Maisha ya ndoa anayo pitia ndugu yangu ni mateso, je amelogwa?

Mwanaume anaogopaje kuanza sifuri?
hajachoka huyo,siku akiwa taabani karibu na kufa ataondoka na kandambili tuu..ila jamani kuna wanawake waajabu hata shetani nahisi anashangaa,.khaa!!! hali hiyo wanaishi kwa KOTA,ingekuwa kwenye bonge la jumba lenye kila kitu??
Mwanamke hakumpenda mkaka toka day 1 ,alitaka shela tu na sio ndoa maana toka miaka hyo Bibie kagoma kuzaa na hazai tena huyo a ndoa inakufa.Mkaka luba tu aondoke akuna namna
 
Habari ya asubuhi wakuu.Naomba niende moja kwa moja kwenye mada husika.Mimi nina umri wa miaka 33 na mke wangu ana umri wa miaka 31.Ndoa yetu ina muda wa miaka mitatu sasa ingawa bado hatujabahatika kupata mtoto.

Mimi na mke wangu,wote ni watumishi katika idara ya elimu ambapo mke wangu yupo msingi na mimi nipo sekondari.Yeye ana miaka 10 kazini (2010-2020) na mimi nina miaka 5 kazini (2015-2020)

Turudi nyuma kidogo,Kabla sijafahamiana na mke wangu nilikuwa na maisha yangu tu ya kawaida..ambapo kwa mshahara wangu nilikuwa namudu maisha yangu, nilikuwa nimepanga.

Mwaka 2016 niliweza kukutana na mwenzangu,tulifahamiana na hatimaye tukaanzisha mahusiano.Tuliweza kudumu kwa takribani mwaka mmoja. Mwaka 2017 tulifikia maamuzi ya kufunga pingu za maisha (NDOA).

Niligharamia harusi kwa asilimia 80,ni kipindi ambacho ilinilazimu kuingia kwenye mikopo mirefu,Maana yeye pia nilimkuta ana mkopo. Nilichukua mkopo wa muda wa miaka 7, kiasi cha pesa kiliweza kutumika kwa ajili ya send off na kiasi kingine kwa ajili ya harusi na pia kiasi kingine cha pesa niliweza kuanzisha biashara kadhaa ambazo pia hazikufanya vizuri maana niliishia kupata hasara.Nilikuwa napata take home ambayo kiukweli ilikuwa haitoshelezi mahitaji muhimu.

Mke wangu nilimkuta anaishi nyumba za serikali (KOTA) ambapo ni chumba na sebule.Ameishi hapo tangu alipo ajiriwa mnamo mwaka 2010.

Baada ya harusi mke wangu alinishawishi nihame nilipo kuwa naishi ili niende anapo ishi yeye (KOTA) ili niweze kusave pia gharama za kupanga. Nilikataa sana kufanya hivo lakini aliweza kulazimisha.

Nilikubaliana na uamuzi wa mke wangu,niliweza kuhamia anapo ishi yeye na hatimaye tuliunganisha vitu vyetu,sebule ikaenea vitu kiasi kwamba vingine vilikosa sehemu ya kukaa.Shule anayo fundisha mke wangu na ninapo fundisha mimi ni jirani saana (Takribani mita 100)

Tatizo linaanzia hapa wakuu,ndoa yetu ilikuwa ya furaha saana kwa kipindi cha mwaka mmoja tu.Kuanzia mwaka 2019 mwishoni mke wangu alionyesha mabadiliko makubwa saana.Alianza dharau,majivuno na kashfa..Akiwa anasema kuwa mimi naishi kwake hivyo natakiwa niondoke.

Wakuu ni maumivu makubwa mnoo,ilifikia hatua akawa hataki hata kupika wala kufua nguo zangu na anarudi nyakati anazo zijua yeye mimi nikiwa nimelala.

