Wakuu nitaendelea kuwapa simulizi hizi za mission za CIA, MOSSAD na KGB maana wenzetu wanaziweka wazi hawana cha kuficha kama bongo. Ile mission ya kumkamata Osama ni kali lakini kwa watu wanaojua mission zilizofanyika hapa duniani, hakuna mission kali kuizidi ile ya Entebbe iliyofanywa na MOSSAD, hata hii ya Osama ilichukua items nyingi kwenye mission ya Entebbe. Ukitaka kujua ile ya Entebbe ni kali kuliko ya Osama linganisha technologia zilizotumika, hii ya Osama walitumia chopa za shinoku zenye technology ya stealth inayoweza kukwepa rada wakati ya Entebbe hakukuwa na technology hiyo. Ndege zilizohusika kwenye mission ya Osama ziliruka kutoka kwenye military base ya marekani iliyopo Jalalabad Afg ambayo ipo ka 20 km kutoka kwenye mpaka na Pak wakati Ndege zilizohusika kwenye mission ya Entebbe ziliruka kutoka Tel Aviv kupita nchi mbili ambazo ni hostile Egypt na Sudan 5,000km kuja Entebbe. Operation ya Osama kulikuwepo na maofisa wa CIA waliokuwa kwenye ofisi ya ubalozi ambao walielekea Abbottabad mapema kwaajili ya ku-monitor situation na kuna maofisa wa ISI ambao walikuwa kwenye jeshi la Pakistani ambao walikuwa wanatoa taarifa kwa maofisa wa CIA kila kinachoendelea kuhusiana na response ya jeshi la Pakistani. Siku nikipata nafasi nitawasimulia ile operation ya Entebbe ilivyopangwa na failures na success zake. kama ilivyokuwa ya Osama zilipangwa plana 4 za kuifanya ile mission ya Osama na zote zilifanyiwa mazoezi ndio maana ile helicopter ilivyokosa thrust na kudondoka walibadili plan kutoka Plan A kwenda plan C, sasa siku nikipata nafasi nitawaeleza Plani A ilikuwa ikoje, plan b,c na d. Na kwa nini ile helicopter ilivyodondoka walibadili plan kutoa A kwenda C, kwa nini hawakuenda plan B.