Maisha ya machimbo ya dhahabu ni zaidi ya jeshi, nilikimbia

Maisha ya machimbo ya dhahabu ni zaidi ya jeshi, nilikimbia

Kazi zingine Mimi siyokuja kudhubutu kuzifanya hata niwe nimepigika kiasi gani
 
Dhahabu unayong'ara hupitishwa kwenye tanuru la Moto... Hakuna kitu rahisi kwenye utajiri, high risk high return jinsi unavyosacrifice Roho yako kutafuta utajiri siku ukitoboa unakuwa level nyingine kabisa

Kuna kaka mmoja nilikuwa sehem ya geita huko alikuwa akisimulia kaka ake alivyotoka kwenye umasikin na kuwa Tajiri wa kufa mtu, yeye alienda Kongo huko bila vibali nakumbuka Kongo kila hatua Kuna magaidi hawajawahi nyoa ndevu.

Sasa alienda huko na kuingia kwenye sehemu za madini unaambiwa alipofika alikaa sio chini ya miaka mitano kuchimba dhahabu Kwa jembe na nyundo huku wajeda wakija kukagua wenye vubali anajificha kwenye mashimo hata siku Tatu bila kula Wala Maji

Kufupisha tu story alikuja kupata jiwe la dhahabu maana Kuna Mawe wengine asilimia sabini ni dhahabu tupu, akaweka kwenye begi akaanza kukimbia pori Kwa pori kurudi Tanzania tena Kwa mguu alipofika kwenye misitu minene alikutana na makundi ya kigaidi waanza kumfurumusha Kwa risasi jamaa akawa anakimbia zigizaga akakuta mto akajirusha ndo pona yake akaja kuibukia ng'ambo japo mto ulikuwa na mamba wa kutosha alivuka salama.

Siku ya pili hajapata kitu mdomoni yupo na jiwe tu la dhahabu japo hana uhakika mpaka akaipime, bahati akafika ziwa tanganyika akapanda boti Kuja Tanzania alipofika kigoma akapanda gari la geita akaenda soko la madini, wakaisafisha lile jiwe akapata dhahabu kilo tano mzee mzima akaingiziwa mpunga CRDB

saizi ni Tajiri pale geita changanya Mali za Fred vunjabei na sandaland hawamfikii hata robo.

Hakuna jepesi hii Dunia ukitaka kubaki masikini basi endekeza uoga na usisumbue watu kuomba msaada wa pesa huwa mnakera
Unakaa unatunga uongo wa kitoto na kutuletea watu wazima humu!!:huo uongo wa kipumbavu wadanganye watoto wenzio.
 
Anaitwa nani?
 
Nljichanganya nkaenda mwakitolyo bila mtaj nkasema ntakomaa asee[emoji119] kwanza jua n kal sana kulko sehem yoyote tanzania dhahabu kupatikana nikwa mbinde sana yan unachakaa mpaka unajisahau siku ukitaka kwenda mjin inabid upumzke hata siku mbil kwanza unyoe uoge mara mbil mbil il kesho hata ukienda mjin uonekane n mtu. Machimbon maisha ni ghal sana na hela ni ngum sana kupatikana
Huko kuko kama kama za wakimbizi wa sudan....kumejaa maturubali na vibanda wanaopata hupata kidogo sana
 
Mkuu....
Hiyo Busulwangili, Nyalwanzaja, Namba 9, Namba 2 unauonaje mziki wake kwa wachimbaji wadogo...??
Wanapata pesa kiduchu ...tajiri nae yuko mob na wenzake wakipata 100m wanagawana na kuishi kunywa bei n wanawake
 
Mwanzishaji thread na waliochangia. Kwenye migodi kuna mengi. Kuna watu wa kada mbalimbali. Wengi wanaozungumziwa humu ni wale wafanyakazi wa migodini, yaani waponjaji. Waponjaji ndio kazi yao. Hawaiogopi na wanaifurahia sana. Hao ninkama vibarua huku mitaani. Niambieni mbeba zege au mchanganya mchanga anayetoboa. Au mvuvi, sio mwenye mtumbwi.
Kule inategemea na mtaji ulio nao. Kuna watu wanaenda kule wao kazi yao ni kununua hizo poont point. Anakusanya zinakuwa gramu anaenda kuuza. Na wanafanikiwa.
Kuna wale wanaonunua makrasha wanawasagia wenzao, wanapata pia.
Kuna wanaosambaza viroba vya sulphate, maana vinatumika sana. Hao ni wafanya biashara.

Nawaomba mtofautishe vibarua na wafanbiashara hata kama wana mitaji midogo.
 
Kwenye shughuli ya machimbo unabeba zana ya jembe?

Basi hiyo ardhi ni soft sana

Nenda Chunya utaoneshwa sululu zilizopinda baada ya kukutana na hardcore rocks na vijana hawataki kukubali kuwa imeshindikana.
Get Rich or die trying....

Wachimbaji wadogo wana imani kali sana kuwa ipo siku tu atatoboa haijalishi kachimba na kutoka hola kwa miaka mingapi.
 
Kwa 25M alidhani atapata nini? 25M kwenye madini is nothing Bora angefuga kuku tu. Tatizo wengi wanadhani uchimbaji is a get rich quick scheme it's absolutely not.
Mtaji mzuri wa kuanzia ni upi chief ?
 
Mtaji mzuri wa kuanzia ni upi chief ?

Mkuu, inategemea unataka kufanya nini kwenye hii sekta. Unataka kuchimba, kuuza madawa na vifaa, kukodisha vifaa, kumiliki plants kama elution na leaching plants.

Uchimbaji unahitaji gharama, muda na utaalamu zaidi. Kadhalika uchimbaji ni risky ila return yake inaweza kuwa kubwa zaidi. Risks za uchimbaji zinaepukika kwa kuwekeza kwenye maarifa na utaalamu.
 
Back
Top Bottom