Maisha ya madaktari wa Kitanzania na umaskini wao na kuishia katika kupata heart attack

Kikawaida madaktari wengi huwa ni wale watoto wa kimaskini ambao wamesoma na kusomeshwa kwa shida na uchungu mkubwa sana familia zao na asilimia zaidi 80% wanatoka katika familia za kimaskini, na asilimia chache au ndogo kama 20% ni wale wanaotoka katika familia bora.
Wapo wanaotoka familia zenye uwezo pia, kama sijakosea kuna mstaafu asiyestaafu ana mtoto ni Dr
 
Napenda kuandika haya yafuatayo kwa uchungu mkubwa sana na kama jamii pamoja na Serikali itapenda kulichukulia jambo hili kwa umakini mkubwa itapendeza sana.

Daktari ni mtu pekee hapa Tanzania anayeongoza kuwa na heshima kutokana na nafasi yake kama daktari na namna ambavyo anatekeleza majukumu yake kwa moyo kuhakikisha wagonjwa wanapona, ndugu wa wagonjwa wanapona pia kisaikolojia lakini huku daktari huyo akiteketeza maisha yake ya kijamii kwa ndugu na familia yake.

DAKTARI ANAPATIKANAJE HAPA TANZANIA.

Kikawaida madaktari wengi huwa ni wale watoto wa kimaskini ambao wamesoma na kusomeshwa kwa shida na uchungu mkubwa sana familia zao na asilimia zaidi 80% wanatoka katika familia za kimaskini, na asilimia chache au ndogo kama 20% ni wale wanaotoka katika familia bora.

Miaka 7 ya shule ya msingi, miaka 4 ya Ordinary level (O-LEVEL), Miaka 2 ya advanced level (3 ya clinical medicine) na miaka 6 ya degree (5 chuo na 1 internship) jumla ya miaka 19 jumla ya kupata degree ya kwanza na kuanza kupractice udaktari kama Medical officier II (Registrar), ambaye kikawaida hadi baada ya makato daktari huyu anabaki na kiasi cha shilingi 840,000/=, kiasi hiki cha pesa anatakiwa kimsaidie katika maisha yake yote kula, kuishi (Makazi), Kuvaa, familia yake kuishi vizuri, familia iliyomlea kuishi vizuri na hata aweze kufanya mambo mengine ya kijamii, hapa ndipo ugundua madaktari wengi kuwa katika maisha yenye stress kubwa ilihari kutimiza majukumu yao kwa moyo mmoja. LAKINI WAPO PIA AMBAO UAMUA KUCHUKUA MIKOPO BANK NA KUJIKUTA PIA ANGALAU AKIHITAJI KUFANYA JAMBO FULANI NA KWASABABU YA MUDA NA USIMAMIZI MZURI ANAFELI SO ANABAKI KUPOKEA HATA SHILINGI 300,000/= AU 400,000/= NI MBAYA SANA HII.

Daktari huyu kwa upendo wa kuwasaidia watanzania uamua kusoma zaidi na kuwa Daktari bingwa mpaka daktari bingwa bobezi maana yake miaka mingine 6 juu uongezeka plus ile miaka 19 aliyotumia katika kupata degree ya kwanza inakua jumla miaka 25, kwahiyo ili umpate daktari bingwa bobezi labda wa Mfumo wa chakula na ini, mfumo wa fahamu, magonjwa ya moyo, upasuaji sanifu, mifupa, ngozi unahitaji miaka 25 mpaka 28 kwa vyuo vingine ambavyo masters ni miaka minne minne.

maana yake almost ujana wake wote wa maisha yake uhutumia katika kudhalisha madaktari bingwa bobezi ambao huwa na maisha ya kawaida sana kuliko mtu ambaye angeamua kufanya biashara zake nyingine kama watu wa KATORO.

Serikali kupitia RAIS aliyepo madarakani
sasa alisikika Dodoma akisema anatambua Madaktari maisha yao yalivyomagumu kwakuwa maslahi yapo chini sana lakini hatambui katika kufanya maslahi ya madaktari yawe juu, yeye pamoja na waziri wa afya wa sasa wanayatambua haya.

lakini kuna wanasiasa ambao wamekaa wanatunga sheria hizi za kuwabana hata madaktari wanalipwa vizuri sana zaidi ya milioni 10 kwa mwezi, lakini si daktari ambaye atakomea 840,000/=, 1,500,000/= na 2,500,000/= kwa registrar, daktari bingwa na bingwa bobezi.

