Maisha ya madaktari wa Kitanzania na umaskini wao na kuishia katika kupata heart attack

Mheshimiwa Dakitare ni kweli Mishahara ya Watumishi wote ni changamoto sio Madakitare peke yao tu, na kitu ambacho unajua kabisa kwneye Kada ya Afya ni Nyie ndio Mna mishahara mikubwa sana pengine kuliko kada yoyote ile iwe Tamisemi au serikali Kuu kwa kuanzia na ndio nyie pekee ukiachana Academicians mna scale za Masters (MMED) na super Soecialist (Msc) hakuna kada nyingine iwe Nursing, Lab, Pharm wala Wengine hawa Mwisho ni Degree tu

Kiufupi Utumishi wa UMMA ni kujisajili kwenye ubangaizaji SMART sio kwenu pekee ni kila kada!! Tena hata Bora nyie hasa waliopo RRH, Zonal, na National mna On call, Extra duty, BIMA kuna Mwalimu maskini wa Mungu yeye anajua Salary Pekee
 
Hela nzuri kwako ni shilingi ngapi ukilinganisha na kazi wanazofanya na muda wanaojitoa kuokoa maisha ya watanzania wenzako, muda na gharama walizotumia kuwa DAKTARI, katika familia yako au yenu mna Daktari au jirani? ushawai kupiga naye story, hospital unajua zilipo basi tembelea pale na kapige story na madaktari
 
Super specialist ni level ya kielimu isiyotambulika katika salary scale hapa Tanzania, lakini pia utumishi wa umma haimaanishi ni kuwafanya watu wateseke na kuwa na maisha magumu ili hari serikali inafaidi, ndio maana katka kitu pekee ambacho ninaomba issue za afya ziwe katika wizara moja tu, mambo sijui wengine ni watumishi wa tamisemi wengine wizara ya afya haina maana, taratibu jamii ya watumishi wa afya Tanzania utendaji kazi utabadilika na wachache sana watakaobaki nao watakata tamaa
 
Upo sahihi kabisa
 
Ndio analipwa hvy fatilia, na changamoto zaidi wanasiasa hapa nchini wanapewa na wanajipa kipaumbele zaidi kuliko watu wenye taaluma zao
 
Naongezea na walimu. Maslahi yaongezwe...
 
Umesema vyema. Nadhani kwasasa jukwaa zuri ambalo lingetufaa kupambania maslahi yetu ni MAT. Changamoto ya MAT sasa hivi imekuwa yakisiasa sana.
 
naunga mkono hoja .umeongea UKWELI MTUPU

Yule RAISI WA MADOKTA ,wa kuitwa DOKFA ULIMBOKA alikuwa anapigania madaktari walipwe kima cha chini milioni tatu .sijui alliishia wapi.
 
Wahudumu wa afya hii nchi wanalipwa hela ndogo sana,haiendani na thamani ya kazi yao, na hawajaliwi. Imagine kuna daktari bingwa wa Sekou Toure alipata ajali akiwa kazini akakosa pesa ya matibabu ikabidi achangiwe, yaani daktari anakosa pesa ya matibabu? Aibu utaona wewe.
 
Madaktari wanalipwa hela nzuri wa hospital gani mkuu? Au unamaanisha Aga Khan na Saifei?
 
Hayo mambo ya daktari kufanya kazi huku anawaza baada ya muda mfupi aende kutafuta pesa za ziada ndo yanafanya ikija issue ya ugonjwa complicated ambao inahitaji daktari akusikilize kwa utulivu anakuwa anarush awahi kupata pesa ya ziada, matokeo yake mtu akiumwa ugonjwa tofauti na yale common anazunguka hospital mpaka anachoka hapati matibabu maana madaktari hawawazi kutibu wagonjwa wanawaza wawahi kwenda kutafuta pesa.
Wahudumu wa afya wanapaswa kulipwa vizuri na kujaliwa ili wafanye kazi bila stress ya aina yoyote. Nchi nyingine madaktari wanalipwa pesa nyingi kuliko wanasiasa.
 
Hii kada sitaruhusu mwanangu haingie hii kada, ina stress shuleni hadi kazini, familia yetu imetoa 2 doctors, nimeshuhudia stress zao wakiwa medical school pale MUHAS hadi leo wapo kazin ila hawana furaha na hii kazi, kuna moja kaenda kusoma bachelor nyingine ya BAF nahic akipata kazi yake ataachana na medical field.
 
Wizara ya TAMISEMI inaingilia wizara mama nadhani hii ipo Tz tu(uvuvi,barabara,afya,elimu).Hii nchi sijui walilenga nini na ukiangalia huko TAMISEMI ndio kumejaa uozo🤔.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…