monopoly inc
JF-Expert Member
- Dec 20, 2016
- 5,256
- 11,377
Oyaa mwanangu Mpwayungu VillageDhahabu unayong'ara hupitishwa kwenye tanuru la Moto... Hakuna kitu rahisi kwenye utajiri, high risk high return jinsi unavyosacrifice Roho yako kutafuta utajiri siku ukitoboa unakuwa level nyingine kabisa
Kuna kaka mmoja nilikuwa sehem ya geita huko alikuwa akisimulia kaka ake alivyotoka kwenye umasikin na kuwa Tajiri wa kufa mtu, yeye alienda Kongo huko bila vibali nakumbuka Kongo kila hatua Kuna magaidi hawajawahi nyoa ndevu.
Sasa alienda huko na kuingia kwenye sehemu za madini unaambiwa alipofika alikaa sio chini ya miaka mitano kuchimba dhahabu Kwa jembe na nyundo huku wajeda wakija kukagua wenye vubali anajificha kwenye mashimo hata siku Tatu bila kula Wala Maji
Kufupisha tu story alikuja kupata jiwe la dhahabu maana Kuna Mawe wengine asilimia sabini ni dhahabu tupu, akaweka kwenye begi akaanza kukimbia pori Kwa pori kurudi Tanzania tena Kwa mguu alipofika kwenye misitu minene alikutana na makundi ya kigaidi waanza kumfurumusha Kwa risasi jamaa akawa anakimbia zigizaga akakuta mto akajirusha ndo pona yake akaja kuibukia ng'ambo japo mto ulikuwa na mamba wa kutosha alivuka salama.
Siku ya pili hajapata kitu mdomoni yupo na jiwe tu la dhahabu japo hana uhakika mpaka akaipime, bahati akafika ziwa tanganyika akapanda boti Kuja Tanzania alipofika kigoma akapanda gari la geita akaenda soko la madini, wakaisafisha lile jiwe akapata dhahabu kilo tano mzee mzima akaingiziwa mpunga CRDB
saizi ni Tajiri pale geita changanya Mali za Fred vunjabei na sandaland hawamfikii hata robo.
Hakuna jepesi hii Dunia ukitaka kubaki masikini basi endekeza uoga na usisumbue watu kuomba msaada wa pesa huwa mnakera
Acha kuleta story za vijiwe vya bodaboda
Utembee misitu ya kongo unaijua wewe
Yani story umesimuliwa
Na aliekusimilia alisimuliwa
Na alisimuliwa na kak yake