Daktari amekuwa mtu ambaye atashinda hospitalini kuokoa maisha ya mgonjwa, kuwatibu ndugu zake kisaikolojia na bad enough hadi ndugu wanatambua hali za madaktari wao kwa umaskini inabaki tu sifa ya kusema yule ni daktari yule ni daktari.

Ndio maana tumeanza kupoteza jamii ya madaktari vijana unasikia tu kafariki kwa HEART ATTACK, kumbe kisa stress nyingi.... Mfano juzi juzi tumepoteza daktari bingwa bobezi wa figo ambaye amefariki akiwa na miaka 35 tu na huyu daktari ametumia miaka 28 kujitengeneza kufika hapo, Taifa likapoteza mtu wa muhimu sana ukiangalia miaka 35 yake ukitoa miaka 28 unapata miaka 7 tu ya yeye ambayo aliishi bila kufanya jambo lolote maana yake alifaidi utoto wake tu wa miaka 7.

Ndio maana madaktari wengi hawahusishi LESENI zao kwakuwa hela yenyewe ya kuhusisha leseni angalau hata ingekua taasis au mahospital inawakatia leseni watu wake lakini hela ipo juu na ndio maana madaktari wengi they are not allowed to practice lakini wanafanya kazi.

Madaktari wamekuwa watu ambao hata akipata 10,000/= kutoka kwa mgonjwa atafurahi ilimradi apate hela ya kula, daktari huyo anayeshinda hospital muda wote anakosa muda wa kufanya hata angalau sehemu ya pili ya kujidharishia kipato na asipoonekana anaambiwa mzembe na hafanyi majukumu yake mnataka ale wapi????​

NDIO MAANA WAKATI MWINGINE MADAKTARI KWA SASA WANACHUKUA WASAHAA WA KUWASHAURI VIJANA WENGINE WALIOPO NYUMA KUTOKUJA KUSOMA KADA HII YA AFYA YENYE SIFA YA JINA LAKINI MAISHA NI MABAYA NA MAGUMU SANA.

MADAKTARI
WENGI SAIV WANAISHIA KUINGIA KWENYE BETTING PIA WAKIAMINI WANAWEZA KUJIPATIA CHOCHOTE KITU NA KUEPUKANA NA FEDHEA YA UMASKINI

SERIKALI NA JAMII KWA UJUMLA PIGANIENI HAYA KWA MADAKTARI WENU

1. ONGEZENI KIPATO CHA MISHAHARA KWA MADAKTARI MFANO NCHI JIRANI KAMA KENYA NA UGANDA MADAKTARI WANALIPWA VIZURI SANA, WANAANZIA MILIONI 4 MPAKA MILIONI 14 KWA DAKTARI BINGWA BOBEZI KUTEGEMEANA NA AMESOMA UBOBEZI UPI, KWANI TANZANIA MNASHINDWA NINI

2. JAMII IPAZE SAUTI MAANA HATA MAT ILIYOPO HAIFANYI MAJUKUMU YAKE YA KUPIGANIA MASLAHI YA WATU WAKE.

3. KUWE NA WIZARA MOJA TU INAYOHUSIKA NA MASLAHI YA MADAKTARI, KUSIWE NA MARA SIJUI TAMISEMI MARA SIJUI WIZARA YA AFYA, KWAMBA KUNDI MOJA LINAPATA MASLAHI MAZURI KULIKO KUNDI JINGINE.

4. KUWE NA MIHULI YA MADAKTARI KAMA JINSI ILIVYO KWA WANASHERIA TUTAMBULIKE HIVYO NA KWA NAMBA ZETU ZA MCT PALE, KWAKUWA ITASAIDIA ANGALAU KUONGEZA KIPATO PALE AMBAPO MUHULI WA DAKTARI MAALUM UTAKAPOHITAJIKA.

5. SERIKALI IANGALIE HATA KUMPATIA DAKTARI MMOJA MMOJA USAFIRI WA KAWAIDA WA KUANZIA AU KUMSAIDIA KUPATA MKOPO NAFUU WA GARI HUKU SERIKALI IKIONGEZA KIASI KADHAA CHA PESA NA DAKTARI KULIPIA TARATIBU KUPUNGUZA AIBU NDOGO NDOGO ZA KUGOMBANIA DALADALA, KUPANDA BODABODA ZENYE HATARI KUBWA YA KUPATA AJALI, NA HATA KUTEMBEA UMBALI MREFU KWENDA NYUMBANI NA KUNYOOSHEWA VIDOLE YULE NI DAKTARI YULE NI DAKTARI AMBAPO INAMUATHIRI KISAIKOLOJIA.

