Maisha ya Kamari yamefanya Vijana wawe wavivu, wazembe ,wasofanya kazi Kwa Bidii

hii kitu bila serekali kuingilia kati tunaenda pabaya km taifa

wapige marufuku aya matangazo ya kubet yamekuwa mengi mno ndo yanahamasisha watu kubet
Serikali yenyewe inahamasisha kamari kupitia TBC.
 
Ushauri murua kabisa huu
 
Hili taifa siyo la baba yako wacha wapotee tu.No hurry in Africa,usiumize kichwa sana linapo kuja suala linalo husu Africa na uongozi wake au na kili kitu kilichomo Africa.Professor Lumumba anasema tatizo la Africa wenge madaraka hawana akili za maendeleo na wenye akili za maendeleo hawana madaraka,ila akashangazwa kwamba unapokuja uchaguzi nguvu ya hao wenye akili ya maendeleo kuwashobokea wenye madaraka ni ya kushangaza sana.Pia rejea Donald Trump alisha sema ukitaka Africa ibadirike inatakiwa iendelee kutawaliwa upya.Pia bear in your mind that hakuna hata raisi mmoja katika bara hili anaye tawala bara hili hawa wote maraisi wa Africa ni vivuli tu vya mataifa makubwa,Akitokea mpiga kelele mmoja anauliwa chini kwa chini ili bara la Africa liendelee kutawaliwa.Sasa vijana wa Africa wasipowekewa mkazo kwenye kubet si itakuwa vigumu kuwatawala huko mbele?Inabidi wajengewe mazingira ya kuwachanganya na maisha kiasi kwamba wasiwaze hata kesho yao itakuweje.

Sent from my TECNO LA7 using JamiiForums mobile app
 
Wakibadilisha mfumo mbovu wa elimu ya kikoloni na kuacha kutumia akili bandia na wazee wasio na mchango wowote katika sekta nyeti ndani ya nchi wanao vurunda kila kukicha . Na badala yake wakawekeza katika matumizi mazuri ya nguvu na akili za hali ya juu zinazotumiwa na vijana kubet taifa litafika mbali sana na kuokoa vijana wengi.

Swali..

Hiv mlilishawahi kujiuliza haya maswali

i) ba+ ba= Baba

ii) ba +ba = 2ba ( kwanini isiwe na hii ""baba"

iii) 2+2 = 4 ( kwanini isiwe 22 kama msingi ulivyojengwa tokea utotoni kupitia swali kipengle cha kwanza)

Je, mlishawahi kujiuliza kwanini hii hesabu inakua hivyo na je, zinakusaidia nini basi wewe katika kujiajiri na kujikwamua kiuchumi ili uweze kujitegemea na kulipa kodi halali kwa maendeleo ya Taifa lako bila kukuletea mchanganyo mchanganyo kama ilivyo hapo juu?

Nb: Mfumo wa uchumi wa vijana na taifa husika umeathiriwa na mfumo wa elimu walioipata vijana miaka yote wa wapo mashuleni na vyuoni huku wakipewa karatasi lisilo wasaidia kujiajiri wala kuajiriwa popote pale ,bali wazee wao wakizidi kung'ang'ania madaraka na sekta za kiuchumi wasizo na uwezo nazo badala ya kukaa pembeni na kuwaachia vijana


Nb: MSINGI UKIWA MBOVU NYUMBA HUHARIBIKA, JE SWALI LA KIPENGELE CHA KWANZA HUKO JUU SINDIYO MSINGI ULIVYO ?

Ba + ba = baba

Kwanini basi ubadilike kila unaposogea mbele?
 
Mimi pia nabet. Naomba ajira niache kubet mkuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…