Maisha ya machimbo ya dhahabu ni zaidi ya jeshi, nilikimbia

Maisha ya machimbo ya dhahabu ni zaidi ya jeshi, nilikimbia

Nyie mnasema ni Tajiri wa madini namm ninavyojua matajiri wa madini hiyo pesa ni ndogo sana hata kukopa hatakopa maana wanaingiza Kwa wiki tu, nenda katoro kaone watoto waliozaliwa 1992 wanachukua mzigo wa kilo tano mpaka kumi wa dhahabu kila siku nahawalingi

Delusional.
 
Dhahabu unayong'ara hupitishwa kwenye tanuru la Moto... Hakuna kitu rahisi kwenye utajiri, high risk high return jinsi unavyosacrifice Roho yako kutafuta utajiri siku ukitoboa unakuwa level nyingine kabisa

Kuna kaka mmoja nilikuwa sehem ya geita huko alikuwa akisimulia kaka ake alivyotoka kwenye umasikin na kuwa Tajiri wa kufa mtu, yeye alienda Kongo huko bila vibali nakumbuka Kongo kila hatua Kuna magaidi hawajawahi nyoa ndevu.

Sasa alienda huko na kuingia kwenye sehemu za madini unaambiwa alipofika alikaa sio chini ya miaka mitano kuchimba dhahabu Kwa jembe na nyundo huku wajeda wakija kukagua wenye vubali anajificha kwenye mashimo hata siku Tatu bila kula Wala Maji

Kufupisha tu story alikuja kupata jiwe la dhahabu maana Kuna Mawe wengine asilimia sabini ni dhahabu tupu, akaweka kwenye begi akaanza kukimbia pori Kwa pori kurudi Tanzania tena Kwa mguu alipofika kwenye misitu minene alikutana na makundi ya kigaidi waanza kumfurumusha Kwa risasi jamaa akawa anakimbia zigizaga akakuta mto akajirusha ndo pona yake akaja kuibukia ng'ambo japo mto ulikuwa na mamba wa kutosha alivuka salama.

Siku ya pili hajapata kitu mdomoni yupo na jiwe tu la dhahabu japo hana uhakika mpaka akaipime, bahati akafika ziwa tanganyika akapanda boti Kuja Tanzania alipofika kigoma akapanda gari la geita akaenda soko la madini, wakaisafisha lile jiwe akapata dhahabu kilo tano mzee mzima akaingiziwa mpunga CRDB

saizi ni Tajiri pale geita changanya Mali za Fred vunjabei na sandaland hawamfikii hata robo.

Hakuna jepesi hii Dunia ukitaka kubaki masikini basi endekeza uoga na usisumbue watu kuomba msaada wa pesa huwa mnakera
Kuna uongo mwingi humu, japo mazingira ya utafutaji wa dhahabu ni kweli magumu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wale wachina wa Saza nilisikia wameondoka ila sina uhakika, kuna wachina wengine Mdimi alinunua claim yao na kavuta umeme kwa 800M TSH. Wachina wajinga wajinga tu.

Wachina walishaondoka kwa sababu za kikodi. Saza ipo Wilaya ya Songwe, wanapeleka marudio kuozeshwa Matundasi (Wilaya ya Chunya), wilaya zote zinataka mapato. Wachina wakasepa. Kwa kifupi hizo ndiyo sababu tulizoambiwa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Safety is given priority than any bullshit.

Ukikaa karibu na moto unakuwa umechagua kuota au kujiunguza.

Ukikaa kwenye mazingira ya machimbo ambayo usalama wake ni mdogo unakuwa umechagua

1. kupoteza kiungo
2. Kuumwa
3. Kufa.

Bahati mbaya 1 na 3 imekuwa ikijitokeza mara nyingi sana with my experience
Anyway, kwani Kuna hasara gani anayopata mtu aliyekufa?
 
Uongo kama upi
Wewe ulimwamini kwa 100% aliyekusimulia?
Story imechanganywa na uongo, nawe ukaamini Kila kitu ni sahihi.