NATAMBUA MADAKTARI NI WENGI SANA WENYE KUHITAJI JAMBO HILI LIPAZIWE SAUTI BASI NA SISI TUFANYE HIVYO NA ANDIKA MATAMANIO YAKO NINI MADAKTARI WAFANYIWE​
Bila shaka wewe ni daktari. Umefanya kazi nzuri kuwasilisha mawazo ya kundi kubwa lililopo kwenye taaluma ya afya japo umegusia Madaktari pekee.

Kinachosumbua watumishi wengi nchini ni Uoga, Kutojiamini na Kutokuwa na misimamo.

Na hapo sekeseke la 'Dr Ulimboka' ndio lilifanya angalau maslahi yao kuwa mazuri.

Laiti kama wangefahamu nguvu waliyonayo, bila shaka 'watawala' wangeconsider maslahi yao.

Ni wakati sasa serikali kupitia upya 'Mishahara' ya watumishi wao ili angalau iweze kukidhi haja za maisha tuliyonayo sasa.

Wanaweza kuboresha maslahi hata kwa kuanza na makundi, mfano 2026/2027 ni walimu then 2027/2028 Afya and so forth.

Itasaidia kurudisha molari yao ya kazi katika kuwatumikia waTanzania.
 
Kabisa mkuu,yaani hii nchi kuna utamaduni wa wafanyakazi kuwa waoga, ajira inachukuliwa kama hisani, kiasi kwamba mtu anakaa kimya hata akionewa. Imagine huko Tamisemi diwani anaenda kumhoji daktari,diwani aliyeishia la 3C!!!!!!!!. Tunahitaji kushughulikia huu utamaduni wa uoga unaofanya wafanyakazi wanashindwa kutetea maslahi yao. Nchi nyingine hata wanasiasa hawachezi na kada za afya, maana wanaujua moto wao . Hapa Bongo, mjamzito akifariki kwa sababu hospital haina vifaa au dawa, manesi wa zamu wanakuja kudhalilishwa na mkuu wa wilaya kwenye vyombo vya habari, tena mkuu wa wilaya ambae hawezi hata kutaja jina la mshipa mmoja wa damu kwenye mwili.
 
Una hoja njema mkuu ila hasahasa kulingana na majukumu ya daktari.

Kuna kipindi nilizani udaktari sio kazi ambayo mtu anasomea kwa lengo la kupata kipato %100, namanisha udaktari kwangu ni kama uchunganji ule wa zamani yaani mtu anajitolea na kuridhika na kidogo atachopata.

Kama serikali haitaki kuwaongeza mshahara madaktari basi ndg watanzania tuwe na utaratibu wa kuwapa asante madaktari wetu pale wanapotuweka sawa kiafya. Binafsi hua siwezi kuondoka zahanati bila kuacha chochote kwa mhudumu wa afya alienihudumia, mf juzikati hapa mke wangu kajifungua salama manesi niliwapa 50,000 ya asante na kweli walishukuru sana ila mimi ndie niliewashukuru zaidi.

Dokta sio kama fundi pikipiki tuwajali.
 
Sekta nyingi serikalini mishahara haiendani na hali ya maisha sio madaktari peke yao, hii inafanya rushwa iwe solution ya ku-survive. Shida inakuja kwenye kada kama ualimu ambao hawana option ya kuvuta chochote kitu.. Hii sio sawa kabisa
 
Umesema vyema. Nadhani kwasasa jukwaa zuri ambalo lingetufaa kupambania maslahi yetu ni MAT. Changamoto ya MAT sasa hivi imekuwa yakisiasa sana.
Nyie machawa ndiyo mmeharibu siyo hiyo MAT tu bali karibu kila sekta kwa tamaa zenu za kuonekana na kupewa nafasi za 'kisiasa' na hao wahuni wanaojiita watawala.
 
Hivi hawa madaktari tunaopishana nao huku Agha Khan siyo waajiriwa wa serikali kweli? Daktari anayelia njaa ni yule hajielewi!
 
Hao sio waajiriwa wa serikali, Aga Khan wanalipwa vizuri sana kiasi kwamba hakuna haja ya kwenda kupambana huko hospital za serikali na madiwani na wakuu wa wilaya.
 
