Maisha ya mtu ya baadaye huendeshwa na akiba

Maisha ya mtu ya baadaye huendeshwa na akiba

Katika kuweka akiba kuna
1. Akiba kimiminika ambayo ni pesa
2. Akiba solid ambayo ni kama ardhi, nyumba,

Akiba kimiminika unaweza kuiweka benki na kula faida kila mwaka. Kama pesa ni nyingi.

Ardhi inategemea na sehemu ilipo. Wale waliowekeza Kariakoo miaka ya 1960-1970-1980 sasa hivi wanakula kivulini. Mchanga wa Kariakoo umekuwa dhahabu.
Bahati mbaya wengi wao maeneo yaliishia kuuzwa na warithi baada ya wao kutangulia na kisha kuliwa bataaaa.

Hata hivyo haikuwa kosa,walifanya vyema sana.
 
Mkuu kununua VIWANJA vingi pasipo kuviendeleza nalo nitatizo. Kama una VIWANJA na bado unalala njaa Ni tatizo kubwa. Wewe NI sawa na mmasai ana n'gombe 2500. Lakini analala kwenye tembe,

Hiyo yote Ni sababu HUJUI unahitaji Nini ufanye Nini Ila unaiga maisha ya watu wengine.
Mkuu nadhani wewe ni mmoja wa wale watu wanaosinziaga mdomo wazi kwenye mabasi na daladala alafu ukiamka unadakia tu mada bila kujua undani wake.

Hapo mimi nimezungumzia kununua mashamba na wala sio mapori kama ulivyoelewa wewe.

Pori likiendelezwa ndio linakuwa shamba na mimi namiliki mashamba.

Hilo swala la kulala njaa lisikuumize kichwa ni lugha ya picha hiyo.
 
Kuna wale wazee waliopata pensheni milioni 90 au milioni 60 then wakazila zote na watoto wazuri na pombe kwa sana huku wake zao wakilalamika...ndani ya miezi 4 hivi zimeisha tayar.....sasa hv wana stress za kijeneza jeneza......
 
Watumishi wa Tanzania watawezaje kuweka akiba wakati hiyo mishahara yao inatumika muda wa siku kumi?Fikiria mtu anapata laki 300000 kwa mwezi hivi mtoa mada umewaza kwa upande upi ?Au upo TANAPA
 
Uanalipwa laki 3 kwa mwez una mke na watoto wa3 na wategemez wengne wa3...kwa siku milo mi 3...hapo akibak itoke wapi?? Umeme,maji,vocha,tv unadaiwa kila mwez
 
Kuna wale wazee waliopata pensheni milioni 90 au milioni 60 then wakazila zote na watoto wazuri na pombe kwa sana huku wake zao wakilalamika...ndani ya miezi 4 hivi zimeisha tayar.....sasa hv wana stress za kijeneza jeneza......
[emoji28][emoji28][emoji28]
 
Ila pia nakushauri hayo mashamba usiishie tu kuyanunua bali uyapime upate hati kabisa na kuyaendeleza ili kuepusha uvamizi au kunyang'anywa na serikali.
Hati inasaidia kuepusha kuvamiwa? Naomba nieleweshe hapa
 
Me nkiwa na ela asee nawashwa balaa mpaka ziishe hata usingiz cpat jaman dah ila n kumtanguliza Mungu mbele
 
Jirani akivuka mpaka wake na kuingia hadi kwenye shamba lako si ni kuvamiwa huko? Au aliyekuuzia akimuuzia tena mtu mwingine. Ukiwa na hati itakulinda kisheria.
Ok mkuu Thanx

Napenda kujua list ya umuhimu wa kulindwa na hati
 
Back
Top Bottom