Maisha ya ndoa hivi sasa yakoje?

Maisha ya ndoa hivi sasa yakoje?

Nilioa 2020 tukakaa miaka miwili tukachana,ndoa ni gereza tosha,ukichelewa kurudi home unaambiwa ulikuwa kwa Malaya zako,ukiwahi unaambiwa leo naona hujapita kwa Malaya zako,huu ujinga storudia
Hapana, usiungane na hawa timu kataa ndoa. Ndoa inatuchangamsha akili wanaume na vile vile inatujenga kuweza kuishi popote. Ukiwa na ndoa hata kwenye kitanda chenye misumari badala ya godoro unaweza kulala!!:CATLUL::CATLUL::CATLUL:
 
Mi home waliacha kunisisitiza. Wamebaki masnitch wa kazini.

Unakuta mtu ananisisitiza nioe wakati kila mtu anajua yeye na mume wake wamezinguana na wanakaa sehemu tofauti ila Dar hii hii.
 
Ngoja waje tusome ushauri ila nadhani wachache wanaopigana na kuuana sio mifano tosha ya kusema ndoa zinashida
Wapo ambao wako almost heaven wanafurahia ndoa
Maisha ya ndoa hayana formula, ni wwe kutafuta formula yako uitumie utakavyo!!
 
Hapana, usiungane na hawa timu kataa ndoa. Ndoa inatuchangamsha akili wanaume na vile vile inatujenga kuweza kuishi popote. Ukiwa na ndoa hata kwenye kitanda chenye misumari badala ya godoro unaweza kulala!!:CATLUL::CATLUL::CATLUL:
Kwa dunia ya sasa ndoa haina maana kwa mwanaume, labda mwanamke ndie anaweza kunufaika na ndoa maana kuna masilahi yake yanalindwa kisheria akiwa ndoani.
 
Unajua kuwa maisha ya kuwa single ni magumu, hivyo tunahitaji kuwa na maisha ya wawili, tupate watoto na tujenge familia.

Kwa wale walioolewa kuanzia mwaka 2020 hadi 2023, maisha ya ndoa yakoje? Visa vipo vingi; wengine wameuana, wameachana na wengine wanaishi pamoja kwa sababu fulani.

Naomba, kama umeoa au kuolewa, utoe ushauri.
Japokuwa sipo katika miaka uliyotaja, lakini yawezekana ukapata mawili matatu.

Mimi nimeoa 2016, kabla ya kuoa nilishatathmini mapungufu ya mwenzangu kuona kwamba nitaweza kuyavumilia na kusaidiana kuwekana sawa (hakuna mwanamke wala mwanaume mkamilifu). Kuna tabia zinaweza kukukwaza na zingine zikakufurahisha, kwa hivyo tathmini mapema.

Alhamdulillaah mpaka leo tuko pamoja, kukwazana kwa hapa na pale hakukosekani. Lakini ni mambo madogo madogo ambayo huwa tunayamaliza wenyewe kirahisi tu. Hatujawahi kumshirikisha yoyote kwenye tofauti zetu.

Kuwa single kunaweza kuwa na faida zake, lakini madhara yanaweza kuwa makubwa. Maana kuna mahitaji ya kimwili kwa mtu aliyepevuka ni muhimu kuyapata.

Wengi wanaoona kuwa single ni bora pia hawajasalimika na uzinzi, watoto wa nje ya ndoa, mwisho wa siku tunakuja kuwasimanga single mothers huku tatizo ni mitazamo yetu wenyewe.

Sisemi kwamba wote waliopo kwenye ndoa wametakasika na uzinzi, la hasha. Lakini hakuna shaka ndoa ni miongoni mwa hatua thabiti katika kujenga maadili ya jamii
 
Unajua kuwa maisha ya kuwa single ni magumu, hivyo tunahitaji kuwa na maisha ya wawili, tupate watoto na tujenge familia.

Kwa wale walioolewa kuanzia mwaka 2020 hadi 2023, maisha ya ndoa yakoje? Visa vipo vingi; wengine wameuana, wameachana na wengine wanaishi pamoja kwa sababu fulani.

Naomba, kama umeoa au kuolewa, utoe ushauri.
Asali tupu Ni kujipimia tuu
giphy.gif
 
Back
Top Bottom