Napenda kuandika haya yafuatayo kwa uchungu mkubwa sana na kama jamii pamoja na Serikali itapenda kulichukulia jambo hili kwa umakini mkubwa itapendeza sana.

Daktari ni mtu pekee hapa Tanzania anayeongoza kuwa na heshima kutokana na nafasi yake kama daktari na namna ambavyo anatekeleza majukumu yake kwa moyo kuhakikisha wagonjwa wanapona, ndugu wa wagonjwa wanapona pia kisaikolojia lakini huku daktari huyo akiteketeza maisha yake ya kijamii kwa ndugu na familia yake.

DAKTARI ANAPATIKANAJE HAPA TANZANIA.

Kikawaida madaktari wengi huwa ni wale watoto wa kimaskini ambao wamesoma na kusomeshwa kwa shida na uchungu mkubwa sana familia zao na asilimia zaidi 80% wanatoka katika familia za kimaskini, na asilimia chache au ndogo kama 20% ni wale wanaotoka katika familia bora.

Miaka 7 ya shule ya msingi, miaka 4 ya Ordinary level (O-LEVEL), Miaka 2 ya advanced level (3 ya clinical medicine) na miaka 6 ya degree (5 chuo na 1 internship) jumla ya miaka 19 jumla ya kupata degree ya kwanza na kuanza kupractice udaktari kama Medical officier II (Registrar), ambaye kikawaida hadi baada ya makato daktari huyu anabaki na kiasi cha shilingi 840,000/=, kiasi hiki cha pesa anatakiwa kimsaidie katika maisha yake yote kula, kuishi (Makazi), Kuvaa, familia yake kuishi vizuri, familia iliyomlea kuishi vizuri na hata aweze kufanya mambo mengine ya kijamii, hapa ndipo ugundua madaktari wengi kuwa katika maisha yenye stress kubwa ilihari kutimiza majukumu yao kwa moyo mmoja. LAKINI WAPO PIA AMBAO UAMUA KUCHUKUA MIKOPO BANK NA KUJIKUTA PIA ANGALAU AKIHITAJI KUFANYA JAMBO FULANI NA KWASABABU YA MUDA NA USIMAMIZI MZURI ANAFELI SO ANABAKI KUPOKEA HATA SHILINGI 300,000/= AU 400,000/= NI MBAYA SANA HII.

Daktari huyu kwa upendo wa kuwasaidia watanzania uamua kusoma zaidi na kuwa Daktari bingwa mpaka daktari bingwa bobezi maana yake miaka mingine 6 juu uongezeka plus ile miaka 19 aliyotumia katika kupata degree ya kwanza inakua jumla miaka 25, kwahiyo ili umpate daktari bingwa bobezi labda wa Mfumo wa chakula na ini, mfumo wa fahamu, magonjwa ya moyo, upasuaji sanifu, mifupa, ngozi unahitaji miaka 25 mpaka 28 kwa vyuo vingine ambavyo masters ni miaka minne minne.

maana yake almost ujana wake wote wa maisha yake uhutumia katika kudhalisha madaktari bingwa bobezi ambao huwa na maisha ya kawaida sana kuliko mtu ambaye angeamua kufanya biashara zake nyingine kama watu wa KATORO.

Serikali kupitia RAIS aliyepo madarakani
sasa alisikika Dodoma akisema anatambua Madaktari maisha yao yalivyomagumu kwakuwa maslahi yapo chini sana lakini hatambui katika kufanya maslahi ya madaktari yawe juu, yeye pamoja na waziri wa afya wa sasa wanayatambua haya.

lakini kuna wanasiasa ambao wamekaa wanatunga sheria hizi za kuwabana hata madaktari wanalipwa vizuri sana zaidi ya milioni 10 kwa mwezi, lakini si daktari ambaye atakomea 840,000/=, 1,500,000/= na 2,500,000/= kwa registrar, daktari bingwa na bingwa bobezi.

Daktari amekuwa mtu ambaye atashinda hospitalini kuokoa maisha ya mgonjwa, kuwatibu ndugu zake kisaikolojia na bad enough hadi ndugu wanatambua hali za madaktari wao kwa umaskini inabaki tu sifa ya kusema yule ni daktari yule ni daktari.

