Maisha ya ndoa anayo pitia ndugu yangu ni mateso, je amelogwa?

Mmh mahusiano haya ni shida
 
Pole sana mkuu

Kubali kuna mahali ulikosea.

1. Kukopa fedha bank kwa ajili ya harusi na nyingine una fadhili hadi send off ni makosa makubwa sana.

2. Inaonekana pamoja na kukaa na huyo mkeo kwa mwaka mmoja hukumsoma vizuri.

Mapendekezo

1. Kwa kuwa bado una miaka 31 .. tafita utaratibu wa taraka haraka iwezekanavyo kwa sababu hamna mtoto, hamjajenga na hakuna mambo mengi ya kigawana.. nenda kaanze maisha, hiyo 140K kwa mwezi itakutosha panga hata chumba kimoja na baadae unaweza panga vyumba viwili.

2. Pambana kwa kutaguta channel nyingine kama kufundisha tuition, biashara ndogo ndogo etc

3. Baada ya taraka, tafuta mwanamke ambaye atakusaidia kusimamia biashara zako kama mkeo.

Angalizo
Kama ni mkristo, hakuna taraka kama sababu sio uasherati au uzinzi.[emoji120]
 
kizazi cha kiume kinazidi kuteketea....kosa la 1: unakubalije kukopa kwa ajili ya harusi,,, then na send off ukagharamia, kosa mla 2: how come uhamie kwa mwanamke...wewe ni mwalimu kweli?? akili zako hazikutoshi je za kutufundishia watoto wetu zatoka wapi?? kosa la 3: kung'ang'ania hapo.......kuna siku atakuletea mme mwenzio..... HITIMISHO hayo makosa yatamgharimu maisha yake yote asipoamka mapema.....bado anayo nafasi ya kujipanga upya......amshukuru Mungu kazi anayo...140.....kisela unasonga.......kama mleta mada una uhakika na hiki na ni ndugu yako kabisa.....na wewe PUMBAFU......unasema mmeshindwa sasa hapa umeleta umbea wa nini........ungelitatua kwanza mbwiga wewe.......ndoa ni ya watu wawili tuu...wa 3 shetani........mwacheni....
 
huwana watoto ondoka baba pole yako.ungekuwa na watoto inakuwa ngumu kuchukua maamuzi
 
Mkuu, salam kwako. Nimesoma mahali umetaja padre, ina maana wamefunga ndoa ya kikristo? Kama ndivyo basi iko mitazamo tofauti juu ya hilo, nami nitachangia mtazamo wangu.

1. Kuna kila dalili kuwa mwanamume alitumia nguvu kubwa sana kujaribu kumnasa huyu mwanamke na kumshawishi awe mkewe. Nasema hivi kwa sababu ndoa ilitumia gharama kubwa mno. Alitafuta kumdhihirishia mwanamke kwamba kile alichomwaminisha ni kweli, maisha yake ni bomba.

2. Kuna uwezekano pia huyo jamaa yako ni mtu wa kutaka sifa za kijinga. Kwamba alitafuta kujipambanua kwenye jamii kuwa ana pesa, ama anamudu sherehe ya kifahari. Kuna ujinga umeshamiri kweli kweli kwamba eti sherehe muhimu ni ndoa kisha kifo!! Usidanganywe na mitazamo hii ya kidunia, matokeo yake ni haya. Ninyi Wakristo licha ya kusoma maandiko bado tu hamtaki kujifunza? Yesu alisema wazi, mwenye dhambi mmoja anapookoka NDIPO HUANGUSHWA PATI LA NGUVU MBINGUNI, ninyi nani anayewadanganya kwamba mkifunga ndoa mbingu zinatikisika? Sasa kutafuta sifa mwishowe ndio kuangukia kwenye madeni yasiyolipika.

3. Kuna uwezekano jamaa yako alioa kwa mtazamo wa kisasa, KUSAIDIANA MAISHA. Yaani alilenga kipato cha mke halafu akapiga hesabu rohoni akijumlisha na chake akaona kabisa dunia inafunguka mbele yake!! Very wrong. Unapofunga ndoa uwe tayari UMEKAMILIKA kwenye kila idara. Ni makosa kuoa ili mtafute pamoja, acheni kuzolewa na uongo wa siku hizi. Utamtoa binti kwao (ingawa siku hizi tunawapata hata kwenye kota za serikali) ili umtunze naye akusaidie kuendeleza ulichokianzisha. Sasa unaoa kisha unafungua biashara, hivi unajua maana ya biashara kweli?

NINI KIFANYIKE

Ni kwamba matarajio ya mwanamke na yale ya mume yanakinzana na hayatokuja yapatane kamwe isipokuwa tu kama wote watakuwa na chanzo kimoja cha hekima na maarifa. Hakuna Kanisa hapa duniani linaloweza kuwapatanisha isipokuwa kama watarudi kwenye msingi wa ndoa yao. Mwanzilishi wa ndoa ni Mungu, sasa wao wasipojisalimisha wake hawawezi kupata suluhu kamwe.