Ukimuuliza ni ugomvi mwanzo mwisho,ni maisha magumu sana ambayo ninapitia.Mwaka huu mwezi wa tatu bodi ya mikopo ikawa imeanza kunikata pesa yao,maana nilikuwa nimesahaulika kwa kipindi kirefu.Hivyo maumivu yakawa mara dufu,maana kwa sasa pesa inayo ingia ni 140,000/=

Baada ya kumjulisha mke wangu juu ya hilo,akazidi kunidharau na ugomvi ukawa mzito.Msimamo wake ukiwa ni ule ule kuwa nichukue vitu vyangu nimuache.Amesahau kuwa mkopo wangu pia uligharamia harusi pamoja na send off.

Nipo njia panda wakuu,najaribu kuwaza naenda kuanza vipi maisha kwa huu mshahara wangu? Nitalipia vipi kodi na hasa nikiangalia mkopo wangu ndo kwanza nimekatwa miaka miwili bado kama miaka mitano,je ntatoboa?

Saivi hali ni mbaya Zaidi,maana amenifukuza chumbani..hivyo ninalala sebuleni kwa takribani miezi mitano sasa. Ndugu,wasimamizi wa ndoa pamoja na paroko wamejaribu kutusuluhisha lakini mwenzangu ameshikilia msimamo ule ule kuwa niondoke.

Niko frustrated mnoo, kuna wakati nashindwa kutimiza majukumu yangu ya kazi vile ipasavyo.

Baadhi ya ndugu wamenishauri niondoke nikaanze maisha,ukizingatia hatuna mtoto wala mali zozote tulizo chuma pamoja,isipo kuwa tuna kiwanja pekee. lakini kila nikitafakari naona sitoweza kusimama kwa huu mshahara wangu mdogo hasa kumudu gharama za maisha.

Naombeni ushauri wenu wadau,nifanye nini katika hii hali ninayo pitia? Maana kiukweli hatuna future yoyote na ninahisi nitakufa kabla ya siku zangu.Nimejaribu kuandika kwa kifupi,lakini mambo ninayo pitia ni mengi mnoo.

HAYA NI MAISHA HALISI ANAYO PITIA NDUGU YANGU WA KARIBU SANA.WANAFAMILIA HATUJUI TUNAMSAIDIA VIPI MAANA HATAKI KABISA KUONDOKA KWA HUYO MWANAMKE MBALI NA MAUMIVU NA MATESO ANAYO PITIA.KUNA MUDA TUNAWAZA ,JE AMELOGWA NA HUYO MWANAMKE? TUMEMSHAURI IMESHINDIKANA.NINI KIFANYIKE?
Pole mwanaume.

Umekopa lini??
Nenda bank upgrade mkopo.

Mwanamke akifika hatua hiyo usiendelee kuwa naye mwache aende zake.

Wanaume hatuna cha kupoteza.

Panga chumba cha kawaida sana cha 10 kwa mwezi anza maisha na USICHUKUE chochote kwa huyo dada.Ondoka na begi lako.

Muda nzuri wa kuondoka ni mchana tena watumishi wenzake wakiwa wametoka kazini.

Zingati:- HAKIKISHA UNACHUKUA cheti cha ndoa.

Pole mwanaume .
 
You are the best, mkuu. Bonge la bajeti
Mkuu 140000 mbona parefu,tafuta chumba Cha 30000 lipa mienzi miwili,60000 unabaki na 80000 na hakika hapo unapo ishi nae Kuna vitu vyako pia chukua godoro hata na shuka mbili tatu,sufuriaa na sahani na kikombee.katika ile 80000,nunua jiko la mchina 15000,inabaki 65000,10000 zama mashine nunua Dona lako,inabaki 45000 buku tano daka dagaa wako,20000 tumia kwa matumizi ya mboga mboga na madiko diko Kama ngongwe,bamia,nyanya na vitungu.20000 inayo baki weka akiba mpawa.ishi mwezi wa kwanza hivyo,wapili ongeza Kodi mpaka ifike miezi sita then Anza kujipanga kwa fenichaa
 
Habari ya asubuhi wakuu.Naomba niende moja kwa moja kwenye mada husika.Mimi nina umri wa miaka 33 na mke wangu ana umri wa miaka 31.Ndoa yetu ina muda wa miaka mitatu sasa ingawa bado hatujabahatika kupata mtoto.