Ndio maana tumeanza kupoteza jamii ya madaktari vijana unasikia tu kafariki kwa HEART ATTACK, kumbe kisa stress nyingi.... Mfano juzi juzi tumepoteza daktari bingwa bobezi wa figo ambaye amefariki akiwa na miaka 35 tu na huyu daktari ametumia miaka 28 kujitengeneza kufika hapo, Taifa likapoteza mtu wa muhimu sana ukiangalia miaka 35 yake ukitoa miaka 28 unapata miaka 7 tu ya yeye ambayo aliishi bila kufanya jambo lolote maana yake alifaidi utoto wake tu wa miaka 7.

Ndio maana madaktari wengi hawahusishi LESENI zao kwakuwa hela yenyewe ya kuhusisha leseni angalau hata ingekua taasis au mahospital inawakatia leseni watu wake lakini hela ipo juu na ndio maana madaktari wengi they are not allowed to practice lakini wanafanya kazi.

Madaktari wamekuwa watu ambao hata akipata 10,000/= kutoka kwa mgonjwa atafurahi ilimradi apate hela ya kula, daktari huyo anayeshinda hospital muda wote anakosa muda wa kufanya hata angalau sehemu ya pili ya kujidharishia kipato na asipoonekana anaambiwa mzembe na hafanyi majukumu yake mnataka ale wapi????​

NDIO MAANA WAKATI MWINGINE MADAKTARI KWA SASA WANACHUKUA WASAHAA WA KUWASHAURI VIJANA WENGINE WALIOPO NYUMA KUTOKUJA KUSOMA KADA HII YA AFYA YENYE SIFA YA JINA LAKINI MAISHA NI MABAYA NA MAGUMU SANA.

MADAKTARI
WENGI SAIV WANAISHIA KUINGIA KWENYE BETTING PIA WAKIAMINI WANAWEZA KUJIPATIA CHOCHOTE KITU NA KUEPUKANA NA FEDHEA YA UMASKINI

SERIKALI NA JAMII KWA UJUMLA PIGANIENI HAYA KWA MADAKTARI WENU

1. ONGEZENI KIPATO CHA MISHAHARA KWA MADAKTARI MFANO NCHI JIRANI KAMA KENYA NA UGANDA MADAKTARI WANALIPWA VIZURI SANA, WANAANZIA MILIONI 4 MPAKA MILIONI 14 KWA DAKTARI BINGWA BOBEZI KUTEGEMEANA NA AMESOMA UBOBEZI UPI, KWANI TANZANIA MNASHINDWA NINI

2. JAMII IPAZE SAUTI MAANA HATA MAT ILIYOPO HAIFANYI MAJUKUMU YAKE YA KUPIGANIA MASLAHI YA WATU WAKE.

3. KUWE NA WIZARA MOJA TU INAYOHUSIKA NA MASLAHI YA MADAKTARI, KUSIWE NA MARA SIJUI TAMISEMI MARA SIJUI WIZARA YA AFYA, KWAMBA KUNDI MOJA LINAPATA MASLAHI MAZURI KULIKO KUNDI JINGINE.

4. KUWE NA MIHULI YA MADAKTARI KAMA JINSI ILIVYO KWA WANASHERIA TUTAMBULIKE HIVYO NA KWA NAMBA ZETU ZA MCT PALE, KWAKUWA ITASAIDIA ANGALAU KUONGEZA KIPATO PALE AMBAPO MUHULI WA DAKTARI MAALUM UTAKAPOHITAJIKA.

5. SERIKALI IANGALIE HATA KUMPATIA DAKTARI MMOJA MMOJA USAFIRI WA KAWAIDA WA KUANZIA AU KUMSAIDIA KUPATA MKOPO NAFUU WA GARI HUKU SERIKALI IKIONGEZA KIASI KADHAA CHA PESA NA DAKTARI KULIPIA TARATIBU KUPUNGUZA AIBU NDOGO NDOGO ZA KUGOMBANIA DALADALA, KUPANDA BODABODA ZENYE HATARI KUBWA YA KUPATA AJALI, NA HATA KUTEMBEA UMBALI MREFU KWENDA NYUMBANI NA KUNYOOSHEWA VIDOLE YULE NI DAKTARI YULE NI DAKTARI AMBAPO INAMUATHIRI KISAIKOLOJIA.

NATAMBUA MADAKTARI NI WENGI SANA WENYE KUHITAJI JAMBO HILI LIPAZIWE SAUTI BASI NA SISI TUFANYE HIVYO NA ANDIKA MATAMANIO YAKO NINI MADAKTARI WAFANYIWE​

Wanasiasa husema "hawa madaktari tumewasomesha kwa kodi zetu", utafikiri daktari kasomeshwa bure kweli lakini ana mzigo wa kulipa mkopo wa HESLB ndiyo maana huishia kupata laki 8 mwisho wa mwezi.

