoza kukosea” alidakia afande Kapanda.

“Amini kwamba hawa si vilaza yaani kuhesabu tu hayajui na sidhani kama kuna atakayefaulu kweli tusubirini matokeo tuone”.

“Yaani lijitu linasoma mpaka form six alafu mwisho wa picha kuhesabu tu kunamsumbua au mlidanganywa huku ndo mtafundishwa kuhesabu my dear kama uliruka darasa imekula kwako.”

“Nasema hivi kama ulichelewa kuanza shule ukajikuta umeanzia la 3C ukaruka chekechea na vidudu shauri lako hapa ni jeshini na kilichowaleta huku ni kifo”.

“Kama hamkuiona vizuri ile migomba kule mapokezi mlikoandikisha PARTICULARS muende mkaiangalie tena kwa umakini kwani afande Kapanda bado hamjawapa LONJA hawa form six kuhusu ile migomba?”

“Sikuwepo kwenye PARTICULARS leo mkuu ila afande Mbega alikuwepo nahisi kawaambia maana friji lake bovu huyu” afande Kapanda alimjibu.

“Eti Mbega”
“Ndiyo mkuu” aliitika afande huyo ambaye nakumbuka alikuwa akiwanyoa WAZALENDO kule karibu na migomba.
“Eti hukuwapa LONJA kweli hawa MANANGA”

“Nimewapa mkuu na kuna form six watano walikuja na wazazi wao nilipowaambia wakawa wanalia wale wazazi walipojua wanacholilia walichukua watoto wao wakaondoka zao”.

“Ila nisamehe mkuu kwa kushindwa kutunza siri za kambi” alijibu afande Mbega.

“Wala hutakiwi kuomba msamaha ni vizuri sana kumwambia mtu ukweli mapema ili ajue cha kufanya siunaona kama hao wazazi wamefanikiwa kunusuru uhai wa watoto wao”.

“Ila kuna hizi nafsi zenye kutapatapa hatima za uhai wao uko mikononi mwetu, ewe Mwenyezi Mungu nakuomba kozi ianze leo ikibidi mana tuna hamu ya kukuletea hizi nafsi mapema” aliongea afande Mvamba huku maafande wengine waliopo eneo hilo wakicheka hali ambayo iliturudisha katika mawazo mazito kutokana na kauli zao zenye ukali ndani yake.

“Sasa ngoja niwape LONJA kuhusu ile migomba kwanza mnajua maana ya neno LONJA nyie MANANGA form six?” alituuliza afande Mvamba ambaye kwa sasa alionekana kutabasamu tofauti na awali.

akiongea akiwa katikati yetu huku akitembea na kuinama akitupiga makofi vichwani.
“Hatujui afande” nasi tulimjibu

“DAWILI mwenye kutoa siri zetu uraiani huyu supu yake tunaenda kukata kinachokeketwa alafu tunaenda kusambaratisha kifua chake bila kujali ni saa sita, ni dodo au rapa yaani mpaka hasira zetu zinaisha kifuani patakuwa ni tambarare”.

“Kwanza tukifika pale kwa MZABUNI hakuna atakayeuliza hayo maswali tutachokichofanya ni kuweka sahani na kuwekewa supu”.

“Na mshajua kwanini mwanamke tunamsupua sehemu mbili tofauti na mwanaume.”

“Hatujajua afande” tulimjibu afande Mvamba ambaye kila neno lililokuwa linatoka kinywani mwake lilikuwa ni lenye kutuzidisha hofu.

“Mafala nyie mbona hamuulizi sasa mmejikalia kimya kama mmegongwa vile”
“Mmmmh” bila kujizuia tuliguna na maafande waliopo karibu na hapo walicheka sana.

“Khaah! mmeguna kwani nimesema mmegongwa na nini mimi nimemaanisha mmegongwa na gari, kwani mtu akigongwa na gari anaweza kuongea kweli?”

“Anhaa kumbe” baadhi yetu walimjibu.
“Tatizo lenu mna kiherehere kama bao la kwanza na ndiyo mana mnawaza ujinga tu, kwani mtu akigongwa kama mnavyowaza haongei? si anaongea utamsikia oi mama! aii! ashiii! taratibu basi, unaniumiza bana” vicheko vilianguka kwa dakika kadhaa kutokana na maneno hayo ya afande Mvamba ambaye kwa wakati huo alifanikiwa kuliteka jukwaa maana alikuwa anasikilizwa yeye tu.

“Nyamazeni muhesabu namba tukalale huko” alituamuru afande Mvamba.

“Ila pot bado hujawapa LONJA” alisema afande Shadi ambaye alionekana kufurahishwa na kile kilichokuwa kikifanywa na afande Mvamba.