Mimi na mke wangu,wote ni watumishi katika idara ya elimu ambapo mke wangu yupo msingi na mimi nipo sekondari.Yeye ana miaka 10 kazini (2010-2020) na mimi nina miaka 5 kazini (2015-2020)

Turudi nyuma kidogo,Kabla sijafahamiana na mke wangu nilikuwa na maisha yangu tu ya kawaida..ambapo kwa mshahara wangu nilikuwa namudu maisha yangu, nilikuwa nimepanga.

Mwaka 2016 niliweza kukutana na mwenzangu,tulifahamiana na hatimaye tukaanzisha mahusiano.Tuliweza kudumu kwa takribani mwaka mmoja. Mwaka 2017 tulifikia maamuzi ya kufunga pingu za maisha (NDOA).

Niligharamia harusi kwa asilimia 80,ni kipindi ambacho ilinilazimu kuingia kwenye mikopo mirefu,Maana yeye pia nilimkuta ana mkopo. Nilichukua mkopo wa muda wa miaka 7, kiasi cha pesa kiliweza kutumika kwa ajili ya send off na kiasi kingine kwa ajili ya harusi na pia kiasi kingine cha pesa niliweza kuanzisha biashara kadhaa ambazo pia hazikufanya vizuri maana niliishia kupata hasara.Nilikuwa napata take home ambayo kiukweli ilikuwa haitoshelezi mahitaji muhimu.

Mke wangu nilimkuta anaishi nyumba za serikali (KOTA) ambapo ni chumba na sebule.Ameishi hapo tangu alipo ajiriwa mnamo mwaka 2010.

Baada ya harusi mke wangu alinishawishi nihame nilipo kuwa naishi ili niende anapo ishi yeye (KOTA) ili niweze kusave pia gharama za kupanga. Nilikataa sana kufanya hivo lakini aliweza kulazimisha.

Nilikubaliana na uamuzi wa mke wangu,niliweza kuhamia anapo ishi yeye na hatimaye tuliunganisha vitu vyetu,sebule ikaenea vitu kiasi kwamba vingine vilikosa sehemu ya kukaa.Shule anayo fundisha mke wangu na ninapo fundisha mimi ni jirani saana (Takribani mita 100)

Tatizo linaanzia hapa wakuu,ndoa yetu ilikuwa ya furaha saana kwa kipindi cha mwaka mmoja tu.Kuanzia mwaka 2019 mwishoni mke wangu alionyesha mabadiliko makubwa saana.Alianza dharau,majivuno na kashfa..Akiwa anasema kuwa mimi naishi kwake hivyo natakiwa niondoke.

Wakuu ni maumivu makubwa mnoo,ilifikia hatua akawa hataki hata kupika wala kufua nguo zangu na anarudi nyakati anazo zijua yeye mimi nikiwa nimelala.

Ukimuuliza ni ugomvi mwanzo mwisho,ni maisha magumu sana ambayo ninapitia.Mwaka huu mwezi wa tatu bodi ya mikopo ikawa imeanza kunikata pesa yao,maana nilikuwa nimesahaulika kwa kipindi kirefu.Hivyo maumivu yakawa mara dufu,maana kwa sasa pesa inayo ingia ni 140,000/=

Baada ya kumjulisha mke wangu juu ya hilo,akazidi kunidharau na ugomvi ukawa mzito.Msimamo wake ukiwa ni ule ule kuwa nichukue vitu vyangu nimuache.Amesahau kuwa mkopo wangu pia uligharamia harusi pamoja na send off.

Nipo njia panda wakuu,najaribu kuwaza naenda kuanza vipi maisha kwa huu mshahara wangu? Nitalipia vipi kodi na hasa nikiangalia mkopo wangu ndo kwanza nimekatwa miaka miwili bado kama miaka mitano,je ntatoboa?

Saivi hali ni mbaya Zaidi,maana amenifukuza chumbani..hivyo ninalala sebuleni kwa takribani miezi mitano sasa. Ndugu,wasimamizi wa ndoa pamoja na paroko wamejaribu kutusuluhisha lakini mwenzangu ameshikilia msimamo ule ule kuwa niondoke.