Daktari aliyesoma kwa mkopo wa HESLB hudaiwa si chini ya million 25 ambayo hulipia kwa zaidi ya miaka 8 kwa hiyo ili afanye mambo ya maisha yake ni lazima achukue mikopo.

Kama hawataki kuboresha mishahara basi waondoe hayo makato ya HESLB (ambayo kwa mwezi si chini ya Tsh. 200,000/-) ili wanaposema wamesomeshwa bure uwe ni ukweli.
 
Wizara ya TAMISEMI inaingilia wizara mama nadhani hii ipo Tz tu(uvuvi,barabara,afya,elimu).Hii nchi sijui walilenga nini na ukiangalia huko TAMISEMI ndio kumejaa uozo🤔.
Uozo mtupu kama nini uliza madaktari wa tamisemi saiv wengi wanajihusisha na biashara tu walishajikatia tamaa hata ya kile walichokisomea, wengi wanatoka huko kwa kwenda kujisomesha na kwenda kujisomesha kuna wale washenzi waliopo maofisini kutoa ruhusa tu hadi uonge au kujipendekeza ushenzi mtupu tu
 
Hii kada sitaruhusu mwanangu haingie hii kada, ina stress shuleni hadi kazini, familia yetu imetoa 2 doctors, nimeshuhudia stress zao wakiwa medical school pale MUHAS hadi leo wapo kazin ila hawana furaha na hii kazi, kuna moja kaenda kusoma bachelor nyingine ya BAF nahic akipata kazi yake ataachana na medical field.
Bora unaushuhuda kabisa wa haya mambo, madaktari wanatia huruma kabisa, unaweza ukamkuta daktari hata ukimpa 5000 hospital anapokea
 
Umesema vyema. Nadhani kwasasa jukwaa zuri ambalo lingetufaa kupambania maslahi yetu ni MAT. Changamoto ya MAT sasa hivi imekuwa yakisiasa sana.
MAT siasa nyingi hamna wa kutetea madaktari kule, wanajali maslahi yao na kukaa kaa karibu na wanasiasa na kusahau kutetea maslahi ya wenzao kitaaluma, hadi leo Level ya daktari bingwa bobezi haitambuliki serikalini kimishahara, lakini watu hao wanahitajika. MAT ya Dr. Ulimboka ndio ilifanya jambo ambalo hadi wewe saiv unanufaika nalo, kina kigwangala wale ndio walipigania maslahi ya wanataaluma wenzao, MAT imeoza na haitokuja kuamka kushughulikia maslahi yenu
 
Haha ha nimbe kawimbo kwanza hapa
Mimi ni nani jamaa Mimi ni mwalimu,
Kada hizi bongo ni ujinga TU , elimu, afya , ulinzi , yaani ukijikuta upo tamisemi kwisha habari yako, hebu fikiria Mimi ni mwalimu kwa miaka zaidi ya kumi sasa, take home yangu ni laki nne kama nusu ni baada ya kukopa, sasa unatoboaje , na hata nisingekopa kabisa ningekuwa nalipwa million Moja na laki mbili, pesa ambayo tunahonga wanawake zetu waliotuzalia watoto ili waendelee kuwatunza watoto,
Solution Kwa SAsa ni ipi nifuate, Mimi nilipogundua na kufahamu salary yangu , nilipochunguza watumishi walionitangulia nilifanya a very very excutive decision and sure it paid me , niliamua kutafta biashara na kuangalia wapi niwekeze, nimecheza na nafaka sana, nimecheza na kilimo sana , ukijumlisha na Mali za urithi sijadili tena mishahara,ila nimekuwa mwalimu asiyekalika kituoni, wananita flying lecture sijali namtuliza headmaster na vichenji chenji ila wakinifuatiia sana nawachia kazi Yao ya ualimu
 
Sasa kila mtu akitoroka kwenye kituo chake cha kazi kwenda kutafuta maisha mitaani, nani atatoa huduma kwa wananchi? Mm nadhani tuyatumie vizuri majukwaa ya vyama vya wafanyakazi kudai maslahi bora wakati huohuo tukiendelea kuwahudumia wananchi.
 
Back
Top Bottom