chiembe
JF-Expert Member
- May 16, 2015
- 16,859
- 28,112
Nikipitia maisha ya Hussein Jumbe, naona kama hakuwa na furaha, japo alikuwa anatumia muda mwingi katika kumbi za burudani zilizotarajiwa au zinazosemwa ni sehemu za furaha.
Moyo wake ulijaa mambo mazito, mzigo mzito, malalamiko, na kilio kwa Mungu. Alikuwa akionewa bila hatia. Hata uso wake haukuwa na Nuru ya furaha.
Mara kadhaa alilalamika kwamba Kuna vitendo vya kishirikina vilikuwa vinafanywa kwake. Aliugua sana, kipindi kile mpaka akatunga wimbo "nachechemea". Chanzo Cha kuugua, aliota nyoka anataka kumdhuru au amemdhuru, baada ya siku kadhaa, yule nyoka akaonekana chumbani kwake katika suruali, nyoka akauliwa na wanamtaa, hapo ndipo aliugua karibu kifo.
Baadae akajikuta tu anavunjika mfupa wa mguu, bila kujikwaa chochote. Hapo napo aliota ndoto ya ajabu, mara hiki na kile, anaamka asubuhi anaenda kusali, anarudi, mguu ukapata shida.
Stori ya huyu ndugu inanifanya niendelee kuiogopa Tanga. Na pia inanifanya nione jamii ya kiafrika Ina ushenzi fulani, kwa baadhi yetu.
Pumzika kwa amani Hussein Jumbe.
N.B: katika mahojiano fulani anaonekana kumsema kaka yake kwamba alikuwa anamzushia kuugua ngoma, kama kuzuia watu wasimsaidie, akapima akawa safi. Lakini bado anaumwa!!!!!
Medi Mpakanjia akampeleka Mombasa, akakutana na fundi, ndio akaponea huko, ila mchawi wake hakuchoka, aliendelea kumpa vitimbi. Bila shaka Sasa roho ya huyo mwanga itakuwa imetulia na atachinja kuku baada ya kusikia habari za kifo.
Sasa jamani mziki wa bendi posho kiduchu, ndio kumpiga mtu misumari hivyo?