“Anhah si kuhusu ile migomba siyo” afande Mvamba alijibu.
“Ndiyo alafu hujawaambia kwanini DAWILI supu yake ni ya viungo viwili tofauti na MANGORONGORO ikatokea wamevujisha siri za jeshi”.

“Kuhusu supu nitawaambia baadaye wakifanikiwa kuhesabu namba vizuri wakatimia ila wakiendeleza UNAGA wao nawaacha maana siyo lazima ni kwa faida yao, eti nyie MANANGA niseme nisiseme? aliuliza afande Mvamba.

“Semaaaaa” tulimjibu wote kwa pamoja.
“Ukweli kuhusu ile migombaah!”
“Enheeh!”
“Kwa kila mgomba mnaouona paleeh!”
“Enheeh!“
"Chini yakeeh!”
“Enheeh!”
“Kuna mwilii” aliposema hivyo kulitawala miguno iliyofuatana na kimya cha sekunde kadhaa.

Nahisi watu tulijua kinachofuata na tukaanza kuamini kinachosemwa maana kabla afande Mvamba hajamaliza wengi wao tuligundua kuwa anachokiongea kilifanana kabisa na kile tulichoambiwa tukiwa mapokezi.

Binafsi nilikumbuka kitambo kidogo nilipokuwa shule nikisoma na Linda aliyekuwa akinielekeza topic mojawapo ya hesabu iitwayo logic (yaani mantiki kwa Kiswahili).

Linda alinifundisha kwamba kimantikiki ni kuwa uongo na uongo huzalisha ukweli yaani pindi uongo ukizungumzwa sana ama ukazungumzwa na watu wengi hupelekea uongo huo kuwa ukweli. ,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,

Linda alinifundisha kwamba kimantikiki ni kuwa uongo na uongo huzalisha ukweli yaani pindi uongo ukizungumzwa sana ama ukazungumzwa na watu wengi hupelekea uongo huo kuwa ukweli.
Nice
 
Kimya hicho kilichodumu kwa muda mfupi kilivunjwa na maneno ya afande Mvamba ambaye alisema

“Anhaah kumbe mnapenda umbea lakini hamuutaki ukweli, ukweli unauma eeh!”
“Sasa ni hivi ile migomba mnayoiona pale tumeipanda baada ya kuwazika wenzenu ambao nao ni WAZALENDO wa mujibu wa sheria kama nyie wapo wa miaka ya nyuma na wengine ni wa mwaka jana tu hapo”.

“Kwahiyo mjiandae kama mmekuja 200 msijihakikishie mtarudi wote, lazima form six kama 180 hivi wafe alafu wahitimu kama 20 hivi”.

“Na katika hao wazima wanaweza wakawa wanne au watano mana katika mazoezi mtakayokutana nayo kama siyo kifo basi kuna wengine watakuwa vilema”.

"Utakuta huyu kavunjika mguu mwingine hana sikio mara anayefuata shingo imekaa upande mara ukute macho yote anayo ila hayaoni vizuri ama hayaoni kabisa au mwingine akili anazo ila anakuwa hana akili yaani kawehuka ili mradi tu tuwapunguze msimalize wote”.

“Alafu mjue bahati mbaya sana huku hatuna mitihani ya kuwapunguza idadi kama wanavyofanya necta, mitihani yetu huku ni mazoezi na kwenye mazoezi hakunaga chabo wadogo zangu si eti afande Kapanda”

“Ndiyo afande na kama wamefika form six kwa chabo aisee imekula kwao, huku ni bidii tu mazoezini ndo kutakufanya uvuke vikwazo ukiwa legelege mgomba wako utawekwa huku mwanzoni mwa shamba la migomba” alijiubu afande Kapanda.

“Na kitu kingine ambacho hamjui ni kuwa serikali imewaleta huku ili mfe, mbaki wachache ila nyie hamjui tu”.

“Unakuta lijitu linaandaa 50,000 ya nauli linafunga safari mpaka kambini ili lifuate kifo ukiangalia limesoma mpaka form six sasa elimu itakuwa imemsaidia nini”.

“Sasa za ndani ni kuwa baada ya serikali kuona mahitimu yamekuwa mengi mtaani halafu inatupiwa lawama hawayaajiri serikali yetu pendwa vile haitaki kulaumiwa ikaona iwalete jeshini”.

“Mnajua huku jeshini kinatokea kitu gani WAZALENDO?” aliuliza afande Mvamba tukabaki kimya asiwepo hata mmoja wa kumjibu wala kukohoa.

“Anhaah mnakaa kimya ili nisiwaambie ukweli, sasa ukweli ni kuwa huku mnakuja wengi ila mtakufa na kuhitimu wachache kwa maana nyingine wachache sana tena saaaana ndio watakaokwenda chuo”.

“Kule chuo mtapunguzwa kwa mitihani kama kawaida japokuwa watu wa chabo hamtakosekana haswa wale waliostuka wakaacha kuja ila watakuwa wachache mana wengi wao mtakuwa tushawapunguza hukuhuku kwenye shamba letu la migomba”.