Niko frustrated mnoo, kuna wakati nashindwa kutimiza majukumu yangu ya kazi vile ipasavyo.

Baadhi ya ndugu wamenishauri niondoke nikaanze maisha,ukizingatia hatuna mtoto wala mali zozote tulizo chuma pamoja,isipo kuwa tuna kiwanja pekee. lakini kila nikitafakari naona sitoweza kusimama kwa huu mshahara wangu mdogo hasa kumudu gharama za maisha.

Naombeni ushauri wenu wadau,nifanye nini katika hii hali ninayo pitia? Maana kiukweli hatuna future yoyote na ninahisi nitakufa kabla ya siku zangu.Nimejaribu kuandika kwa kifupi,lakini mambo ninayo pitia ni mengi mnoo.

HAYA NI MAISHA HALISI ANAYO PITIA NDUGU YANGU WA KARIBU SANA.WANAFAMILIA HATUJUI TUNAMSAIDIA VIPI MAANA HATAKI KABISA KUONDOKA KWA HUYO MWANAMKE MBALI NA MAUMIVU NA MATESO ANAYO PITIA.KUNA MUDA TUNAWAZA ,JE AMELOGWA NA HUYO MWANAMKE? TUMEMSHAURI IMESHINDIKANA.NINI KIFANYIKE?
Huyo matatizo kanunua mwenyewe,yani unaenda gharamia sendoff kwa pesa ya mkopo?yani hana tofauti za akili za polepole au lusinde
 
Sass anasubiri nini kuhama yaani kuhama tu anashindwa huyo kweli ni kiazi
 
Mimi nilishasema Ndoa sio kwa ajili ya Mwanaume.. Ni mtego wa Wanawake huo.. na Kama Mwanaume nnae jiamini ipasavyo ndoa SIFUNGI na Watoto Kama watakuja fresh Ila hata Ngono bila Kinga sitafanya na hela lazima niwe nazo nyingi sana... Alafu tuone Kama nitatoboka!!!
 
Kutoboka wapi sasa mkuu?
 
Hii ndio mistake kubwa iliyomtumbukiza shimoni huyo jamaa.
Hakujua kwamba kazi ya mkopo sio kufanyia harusi.

Hapa naona katika simpo logic jamaa hakuwa amependwa na mwanamke ,kuna vitu vilikuwa vinamsukuma nadhani ni vipesa,na huyu jamaa ili kumuwini zaidi mwanamke huyu ndio maana akaenda kopa mamilioni ya pesa kwa ajili ya ndoa akidhani kuwa mkopo ni zawadi.

Hivi wanaume tunakwama wapi? Kitu cha siku moja kikuingize kwenye majuto ya maisha,believe me mimi nilifunga ndoa kanisani baada ya kuisha kila mtu alienda kwao utadhani vile watu hutawanyika baada ya mechi ya mpira kuisha,na katika ndoa yangu nilitumia shilingi 15 elfu ya picha ambayo tulichanga na wife,shilingi 30 elfu kwa ajili ya kumfuata mchungaji kwani kanisa lilikuwa mbali na pesa kiasi cha shilingi 20/elfu kwa ajili ya chakula na malazi ,vijana mbadilike vinginevyo mtaendelea kuwa wahanga wa mapenzi kila siku.

Mwisho namshauri huyo mwalimu ahame hapo,na kama kweli huyo mwalimu anatendwa hiana na huyo mke wake wa ndoa naamini the supernatural power itatenda haki kwa muhusika na hakika atajuta sana .
 
Kutoboka wapi sasa mkuu?
Nione Kuna baya gani litakalo nitokea.. Maana naskiaga wanaume tunaambiwa hatuwezi kuishi bila kuoa.. but I don't see any reason to do so plus I respect women so much kiasi Kwamba I am not ready to waste my energy and other resources just to make her happy... Si unaona yaliyo mkuta jembe hapo.. Hakuna ndoa hapa Tena tunapoelekea hata mahusiano nahisi nitasitisha pia..
 
Back
Top Bottom