Maisha ya machimbo ya dhahabu ni zaidi ya jeshi, nilikimbia

Ningetangulia kuusoma huu uzi wala nisingeenda machimboni kabisa..
Ila nilienda mwezi wa kumi na moja mwaka huu nimerudi mwezi wa kumi na mbili kati kati aisee aisee aisee..
Na sisi tulifungua duara tukiwa wanne tu so mgao unaenda kwa jina kamili ama jina nusu.
Na huko ni mgodi wa dhahabu pure ama vikole na sample..
Oyaa nyie viroba 30 vinatoa pointi mbili au mbili na nusu daily na hapo mko karibia tisa pamoja waoshaji kwenye ushirika huo.
Nilichoishia kukipata huko ni elfu ishirini mpya mpya tu
Sijapata hata ile ya kujitetea maisha yangu..
Hapa nilikuwa nimekaa navuta pumzi niibukie huko mbeya mara paaap uzi huu hapa..
Na hapo mimi ni nyoka tu wa fonko.
Aisee sijui niende mgodi mwingine sijui nitafute vibarua vingine nifanye tu maana daah sio poa..
Au niende Shinyanga kwenye almasi yaani hata sielewi niko dilema wakuu
 
Sijui kuhusu upande mwingine wa hayo madini hali yake ikoje.

Ila dhahabu naijua misoto yake. Machimbo yanafilisi, machimbo yanahitaji roho ngumu haswa.

Ukishaona mpaka wamiliki wa makarasha wanafikia hatua ya kuwasagia watu bure ndio ujue kiasi gani soko limekuwa gumu.

Kama kuna ushauri ambao naweza kumpa kijana mwenzangu katika harakati za kujitafuta, siwezi nikamshauri afanye kazi ya machimbo hususan dhahabu.
 
Wale walioko kwenye Tanzanite na Almasi wanipe koneksheni basi nichomoke kutoka huku Rock city nizamie mgodini tupige kazi naamini wapo humu..wanaojua machimbo ikibidi na namba waweke kwa msaada zaidi..
 
machimbo ni zaidi ya kamari,...nimechimba chunya,..lile life ni 🀐πŸ”₯πŸ”₯πŸ™ŒπŸ™Œ
 
Tupe hiyo historia ya huyo mzee mkuu
 
Elekea Katoro au Kakola

Ukifika Katoro ulizia Lwamgasa
 
😹😹😹
Huyo baba yako mimba yako itakuwa mama yako alimsingizia..!!
Nimecheka hapo wewe ulivyochakaa kuliko uliokuwa unawashangaa mwanzo 🀣
 
Nimekwenda mchimbo ila, Kazi yangu ilikuwa ni kusupply water pumps kwa. Ajili ya kusafisha mchujo wa dhahabu, kwangu haikuwa kamali maana ni kazi mnapatana kabisa, ila kwa wachimbaji ni bahati nasibu sana
 
Hujapiga hata M5 in summation mkuu?
sijui labda,.. lakini kuna kipindi hadi msosi ilikuwa mzozo,....unashusha nyundo ukiwa na njaa,.....hili life hapana,.....kwa ufupi maisha ya chimbo yameniachia, funzo, trauma na makovu,..πŸ™ŒπŸ™Œ
 
sijui labda,.. lakini kuna kipindi hadi msosi ilikuwa mzozo,....unashusha nyundo ukiwa na njaa,.....hili life hapana,.....kwa ufupi maisha ya chimbo yameniachia, funzo, trauma na makovu,..πŸ™ŒπŸ™Œ
Kwa ushuhuda huu acha tu nikawe kondakta DSM tu nitatibu njaa
Na kumake chapaa japo ni ado ado but nitafika target hata kama ni baada ya miaka mitatu sawa
Maana naweka targets za miaka mitano mitano..
 
Aisee mbona umekata moto mapema hivyo jomba ?
Miners huwa ni roho ya paka ,sasa wewe unakata tamaa mapema hivyo vipi wewe ,,?
 
Aisee mbona umekata moto mapema hivyo jomba ?
Miners huwa ni roho ya paka ,sasa wewe unakata tamaa mapema hivyo vipi wewe ,,?
Mjomba,, we only need to be stable financially and On top of that,, kuna kupiga mark-time huku ukiwa unapoteza kila kitu only to chase for money!!
Konda wa Dar analaza 25k to 15k per day thats a lot of money if well managed..
Hakuna kikubwa sana kurisk life lako underground ukisaka tofali man
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…