“Nina uhakika miaka kumi baadaye wahitimu wasiokuwa na ajira mtaani watakuwa wachache ama hawatakuwepo kabisa na hapo serikali yetu tukufu itakuwa imefanikiwa kuzikwepa lawama nyingi kama ilivyo sasa” aliendelea kututisha afande Mvamba.

Tulibaki kimya kwa muda na hakuna aliyekuwa akinong’ona kwa wakati huo, woga ulituvaa miongoni mwetu kwa kile tulichokuwa tukiambiwa.

Baada ya kumaliza mazungumzo hayo afande Mvamba alituamuru tuhesabu namba.

Tulihesabu kwa usahihi na umakini wa hali ya juu tofauti na awali, afande Kapanda na afande Shadi walihusika kwa kiasi kikubwa kufanikisha hili kwani walituelekeza namna ya kuhesabu na wakasimamia pia zoezi lote mpaka mwisho.

Tulihesabu wote tukiwa tumekaa chini isipokuwa waliohesabu namba 10 wao walisimama na hakukuwa na namba kubwa zaidi ya 10 maana kila ilipofika 10 aliyefuata alianza upya yaani 1.

Tulishangaa namna ilivyokuwa rahisi kuhesabu na hatukujua ni kipi kilichofanya tushindwe hapo mwanzo ila nafikiri ilikuwa ni kitete tu kuwepo eneo lile, eneo ambalo kombati ya jeshi haikuwa tofauti na shamba dress tukiwa mabwenini.

Afande Mvamba aliwaamuru waliosimama wahesabu namba isipokuwa wa mwisho kabisa ambaye aliitika namba 8, walikuwa 23 ambao ni 230 na yule aliyehesabu 8 maana yake tuko 238 namba ambayo haikuwa tofauti na mwanzo.

MADAWILI waliitwa tena mbele wakahesabu namba kwa mara nyingine, walihesabu na walikuwa 47 na kipindi wanaenda bado kidogo na mimi niende ila kuna jamaa alinitonya kuwa mademu ndiyo wanaohitajika.

Akili yangu bado ilikuwa inaniambia kuwa MADAWILI ni wageni na wala sikujua kama tunatofautiana kimaumbo maana sehemu tuliyopo mwanga ulikuwa hafifu na wote tulivaa suruali ya truck na shati kitu ambacho kinafanya tuonekane tunafanana.

Kulibainika kuwepo kwa upungufu wa WAZALENDO watano kama ilivyo mwanzo ila wakati huu aligundua kuwa katika MADAWILI 49 waliosajiliwa wawili hawapo hivyo katika wale watano wasiokuwepo watatu ni wanaume.

Katika kujiuliza wako wapi wengine ndipo afande Shadi alipowaza na kusema huenda wasio kuwepo wakawa ni walinzi wa HANGA, wakateuliwa wanne kati yetu yaani wawili kutoka kila upande wakaangalie idadi ya walinzi waliopo huko.

Nilivuta kumbukumbu ni wapi nilisikia neno hilo nikakumbuka ni kipindi tupo kule ambako tuliacha vitu vyetu tukafuata magodoro afande Shamte aliwaita hivyo wale tuliowakuta nilikumbuka hawakuwa wengi maana wengine walipoulizwa kuwa ni walinzi wa HANGA walikataa.

Niligundua kuwa walinzi wa HANGA ni wale wanaoachwa kutazama usalama wa mali zilizopo mabwenini kwani jeshini bweni hufahamika kwa jina la HANGA.

Tukiwa tunawasubiri waliokwenda kuangalia idadi ya WALINZI WA HANGA masimulizi yaliendelea kama kawaida na kama ilivyo mwanzo afande Mvamba ndiye aliyekuwa msemaji mkuu.

Aliuliza kama kuna swali na ndipo afande Shadi akalirudisha swali la mwanzo lile linalohusu supu kwa atakayevujisha siri za jeshi uraiani.

Afande huyo mzee wa vitisho alisema
“Jeshi linaamini kuwa siri ama habari zinasambaa kwa haraka pale zinapowasilishwa na mwanamke tofauti na mwanamume, kwahiyo kwa sababu wewe kiumbe umetoa siri zetu huko chegani kwenye kusuka ama kwenye kijimeza chenu cha kasusu na sisi tunaamua kuchukua sehemu zako siri ili tuone je, siri iliyotoka ni yetu au ni yako”.

Waliporudi wale jamaa walioagizwa kwenda MAHANGANI walithibitisha uwepo wa walinzi wa HANGA watano kati yao wawili ni MADAWILI na waliobaki ni upande wa pili hivyo idadi ilikaa sawa.,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,

******Itaendelea……………………………………………...
 
Back
Top Bottom