Mazingira ya uchimbaji madini DR Congo huyajui (pengine hata kidogo), lakini nawe ukaamini uliyosimuliwa Kwa 100%, ndiyo maana umeleta story kama ilivyo kwamba "akadumbukia kwenye Mto wenye Mamba, mara Wanajeshi amewakwepa, mara hajala siku kadhaa..... Bla bla bla bla". Ndugu, story yako inamkanganyiko Kwa sababu imechanganywa uongo na ukweli.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mwambe nishamsikia 🤣 ujanja ujanja ulikua mwingi kipindi kile hadi sasa upo ila kama unajua unachokifanya na una mtaji hii biashara inalipa.
huyu mzee Mwambe alikuwa anakusanya dhahabu na kuweka Store, alikua ana handaki ndani ya nyumba yake. Kuna mambo aliyokuwa akiyafanya na hakuna mtu yeyote aliyekuwa akijaribu kupanga kumvamia ili kuiba dhahabu. Unaambiwa alikuwa na kiasi kikubwa maana kilasiku alikuwa akiletewa na wapambe wake aliowapa vipimo na kuwagawia pesa kwa asilimia waliokuwa wamekubaliana. Sasa wazungu katika survey yao kwa ndege wakagundua eneo la nyumba ya yule mzee Kuna azina kubwa sana ya dhahabu. Sikumoja wakamuibukia na kumwambia wanakitaka lile eneo, wapo tayari wampe 1 Billion pia watamjengea nyumba ya kifahali eneo lolote analotaka Mbeya mjini na ahadi ya kuwasomesha watoto wake mpaka level ya chuo.
Mzee akawasikiliza na kunyanyuka kwenda ndani, alirudi na mfuko na kumwaga dhahabu mbele za wale wazungu na kuwaambia "Hizi nimewapa kama dhawadi kwa kunitembelea, nimewasikiliza na naomba muondoke."😃😃
Wazungu wakatoa macho baada ya kugundua kuwa sio kama dhahabu ipo chini ya ardhi bali mtu anayo ndani ya nyumba yake kaitunza na kiasi kile amewapa kama dhawadi tu, je huyo mtu huko store ana kiasi gani?😃😃
 
Leo nimepokea taarifa ya kifo cha ndugu yangu akiwa machimboni huko Mkwajuni.

Sababu ya kifo bado haijaelezwa ila taarifa ya mwanzo tuliyopokea tulibiwa kulitokea ajali.
Pole sana mkuu, uchimbaji mdogo wa maduala ajari ni nje nje especially Kama duala halijafungwa timba vizuri au wakazembea kufunga duala baada ya koleo zaidi ya nne.
Rest in peace bro wetu
 
Wewe ulimwamini kwa 100% aliyekusimulia?
Story imechanganywa na uongo, nawe ukaamini Kila kitu ni sahihi.

Mazingira ya uchimbaji madini DR Congo huyajui (pengine hata kidogo), lakini nawe ukaamini uliyosimuliwa Kwa 100%, ndiyo maana umeleta story kama ilivyo kwamba "akadumbukia kwenye Mto wenye Mamba, mara Wanajeshi amewakwepa, mara hajala siku kadhaa..... Bla bla bla bla". Ndugu, story yako inamkanganyiko Kwa sababu imechanganywa uongo na ukweli.

Sent using Jamii Forums mobile app

Sio uongo na ukweli bali ni uongo tena uongo wa kitoto mwanzo mwisho. Inabidi uwe zwazwa kuamini hiyo story. Hizo ni story za vijiweni watu wakishatumia mihadarati wanaanza kudhani wapo mbele.
 
Uongo ni upi taja?? :kwani mto wenye mamba ni kila sehemu?
 
Sio uongo na ukweli bali ni uongo tena uongo wa kitoto mwanzo mwisho. Inabidi uwe zwazwa kuamini hiyo story. Hizo ni story za vijiweni watu wakishatumia mihadarati wanaanza kudhani wapo mbele.
Sehemu ipi niyauongo ambayo Duniani haiwezi kututokea kama binadamu?? Au tumwite Scars nae aje atoe maoni yake
 
So illogical. Mtoto inabidi aendelee mzazi alipoishia na mzazi ana wajibu wa kufanya maisha ya mwanae marahisi sio kumrudisha nyuma makusudi kwa kigezo cha kujifunza, hakuna tuzo ya kupitia maisha magumu zaidi ya kukuharibu tu. I hope wewe hautakua na mawazo ya kijima ya kumfukuza mwanao.
vyema sana... Wazazi wengi wa kiafrica wakifa wao hata biashara zao zinakufa...sababu hazina warithi wa kuweza kuziendeleza kweli...
 
Back
Top Bottom