Inaposemwa hofu ya Mungu ni chanzo cha maarifa ni kwa sababu ya upuuzi kama huu. Huyo mwanamke angekuwa na hofu ya Mungu tusingekuwa tunajadili haya hivi leo. Kuwa Mkristo ni kitu kimoja na kumjua Mungu ni kitu tofauti kabisa. Kama mwanamke amefikia hatua ya kukutana sebuleni (nina hakika unajua pia kuwa kiu yake ya ngono anakata kwa njemba tofauti) maana yake hata hofu ya Mungu kwamba wewe ni mune hana kabisa. Kwa lugha nyepesi umeoa KAHABA aliyekuwa na matarajio tofauti kwako, sio ndoa bali atapata nini kwenye ndoa.

Lakini maadamu umeshafunga naye pingu KWA IMANI YENU KANISANI, basi inasemwa UNTIL DEATH DO US APART!! Kwa sababu mlifanya sherehe kubwa kuwafurahisha watazamaji, nao wakawasifieni kwelikweli, mmeshapata thawabu yenu tayari, kwa nini sasa kushangaa!? Fanya hili nawe utaishi:

Mtafute Yesu Kristo kwa moyo wako wote, huku ukimshauri na kumwombea mkeo pia nuru imzukie. Kama utautoa moyo wako kwa Yesu Kristo, nakuhakikishia mambo yote yatafunguka nawe utakuwa mwenye amani maishani mwako. Yesu Kristo PEKEE ndiye chanzo ya hekima na busara, unahitaji neno lake pekee kuiponya ndoa yako. Kwa sasa inaonekana Yesu Kristo tumekaa naye jukwaani sisi watazamaji tukishuhudia kinachoendelea kwenu. Lakini siku ukitaka kuijua siri ya ndoa utamkaribisha awe MC wako afu uone kama kuna uchafu utarejea tena.

Tujifunze ndoa ni nini, tuache maigizo ya ndoa. Ni muhimu tutambue ndoa ni nini. Tusijiingize kwenye ndoa kwa sababu tu ni utaratibu tulioukuta. Habari za starehe inayopatikana kwenye ndoa ni upuuzi wa kisasa, ni upofu wa kutokujua maana halisi ya ndoa.

Ni hayo tu
 
Jibu ni moja tu, hakuwa tayari kuanzisha familia. Kadandia treni kwa mbele
 
Kenge huwa hajui kuwa kaumia hadi damu itoke masikioni.

Kama nduguze wamemshauri amekataa hapa Jf ndio atawasikiliza?
 
Hata kama mngekua na watoto hawatakiwi kugeuka kamba ya kukunyongea.
Unashangaza sana kushindwa kujitegemea na umeajiriwa wakati kuna watu wanaamka na kutoka majumbani hawajui watapata kibarua gani kwa siku lakini ukiwaona wanavyotembea kwa kuvimba na kufurahia maisha huwezi kuamini.
Ni bora ule uji wa chumvi kwako kuliko uzungukwe na mahotpot kwa mwanamke asiyekuheshimu,wala kukuthamini,unaweza mgegeda nae akakuingizia kidole dadeki.
 
Mkuu 140000 mbona parefu,tafuta chumba Cha 30000 lipa mienzi miwili,60000 unabaki na 80000 na hakika hapo unapo ishi nae Kuna vitu vyako pia chukua godoro hata na shuka mbili tatu,sufuriaa na sahani na kikombee.katika ile 80000,nunua jiko la mchina 15000,inabaki 65000,10000 zama mashine nunua Dona lako,inabaki 45000 buku tano daka dagaa wako,20000 tumia kwa matumizi ya mboga mboga na madiko diko Kama ngongwe,bamia,nyanya na vitungu.20000 inayo baki weka akiba mpawa.ishi mwezi wa kwanza hivyo,wapili ongeza Kodi mpaka ifike miezi sita then Anza kujipanga kwa fenichaa
 
Kama unataka kuona mwanamke sababu ya papuchi acha kabisa utajuta Lia siku moja
 

Kosa la kwanza nikuchukua mkopo kwa ajili ya kufanya harusi. Aondoke haraka atateseka sana
 
Aseee ni matokeo ya kukurupuka kuowa bila kupeana muda wa kuchunguzana,Mim na mke wangu mwaka wa 4 sasa naishi nae Tu sijafunga ndoa wala mahari bado nasoma ramani km atanifaa nisajili mazima
 
Pole sana Mkuu mambo ya ndoa ni Magumu sanaa lakini kosa sio lakoo tatizo Ulioa Mwanamke shetanii...!! Wanawake sio watu wakuamini kauli zao maana hubadilika ndani ya Sekunde hata wanandoa wenyewe wake zao wanavyobehave kipindi una hela ni tofauti na kipindi huna lakini haya yote ni mapito mkuu so Long Hujazaa naee.. ANZAAA UPYAAAAAA...ANZA HATA KWA KULALA CHINI SO LONG UNA AMANI YA MOYO ACHANA NAE TENA AMEKWAMBIA CHUKUA VITU VYAKO HAMAA MKUU... UNGEKUWA UPO DAR NINGEKUJA KUKUSAIDIA KUBEBA VITU LEO HII
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…