Maisha ya mtu ya baadaye huendeshwa na akiba

Maisha ya mtu ya baadaye huendeshwa na akiba

Victor Mlaki

JF-Expert Member
Joined
May 1, 2016
Posts
4,151
Reaction score
4,277
Ukiufahamu vizuri wakati ujao utaelewa namna ya kuutumia wakati wako wa sasa kwa sababu wakati hupita kupisha wakati mwingine huku ukiacha alama.

Maisha yako ya baadae kwa zaidi ya asilimia 80% yatandeshwa na kile ulichohifadhi baada ya kutumia na siyo kile ulichopata katika wakati ukiwa na nguvu.

Jifunze kuweka akiba hata kwa kujilazimisha,akiba itakutunzia na kukuondilea aibu yako na pia nitakupa matumaini na hamasa ya kufanya zaidi juu ya kile unachofanya.

Inahitaji kupigana sana na kuvumilia mengi katika wakati uliopo ili kuweka akiba itakayokuwa nguzo yako katika wakati. unapoielekea. Serikali nyingi Duniani zimeitambua nguvu ya akiba nimeweka utaratibu wa mifuko ya huhifadhi ya jamii kwa watumishi wake.

Jizoeze kuweka akiba, hutajuta lucha ya kuona kama ni zoezi gumu. Amua sasa kwa ajili ya wakati wako na wakati wa kizazi vyako.
 
Katika kuweka akiba kuna
1. Akiba kimiminika ambayo ni pesa
2. Akiba solid ambayo ni kama ardhi, nyumba,

Akiba kimiminika unaweza kuiweka benki na kula faida kila mwaka. Kama pesa ni nyingi.

Ardhi inategemea na sehemu ilipo. Wale waliowekeza Kariakoo miaka ya 1960-1970-1980 sasa hivi wanakula kivulini. Mchanga wa Kariakoo umekuwa dhahabu.
 
Akiba utaweka ka kunamfumo mzuri Wa kukufanya upate ,we unaeza kwenda kumwambia raia wa somalia aweke akiba ya chakula?au Wa libya
 
Back
Top Bottom